Mdau mkuu wa Libeneke na nanihii
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT "THE SMART CHOICE" Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Ila nawaomba tuweze kujieshimu kila mmoja wetu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya globu ya jamii, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoeleza vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.



 

Friday, August 29, 2008
afande chemi che mponda

Wadau tangu jana ninaigiza katika sinema, Edge of Darkness, hapa Boston. Stelingi wake ni Mel Gibson na Robert DeNiro.

Ninacheza kama askari polisi wa kike (background). Nitaitwa mara kwa mara kuigiza kwenye background hadi wanapomaliza ku-shuti mwezi Desemba.

Nilipatwa na butwaa nilipopigiwa simu wiki mbili zilizoipita na kuambiwa kuwa nimechaguliwa na mwongoza sinema, kuwa askari kanzu wa kike. Na tena si kwa siku moja tu.Haturuhusiwi kupiga picha kwenye set hii nimepiga mwenyewe Dressing Room.

Ninavaa bastola bandia na madude mengine wanaovaa polisi wa Boston.Mel Gibson mtu poa sana, jana alikuwa anatuchekesha kwenye set, leo alikuja kula lunch kwenye meza tuliyokuwa tunakula. Kaongea vizuri tu na sisi. Tulishangaa kuona mtu "A" list kama yeye anafanya hivyo. Mara nyingi wanaenda kula kwenye trela au hoteli lakini siyo na extras.

Haya nitawapa updates.

Mcheza sinema, Gbenga Akkinabe (The Wire) mwenye asili ya Nigeria anaigiza kwenye hiyo sinema kama mpelelezi. Nimeongea naye kidogo, alisema kuwa ana marafiki wengi kutoka Tanzania huko New York.

Habari na picha kutoka:
-------------------------------------------------------
Hongera sana da'chemi kwa mafanikio yako ambayo yanakuja taratiiiiiiiibu. iko siku tutasikia wewe ndiye stelingi. ukija bongo tutakuwa tunakugombea kama kina will smith. he, mbona watani wa jadi watatukoma! iko siku dada, kaza buti tu
-michuzi
 
© Michuzi | Friday, August 29, 2008 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako |


Maoni: 14


  • Tarehe Fri Aug 29, 10:41:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    hahahahah watatukoma sana tu watani wetu halohalooo,da chemi hongera na umependeza na nguo hizo.

     
  • Tarehe Fri Aug 29, 10:46:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    kaka michuzi nimeona maada kwa da chem kuwa mtoto alazimwishwa kufanya mapenzi na mbwa,itakuwa uzuri ukaitoa kwako ili ijadiliwe,inasikitisha sana

     
  • Tarehe Fri Aug 29, 11:43:00 AM, Mtoa Maoni: Blogger Chemi Che-Mponda

    Michuzi,

    Asante sana.

    Na ninakutakia Happy Birthday!

    Chemi

     
  • Tarehe Fri Aug 29, 12:05:00 PM, Mtoa Maoni: Blogger BRAYAN

    Inatia moyo na kufurahisha sana kuona watanzania sasa mambo yetu safi pande hizo nice mysister do it .

     
  • Tarehe Fri Aug 29, 12:42:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Dada Chemi!!

    A hero is an ordinary individual who finds the strength to persevere
    and endure in spite of overwhelming obstacles."

    Well done! and keep it up.

    Yasini - UKerewe

     
  • Tarehe Fri Aug 29, 01:45:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Tulikuwa US tunajua kwa nini dada chem umechaguliwa. Majority ya security guard wapo kidogo kwenye watch list na ma diet physician.

     
  • Tarehe Fri Aug 29, 04:43:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Mmarekani Mweusi

    Huyo NDO Dada Chiku.. Kama umesoma zile sorded stories za Mapenzi..

    Holla!

     
  • Tarehe Fri Aug 29, 04:55:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Chemi hakuchaguliwa kutoka kwenye group of secutity guards. Amepata nafasi kutokana na her acting resume na fit kwenye position aliyotakiwa kucheza. Hongera dada yetu and keep it up!

     
  • Tarehe Fri Aug 29, 07:24:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    nampongeza mtanzania mwenzetu chemi che mponda,maana tukiitizama movie hiyo pia tutapata cha kuonyesha kwa wenzetu kuwa huyo naye ni mtanzania. hongera chemi.
    MZEE YASIN -UKEREWE napenda mimi niongeze definition yangu ya a hero!!nikizingatia neno lenyewe na matumizi yake maranyingi.
    - a hero in most cases is an individual dare to act stupidly whose stupidity turn out with postive rewards either to him/herself or to others,otherwise when he/she doen't make it out he/she apears to be a fool and stupid one!hahaha
    DOUBLE 'P'

     
  • Tarehe Sat Aug 30, 01:54:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Da-Chemponda, hilo jicho, mashallah. Mwanamke jicho eeh!!!!!

     
  • Tarehe Sat Aug 30, 05:23:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    He watani wetu wa jadi wamekua kwenye extras za movies tangu zamani . Kwa mfano Out of Africa hata sisi wabongo pia tulikua extras.

     
  • Tarehe Sat Aug 30, 05:27:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    jamani kawaambieni yeye yuko kama extras siyo actor

     
  • Tarehe Sun Aug 31, 08:00:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Anony 5:27 Background ni sawa na extra.

    Hongera Dada Chemi tunagojea kwa hamu kusikia una role kubwa. Unaanza chini na kupanda kwenda juu! Kwa sisi wabongo umefika mbali.

    Kuna shombe fulani huko Hollywood wala hasemi asili yake ya TZ! Anaona haya! Wee Dada Chemi unatangaza Tanzania. Asante.

     
  • Tarehe Sun Aug 31, 11:24:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Godfather

    Wadau wenzangu. Huyu dada ni mwanachama wa Screen Actors Guild. Hicho ni chama kikubwa sana huko Marekani akina Denzel, Halle Berry, Angela Bassett wamo. Mafanikio yake si madogo ingawa kwa sasa anaigiza kama extra. Navyoelewa kuna watu ambao wanajitahidi miaka kuingia kwenye hicho chama lakini wanashindwa. Hongera sana dada yetu.

     


Idadi ya watu
eXTReMe Tracker