Nimeikuta hii katika yahoogroup moja Katika hali ya kukumbushana tulipotoka nikaona ni vyema kuiweka hapa uwanjani wadau watupe kumbukumbu zao enzi hizo:
Binafsi wadau wamenikumbusha sana mambo mbalimbali kama ifuatavyo; yale mambo ya kuwahi namba asubuhi, kubeba kidumu cha maji, ufagio, mbolea wakati mwingine.
Ukija darasani ndio usiseme zile hadithi za"Musa, Neema na Baraka""Juma na Rosa""Kibanga ampiga mkoloni""Siku ya gulio Katerero""Mtakuja Village""Andunje Mtoto Mdadisi""Nganenepa Ang`atwa na Nyoka""Lindu amuokoa Kapilima"

Mashairi kama;"sizitaki mbichi hizi""Sadiki na Fikiri"
Nakumbuka pia enzi zile siku mwalimu akiwa mgonjwa tunafurahia kwani siku hiyo tutakuwa na muda mwingi zaidi wa kuchezaPia ile michezo ya baada ya kutoka shule kama,Mechi za mpira kati watoto wa mtaa mmoja na mwingine,Kwenda kuwinda ndege na manati, urimbo,Kutafuta matunda Kuogelea, Kombolela, mchezo wa baba na mama..
Daahh..!!! sio siri it was a very wonderful moment in a life time. watoto wa siku hizi wanakosa mambo mengi sana.Manake siku hizi ni mwendo wa tuition tu tangu mtoto akiwa primary mtoto anashida na vitabu tu na kupigania daladala siku nzima.
Mdau wewe unakumbuka nini enzi za primary….!!!????
Mdau wa Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 54 mpaka sasa

  1. Yaani hapo mdau umenikumbusha mbali sana,almost vitu vingi umeviweka ambavyo watu wengi enzi hizo tumepitia,ila kitu kimoja nilikuwa sikipendi,'fimbo'....dah yaani yaani ukichelewa namba tu unatandwika fimbo kama punda,halafu adhabu za pushap na kichurachura,si unajua viranja wanavyokuwa na nyodo,hizo adhabu zilikuwa kero kishenzi,kundi lingine ni la wale masela gogo,yaani wao sifa yao wanabonda shule nzima,hadi kaka mkuu wanambonda,ukikohoa kidogo wanakupiga,madem ni wao kila kitu wao,nilikuwa siwapendi,hasa ukicheki nilikuwa chalii tu class,kuchezea magari ya udongo,ule mchezo wa 'tule tumuachie baba', 'yai bovu yai bovu'.....na kile kipindi cha maandalizi ya mahafari...yaani FULL ENJOYMENT,IZ FANTASTIC MOMENT, NI TAMBARARE TU MDAU.....NAWAKILISHA.

    ReplyDelete
  2. Ebwanaeee huyu mdau wa Dodoma kanikumbusha mambo mengi sana kuhusu enzi za shule, maana sijapata kufurahia maisha tena kama wakati huo.

    Hivyo vitabu na Hadithi zake hasa Kipanga ampiga mkoloni ilitupa hamasa na kuwachukia wakoloni enzi hizo mandela bado mfungwa, Namibia bado na msumbiji inasumbuana na RENAMO kwa ufadhili wa makaburu.

    Nakumbuka nilianzisha vagi la nguvu baada ya kuitwa Andunje maana sio siri nilikuwa mfupi lakini bright. Asante mkuu umeongeza furaha yangu huku ughaibuni kila mtu kanuna yuko biza

    Mdau Mgungu Jr. OSLO NORWAY

    ReplyDelete
  3. KWELI HII NI BLOGI YA JAMII MAANA KWA HARAHARAKA TU NAONA MDAU HUPUNGUI OPERATION NIDHAMU. NGOJA NI KUPIGIE BJUGLA HIIIP HIP HIIIP.

    ReplyDelete
  4. Mdau naona umetoa yote. ila umesahau kupigana, hizi ngumi huwa ni nyingi sana kati ya watoto wa primary hasa enzi hizo, halafu kunakuibiana madaftari na pencil, ukaguzi wa usafi shuleni kila siku ya Alhamisi, Je unamkumbuka mwalimu wa hesabu darasa la pili mambo ya hesabu za mara. Akiingia tu darasani anaanza 2x2, 6x7!!!! Na je unakumbuka table ya 6, 7, 8 na ya 9 ndio zinasumbua zaidi wanafunzi?. Je unakumbuka ni viatu gani ulikuwa unavaa shuleni?? haha kama sio matairi ya gari???? na zile nyimbo za darasa la kwanza? a e i o u!!!!. Mengine nawaachia wadau wamalizie.

    Na Cyperus rotundus, Iguguno.

    ReplyDelete
  5. unanikukumbusha mlimwa primary school, Mdau wa area C. Finland

    ReplyDelete
  6. hee umesahau wanted siku ya kufunga shule. umemkosea gangwe basi siku ya kufunga shule anza mapema!!thanks for reminding us those golden days.

    ReplyDelete
  7. thanks for reminding us of those golden days!!umesahau wanted? siku ya kufunga shule!

    ReplyDelete
  8. umenikumbusha mbali mdau,mimi nakumbuka ngumi siku ya kufunga shule kama uligombana na mtu,,unajifikiria kurudi nyumbani.

    ReplyDelete
  9. Mdau wa dodoma umesahau Shairi la "KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".

    Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
    kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
    watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
    wakataka na kauli, iwafae maishani.

    Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
    hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
    roho naona yachinjwa, kifo kina nikabili,
    kama mnataka mali, mtayapata shambani.

    Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
    baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
    akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
    kama tunataka mali, tutapataje shambani?

    Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
    fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali, haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
    kama mnataka mali mtayapata shambani.

    Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
    mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
    na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
    kama mnataka mali, tutayapata shambani.

    Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
    mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
    wote wakashangilia, usemi wakakubali,
    "KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".

    ReplyDelete
  10. hahaha jaamni mmenivunja mbavu mie loo dodoma oyee .Ngoja niongezee mmesahahu kuaka chini bila madawadi? au wale watotow a vibosire moja wapo mie tunatengenezewa madawati unachagua rafiki w akukaka naye LOL hahahahahahaha love those time sasa sijui life ikoje loo

    ReplyDelete
  11. Mimi shule nnamiss "uchokozi" kuchokoza wakubwa kisha kukimbia, nkikamatwa napigwa mtama au konzi, akinipa kisogo tu, mchezo ule ule! raha kweli!
    Pia nakumbuka, siku nikichelewa kuwahi dawati, najifanya mnyonge/ mgonjwa, kisha wavulana (ambao wanawahi asilimia kubwa ya madawati darasani) wananipa viti vyao nikalie! nilikuwa tapeli si haba!!

    ReplyDelete
  12. Mimi nilisomea Arusha mjini duh kumbe wababe walikua kila kona......nimecheka sanaaaa tu .......I hope kungekua na maury show tuwaite hawa wababe waje kuappologize. Namkumbuka Babu wa kale alikua anaogopwa sana tu enzi za kaka zangu halafu sijui ni mdogo wake huyu alikua enzi zetu alikua anaitwa exsupey. Alikua na kundi lake hilo!!!!!!!!

    Siku moja Jumamosi kuna waliomwana mwalimu wa kiume ambaye alikua ndio mwanamme mwalimu kila mtu anataka kuwa kama yeye... anafukuzwa na hawa watu basi ikaleek jumatatu...mwalimu bachubira kakimbizwa mtoni.....teh teh etehe

    Lumbukumbu zangu

    Siku ya kupeleka majembe shuleni na
    maslasher

    kufagia uwanja asubuhi na wale viranja mweeeeee.

    kumwagilia maji maua

    Chipukizi kucheza gwaride

    Sanaa kutengeneza visu vya mbao na kufinyanga udongo na kutengeneza vyungu

    Kwenye kuandaa sherehe za graduation wasichana kupeleka visu. Inabidi uibe kisu nyumbani manake mama alikua hataki na ukienda shule bila kisu ni viboko

    Those were the days

    ReplyDelete
  13. yaani mdau umenikumbusha mbali sana
    siku ya gulio katerero ,but mimi nakumbuka sana Manenge na Mandawa
    na kitu kingine nikukumbushe mdau kuhusu walimu wanaleta biashara zao then wanawataka mkope

    ReplyDelete
  14. Ninae ndege mzuri mrembo wa kupendeza, rangi zake mashuhuri ni nne nawaeleza. Ndege huyo ndege gani hapa kwetu Tanzania? Halafu sitosahau kichangani, kabla ndondi tunaanza na puta mchanga, tia dole enzi hizo c mchezo.

    ReplyDelete
  15. Dah, ebwanaee hii kali, mbali kinoma wazee. TVZ Kicartoon ahsant kwa "Mtayapata Shambani", noma. Mi nakumbuka tukitoka shule pale mwongozo mkwajuni tunaingia garden kwa mzee mkude kula mihogo, enzi hizo muhogo sh 1 kipande, mkiwa wengi mkichanga noma mihogo kibao na pilipili yake ya unga, dah!!! Madumu, mifagio, mbolea noma!

    Jamani wadau nikumbusheni wimbo wa aeiou!

    hii ndio a,aaa aaa aaa,
    ina mkia mfupi aaa aaa aaa

    hii ndio e, eee eee eee
    iko kama embe eee eee eee

    hii ndio i, iii iii iii
    (hapa sikumbuki)

    malizieni wadauuuuuu!!!

    ReplyDelete
  16. tiari bado,,, bado! Hapo kwa kweli ndiyo tulijifunzia ngono enzi zetu. Jinsi tulivyokuwa tukikandamizana na vitoto vya kike, sijui shetani yule alitoka wapi! Wanaosema watoto wa siku hizi wameharibika, nawashangaaga tu. Sisi wakate ule kulikuwa hakuna video wala porn magazini. lakini ma-style yote kwenye... tiari bado,, bado!

    ReplyDelete
  17. Anybody from Amani primary school dodoma enzi zileee za mwalimu Mwaluko mwenye ki-sumni nawapa Hi!

    ReplyDelete
  18. UMENIKUMBUSHA MBALI SAAANA. KILA ULICHOSEMA NILIFANYA,NINACHOSHANGAA NI KWAMBA WALA SIKWENDA TWISHENI KAMA WATOTO WA LEO LAKINI AKA, NAKULA KUKU TU NCHI ZA WATU.

    ReplyDelete
  19. Kwa wale tuliosoma Dodoma Mlimani enzi hizo mwalimu anakukopesha ubuyu, kashata, ufuta, vitumbua nk ... na kesho yake akiingia darasani kabla hajaanza kufundisha anatoa karatasi yake yenye majina ya waliokopa jana yake....ole wako uwe hujaleta hela yake itakuwa ni zamu yako kuuza biashara zake siku hiyo:( .... Mwalimu akiingia kuita majina darasani kama alisahau jana kuita majina inabidi uitikie "Jana na leo Mwalimu" Siku treni ya abiria imekuja karibu nusu ya wanafunzi darasani watakuwa ni wagonjwa kwani hiyo ndio siku ya kutengeneza hela!! Siku ya kufunga shule inabidi utembee ukiangalia pande zote bila hivyo utashtukia ngumi mgongoni na huyo alikupiga yuko mbio sana huwezi kumpata:) Bado maisha yalikuwa raha hasa nikikumbuka mpira wa soksi au wa kufuma kwa manila...hahaha!!!

    ReplyDelete
  20. Kwakweli wengine mmetupeleka mwaka 47! Tvz Kicartoon hicho kitabu unacho au shairi bado unalo kichwani mpaka leo?Hongera kwa hakika umelipatia kabisa! Mimi labda ni wa zamani zaidi. Pamoja na yaliyoelezwa na mdau wa Dodoma wale wenzangu na mimi watakumbuka wakati huo wanafunzi wengi vijijini walikuwa wanatoka mbali na shule na hakukuwa na usafiri zaidi ya miguu. Ninachokumbuka ni kuwa wanafunzi walikuwa wanakuja na mahindi makavu yaliyochemshwa usiku mzima ambayo hayako katika magunzi yake. Yanawekwa chumvi kidogo na kisha huwekwa kwenye chupa za orange squash (walizoziokota jalalani) wakichanganya na maji kwa ajili ya kukata kiu baada ya kula wakati wa 'break'! Aidha, tulisoma mambo ya Taa na saa, pete pete pete, Omari Hodari kaenda safari yoho!Kakakanzi na Bibikuku n.k Kulikuwa na kisa pia nilichokipenda katika moja ya vitabu hivyo ambacho mpaka leo huwa nakitumia: Mgeni siku ya kwanza, mpe mchele na panza, mtilie kifuuni mkaribishe mgeni; ...Mgeni siku ya pili mpe wali na samli...Mgeni siku ya nne mpe jembe akalime akirudi... Mgeni siku ya sita mkila mnajificha...Mgeni siku ya kenda (tisa) enenda bwana enenda usirudi mgeni usirudi mgeni; mgeni siku ya kumi, kwa mateke na magumi...! Pamoja na michezo iliyoelezwa na wadau wengi mimi nilikuwa napenda sana mchezo wa kujificha; tulikuwa tunawashwa na majani lakini wapi, hatuachi; na tulikuwa na mchezo wa kubaka panzi na vipepeo! Tulikuwa tukiwapata tunachimba kishimo kidogo tunawaweka na kufunika kioo (Glass) kisha tunaangalia ndondi (tulikuwa tunaita sinema)!Hata enzi zetu tulikuwa pia na watoto watukutu; Enzi hizo hatukuwa tunavaa viatu wala nguo za ndani (Chupi)shuleni kwahiyo wale watoto watukutu hasa wavulana walikuwa wanatembea na vipande vya vioo ukisimama bila kujua wanakunyatia kwa nyuma na kuweka kioo chini kati ya miguu; Kuona sinema!
    Siku nyingine naomba wale waliopitia Jeshi la Kujenga Taifa tukumbushane mambo ya huko na wale wasiopitia angalau wapate picha! Mpaka sasa binafsi naamini wasiopitia JKT wamekosa 'adventure' ambayo hawatakaa waipate maishani!

    ReplyDelete
  21. MDAU HIZO NDIO TOFAUTI ZINAZOTENGANISHA VIZAZI (GENERATION) KIMOJA MPAKA KINGINE. KWAMFANO UKIMWULIZA BABA YAKO AU BABU YAKO ALIFANYA NINI SHULE ENZI HIZO WAKATI WA MKOLONI BASI UTAPATA MAJAWABU TOFAUTI KABISA. SASA KAMA ULIVYOONA WATOTO WAKO SASA HIVI NI VITABU NA TUISHENI NA DALA2, JARIBU KUFIKIRIA VITUKUU VYAKO VITAFANYA NINI???? TEKELINALOTUJIA LIKIINGIA KWENYE FOMULA PAHI AU MLINGANO BASI KILA KITU KITAKUWA NI KUPAGANYIKA TU NA. MAISHA HAYA NI MCHUCHUMIO TU

    ReplyDelete
  22. Mmj jamani kweli tumetoka mbali..kinachonishangaza sijui ndio ile ideology ya ujamaa na kujitegemea! Yaani hayo matukio yalikuwa yanatokea shule karibu zote bila kujali shule zilipo. Binafsi, nilisoma shule ya misheni ya wasichana watupu, lakini hivyo 'vidume - vibabe' vilikuwepo bwana! Darasa lililokuwa mbele yetu, hivyo vidume vilitusumbua kweli, yaani hata share yako ya mkate unampa tu kiulainii...na hapo tuko primary siyo hata sekondari kusema watu wameshajifunza ubabe...Leo hii nikiwatazama hao wababe wangu nabaki kucheka peke yangu, na kujiuliza hivi kweli wanakumbuka walivyotusumbua wenzao?

    Wadau, you made my day..yaani nimecheka sana...

    ReplyDelete
  23. Yaani kweli mdau umenikumbusha mbaali ile kishenzi! yote uliyoandika hapo tumeyapitia, na hasa hilo la kutovaa chupi yaani maisha bwana! naimagine sasa hivi inawezekana kweli kutembea bila chupi??? kweli maisha ni ya ajabu sana hasa ukikumbuka about the past ambapo mambo mengi tuliyofanya hapo zamani kwa sasa ni impossibilities!!!

    ReplyDelete
  24. kaka mimi nilikuwa busy nikawa sijaperuzi blogu ya jamii kama siku 2 hv kumbe kuna vitu vya home kabisa?

    binafsi umenikumbusha mabali sana mimi nilisoma kizota primary pale dodoma umenikumbusha mwalimu wangu 1 mwalimu simba akitufundisha somo la muziki darasa la 4.

    kabla ya kwenda mstarini(paredi)tulikuw atunakimbia mchakamchaka tukimba
    mchaka mchaka chinjaaa
    hadi mselama hadija
    mchaka mchaka chijaaa
    hadi mselema hadija

    jua lile literemke mamama
    haiyaiya literemke mamaa

    kulikuwa na methali bwana mfano unaambiwa ganda la muwa la jana?

    mnakumbuka magazitujo?
    ma-mabano
    ga-gawanya
    zi-zidisha
    ju-jumlisha
    to-toa

    mnakumbuka mamoja,makumi,mamia na makumi elfu?kulikuw an somo la sanaa,sayansi kimu,daaa

    mithupu umenikumbusha mbaliiii saaaaaa kizota primary school dodomaaa-
    titusboniface@yahoo.com
    mdau -uk

    ReplyDelete
  25. mdau wa dodoma umenikumbusha mbali saaaaana ,nimecheka kufaaa yaani.kweli enzi hizo maisha yalikua raha..
    mnakumbuka siku ya ukaguzi wa usafi woote mmepanga mstari mmoja ulionyooka ili mwalimu na kiranja aweze kupita, sasa uwe hujasugua meno si unajua enzi hizo, wakati huo ndo unatumia shati au sketi yako au kijiti cha mfagio kusugua yale ya mbele tu amabyo mwalimu au kiranja atayaona,
    Pili kwenye ukaguzi huo huo si unakuja hujaoga wale wa vijini wenzangu si unajua unanawa tu miguu wakati mwingine unapaka mafuta au sabuni au hupaki sasa umepauka na soksi zako mpira ushalegea, mwalimu anapita na fimbo nyembamba baasi wewe ulopauka miguu utapewa za miguuni unaruka kisha unaambiwa songa mbele...
    Mankumbuka enzi hizo eti kaka mkuu au dada mkuu naye anachapa eti..
    Duuuhhh.you just made my day..
    Nawaunga mkono wadau wale wababe wengi wameishia hovyooo,wengi wao..
    Mnakumbuka pia kupiga mchanga au kuchora mstari kuhamasisha kupigana,mtu anafuta msitari wake na wako kukuonehs ubabe... au anapiga michanga yote miwili huku akisema amepiga maziwa ya mama yako nawe kwa hasira unaamua kuanza ugomviii...
    na ngumi hazianzi ghafla hapana..inaanza ile moja moja na sio kutumia nguvu na kadri muda unavyokwenda kasi idadi na nguvu vinaongezeka..
    wadau nawakilisha..nimecheka saaaaaaaaaaaaaaaaana

    ReplyDelete
  26. Mi sina cha kusema maana yote mmemaliza,ila mi nakumbuka nyonya damu tunakimbia mpaka tunataka vunja miguu, pia shati la shule km halina lebo ni big issue, wale wa Mgulani pr school enzi za mwl mwailafu,masawe na Mwl charle fimbo za mpera mstarini balaa. Bila kitabu cha JIANDAE hesabu hazipandi.

    ReplyDelete
  27. duh ebwaana hee hii kali,

    kwa wale tuliosoma Mazimbu primary school morogoro mtakumbuka hizi,

    mnakumbuka enzi zile mwali kobelo mwanaume na mtindo wake wa nyuzi tisini, alafu mwalimu sombi na mgalula kutambishiana kuchapa,

    na hii hapa mwanangu ya kuleta michongoma na kukaa chini ya msufi tukisubiri kwenda shamba.

    alafu kipindi cha michezo ya umishunta mwanangu tulikuwa tunapigwa kila siku tu

    ni hayo tu

    ReplyDelete
  28. Jamani mimi kuna teacher mmoja nikiwa darasa la sita/saba pale mazoezi primary school 1988-1999 anaitwa Dodogoli sitasahau alinichapa sana viboko, yaani makalio yangu hadi yaliweka alama!!
    sijui kama bado yuko hai. Nilishamsamehe

    ReplyDelete
  29. Lo nimecheka sana, wale wa upanga primary nimekumbukua mwl. kisebego kama hujafanya home work unafinywa makwapa, huyu mwl alihamishwa kutoka bunge nadhani waliosoma bunge wanamkumbuka

    ReplyDelete
  30. wadau tumekumbushana mbali sana, wameshasema mengi sana wadau labda kuongezea tu mnakumbuka ile michezo ya kibaba-baba (ki-mama mama...???
    mdau mmoja kanikumbusha Dodoma Mlimani primary school karibu nusu ya wanafunzi walikuwa wanatoka kota za railway na polisi siku ya treni mahudhurio shuleni siku hiyo yanakuwa sio mazuri kabisa, wale mliosoma Amani,Mlimwa, Mlezi, mazengo, Chamwino, Uhuru, Makole, K`ndege, Ma- LY wa 1993,1994,1995 bila shaka mtakuwa mnawakumbuka Kina Isaka na Kikanya walisaidia sana wanafunzi kwenda sekondari.

    Mdau wa Dodoma Mlimani P/S 1988-1994.

    ReplyDelete
  31. ile ya "kuputa" mchanga kabla ya kupigana? dah chupi ilikuwa noma mwanangu,uvae ya nini? ila waliovaa walikuwa wanavaa za VIP, wanakuja kustuka zishafika tumboni hasa wakati wa mpira!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  32. BULICHEKA,UKUTI WA MNAZI,TUISHENI YETU CHUO,SOMO LA SIASA SIJASIKIA DUNIANI MTU UNASOMA SIASI DARASA LA TATU. SHAMBA AU BSTANI LA SHULE.CHANDIMU GOMBANIA GOO, DOBO KISI,THOSE WAS THE DAYS THAT WAS.
    MDAU AGALI.

    ReplyDelete
  33. wadau mmesahau enzi hizo utoro ulikuwa umeshamiri,na ilikuwa ndio sifa hujafika shule wiki.unajiona gangwe yaani wengine walikuwa wanasifika kwa kubana job(utoro)

    ReplyDelete
  34. yan km kuna siku nilocheka na kukunwa ndo leo hii mada dah!!
    jamen wale wa muhimbili pr school mwl Ndosi na Chuwa hesabu apa ndo ilikua balaaa,,yan bakora adi kuzimia,
    nywele sasa prifect anapitisha pen/penseli ole wako izame unakatwa nywele za mbele upara,sun-vita na chips watoto wa vibosile unaomba weee upewi,au watemea matee na kohozi usiombwe na bado mijaa waliomba teh teh,zamu ya usafi chooni ndo balaa prifect kasimama nje kashika kiuno kawapangia maeneo afu aja kugau mkishasafisha ole wako-me nilikua prifect yan ndo nachoshukuru darasa la 4 tu,la 1-3 monita au wale special madent hamguswi na mtu walimu wanawapendaaa yan ndo mfano wa shule.afu kibosile wapokelewa unapokuja shule wanakubebea begi na mzigo wowote uliokua nao,unawatuma weee canteen wakuletee vyakula afu ujira wake ni sh5 au unammegea sun-vita dah!!utumwa ule Mungu atusamee ila ilikua raha saaaaaaaana,unafutwa vumbi na wezako,ole wako mtu akukanyage unamchapa kibao live afu unawaambia darasa zima wamzomee jamaa aishia kulie weee na bado adhabu utampa tu,msatrini kuwai namba asubui yan namba ya 1-3 ilikua na watu special wale masupastaa/magenious wa darasa,ata akija gangwe lzm apishe pale mbele tena ukifika tu unasimama mbele yake au unajipanga pembeni wengine wooote wanaamia nyuma yako wabishi ina inabidi nao wafate tu hahahahaa
    ukifeli sasa maksi itangazwe darasani duh ilikua zinga la adhabu asa hisabati na english kesi.sasa wale wavulana mambo safi kwao wavokua wanaringa afu jamaa anatafuta "mchumba" kibinti genious au matawi,,mnafukuzana weee uku watu wanashangilia akukamate then zinga la busu,,,,hahaaa hii ilikua danger sana (jamaa mmoja ivi BRAYAN SITAMSAHAU KAMWE)yan apo ni std 1 adi 4 ivi malavi-davi nje nje, hatari.
    table ndo balaa std4,english sasa kichekesho watu walikua wanaugua ghafla wanapandisha mapepoz teh teh yan very few madenti ndo walikua wanasoma kile kitabu gani cjui nshavisahau.
    madawati sasa waliokaa ni watoto wa vibosile na magenious basi tena mnachagua nani ukae nae afu mnakaa wachacheee mnakaa ata 3 au 2 tu dawati la watu 4.
    siku ya mtihan anayewai kutoka ndo mwenye akili hahahaaaa,siku ya kufunga shule na kutoa washindi kila std mshindi wa 1 adi wa 3 unaitwa jina unapita mbele kwa makofi na kujidaiiiii wapewa zawadi yako compass,daftariz,peni nk ile ilituhamasisha sana kupiga buku sio siku izi ata upate ziro km kawa tu,siku ya kufungua shule mwazo wa mwaka mnavoringishiana vitu vipya uniform adi viatu;chachacha,lambada,skuna,mokas,raba za kupanda zile nk
    mwl wangu std 1 Swai na Mama Kahwa duh sitawasahau walinipenda saaana na upendeleo A,,
    wadau mnakumbuka daftari maalumu la kuandika HERUFI??unaambiwa andika w,a nk duh.
    tht life never comes again--nimemis mnoooo

    ReplyDelete
  35. Mi nakumbuka KUWEKA VIPANDE VYA MANYOYA YA TAUSI KATIKATI YA DAFTARI...kila siku unakatia maganda ya penseli(iliyochongwa na kichongeo)na pamba eti ili akue...kweli ule ulikuwa ujinga lol!

    ReplyDelete
  36. mdau wa muhimbili primary umenikumbusha mbali umesahau sanvita kwa baba taibali na maembe ng'ong'o kwa yule mzee kanteen. kipindi cha michezo tulikuwa tunakimbia uwanjani na mwl. kitutu.
    alafu jamani mnamkumbuka magambo!! anapita mtaani anauza karanga uku anaimba
    nakumbuka butua mtu unajivalisha nguo unajifanya kama mpita njia basi anayezinga anashangaa shangaa wewe unaenda unabutua unawaokoa wenzio hahaha duh! kweli tumetoka mbali

    ReplyDelete
  37. DAH MDAU UMENIKUMBUSHA MENGI SANA MIMI NILISOMEA MANYONI PRIMARY SCHOOL ENZI ZA 1990-1996 KINA MWALIMU MWANDULE ,GANSAO,MKOMBORA KWA STIKI NOMA PIA ALIKUWEPO MWALIMU PAULO,LECHIPYA HAWA NDO WALOKUWA WAPOLE KINOMA.
    DA MAMBO YA MWAGANO SIKU YA KUFUNGA SHULE PIA UBABE WA KUGOMBANISHANA NGUMI,KULIKUWA NAMIJITU MIBABE KINOMANOMA NA MITORO YA CLASS KAMA SIMBA JUMA SHAUGENI,OMARY MATEGE NA WENGINEO KIBAO,STD SEVEN MWANANGU ASBH MNAPIGA HESABU MCHANA MAARIFA JIONI LUGHA DAH SIKU MOJA KTK KUBADILISHANA KUSAHIHISHA JAMAA SIMBA JUMA SI AKABAMBWA WANAPENDELEANA KUPEANA TIKI DUH MSHIKAJI ALIPIGWA FIMBO NA MZIZIMA(TICHA-BIG) MPAKA AKAJAMBA KWA SAUTI CLASS,WATU MBAVU HATUNA.
    MAMBO YA KAMBI UMITASHUMTA USISEME FULL KUPATA MADEMU WA SKULL TOFAUTI,WALIKUWA WANANIACHA HOI MASELA WANAINGIA STD IV HAWAJUI KUSOMA NA PIA JAMAA AKIONA SIKU YA MATOKEO(KUFUNGA SKULI) HATII TIM AU ANAHUDHULIA MECHI YA A NA B HALAFU NDUKIII MBAYA.

    MDAU MZEE WA UK

    ReplyDelete
  38. Mmesahau ile imani ya kuwa ukiweka kijiti utosini kama umefanya kosa ticha anasahau?au ile ya wakati wa mazingaombwe kuwa ukila limao unaona kila uongo? au mmesahau ile ya kuvaa kaptura mbili ili fimbo zisiingie?
    Unakumbuka ile ya kuandikia madem vibarua unachana karatasi za katikati ya daftari?
    Hahaha I miss those days!
    Nilikuwa Ngara Primary School.Kuna ticha mmoja alikuwa anaitwa sebahene alikuwa anatupigisha gwaride hadi mtu azimie ndo tunaruhusiwa kwenda home.Kuna mwingine alikuwa anaitwa oswald rujuba style yake ilikuwa ni kulazimisha tuongee kiingereza.

    Alaf nilikuwa na mchumba darasani ilikuwa raha sana, nikichapwa mimi analia yeye ila tukishatoka darasani nikienda kumuongelesha ananichunia.

    OLD IS GOLD JAMANI.

    ReplyDelete
  39. Jamani mbona sijawasikia wanafunzi wa Uhuru Girls enzi hizo za ,Mrs Mahiga, Mrs Simkoko, Mrs Hiza Mama Mtawangu Mrs Mhundi ilikuwa ni mwisho. Kutoka hapo tukaenda kinondoni secondary enzi za Ngunangwa. Chindakta uko wapi, maana jamaa alikuwa na zali ya kupendwa ile baya.Bush Queen Kisarewe.

    ReplyDelete
  40. mm hii ni nzuri,lakini mmesahau"wagagagigikoko",kitabu hicho!hilo jina tu kulisoma ilikuwa shughuli,Mmenikumbusha gwarde la chipukizi!basi ukichaguliwa chipukizi unaona siiifa,Mnashinda uwanja wa taifa kutwa!Du mnawakumuka wale jamaa ambao walipewa ofa ya kwnda sekondari(form one)na mzee wetu Kawawa?kisa?waliongoza vizuri gwaride la chipukizi!Yule binti aliitwa doto.Haya mambo ya kushinda pugu road mnasubiri kumpokea kiongozi fulani?!jamani madenti wanaanguka na kuzimia kwa joto na kiu!Du hata hivyo nakumbuka nyimbo za chipukizi kama "sisi tunataka kuwasha mwenge"dah ile midundo ya bendi ya polisi,Halafu siku ya uhuru wa Msumbiji "Ife ana Frelimo sowona,tinapata ko masambiki!!"Wale wa Chan'gombe pr Dar mnamkumbuka Mwl Matanyanga?dah yule jamaa sijui alikuwa anakula nini,anachapa hachoki!mi alininyima hamu ya hesabu kabisaa.Somo la needle work lilikuwa safi limenifaa hadi leo,ila mazoezi tulikuwa tunafanyia kwenye nguo za mtoto wa Mwl Mabula,ambaye wakati huo alikuwa anasoma "kifungiloooo"Du huyu mtoto sijui yuko wapi siku hizi hata atupe asante ya mdomo tu.Kubanwa kwenye UDA mnakumbuka?alafu enzi hizo kulikuwa na mibaba isiyo na adabu inashika nyonyo na makalio ya wasichana hadi kwenye UDA(Usafiri Dar),
    Kioo,kioo alikivunja nani,sijui sijui,waongo nyie wote,
    Namtafuta rafiki namtafuta rafiki,A nyimbo hizi sijui alikuwa anatunga nani,
    Wenzangu wa Forodhani mpo?mwl Khamsini mnamkumbuka?ile sekondari ilikuwa poa

    ReplyDelete
  41. WAGAGAGIGIKOKO...... BULICHEKA LOOOOOOO SIWEZI SAHAU HATA, MWALIMU NYAKABUNGO MWANZA DARASA LA NNE SOMO LA KIINGEREZA, WEWE SAY THE BOOK IS MINE***** ZE BUKU ISI MAINI.... AAAAAH PUMPAFU WEWE ZEZE UMELIACHA NYUMBANI LIMELALA. KWELI TUMETOKA MBALI

    ReplyDelete
  42. Wale wa Dodoma Secondary mbona siwasikii humu??!. Na Headmaster wetu wakati huo, Degera ambaye ni mbunge sasa. Pia kuna Ntarukundo mwalimu wa Physics, kila siku anakuja na ngeu. Kapigwa kilabuni!. Bado yule mwalimu wetu chizi wa kike wa Geography, Ati wamemroga kwa kuwa ni mzuri sana na amekataa kuolewa!! Wale wanaomkumbuka mwalimu Lomoni, kaja kutoka shule anafundisha huku anaangalia nje. Anaona aibu midume ina ndevu darasani! Yuko wapi siku hizi yule mwalimu beautiful?! Jamani!

    Jamani, wapi Daniel majala, wapi Wille Haji, wapi Hilda Msemwa, wapi wewe Nico Mngulu, wapi Nsajigwa, wapi Sauda Zuberi the queen, wapi that black beautiful lady of all the time; Chausiku Maggoti! Wapi nyie wote?! Was a fantastic time never to reverse!

    ReplyDelete
  43. Naura Primary school....sitamsahau mwalimu wa darasa la kwanza mama Mtibili...I owe he big time. Yule mama alikua mwalimu haswa.

    Halafu kuna mwalimu mkuu alikuawa pale Mr Temba alikua nachapa huyo sio kawaida....Mwalimu Mollel mwanaume lakini alikua anacheza na sisi nage.

    Enzi za kuomboleza yule padri alikufa pale kanisa la katoliki. Mimi ndio ilikua mara yangu ya kwanza kusikia msiba.

    Mwalimu wa english mama kilindo...uwiii alikua mkali huyo na kuna mwingine wa hesabu pia sijui nani jina nimelisahau.

    Enzi hizo ilikua wenye akili wanakaa A, wanaofuata B, waliofell wanakaa C.

    Kwa hiyo ukienda la pili, tatu, nne, tano, sita na saba A unajua unakutana na genious people ukienda C unajua unakutana na watoro etc.

    ReplyDelete
  44. HABARI YA DOM SEC WATU EEH....ILE ENZI ZA YULE HEAD MASTER SHIRIMA. MNAMKUMBUKA YULE MWALIMU WA SIASA MWALIMU MAALIMU WALIKUWA WANASEMA ETI NI JINI, MANAKE ALIKUWA MREFU KAMA NJIA KUTWA NA USHUNGI HALAFU ANANUKIA PERFUME ZA MAITI.

    ReplyDelete
  45. KUHUSU AMANI PRIMARY SCHOOL PALE DODOMA, JAMANI MASHAKA MUUZA NGWERU, MIWA, MAEMBE, NK ALIENDA WAPI? MASHAKA WAS ALL WEATHER...HALAFU MIKONO YAKE MICHAFUU LAKINI ANAKUKATIA EMBE ANALITIA PILIPILI UNASAHAU UCHAFU WA MIKONO YAKE. MWALIMU MWALUKO KUTWA NA BIASHARA ZA UBUYU, HALAFU IKIFIKA WAKATI WA SANAA ANAWAAMBIA MKANUNUE MIFAGIO SOKONI NDO MLETE KAMA SANAA, KUMBE ANA AGENDA YA SIRI. HALAFU MTOTO WAKE PETER ALIKUWA NDO MBABE WA SHULE, UKICHEKA ANASEMA UNAMCHEKA SIKU YA KUFUNGA SHULE ANAKUVIZIA. ALIMPIGA KIBIBI YULE MWARABU TEKE LA TUMBO HADI AKATAPIKA!

    ReplyDelete
  46. kwa wale wa dom sec, mnaukumbuka huu wimbo wakati degera anahama?

    la mgambo limelia, hayaa, lamgambo limelia kwa wana wa dom sec, tujumuike pamoja tukiwa wenye majonzi...

    kuagana na baba degera, ni muda umefika, hayaa, kuagana na baba degera ni mambo mengi umefanya upewe shukurani nyini baaaba sisi vijana wako tutakukumbuka....

    ReplyDelete
  47. Safi saaana!!! Imebidi nirudi tena...Dodoma Mlimani ulikuwa ukichelewa inabidi uchane mitunduru(miti yenye miiba) ili Mwalimu asahahu au tunaenda kujificha korongoni mpaka Mwalimu wa zamu anayepita kuchapa walikosa namba apite. Ole wako uchelewe namba na iwe zamu ya Mwalimu Msalila...huyu anatokea darasani saa yoyote mpaka akupate na viboko vyake juu ya matako na anapandisha shati juu ili akupate kisawasawa. Halaiki:) ....ilikuwa ni sifa kuchaguliwa chipukizi. Wale tuliocheza halaiki ya mwaka 1985 kumuaga Mwalimu Nyerere alipong'atuka tunamkumbuka afande Abdalla na afande Ngoliga..ukichelewa kwenye mazoezi utawatambua hao maafande kwa kichurachura na push-ups!! Wakati wa halaiki Red Cross walikuwa "busy" kuwabeba wenzetu waliokuwa wanaanguka kwa "dehydration"!! Kuna mdau wa Dodoma Sec hapo juu kanikumbusha mbali ingawa sikumkuta Degera...Headmaster wangu alikuwa Shirima baadaye akaja Kaishozi!! Ila Ntarukundo alinifundisha Physics na sasa hivi ni marehemu (RIP). Kuna mwalimu Massawe alikuwa anashinda kwenye mifugo..Mwalimu Mwinyi na vibao vya kushtukiza, ukiongea naye inabidi umwachie umbali wa kutosha la sivyo atakuotea bonge la kibao usoni!! Kulikuwa na Mwalimu mmoja mzuri Mwalimu Mahagi...:)...Mwalimu Namilikwa, mwalimu wa social...huyu siku ya disco la shule "Welcome Form one" au graduation ya Form IV alikuwa na kamera yake na anataka mpige picha kwake. Mikanda ya picha ikimwishia basi ujue na disco litaisha maana ataanza kupita akiwaonyesha vidole vya dakika zilizobakia ili disco lifungwe...hapo ukitoka nje bado kweupe. Wow, Old is gold.....ya kale ni dhahabu..hizo ni za DJ Kessy!!

    ReplyDelete
  48. mdau wa uk nimerudi tena,hii mada ni kiboko!!

    mnakumbuka banzoka?bubunda?visheti?ice cream za ubuyu?

    mnakumbuka enzi hizo darasa la pili ukimchungulia mwanamke na kuona rangi ya chupi yake duuuu utatangaza shule nzima!!!ifuatayo ni barua niliyandikiwa na kishtobe wangu enzi hizo

    kwako mpenzi uliyembali na upeo wa macho yangu,utakapokujua hali yangu mimi ni mzima.
    Dhumuni la barua ni kutaka kukufahamisha kuwa kesho nitakpokuw anenda tuisheni kwa mwalimu kikanya chamwino nitapitia kwako kukusalimia.naomba unisubiri"
    nimekuwekea na hii zawadi ya banzoka(big g).

    basi noma ilikuwa barua uniichicha kwenye madaftari,mwalimu akianza kusahihisha anaikuta,inakuwa bonge la kesi.

    mnakumbuka ukifika msimu wa zambarau,au mabibo?ile staili ya kupanda kwenye miti na kucheza kidali po?

    ufutao ni wimbo tulioiimba darasa la kwanza hapo kizota primary school dodoma enzi ya mwalimu ndandala

    asiyesoma ni masikini,asiyesoooma ni masikini.saini yake hiyo saini yake hiyo saini yaaaaake ni dole gumba!!!!

    wadau wazamni tumbukane bwana kupitia titusboniface@yahoo.com
    au titusboniface@hotmail.com

    ReplyDelete
  49. Nami pia nimekumbuka mbali mbali japo ni 90s lakini duuh sehemu ya masumbwi inaitwa kiwanja cha dhambi,cku ukikosa shule basi kesho yake wala hamna haja ya kuandika tena notes,tuliosoma bush kulikuwa na design flani ya kuagizwa majembe ya kulimia mchana sasa cku teacher wa zamu akisahau basi tunatoka nduki mbaya ukiskia ajuaaaaaaa!!! ajuuaaaaaaaa!!! basi teacher wa kilimo ashakumbushia na nyingine sku za jumatano tulikuwa tunachelewa kwenda home coz mchana haturudi so mpaka mida ya saa saba na nusu hivi tulikuwa tunaita saa nane weee usipimie hiyo njaa yake.

    ReplyDelete
  50. Chacha nae anapenda sana kukumbusha mambo ya zamani, kweli hapa mmempata. Eti kipanga ampiga mkoloni, mara bulicheka, nondo mla watu...... Kweli nimecheka sana. Wadau wa Temeke primary mbona siwaoni. Mnamkumbuka mwl. matutu wa hesebu alivyokuwa mfupi na miwani yake. Mkwara wake usipime.

    ReplyDelete
  51. Daah, jamani mnazikumbuka biskuti za muhogo? zilikuwa kama za mstatili ambao katikati kama umeingia ndani hivi. Daaah wadau nimefurahi sana leo nikikumbuka Muhimbili Primary enzi za mlm Ndossy, duh, na twishen yake, ebana tulichapwa viboko utadhani hatuna akili nzuri

    ReplyDelete
  52. Wadau wa Nov 12 at 3:01 and 3:55 mmenikumbusha mali saaaana mambo ya Muhimbili primary. Mnakumbuka kipindi cha dini kila jumanne na alhamis?, kipindi kipo just before ooo-time ya saa sita, basi watu tulikuwa hatuingii dini so break inakuwa ndefu kishenzi(sina uhakika muda gani though), basi watu mnavuka barabara mnaenda kununua Potelo na Jam cake au Jugu (Njugu) cake kwa baba taibali(RIP) pale Duka Shop, daaaah, jamani maisha yale yalikuwa matamuuu.

    Mwalm Chuwa alikuwa anamgeza ukali mlm Ndossy basi anazidisha chumvi akikuchapa utajuta, mara anakupa adhjabu ya kuleta debe la mbolea (Muhi2 primary tulikuwa hatuji na madumu, mbolea au mapanga, ni mifagio tu), basi ukitumwa mbolea ni bonge la adhabu, mzazi inabidi akusaidie kuitafuta kwa marafiki zake, nakumbuka maskini mama yangu alifuata mbolea oysterbay kwa rafiki yake akaibeba kichwani from oysterbay hadi home upanga, halafu kesho yake mlinzi wa jirani akanibebea hadi shule hiyo mbolea, na bado tukaambiwa eti tumeleta mbolea kidogo,jamaniiii.Hkyanani sitamsahau mlm Chuwa yaani.

    Ukiachana na hilo la mlm Chuwa, nawakumbuka sana walimu wangu Mlm Nyamageni(darasa la kwanza na la pili), mlm Kitutu(Hesabu la nne), Mlm Hanga (Geography la tano), Mlm Bakari(Sayans kimu la tano), Mlm Mhumbira (Sayans la sita), Mlm Rutabingwa(Hakunifundisha ila namfagilia)...daaah, yaani hawa waalim hadi leo wakiniona wananikumbuka hadi jina, nawashukuru sana walimu wangu hawa maana ndio walinipa msingi bora hadi leo hii nipo hapa namshukuru Mungu.

    Shule ya muhimbili watoto tulivyokuwa na kelele, lakini mara mnasikia kimyaaaaaa, mara mtu anasema...Jamani shetani mwekundu kapita, hahahaha

    Mabungo kwa mzee Kijicho, mihogo kwa mzee Rashidi, vimishkaki vidogooo kwa Nyakunga, hahahahaha

    Hapo darasa la kwanza unapewa Ufuta na Mlm Lazaro umuuzie, duh jamani

    Muhimbili Primary oyeeeee

    ReplyDelete
  53. Kweli mmenikumbusha mbali sana wadau! Mada imetulia Mithupu tupe vitu kaka.Wale wa shule za kilimanjaro mbona siwaoni??

    ReplyDelete
  54. mhh nimefurahi sana kwa kumbukumbu kwani yote yaliosemwa tumepitia historia hua tamu sana kwani kumbukumbu inarudisha nyuma unakumbuka uliosomanao,mazingira ya shule,mazingira ya nyumbani,walimu waliokufundisha,na mambo mengi kadha wa kadha kikubwa vizazi vinabadilika kila kizazi kina michezo yao mengine yanafanana na sisi tuilopitia mengine hayafanani kabisa na michezo tuliopitia.mtoto wangu aliniuliza swali moja nikashindwa kumjibu aliniuliza kua baba unasema enzi za ujana wako mlikua hamutumii simu za mkononi kwa hiyo mulikua munaishije kwa mfano kusalimia mtu alie mbali au kumuendea mtu ambae huna uhakika kama yupo numbani au la je ukienda bila tarifa ukifika ukamkosa inakuwaje .kwa hiyo hayo maswali yote na mengi na ya mshangao kwa kua amezaliwa na kukua amezikuta simu.sawa na sisi wakati tunakua tulielezwa kua zama za hapo zamani hapakuwepo moto yaani ninamaanisha kiberiti au mafuta ya taa nk tulikua tunashangaa na tulipekea hata kutokuamini ila ukweli ndio huo jibu la haraka haraka ni kwamba kila kizazi na mambo yake na michezo yake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...