Mdau mkuu wa Libeneke na nanihii
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT "THE SMART CHOICE" Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Ila nawaomba tuweze kujieshimu kila mmoja wetu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya globu ya jamii, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoeleza vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.



 

Friday, July 11, 2008
uchunguzi wa ushirikina bungeni
Jeshi la Polisi limetoa ripoti yake kuhusu uchunguzi wa kile kilichodaiwa vitendo vya kishirikina Bungeni karibu mwezi mmoja uliopita ambapo ilidaiwa mmojawapo wa wabunge alionekana akimwaga unga kwenye viti mbalimbali.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa (kati ya niliyoyanasa kwa haraka)a. Hakuna Kamera iliyozimwa kuanzia mwaka 2006 (don't ask me walisema zilikuwa zimezimwa)

b. Kwenye mkanda uliodaiwa hakuna mtu aliyeonekana akifanya jambo lolote lile (mkanda mtupu?)

c. Vumbi lililoenda kuchunguzwa halikuwa na sumu yoyote inayotambulika.

d. Hakuna kitendo cha kishirikina.

Hayo yamesemwa na Kamanda huyo wa Mkoa Bw. Omar Mganga alipotoa taarifa kwa Kamati ya Uongozi ya Bunge kuhusu uchunguzi huo uliofuatia matukio ya wiki chache zilizopita. Vyanzo vingine vinasema kuwa kati ya mambo yaligundulika katika uchunguzi huo ni pamoja:a.

Kamera mbili kuwa mbovu kwa muda mrefu bila ya kufanyiwa matengenezo na nyuingine mbili zilikuwa zimegeuzwa (tilted) ingawa sijui zilikuwa zinaangalia upande gani!

b. Na mojawapo ya madai ya kushtua kabisa ambayo wenu mtiifu ameyasikia ni kuwa baadhi ya watu wanaolipwa kuzikodolea macho hizo kamera walikuwa wameuchapa!

Uchunguzi huu unatulazimisha kujiuliza kama kweli bila ya kuwa na mfumo mzuri unaohakikisha uhuru wa taasisi zetu tunaweza kweli kuendesha uchunguzi wowote ambao matokeo yake yakashawishi uaminifu?

Baada ya uchunguzi wa TAKUKURU kuhusu Richmond ambao baadaye ulioneshwa na Kamati Teule ya Bunge kuwa ulikuwa umelenga kupotosha jamii, hatuna budi kujiuliza tena kama vyombo vyetu viko huru na vinaweza kuaminika.

Endapo hatuwezi kuwaamini hawa ambao wamepewa jukumu hilo la kufanya uchunguzi na kutoa taarifa au kufanyia kazi taarifa basi inakuwa vigumu sana kuhakikisha kunakuwepo na utawala wa sheria.

Mfano mzuri ni suala la uchunguzi wa EPA ambao ulitakiwa kukamilika ndani ya miezi sita. Hadi sasa hakuna anayejua kinaendelea nini baada ya Mwanyika na timu yake kushindwa kutekeleza kazi hiyo ndani ya miezi sita licha ya ushahidi wote kukusanywa na kupelekwa mbele yao?

Kwa mtindo huu sidhani kama tutafika, tutaendelea kuzugwa, kuzugana, na kuzugika. Sikiliza matangazo haya "live" kupitia KLHnews.comTitle: KLH News Episode: Uhuru wa Taasisi zetu, kiini cha Utawala wa sheria!
http://mwanakijiji.podOmatic.com/
entry/2008-07-10T21_27_18-07_00

Enjoy!
http://mwanakijiji.podOmatic.com/mymedia/thumb/13384/300x300_1093106.jpg
 
© Michuzi | Friday, July 11, 2008 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako |


Maoni: 3


  • Tarehe Sun Jul 13, 11:50:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    akuna mtu yeyote amesema unga ulikua na sumu. mtanzania yeyote anajua wachawi wanatumia unga, poda, vumbi na vingine vingi. swali la kujiuliza ni unga huo ulifikaje bungeni na kwa matumizi gani?

     
  • Tarehe Mon Jul 14, 09:30:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Hii ndo BONGO bwana mwisho wa yote HAKUNA cha EPA , RICHMOND wala nini na watu watajinafasi kwa raha zao ( TATIZO LINAKUJA ' NANI ALIYE MSAFI AMNYOOSHEE KIDOLE MWENZIE '

     
  • Tarehe Mon Jul 14, 12:54:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Wadau nawauliza tunawezaje kujua kuwa hapa hakuna ushirikina? Maana mkemia mkuu anaweza kuongelea sumu sijui kama yeye au kamanda wa polisi wanao utaalamu wa kusema hakuna ushirikina!!

     


Idadi ya watu
eXTReMe Tracker