Wengine huku ughaibuni at 1200hrs / 12.00noon unakuta ni giza totoro! Je, hapa nitaita mchana au usiku?

Mtazamo mwengine: Majira ya Usiku na Mchana yanatokana na kiasi cha mwanga au muda katika saa?
Naomba maoni yenu!
Mdau Ughaibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. we mdau wa ughaibuni ukishasema 12.00 noon manake ni mchana hata kama kuna giza.

    ReplyDelete
  2. Kama ulipita angalau shule ya msingi na kichwa chako kina kumbukumbu basi nadhani utakumbuka kuhusu mambo ya "usiku mrefu" au "mchana mrefu",kwa hiyo uwepo wa mwanga ndio unaoonyesha mchana na uwepo wa giza ndio usiku.

    ReplyDelete
  3. Uongo mtupu, sisi huku tunaishi Ughaibuni pia. Usitake kudanganya watu hapa. Hakuna giza 12:00 noon. Wakati wa winter, giza linaanza kwenye saa tisa jioni na kuendelea. Summer mwanga mpaka saa nne usiku.

    ReplyDelete
  4. Wewe mdau uliyesema uwepo wa mwanga ndiyo unao0nyesha usiku na uwepo wa giza ndiyo usiku. kwahiyo unamaana kwamba huku 12.00 noon na 12.00 midnight wakati mwingine unakuta ni mwanga mkali tu, vyote niite Saa 6 mchana?

    ReplyDelete
  5. Kumradhi Kaka Michuzi lakini mimi naona hii mada hainipunguzii tress bali unataka kuniingiza mwaka mpya na tress za mawazo yasiyo muhimu hivyo unaniongezea. Hebu bania hizi mada nyingine kwa sasa tuache tuuage mwaka tress free tafadhali

    ReplyDelete
  6. SAFI KABISA MTA MAONI JUU HAPO,WATU WANACHANYANYA MIDA USIKU NA MCHANA,KINACHOTENGANISHA USIKU NA MCHANA NI MWANGA,HAPA NORWAY GIZA LAANZA SAA 4 PM, NI USIKU TU,LAKINI MKANGANYO HUU UMEANZIA KATIKA BIBLIA WAKATI WA UUMBAJI,WAANDISHI WALIPOSEMA ,IKAWA ASUBUHI ,IKAWA JIONI ,SIKU YA KWANZA,HALAFU WAKAANDIKA KUWA MUNGU ALIUMBA JUA NA MWEZI SIKU YA NNE,UNAWEZA KUULUZA ,ASUBUHI NA JIONI VILISABABISHWA NA NINI, ITS A MESS.

    ReplyDelete
  7. Kutumia masaa 24 ndiyo suluhisho, hivyo huna haja ya kutaja asubuhi, mchana, jioni, usiku nk. Unasema tu saa 13. Mkuu tukutane pale chekipointi saa 16!

    Macho

    ReplyDelete
  8. Yaleyale ooh 'tofali la barafu halijengi nyumba' huku Bongo wakati huko Greenland waEskimo na Wachina 'tofali la barafu linajenga nyumba.

    Kwa hiyo ya huko giza @ 12noon/12:00 Hrs ni ya huko kwenu sisi TZ taimu yetu inafuata mwanga wa jua wakati huko ughaibuni inafuata 'watch/clock'.

    ReplyDelete
  9. Wadau mnaoishi UK(kama kuna wadau waliosomea hii fani itakuwa vizuri zaidi).Sisi tunaongalia Premier league huku Africa(TZ) utakuta kuna wakati UK wanasema 1500UK huku bongo ni 1700(yaani 2 hrs difference) halafu miezi mingine 1500UK hiyo hiyo unakuta huku bongo ni 1800hrs(3 hrs difference).Inatokraje?Msinicheke na ushamba wangu.

    ReplyDelete
  10. MCHANGIAJI MMOJA HAPO JUU ANAMKOSOA MTOA MADA/MAONI/SWALI NA KUMWITA MUONGO ETI ANASEMA HUKU MAJUU HATA YEYE ANAISHI BASI ASIDANGANYWE ETI GIZA HALIANZI SAA SITA MCHANA LINAANZA SAA TISA JIONI. NAMI NAMKOSOA YEYE ANAONEKANA AKILI YAKE NZITO, WAZUNGU WANASEMA YUKO THICK WATU WALIO MAJUU HATA KATIKA NCHI MOJA HAWAKAI MJI MMOJA KWANI HATA MIJI TU INATOFAUTIANA UINGIAJI WA GIZA KWA MFANO LONDON NA MANCHESTER SEHEMU MOJA GIZA HUANZA NI NYINGINE UCHELEWA, HATA TANZANIA KIGOMA HUTOFAUTIANA NA MTWARA UINGIAJI WA GIZA NA MCHANA, JAMBO LINGINE WALIO MAJUU SI WOTE WANAKAA NCHI MOJA KWANI KUNA TOFAUTI KUBWA KATI NCHI NA NCHI KWA MFANO ITALY NA ICELAND KWA MFANO HUTOFAUTIANA UINGIAJI WA GIZA NA MCHANA, PIA KUNA SEHEMU MIAZI MITATU HAWALIONI JUA NINA MAANA HALITOKI KWA VILE LIKO HORIZON YA MBALI WAO KUWAFIKIA, HII NI GEORAPHY SIMPLE TU. MWISHO KUHUSU MAADA; USIKU NA MCHANA HUHESABIKA KWA MASAA KITAALAMU SI GIZA NA MWANGA, NA SI PENYE GIZA MAANA YAKE NI USIKU, KWANI UKIJIFUNGIA NDANI MCHANA NA KUFUNGA MILANGO NA MADIRISHA IN MAANA ITAKUWA NI USIKU KWA VILE KUNA GIZA? AU USIKU UKIWASHA TAA NA KUPATA MWANGA MAANA YAKE NI MCHANA? GIZA NA USIKU NI VITU VIWILI TOFAUTI KABISA, HALI KADHALIKA MCHANA NA MWANGA NI VITU VIWILI TOFAUTI EITHER.

    ReplyDelete
  11. noon ni noo hata kuwe na giza. Kwani kupatwa kwa jua yale madakika machache uanita ule usiku?

    @2:44 umeshaenda alaska....watu siku nyingine hata hawauoni mchana kabisa kwa hiyo huyo mtu sijui yuko wapi lakini alaska nimeona hii.....

    ReplyDelete
  12. Thats true kuhusu Alaska!,kwa hiyo mtoa hoja hii hakukosea somehow!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...