WAFANYAKAZI WANNE WA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) LEO WAMETINGA MAHAKAMANI KUJIBU MASHTAKA YANAYOHUSIANA NA WIZI WA PESA ZA EPA WA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 207 MALI YA BOT.
WAFANYAKAZI HAO WALIOSIMAMA KIZIMBANI NI PAMOJA NA:
1. KAIMU MKURUGENZI WA IDARA YA MADAI BI. ESTHER KOMU.
2. KAIMU KATI BU WA BENKI BW. BOSCO KIMELA
3. IMANI MWAKYOSA
4. SOPHIA JOSEPH
WOTE WAMEFIKA MBELE YA HAKIMU MKAZI WA MAHAKAMA YA KISUTU MH. HEZRON MWANKENJA. HABARI KAMILI BAAADAYE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. watatajana tu nani alikuwekea pesa nani kakupa huu mchongo nahakimu bwana atutaki longolongo hawa watu wametutesa kweli lazima wapewe adhabu kadili sheria inavyo sema nakama mtu ameonewa pia apewe haki yake.

    ReplyDelete
  2. duu nina mjomba wangu pale bot wasije wakampeleka na yeye

    ReplyDelete
  3. MBONA TENA SH. 207 BILLIONI? SIYO 133 Bilioni? KAKA MICHU HIYO IMEKAAJE?

    ReplyDelete
  4. Hao sidhani kama wanahusika, Inawezekana tunapigwa changa la macho tu

    Kalagha bao

    ReplyDelete
  5. hii cheni ni ndefu sana wameamua kuanzia chini mpaka atapatikana aliyechota mabilioni yote hayo

    ReplyDelete
  6. Wa Tz vichwa maji!

    kabla ya hao mafisadi kuletwa kila kona ohoooooo JK kaamua kuwaachia..

    sasa wameletwa ohooooo sio wao!

    Pelekeni basi majina ya hao mafisadi!

    otherwise, weka plasta kwenye midomo kwani mnavunja nguvu kwa siye tunaofanya kazi ngumu ya kufuatilia nyengo zao.

    wengi wanaletwa siku za usoni

    ReplyDelete
  7. Dunia ndivyo ilivyo wapendwa.wapiganapo mafahari ziumiazo ni nyasi na Siku zote hakuna kafara bila kondoo wa machinjo.Poleni kama hamkuhusika Mungu atawasaidia. Lakini kama ndio wachongaji wakuu "you receive what you deserve".Hata kama watayeyusha baadaye wawaachie, hiyo ya kuumbuliwa mahakamani inatosha

    ReplyDelete
  8. hivi kweli kama hao wangeiba hizo hela wangekua hapo? wenyewe walio iba wamesha honga wanakula kuku saa hizi.kweli mtu mwenye mamilioni yupo hivyo? tunapigwa changa ya macho tu hapa. no justice.

    ReplyDelete
  9. Walohusika hasa hawatapandishwa mahakamani maana serikali inajua ikiwapandisha watatajwa wengi wenye madaraka. hao ni wanyonge tu tunazibwa macho.

    ReplyDelete
  10. Hawa wote ni mashahidi tu watuhumiwa halisi, mafisadi bado wanakula kuku. Hawa walitumiwa kama daraja tunataka wale waliochota (ninaimani hawa wa BOT watawaja waliowaambia kutoa hela na kuonesha vimemo walivyopewa).

    ReplyDelete
  11. ebwana eeeh bilion 207 si mchezo

    ReplyDelete
  12. Waosha vinywa mnapigwa la macho lingine. Hawa wakirudisha kidogo goma linaisha.... dawa ni kurudisha na kufilisi kabisa. Wadau mpo?

    ReplyDelete
  13. Wabongo bwana!!! sasa kama mnasema hawa hawakuhusika ni nani kahusika? au wewe unaesema hawa hawahusiki? Acheni sheria ichukue mkondo wake, kama hawakuhusika mahakama zitawaachia. Hawa ni watu wabaya sana kwani wakati watanzania wanataabika kwa matatizo wao wankula raha kwa pesa za umma. Huu ni mwanzo mzuri, tunataka Slaa kama ana mabomo mengine alipue

    ReplyDelete
  14. Mbona kila siku BOT wanakamatwa kondoo wa kafara tu?

    Kwa kweli inasikitisha kwa wadau wa blog hii kufurahia dagaa wakikamatwa wakati mapapa wenyewe bado wanatanua mtaani.

    Naomba kwa anayejua namna ya kujiandikisha kutoa ushahidi anisaidie hapa bloguni.

    ReplyDelete
  15. Bongo kweli nchi ya kisanini...watu fulani wanajichukulia madaraka mkononi na kupora uchumi wa nchi na watu wake na kuacha nchi kwenye madeni ambayo tutalipa mpaka vizazi viwili vipite ...mie siwezi kupata majibu katika maswali yafuatayo:-
    1. mkaguzi wa maesabu ya fedha za serikali alikuwa wapi.???
    2.Azina (treasure) ili kuwa likizo kwa muda gani mpaka watu wakaiba fedha zote bila kugundua..????
    3.Gavana mkuu alikuwa IC (intensive care) basi kaimu wake alikuwa wapi...?
    4.waziri wa fedha.....???? naona niishia hapa maana list inaweza kuendelea bila mwisho---- (kwa maana pesa inayo tajwa hapa kwa nchi kama Tanzania ni hela nyingi sana kiasi kwamba wizara fedha ingeweza kushutuka mapema hata kuathiri bajeti ya nchi.. mie kwanza siwezi kuamini kama kitu hiki kinawezekano kwa nchi maskini kama Tanzania..hii deal ina mizizi mirefu hawa watu ninaowaona hapa ni misheni tauni(wamekuwa chambo tu) deal zina wazee wenyewe , kwasababu kuchukua pesa kiasi kama hiki bongo lazima upite ngazi elfu mia moja...(urasimu), sasa ilikuwaje watu wakawa wanajichotea pesa bila udhibitisho na confirmation from authorised figures hapa ndugu zangu watanzania kama kawaida yetu kichwa cha mwendawazimu kila mtu ujifunzia kunyoa..hapa jamani hii issue ni kiini macho.
    Hizi billion billion zilizoandikwa humu ukichanganya zinakaribia hela aliyotuahidi W.Bush wakati wa ziara yake bongo na majority ya watanzania walikuwa na matumaini kwamba fedha hizo tukizipata zitasaidia sana nchi yetu kumbe misaada tunayopewa na wazungu kwa kutuonea huruma kwa umasikini tulio nao ili kusaidia 42millions of Tanzanians,single group of people so called wazee wa EPA wanagawiana watu 40 ,matokeo yake ni kama ifuatavyo:- muhimbili watu wana lala chini... umeme wa mgao...,shule hazina madawati...., nchi haina maji..., nchi haina usafiri..., barabara zinabadilika kuwa vichochoro..., Dar usiku mji mzima giza...,majority ya wabongo wanakula mlo mmoja...,matatizo haya unaweza kutunga kitabu.. halafu eti tunawaomba watuhumiwa warudishe hela as if tuliwapoka kwa mashariti fulani jamani kama siyo usanii ni nini..?mie ninawaonea huruma wabongo mlioko nyumbani ambao maisha yao hayausiani kabisa na maisha ya ki -EPA-EPA watu wanateseka sana ukizingatia hali ya kiuchumi sasa hivi duniani maana maisha yetu Africa yanategemea sana overseas economy na vimsaada vyetu tunavyo pewa vinaliwa na wachache hali nyumbani itakuwa ngumu- ngumu sana haya mambo siyo ya kujadili hivi hivi kama mchapo ni issue mzito sana ambayo inamgusu kila mmoja wetu doesnt matter we are in europe or america but our relatives ,brothers and sisters they are suffering and will suffering so much if this problem will not be considered as tragedy for Tanzanian people.
    MTU KWAO.....

    ReplyDelete
  16. Mimi nadhani hakuna mabadiliko yeyote yatakao tokea hawa wezi wa EPA kukamatwa na hata kufungwa tuangalie adui mkubwa ni nini na ni nini kinatugusa zaidi?

    EPA haikua fedha za serikali so hizo hela labda zinge kua a\bado zipo zipo tuu, Angalau Kina Johnson waliziiba na kuzi Invest na kutengeneza ajira kiaina fulani.
    Adui mkubwa ni nani? .Adui mkubwa ni rushwa na wizi wa pesa za TAx pamoja na matumizi mabaya ya pesa za Umma, jamani je ingekuwa Tanzania bila kuombwa kitu kidogo wakati unapata huduma ospitali ,Wizara ya Ardhi au tunapo omba sponseship kwa hawa marketing manegers wa hizi kampuni , je tungekuwaje?

    ReplyDelete
  17. Tunataka kuona mawaziri wahusika pia

    ReplyDelete
  18. WaTanzania ni watu wa ovyo sana,sasa hao watu wamekamatwa na kufikishwa mahakamani,wanasema sio,oho mara changa la moto.Semeni basi ni wakina nani hao vigogo,na msikalie kuongea ongea tu.Ni ngumu sana kudeal na wabongo kutokana na kupenda kwao kuongea ongea pasipo kuwa na ushahidi unaosupport hoja zao.

    ReplyDelete
  19. Anon wa Nov 08 3.29 AM nakuunga mkono kwa sana tu. Mi naboreka sana na hayo mambo ya ' oh changa la macho', mara oh 'kondoo wa kafara'sasa basi leteni hao ng'ombe wachinjwe kama mnawajuwa ili kondoo wasitolewe kafara! Mi ninachoamini ni kuwa kwa kipindi cha mwaka mzima kamati teule ilifanya kazi ya kuchunguza na kuhoji. Na naamini hao watu waliitwa wakahojiwa wakatakiwa kurejesha lakini kwa maoni yangu waliona kuwa warejeshe pesa wasirejeshe kesi itawakabili tu wakachaguwa kusubiri kesi! Mbona hatujaelezwa kuwa watuhumiwa walikuwa wakipiga kelele Mahakamani kuwa hawahusiki? Ndani ya mioyo yao na mbele ya Mungu wao wenyewe wanajua walihusika vipi!Sasa tuache wakajibabaduwe wenyewe huko Mahakamani kwa nini tunawasemea? Kama tunaona hawahusiki basi si tuwataje wanaohusika? Naamini kila siku wataongezeka tu wengine na pengine tutashangazwa sana na watakaoendelea kuletwa!Wale tuwadhaniao pengine sio! Mbona wapo wengine wamejijengea heshima kubwa tu katika jamii, na si lazima kuwa serikalini,lakini ukifuatilia walikotokea ndo huko huko kwenye wizi na ufilisi wa Mabenki?

    ReplyDelete
  20. anatakiwa hapa Apson, shehe Nkapa na RA

    ReplyDelete
  21. EPA NI FEDHA YA SERIKALI,SI YA SERIKALI??NI NINI ASA NAULIZA
    MANA WAZIRI MKULLO SIKUMUELEWA KBS SO IS BUNGE ZIMA SIKU ILE.

    ReplyDelete
  22. WANANCHI WANALIA SHIDA KILA SIKU KUMBE PESA ZIPO MMEZIWEKA MAKABATINI KAMA VYOMBO VILE SASA HAO WALIOZIBEBA WAACHENI TU WAZIBEBE WAMEONA LABDA HAZINA KAZI NA WAO WANASHIDA NAZO.....

    ReplyDelete
  23. Hawa kwa kuwaangali inaonekana zile paper zilipitia kwao wakaambiwa waweke saini halafu wakapewa Prado. Wahusika wenyewe tumeambiwa walirudisha hela na hawatajwi

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 12, 2009

    hayo ndio matatizo ya kuwachagua maskini wenye njaa kuongoza nchi na kutegemea watatulindia pesa,hiyo haitatokea, Kama una njaa karibia kufa utakula chakula ulochoambiwa ulinde sio Kwa hiari yako.labda ktk nyadhifa fulani tungechecki assets na bank statements za watu badala ya kusikiliza politics zao.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 24, 2009

    nadhani kwa wenzetu nchi zilizoendelea kama mbunge akikutwa na kashifa au kuwekwa lumande harusiwi tena kurudi bungeni/inabidi ajiuhuzuru kwa manufaa ya umma.naomba mlifikilia hilo swarakwa undani.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 12, 2009

    wabongo tko nyuma kwa kusema ukweli,hao watu walianzajeanzaje kuiba?hebu tuamke majameni coz tumelala fofofo

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 15, 2009

    katika kuweka mikataba/sheria ya nchi zilizo wanachama wa afrika mashariki,ndugu watanzania wenzangu naomba chonde mkataba wa ardhi ubakie kwa watanzania [wazawa]msitoe ardhi kwa wageni .

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 16, 2009

    hi tanzania ni nchi kwa maana nyingine tunaweza kusema ndiyo makao makuu ya nchi zinazotunguka/ kwani iko katikati ya jirani zetu. La kushangaza linapokuja katika mambo ya biashara/bandarini nashindwa kuelewa ni namna gani kampuni moja kukidhi matakwa ya bandari nzima? hata nchi za ulaya kila bandari kuna makampuni zaidi ya moja yanayoshughulikia mizigo mbalimbali ili kurahisisha na kuondoa usumbufu kwa wateja wake naomba serikali ilitolee macho hilo.ziwepo hata kampuni mbili ama tatu si mbaya zigawane vitengo.

    ReplyDelete
  29. Richard from S.AJuly 02, 2009

    Veri sad, esp for the country like Tanzania, veri poor country that really need help, look at the roads!! traffics jams!!! everything is just messed up and these few people eating mani like no one bsness, they have 2 pay 4 it so let them suffer the consiquence......

    ReplyDelete
  30. Hongera chuo kikuu MZUMBE ambacho kimeundwa na kampasi tatu,yaani morogoro,mbeya na dar es salaam campus.

    mimi ni mwajiri kwenye shirika flani lisilo la kiserekali, mwaka jana tulimwajiri graduate mmoja katika fani ya sheria kutoka chuo kikuu mzumbe kiukweli yoko competent na organization nzima tumeapriciate kua chuo kikuu mzumbe huenda huko baadae kikateka soko la Tanzania na Afrika mashariki ukikompare na vyou vingine.

    ReplyDelete
  31. Mimi kwa sasa sidanganyiki nchi hii watu wamezoe sana kula mali za umma waziri anaapishwa anakula kiapo lakini muda mchache tu anakiuka kiapo chote nadhani tuanze wenyewe kwa vitendo tuache maneno baba ukiwa mlevi hupelekea na mtoto pia akafuata nyendo zako nchi hii watumishi wa umma wengi wezi hawatosheki na kidogo au ndio waliokua nacho wataongezewa na wasio nacho hata kidogo watanyanganywa? wizi umekithili sana serikalini mpaka watu wamechakachua hazina ya taifa hata kama EPA si za serikali kwanini waibe ? si bora mngesaidia hizo pesa kama hazikua na mwenyewe kuleta maendeleo mikoa ambayo imesahaulika katika nchi hii ambayo imechangia asilimia kubwa harakati za Uhuru kama Tabora,Kigoma,Tanga nakadhalika tutafika kweli Tanzania Bila uzalendo hatutofika safari yetu...............

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 04, 2011

    HICHO KIINI MACHO 2,COZ WALAJI SO HAO 2 WAPO KIBAO..... SO UCFALIJIKE SAANA KUONA WANAPELEKWA HUKO

    ReplyDelete
  33. Ngoja kwanza, yesu na Maria, bilioni 207..uuwi..kimahesabu ya haraka haraka ni pound £53000000,na bado mgao wa umeme kama kawa, na ni wasomi wa hali ya juu....kama ni wa kwetu lazima tungeona mabadiliko flani fulani lakini sio.nchi kama Korea hao ni hukumu ya kifo tuu...

    ReplyDelete
  34. wanablogu wengine bhana kama hamjui mambo vile, pia mi naona kama inatokea hamjui hebu tuwaache wanao jua waendelee kusema kweli. katika hali halisi sioni umuhimu wa baadhi ya watu kushikilia bango eti watajwa ndio wahusika na hakuna mwingine kwasababu hao jamaa zetu (kondoo) hawajapiga kelele mahakamani!!!! aaaa...haaaa!! hata kama jujaenda tution utaelewa tuu michongo hii ya kiujafanja bhana, Bushoke kaasema "jiulize kwanini walio wengi magerezani wengiwao ni masikini" aaaah pia nasisitiza watajwa ni kondoo ama sisimizi khabisaaa ila tembo wananeemeka mijini. mfano mdogo tuu, jeuri ya chenge baada ya kumuua mtu kwa kigari chake (pick up), lkn alidunda kitaa na kesi imeisha kwa chenge kutoa sijui tuite vijisumuni au vitugani, cozi yule mzee mabilioni anayaitaga VIJISENTI, so ndo kama ivyo bhana watu tunaweza jaza mabook na mabook na bado tusimalize, hapa bongo wanofaidi matunda ya nchi na wachache ila ipo siku kitanuka mbaya.tunasema ivii "Fool me once, shame on you, Fool me twice", shame on me! If you are not part of the cure, then you are part of the problem. try to be curing busiiiiiiiiiiii.......

    ReplyDelete
  35. Siamini iwapo kuna kesi ya kweli kisheria hapa zaidi ni kuwaridhisha wafadhili wetu hasa wale wenye 'kidomodomo sana' kama nchi za Scandinavian ili waone tuwajibika kushughulikia swala husika. Namsikitikia schoomate wangu Farijalla na nduguye Maranda waliopigiliwa misumari ya kwenye miti ili kuwa kafara. Eti kuna watu wanaitwa mboni ya jicho la watawala hao waliuhusika na bado tumeona wakipigiwa kelele tu za mwizi bila hatua za kisheria kuchukua mkondo dhidi yao. Hawajaishia hapo bado wakageukia na Richmond na baadaye Dowans hao mbona hawawajibishwi? Hao wafanyakazi watabaki wahanga au ni namna ileile ya kuzuga tuonekane walau tumewawajibisha baadhi yao wafadhiri wafurahi. Kama Rost Tamu na wengine vinara hawatapelekwa mbele ya sheria basi yote ni ubatili mtupu hapo hakuna kesi ni geresha tupu. Au basi kweli hao wengine ni mboni ya jicho la watawala kama watu wasemavyo ndio maana hawaguswi wao ni wamenenewa kula migongoni mwa walalahoi watz. Yana mwisho neema ya Mungu itaamua muda si mrefu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...