baada ya kufungiwa siku kadhaa kupaa angani, hatimaye shirika la ndege la atc limepewa tena leseni na kufunguliwa mbawa zake leo. ila wafanyakazi wake bado wako hoi bin taaban kwa kukosa mshiko wa mwezi desemba ambapo krisimasi hii waliishia kuula wa chuya. soma zaidi habari hii kwa kubofya hapa kwa ung'eng'e ama bofya hapa kwa kimatumbi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Chako ni chako..cha kukodisha sio chako!!!

    ReplyDelete
  2. Hi wenzangu, habari gani? mimi ninasema nje ya topic. sasa napende kuliza swali moja tu. jina lengu ni Jennifer, na mimeoa mtanzania for 4 years. sasa, nimemupikia pleu na maharagwe, lakini napende nifahamu namna gani ya kutunza huu mme wangu vizuri. Naomba shauri ndugu.
    Jenny

    ReplyDelete
  3. Michuzi acha kamba au usichukue na kupost habari ambayo hujaifanyia uchunguzi,atc bado hawajaanza kazi na hata leseni hawajarejeshewa.Na huenda ikawa si leo wala kesho.

    ReplyDelete
  4. TCAA imeirudishia ATCL licence to fly na hivyo itaanza kuruka sasa. Lakini cha kushangaza ni kuwa - IATA bado imeifungia ATCL na haitaifungulia mpaka warekebishe mambo yao, hasa ya kiusalama wa anga na abiria.

    Inaonekana TCAA imepewa pressure kubwa na serikari na vigogo wake mpaka imekubali kuwafungulia leseni bila kujali kuendelea kufungiwa na IATA na bila kujali kuwa ndege za ATCL hazina maintenance-service ya kuaminika kutokana na ukata. Maamuzi hayo hayajali maisha na maslahi ya watanzania.

    Itambulike kuwa TCAA inaweza kuiruhusu ndege za ATCL ziruke nchini kwetu tu, kwani nchi nyingine hawataruhusu ndege za ATCL kuingia anga zao zikiwa zimefungiwa na IATA hazikidhi viwango vya kimataifa vya usalama wa anga na abiria na zinaweza kuleta ajali zikiwa nchini huko. Pia ndege za mataifa mengine zinapoingia anga yetu huwa na wasiwasi sana kwani huenda wakakutana na ndege mbovu na sisizofuata taratibu za kimataifa huko angani na kusababisha hatari.

    Hatua ya TCAA ni kuonyesha ukaidi wa Serikali yetu na itaweza kuleta madhara kwa raia.
    Ni Bora TCAA ifanye kazi zake kwa - ki-professional and kuwa independence. Wasikubali pressure za kisiasa.

    Jambo ya pili ni hatua ya Bodi ya ATCL kuwakodisha maconsultant wa Price Water Coopers kwa fedha nyingi sana. Kampuni kama TAC Associates au Kampuni ya Tija ya Taifa ingekuwa ya nafuu sana kulinganisha na Price WaterCoopers

    Pia:

    ATCL haikuitisha zabuni ya kazi hiyo waliyopewa Price Water Coopers, Rushwa imetembea kutokana na urafiki wa Partner Mndolwa za Price Coopers na Mr. Nyanganyi na Mataka
    Hii pia ni kinyume cha taratibu za Public Procurement regulatory Authoryt - Dr. Angalia hapo

    Kampuni ya Price Water Coopers pia ni wakaguzi wa mahesabu wa ATCL. Hivyo kwa taaluma yao huirihusu wao kujiingiza katika kazi za manajimenti ya kampuni. Wakaguzi huru kuruhusiwa kuwa Management Consultant kwa kampuni wanayoikagua ni kunyume cha professional ethics zao na pia kunawasababishiwa kukosa independence - Bodi ya wakaguzi iliyolala, na inayoongozwa na maPartners hao wa PriceCoopers wanatakiwa kukemea hili

    Ukaguzi wa ATCL kwa kutumia Price Coopers Waters imegharimu zaidi ya millioni harobaini wakati TAC Associates walikuwa wanakagua kwa shillion million zisizozidi kumi

    PriceCoopers imepeleka wafanyakazi ATCL akiongozwa na Mkuu wa idara ya fedha, mkuu wa ukaguzi ndani, hivyo hawa watendaji wakuu wamekuwa kwa muda mrefu wanapeleka kazi kwa mwajiri wao wa zamani. Hou ni Eliasaf Methew, William Haji (kaondoka) na Maria Lyimo wa Kimara.

    Kuna rushwa tupu inanuka ATCL katika mambo ya procurement.

    ReplyDelete
  5. hi wewe
    dada unayeitwa jenniffer ambaew unauliza ni jisi gani ya kumtunza mumeo mtanzania,unataka ushauri kama upi?
    kwa kukuliza wewe mwenyewe ni wa taifa gani?ni mwafrika au unatoka nchi gani?.je umewahi kumuuliza mumeo ni chakula gani yeye hupendelea?sikosei kila mtu anapenda aina fulani ya chakula..je mnao watoto?kama mnao watoto hebu jaribu kuwaulizia watoto wako wanapendelea chakula kipi pia..kama una zaidi toa e-mail yako tutakupa mawaidha through e-mail kwa kirefu..tutawasiliana nawe na kukupa ushauri ..dada
    mimi ni mwana dada kama wewe,ambae nimeolewa pia
    asante..esther

    ReplyDelete
  6. Kwa mambo haya...watani wetu wa jadi ..Kenya wataendelea kutuacha kwa mbali..wakati tunaendelea kutambaaa..Mungu Tubariki nasi tuwe kama wenzetu.....

    ReplyDelete
  7. Ufisadi katika Shirika la Ndege letu haukuanza jana!

    Mwaka 1980 tuliamua kununua ndege mpya mbili kutoka Amerika.

    Moja ikafika siku ya Jumapili asaa kamma tau na ushee hivi kwa nderemo za kuzunguka jiji la Dar kabla ya kutua...kumbe TUMBA la mi-ji-tumba!

    Ya pili nayo baadaye ikawasili.

    Ndege ya kwanza ikaaza safari za kwenda Uingereza uwanja wa Gatwick. Ikatua salama lakini haikuruhusiwa kuruka tena.

    Achilia mbali gharama ya kulipia kuwepo kwa ndege hiyo hapo uwanjanai na ya kruu wetu kabla ya kurudi nyumbani. Hatimaye, kruu wetu wakarudi kwa ndege ya shirika lingine!

    Hilo dege likaozea hapo!

    Dege hili lilikuwa la kampuni moja ya Amerika ya TWAA likifanya safari kati ya West Afrika na New York miaka ya 1960’s.

    Sijui lilikuwa limeishapelekwa huko makaburini Jangwa la Mojave - kwenye makaburi ya madege Amerika (fungua: http://www.aerospaceweb.org/question/history/boneyard/mojave.jpg) - lakini likafanyiwa ukarabati na kudanganywa kuwa ni dege jipya baada ya wakubwa kuweka zao mifukoni!

    Dege la pili nalo likaletwa na likaruka ruka kati ya Dar na KIA na kukwama hapo KIA! Sijui lilishia wapi?

    Hili nalo lilikuwa dege zee lililokarabatiwa na kuuziwa kwa bei ya juu na wakubwa kuweka zao mifukoni!

    Si mnajua cha 10% (siku hizi ni juu zaidi na zaidi licha na nyingine kulambwa na mawakal – ni kitu cha kawaida wakati mwingine kiasi ambacho kingepewa shirika!

    Lakini kinakuwa cha wanunuzi wenye kutia saini, kana kwamba ni mali yao binafsi.

    Na kama mwuzaji akikataa kuwa % hiyo ya mrungura ni juu sana, wakubwa wanasema ongeza hiyo %-age kwa bei ya ununuzi na utuwekee vi-ji-senti vyetu pembeni!


    Eti kuna TAKUKURU!

    ReplyDelete
  8. Hivi ni kwa nini serikali inaendelea kulishikilia hilo shirika wakati haiwezi kuliendesha katika huu ushindani wa biashara? Mimi ningeshauri wauze hisa zote za serikali ili shirika liendeshwe na watu binafsi kama jirani Kenya Airways walivyofanya. Waliondoa siasa kwenye shirika lao la ndege na sasa wako mbali i.e. Kenya Airways ni moja ya mashirika ya ndege yanayotamba Africa na huo ni ukweli ambao lazima tuukubali.

    ReplyDelete
  9. Hivi kweli nchi yenu haiwezi kununua ndege 2 tu aina ya Boeing 737-800??(ndege hizi nadhani moja ni kama USD mil.220-230,I am not sure) halafu kama alivyochangia mdau hapo juu siasa zikatolewa shirika likaendeshwa na watu binafsi,then we can take off from there.

    ReplyDelete
  10. Watanzania hatuhitaji hesabu za hali ya juu kuelewa kuwa ATC itaendelea au vipi, kuna siasa nyingi na menejimenti haina ujuzi wa kuongoza mambo ya ndege hususani atc iliyopo intensive care unit.

    kenya airways iliongozwa na professonional kutoka UK, na aliposhuka nairobi siku ya kwanza alimwambia raisi moi hatasaini mkataba mpaka atakapohakikishiwa kuwa bodi haitaingilia maamuzi yake.

    Mojawapo ya wajibu kwenye mkataba wake ni amfundishe meneja ambae yupo sasa, matokeo yake ni supa na wala sihitaji vielelezo vingi.

    Kwetu sisi meneja hana ujuzi wowote na mashirika ya ndege na mwenyekiti wa bodi ni balozi aliyestaafu - hapo hamna anayefahamu chochote kuhusu mambo ya anga kwa kifupi wote ni mambumbu kwenye mabo ya ndege.

    RSVIP ATC, huna viongozi ni wauaji tu - ugua pole na uombeee muujiza utokee serikali ikupatie viongozi wazuri.

    ReplyDelete
  11. Wee anonymous wa January 01/ 2009 4:46 PM.
    Kwanza be respectful kwa watu wazima walioitumikia nchi hii. Huna haja ya kuita watu mambumbu huku kumbukumbu zako hazipo. Balozi Nyanganyi alikuwa waziri wa Mawasiliano kwa muda fulani na alifanya kazi nzuri mashirika yote reli, ndege yalikuwa super hadi alipoondoka mwisho wa uongozi wa Mwalimu Nyerere na kwenda kuwa balozi wetu USA. Uzoefu anao na aliowafanyia kazi wanajua! Kama una point iandike na siyo kutoa kashfa. Uzoefu alionao si wa kitaifa tuu. Kama unataka kujua kazi alizofanya kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi (USA NA U.A.E). Google jina lake kamili. Waatanzania shida yetu ni lugha chafu bila vigezo muhimu, na kwanza yeye si mtendaji bali ni mshauri wa ATCL. Bwana Mataka ndiyo mtendaji mkuu wa shirika hili na wameisha sema tatizo si uongozi bali ni pesa za kuendesha shirika ambalo serikali iliahidi na haijatoa senti moja. Mbona hamuilaumu serikali yetu? Mmewakalia kooni viongozi, wameishawaeleza kilichotokea na serikali mpaka leo hii hawajakanusha statements za mataka wala Balozi Nyanganyi. Kustaafu siyo kuwa mbumbu. Baloz Nyanganyi ni Graduate wa HARVARD, KENNEDY SCHOOL OF GOVERNMENT IN USA, ULIZA MTU YEYOTE ALIYEKAA MAREKANI ATAKWAMBIA HAKUNA MBUMBU ANAYESGEA HUKO! ACHENI USHAMBA NA MATUSI ANDIKA VIGEZO VYAKO

    ReplyDelete
  12. Nashukuru kwa maoni kutoka kwa anon wa january 02 2009, 6.38 a.m.

    Naomba kufafanua kuwa nilichoandika siyo mbumbumbu passe ila 'mbumbumbu wa mambo ya ndege'

    Kuitwa mbumbumbu kwenye taaluma fulani sio tusi, huwezi ukawa mtaalamu kwenye fani zote, mimi mwenyewe nimesoma karibia mwisho wa madarasa yote lakini ni mbumbumbu kwenye masuala ya ndege.

    Inaelekea pia wewe una mawazo yaliyotukwaza baada ya uhuru kuwa ukishasoma chuo kizuri basi utaweza kila kitu... nakuhakikishia na kutokana na uzoefu wangu ughaibuni...hiyo haipo dunia iliyoendelea, darasa linakupa funguo ya utaalamu...zaidi ya hapo na ili wewe uitwe mtaalamu ni lazima ufanye kazi na uonyeshe kwamba... yes i can.......it does not matter whether it is harvard or chuo kikuu mlimani...ukishaingia anga za professionalism kwenye capital world unatakiwa kuprove... yes you can deliver.

    Balozi Nyanganyi amesomea Harvard schoool of government, track record yake ni diplomat, waziri, etc...

    kigezo changu nipe ushahidi kuwa mkuu wa bodi wa shirika la ndege lolote duniani (USA, Britain, Middle East, Scandinavia, asia..etc) lililofanikiwa ambalo lina body chairman and CEO ambao hawana ujuzi wa kutosha kwenye mambo ya ndege...????...jibu ni hakuna.

    Sasa ndio itakuwa ATCL ambalo linahitaji utaalamu wa hali ya juu kuliokoa kwa sababu lipo ICU..hapo hahitajiki daktari mwenye kigugumizi...eti ulpeleka memo serikalini haikushughulikiwa basi jiuzulu.. au fanya kama wenzako wengine sema nitashindwa kuongoza na hivyo ni tastep aside kama hili fungu halikupatikana....si umeona chief execuitive wa kampuni za magari marekani, wanaomba hela za miezi ijayo.

    Wakati huu ni mwingine na tuwaachie wengine wenye ujuzi wa mambo ya ndege hizi nafasi, kwa kifupi wakati wa kustaafu umefika...

    Sio ushamba wala matusi ni ukweli wa mambo...wameshindwa kudeliver...kaa kando pisha wenye uwezo.

    ReplyDelete
  13. ..........ndio raha ya Tanzania tofauti na nchi yoyote duniani kwamba ukipewa dhamana kwenye ofisi ya serikali huna hofu hata kidoooogo ukiboronga!!! Mambo yapo wazi kabisa,wahusika walioboronga wapo wanajulikana serikali inaanza kuzunguuuuka weeeee!!! Kamata-nyonga kama china!
    Shirika la ndege la nchi(State airline charter) ni mhimili muhimu sana kwa uchumi. refer KQ(Kenya) wanaiingizia nchi mabilioni yadola kwa mwaka.

    ReplyDelete
  14. hii fweza si serikali wangesaidia wasomi wangapi wa chuo kikuu wasiowezaq 40%??au watoto wangapi yatima hawana shule,chakula nk na hospital ngapi hazina miundombinu na dawa za MSD ndo kasheshe jingine??
    jaman mbona mwatuua??nini iki ATCL?yan shirika haliendi wamekalia weeezi tu apo na vya juu,haiingii akilin kabisa shenzi zao saana awa.
    yan ile airbus walonunua juzi tu apa iko wapi???
    **@@&$::<. zao saaaana awa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...