Mpiganaji Zephania Musendo akifurahia uhuru wake baada ya kutoka gerezani jana
Zephania Musendo akilakiwa na kupewa kumbato kutoka kwa mkewe kipenzi Pascalia mara baada ya kutoka kifungoni jana

MWANDISHI wa Habari Mwandamizi Mpiganaji Zephania Musendo aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano jela ametoka gerezaji jana.Musendo aliyeanza kutumikia kifungo chake Mei 17, mwaka 2005 katika gereza la Keko kwa kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa aliachiwa saa 9:54 na kupokelewa na wanafamilia yake waliofika kumpokea katika gereza la Mahabusu Mkuza mkoani Pwani.

Musendo aliyelakiwa na watoto wake Richard na Victor,mke wake Pascalia pamoja na shemeji yake Elizabeth N’gabo aliiteua siku yake ya kutoka gerezani na kuwa siku yake ya kuzaliwa baada ya yeye kutokuifahamu rasmi tarehe yake ya kuzaliwa.

“Leo ni siku yangu ya kuzaliwa maana ninafurahi sana kuwa hutru na kutoka katika matatizo haya ambayo yamenikabili kwa kipindi kirefu,baba yangu hakujua nilizaliwa lini zaidi ya mwaka kuwa ni 1947,”Wanafafamilia hao wanasema wanafurahi sana babayao kuwa huru na wanamshukuru Mungu kwa kutoka jela akiwa hai na mwenye afya njema tofauti na walivyodhania.
Akisimulia maisha yake ya miaka mitatu na miezi mitano aliyoishi katika magereza mawili ya Keko na Mkuza anasema ni maisha hatari yasiyozoeleka na mwanadamu wa kawaida.“Jela hakufai maana kitendo cha kutengwa na jamii,familia yako,nyumba ndugu jamaa na marafiki na kufanya mambo yako kwa uhutru ni hatari sana,” alisema.

Anasema alipokaa katika gereza la Keko kwa muda wa mwezi mmoja mambo hayakuwa mazuri sana kutokana na afya yake kutokuwa nzuri na yeye kulazimika kutumikia kifungo sambamba na kazi ngumu.Licha ya kuwa hakupata usumbufu wa mateso kutoka kwa wafungwa wenzakwe lakini alipata tabu mwanzoni kutoka kwa Askari Magereza kwa kutekeleza adhabu yake kwa upande wa kazi ngumu.

“Nilipata shida kutoka kwa askari maana walikuwa hawanielewi kuwa ninaumwa , wao walishikilia midhali nimehukumiwa kazi ngumu lazima nizifanye tu,”alisema.Alisema wakati akiwa katika gereza la Mkuza mkoani Pwani wakifabnya kazi ya kubeba kifusi katika jingo la Mkuu wa Mkoa alianguka katika ngazi na kushindwa kuendelea na kazi lakini hakupelekwa Hospitali siku hiyo kupatiwa matibabu.

Alianza kupatiwa matibabu ya Kisukari pamoja na Presha katika Hospitali ya Tumbi na kuandikiwa na daktari awe anakula mayai,maziwa na mboga za majani lakini aliporudi gerezani hakupata vitu hivyo hadi pale familia yake ilipoamua kumuwekea bili ya maziwa kutoka katika Ng’ombe gerezani hapo.

Aliendelea na kazi nyepesi gerezani hadi pale alipochaguliwa kuwa Nyapara mkuu Aprili 2007 nafasi ambayo aliitumikia hadi alipotoka gerezani humo.Baadhi ya Askari Jela walisema watamkumbuka Musendo kwa nidhamu,Busara na Uongozi mzuri alipokuwa Nyapara mkuu katika gereza hilo ambalo linawafungwa 78 na mahabusu 129.

Aidha Musendo anasema maisha yake yalibadilika pale alipochaguliwa kuwa Nyapara mkuu na wenzake kumkubali na kumheshimu kutokana na umri wake.“Kazi zangu kubwa zilikuwa kusimamia chakula,magenge ya kazi,usafi wa gereza na uandaaji wa risala kwa wageni zihusuzo wafungwakuna wakati niliandika hata risala za mkuu wa Gereza”.

Akizungumzia juu ya tuhuma zilizo mtia hatiani Musendo anasema yeye kwa sasa anafurahi na kushukuru Mungu kuwa yupo huru lakini Kubwa zaidi anafurahia kuwa habarizilizokuwa zikiandikwa katika gazeti zilikuwa ni zakweli.

Juu ya kurejea katiika ulingo wa habari Musendo anasema hatoacha kuandika na kampuni yeyote atakayopata ataanza kazi yake ya uandishi na kulitumikia taifa.Gazeti la HabariLeo ndio gazeti pekee lililopata picha za tukio hili pamoja na Habari.
Usikose Makala yake toleo la Septemba 18 2008 katika HabariLeo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. how do we interview you'?

    ReplyDelete
  2. Sikujua kabisa kuwa Mr Musendo alikuwa gerezani-mpaka wakati huu nilipoona picha yake kuwa ametoka. Ninamkumbuka sana Mzee Musendo wakati ule alipokuwa News Editor wa the African. Pole sana kwa yaliyokukuta na Mungu atakujalia rehema zake na utarudi katika viwanja vya mapambano.

    ReplyDelete
  3. Wamemuonea tu huyo. Alikula rushwa gani hiyo wakati wala rushwa wakuu wanaishi kiulaini?

    ReplyDelete
  4. KATIKA KOSA KKUBWA LA UCHUNGU WA UKOLONI NI KURITHI MAGEREZA HILI NI KOSA KUBWA SANA . KOSA LINGINE TO KURITHI SHERIA PENEL CODES NA KUTUMIA KINGEREZA KATIKA SHERIA ILI WATU WAFUNGWE OVYO. MUNGU MKUBWA HONGERA SANA

    ReplyDelete
  5. Hivi Tanzania ni nchi ya kumfunga mtu eti kala rushwa? mbona ni daily, routine, normal practice!

    Mungu kweli ibariki Tz, viongozi na hasa watu wake we mean it!!!

    Grandma

    ReplyDelete
  6. WATU KAMA HAWA NDIO WANAOFUNGWA KIRAHISI TZ.MWANDISHI ALIYEOMBA RUSHWA KIDOGO,ASKARI WA TRAFIKI,MJUMBE WA SHINA,MWALIMU WA SHULE N.K. LAKINI WALE WANAOIBA MABILIONI NA MABILIONI AU KUIINGIZA SERIKALI KENYE MIKATABA MIBOVU KWA RUSHWA WANAACHWA WAKITEMBEA KWENYE MAGARI YAO YA KIFAHARI NA KUISHI KWENYE MAJUMBA YAO YA KIAJABU NA HAKUNA ANAYETHUBUTU KUWAGUSA.WANAENDELEA KUWA VIONGOZI WETU KATIKA MABUNGE NA SERIKALI NA TAASISI NYENGINE KWA MBWEMBWE NA KEJELI.
    BADALA YA KUKAMATWA NA KUPELEKWA MAHAKAMANI SERIKALI HUUNDA TUME ZA KUCHUNGUZANA NA KUSAFISHANA.NI WAO KWA WAO, WANAGAWANA NCHI.
    MUNGU IOKOE TZ.

    ReplyDelete
  7. kaka musendo, pole sana. hayo ndiyo mambo ya kazi ya uandishi wa habari. kila mtu anaamini kuwa ulionewa na hakimu aliyesikiliza kesi yako kwani alitoa hukumu hiyo kwa kushinikizwa na aliyekuwa mkurugenzi wa upelelezi wa PCB wakati huo Edward Hoseah ambaye ni fisadi namba wani nchini. Mungu yupo atakulipia tu

    ReplyDelete
  8. Chenge and Co. should be serving their life sentences at this very moment!

    ReplyDelete
  9. hapo ndipo mke anapoonekana wa maana. mtazame mama huyo, yupo nawe mpaka unatoka gerezani. hakika aliyeita ndoa pingu za maisha, hakukosea.

    ReplyDelete
  10. kama jadi yani mnyonge ndiyo ambae huwa ananyongwa tanganyika, kuna watu wameiba mamilioni ya pesa na wanajulikana lakini mpaka leo bado wako urahiani na wengine bado wanazishikilia nafasi zao za kazi,kuna wanyonge kibao ambao wanafia jela bila hata ya hatia yeyote ile, inajulikana kuwa hata viongozi wenu wa nchi ni mamalaya sasa iweje mtu kana Nguza yeye anafungwa kifungo cha maisha kwa kula uroda? eti wanadai kuwa alikula uroda na watoto wadogo, ninani kasahau kuwa vingozi wenu walikuwa na mpaka leo wanatembelea mashuleni kutafuta vijitoto vidogovidogo?. inajulikana kuwa hakuna tofauti kati ya mahakama na serikali huko kwenu sasa iliyobaki ni kuunda mahakama zetu wenyewe mitaani.

    Mbega

    ReplyDelete
  11. Mr.Musendo shikamoo.Pole sana.Pole sana Mrs Musendo na wanao kwa kuwa mbali na 'mzee' kwa kipindi kirefu.Mimi sikufahamu,ila Physiologically(kisaikolojia?)wewe inaonekana wazi kabisa ulionewa.Endelea na kalamu mzee hakuna kilichoharibika.Inauma sana kwakweli kama blogger walivyosema hapo juu kwamba watu wanaiba mabilioni ya wananchi milioni 35 hawafungwi,wanadunda tu.Hawa wadogo wadogo looooh!Siwaingilii dola lakini huo ndiyo ukweli.

    ReplyDelete
  12. Musendo alikomeshwa kwa kumwandika mtu fulani vibaya. Ni waandishi wa habari na wapiga picha wangapi wanaoomba rushwa huko Bongo! Mkianza kuwafunga hakuna atakayebaki!

    ReplyDelete
  13. Zeph! Mzee Zeph, nafurahi kuona umetoka gerezani. Mungu akubariki wewe na familia yako. Mungu amekulinda.

    ReplyDelete
  14. Michu mimi naomba nimpongeze sana Mroki Mroki kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kupata picha hii ya pekee maana siku nzima Mroki alikuwa Gumzo katika vyombo vyote vya habari Tanzania. Anastahili kuitwa mpigapicha bora Tanzania 2008. na Hongera sa habariLeo na Daily noise kwa kuwa kumpa nafasi magazetini. Nilidhani IPP ndio wangetupa hii lakini hata magazeti ya serikali. Sfi sana.
    Mashaka

    ReplyDelete
  15. michuzi nataka niulize hivi mtu anajisikiaje anapoamua kumtesa au hata kumuua mwenzake kwa makusudi eti kwakuwa ana nguvu au madaraka? halafu utawakuta watu hao hao wakiabudu mungu sasa sijui wanamwabudu mungu yupi?.Msijisahau jamani hapa duniani kila mtu anapita tu kwa maana nyingine kila roho itaionja mauti. Marehemu Marijani aliimba kuwa walikuwepo ambao walijiona wana nguvu na mpaka wengine wakadiriki kujiita mungu lakini cha kujiuliza wako wapi kwa sasa?

    ReplyDelete
  16. MTOA MAONI WA 18,2009:908PM NAKUUNGA MKONO KABISA NA ULIO YASEMA YAMENIGUSA NA NAJUA YATAWAGUSA WENGI... DUNIA HIII WEE WACHA TU

    ReplyDelete
  17. Chenge and Co. should be serving their LIVES sentences at this very moment. UNAONA HAPO WAKO WENGI CHENGE NA WENZAKE HIVYO LIFE LAZIMA IWE PRURAL NDO MAANA NIMEWEKA LIVES INSTED OF LIFE HII NI SINGULAR, PIA SIZANI TANZANIA KOSA LA RUSHWA MTU HUFUNGWAGA MAISHA TANZANIA, HIVYO INGEKUWA HIVI:

    Chenge and Co. should be serving their TIME in prison at this very moment.

    OR

    Chenge and Co. they should be serving their time in prison at this very moment.

    KUTOMIKIA KIFUNGO WANASEMA TIME IN PRISON, UKISEMA LIFE NI KIFUNGO CHA MAISHA.

    ReplyDelete
  18. Yaani kafungwa muda wote huo kwa ajili ya shs. 100,000/-! Laki moja!Ameonewa huyo. Waliomfanya mbaya watapata chao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...