Habari ya kazi bro Michu?
Naomba utoe kisa hiki, ila sina nia mabaya na Mtu yoyote. natoa kisa cha kweli kilichonitokea mimi.
Kuna kipindi niliumwa malaria sana nikaenda Hospital fulani kubwa (private hospital)sitaitaja jina kwa sasa ila mkitaka niwapa jina baadaye., sasa nikaenda hospitalini hapo ilikutibiwa nikaulizwa unataka tukuchome sindano au tukupe vidonge, nikachagua nipewe dozi ya vidonge, nilichagua sio kwa kubana matumizi wala nini ila kampuni ilikuwa inalipia matibabu kwa wafanyakazi wake kwa gharama yoyote.
Sasa nikapewa vidonge hivyo nikaenda navyo nyumbani kwenda kutumia, kilichotokea baadaya ya kama dk 40 mdomo ukaanza kubana na kisha sehemu ya chini kwenda upande kwa nguvu na kisha kuacha kidogo na kisha kurudia rudia rudia, wewe...nilipiga kelele nikamwambia mdogo wangu aendeshe gari langu anipeleke kurudi hospitalini hapo.
Tulipofika akasimulia yalonikuta na tukaonyesha dawa tulizopewa. Chap chap nikachomwa sindano ya kukata makali ya dawa hiyo na mdomo ukatulia, na ulipotulia nikauliza je kwa nini mlinipa dawa hii, wakasema sorry hii dawa ilikuwa kwenye majaribio inatoka India, na ina allergy kwa watu wengi. Sorry tutakupa ingine.
Nikachanganyikiwa kidogo. Nikasema it's enough. Ngoja nikajaribu hospitali ingine. Nikaenda huko kwingine ndio nikapata tiba ya vidonge vinavyofahamika.
Sasa je kwa namna hiyo je tutafika kweli, na hospitali hiyo kubwa sasa majaribio ya nini tena wakati kampuni kubwa zinagharamia kwa gharama kubwa matibabu kwa wafanyakazi wake ?
Na Hospitali hiyo inatumia dawa ambayo hata jina lenyewe huwezi kulipata kirahisi kwenye Pharmacy za mitaani mje kujaribia kwa wagonjwa wanaokuja hapo? hiyo inakuwa sio vizuri kwani mnaweza kuua watu wengine au kupoteza biashara naomba kuwasilisha kwa wale wenye Hospitali jaribu kujali maisha ya watu tumieni madawa yanajulikana na yaliyopitishwa kwenye viwango vya ubora.
Kama mnaona Gharama ni kubwa kwa Madawa hayo ni Bora Mkaomba serikali iangalie kwa makini swala hilo.
Asante
Mdau E.K

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Mimi ninamaswali kwako kwanza kabla sijailaumu hiyo hospital. je walipokupa hizo dawa zilikua zimeandikwa jina lake kwenye kichupa ua karatasi waliyokupa? Mimi nisingejaribu kunywa dawa ambayo haina jina. halafu siondoki hospital kabla Dr au mtu yeyote kunieleza side effect za dawa hiyo.

    Na siku hizi mtandao ulivyo wazi dawa siko nyingi online ukigoogle tu jina lake unapata maelezo yete kuhusu hiyo dawa, side effect zake etc.

    Mambo ya kuwaachia maisha yako maDr siku hizi na kuwaamini katika kila jambo yamepitwa na wakati. Inabidi uwe makini , uwe muuliza maswali na uwe na living will. Labda niwe mahututi ndio sitaweza kuuliza swali, na kukataa dawa ambazo nina allergy nazo au ni nyingi kuliko wight yangu.

    Hata kama ni private hospital haina maana wao ni bora zaidi ya maDr wa public hospital. Tofauti ya private na public hospital ni vifaa tu vya kufanyia kazi lakini kwa upande wa madoctor wote ni sawa.

    ReplyDelete
  2. wewe ulieandika hii baruwa unanitia kichefu chefu na unaniudhi mnoooooo!!!!! sasa kwanini hutaji jina la hospitali ili uokowe maisha ya watu kama kweli unajari?
    au kama unaona haukutendewa haki si uende washitaki wafuatiliwe na hizo dawa zikamatwe na selikari ichunguze zimeingiaje nchini?
    unaniudhi unapoficha jina la hospitali sasa unataka nini hapa?
    hospitali ichukuliwe hatuwa au unatahadharisha binadamu wengine? sasa utawaepusha vipi kama usemi jina la hospitali?
    basi kwa taharifa yako hivi sasa kuna watu wengine hospitali hiyo hiyo wanapewa dawa iliokufanya sehemu za siri zipinde pinde na mdomo kubana sasa unajisikiaje?
    na hiyo hospitali nyingine ilikupa dawa gani? iliokuponesha? sema watu tuijuwe.

    ReplyDelete
  3. Mdau, tafuta mwanasheria na washitakia hiyo hospitali kwa kukufanya wewe panya wa majaribio "guinea pig" bila ya idhini yako na kukusabishia machungu ya kimwili na kifkra " emotional and physical pain" washitaki"wa-sue" ukitaka ulipwe fidia kwa madhara uliyopata.

    Nafikiri wewe na mwanasheria wako muanzie kudai fidia kama bilioni 100.

    Kazi kwako sasa, sio kusua sua eti serikali hivi au vile.

    Take care.

    ReplyDelete
  4. Hii ndio sababu iliyosababisha wengine tuhame bongo... Sasa kama wewe umepewa dawa ya majaribio na umemsikia kabisa mtu anakwambia kwamba amekupa dawa majaribio badala ya kufile Law suit unakuja kulalama kwa michuzi. Haya file law suit

    ReplyDelete
  5. POLE KWA KUWA NA ALEJI NA DAWA HIYO LAKINI SIO KWELI KWAMBA DAWA ZINAFANYIWA MAJARIBIO KIHIVYO.HUYO ALIYEKWAMBIA HIVYO NINAUHAKIKA SIO DR WALA PHARMACIST BALI WALEWALE.DAWA NYINGI ZINAREACT NA MIILI YA WATU LAKINI HAIMAANISHI KWAMBA ZIKO MAJARIBIONI.PPIA NI KWELI KWA SABABU YA UBOVU WA SHERIA ZETU, KUNA DAWA 40% SOKONI AMBAZO NI FEKI,NYINGI TOKA INDIA ZA BEI NAFUU,KOSA LIPO KWA WATU WAJIITAO TFDA, HAWA WAMESHINDWA KUDHIBITI SOKO,LAKINI LAWAMA SIO KWAO MOJAKWAMOJA, BALI SHERIA MBOVU ZA SERIKALI KAMA ILVYOKUWA KWA MALI ZISIZO NA UBORA KWA MASOKO YA TZ.
    POLE SANA ,NDO SERIKALI YETU TENA.

    ReplyDelete
  6. Pole Sana.Sasa tafuta mwanasheria wa nguvu akupiganie ili angalau na wewe upate chochote. Kamwe usithubutu kuwaachia hivi hivi maana wamevunja sheria kukupa madawa yenye sumu ambayo yangeweza kumaliza uhai wako.Ingekua hapa UK wanasheria wangekugombea ila huko nyumbani sijui kama wanaona hiyo ni deal.
    Mdau

    ReplyDelete
  7. hahaha!1
    Asilimia themanini uliona dawa ya majaribio inakukataa ujue kwamba una matatizo aidha ngoma au magonjwa ya virusi kama HP C.
    Madawa ya majaribio yamekuwepo hewani kwa muda mrefu sasa na wengi wasio na maambukizo mengine huendelea vizuri hadi kupona.
    Jaribu kupima mgoma uone.

    ReplyDelete
  8. WEBMD inasaidia watu wengi sana siku hizi,mdau mmoja ameuliza je bwana kaka umeuliza side effect ya hiyo medisin?Mimi kwakweli siwezi kutibiwa mafua nikapata ugonjwa wa kuhara.

    ReplyDelete
  9. DAWA HAZIFANYIWI MAJARIBIO HOSPITAL, HUFANYIWA MAABARA, DAWA HADI IFIKE SOKONI IMESHAFANYIWA MAJARIBIO, HIYO NIM ALLERGY TU, HATA CHLOROQUINE WATU HUENDA MDOMO PEMBENI.

    ReplyDelete
  10. hiyo itakua ni hospital ya mafisadi tu

    ReplyDelete
  11. comment nzuri saana. na nafikiri utaenda fanya homwork ulopewa na wadau 1. jina la dawa
    2 jina la hiyo zaanati
    3 jina la huyo aliyekuambia kuhusu hiyo dawa. kwa ushauri mwingine sindano ni bora kuliko vidonge. juu sindano haigusi ini pia ina act fast. tuletee majibu kwanza then ndo kazi ianze.

    ReplyDelete
  12. Huyu jamaa hana lolote yeye amepata ALLERGIC REACTION ya dawa ambayo hata ukisoma kwenye leaflet ya dawa zozote utakuta wameziandika ila huwa zinatokea kwa watu wachache sana wenye matatizo kama huyu jamaa na hakuna njia yeyote huyo daktari angeweza kugundua bila yeye mwenyewe kumuambia dakatari kwamba an allerg ya dawa za aina fulani,otherwose itabidi wagonjwa wote kabal ya kupewa dawa yeyeote hata panadol wawe wanafanyiwa allerg test,hivyo basi sioni mantiki yeyote ya huyu bwana kwenda mahakamani kwani hata pata kitu,ushauri mwingine ni kwamba arudi kwenye ile hospitali aombe jina au aina ya dawa hiyo ili akienda hos[itali nyingine yeyote awaambie kwamba ana allerg na dawa fulani,dawa sio ubuyu unakula tu bila kuangalia dozi na matatizo mengine.Pili ndugu zangu wabeba maboksi kukaa nje ya TZ sio kuwa ndio mnaakili kushinda wengine hata ulaya kuna wajinga na wapumbavu vilevile kwa hiyo issue zikitokea Tz msifanye watanzania hatuna akili ila nyie mnaobeba boksi ndio werevu!
    Nawasilisha!

    ReplyDelete
  13. huna mpango kama unagoma kuandika majina usingeandika habari yako humu, maana husaidii jamii wewe!

    ReplyDelete
  14. hahaha1! naona ametoa ushauri mzuri sana. Pole ndugu yetu kwa hali iliyokupata. Hii yote ni dalili za awali za ngoma. Allergy kwa madawa, ulimi kutetemeka na dalili zingine ulizozisikia. Ukiona hivyo tu wahi ukapime na ikionekana una maambukizi basi unaanzan kuishi kwa matumaini. Pole sana ndugu yetu na wala usijisumbue kwenda mahakamani kudai bilioni 100 utakuwa kama Mrema. Angalia kwanza afya yaok.
    Mdauzzzzzzzzzz

    ReplyDelete
  15. Mada hii imekuwa nzuri kidogo hivyo basi nami naomba nitoe maoni yangu:
    - Kwanza huyu jamaa kama ana nia ya kuwasaidia watanzania wenzake ni bora akaitaja hiyo hospitali ili watu wengine wachukue tahadhari wanapoenda kutibiwa hapo
    - Inawezekana huyu jamaa amepewa dawa za majaribio kwani kuna dawa nyingi kutoka india na china zinaingia kinyemele bila kupewa kibali na TFDA. Mara nyingi hizi dawa ni zile crude ambazo zimetengenezwa kwenye vidonge au aina nyingine
    - Naomba kuwatahadharisha wanaopenda kuagiza dawa kupitia internet kwani utafiti umeonyesha kuwa >40% ya dawa zinazouzwa kwa njia hii ni feki.
    - Pia anaesema kakimbia bongo kwa sababu ya watu kupewa dawa feki huyu bado ana mawazo ya kitumwa kwani dawa feki na makosa ya kitalam yapo hata kwenye nchi zilizoendelea
    - Mamlaka zinazohusika na bidhaa kutoka nje (siyo dawa pekee) inabidi ziwajibike kwani kuendekeza shurwa katika maeneo hayo ni kuleta maafa kwa raia na pia kuitia aibu nchi na usomi wetu kama wanataaluma

    ReplyDelete
  16. ANY ONE CAN HAVE AN ALLERGY REACTION,S/S RANGE FROM HIVES, SWELLINGS,BRONCHOSPASM, SOB,TOUNG SWELLING, FACIAL/MUSCLES TWITCHING ,,,,,and many more.NEXT TIME, NEED TO KNOW YOUR SIX RIGHTS. THE RIGHT PATIENT, MEDICINE, DOSE,TIME,ROUTE AND DOCUMENTATION. INFORM YOUR DR. FOR ANY KNOWN/SUSPECTED ALLEGY. YOUR DR IS RESPONSIBLE TO EXPLAIN SIDE EFFECT/BENEFITS OF YOUR MEDICINE.POLE SANA MPENDWA KTK BWANA

    ReplyDelete
  17. pole kwa kupewa madawa ya kujaribiwa bila kuarifiwa. kwa miaka mingi nchi za 1st world zimekua zikitumia watu wa 3rd world kama guinea pigs kwenye majaribio ya dawa zao mpya kabla ya kuzitumia kwa watu wao. hii ni kwasababu wanataka kwanza kuakikisha hizo dawahazina problem kwa watu wao. ninashangaa mtu kusema eti ukipata madhara na hizo dawa ni kwasababu una magonjwa mengine. alifanya wapi hiyo research na kwa watu wangapi. mara nyngi serikali au wahusika kwenye nchi masikini hukubali hayo majaribio za hizo dawa yafanyiwe watu wao kwasababu wanaogopa kukose misaada. wengine huongwa ili wakubaliane na hayo majaribio.

    ReplyDelete
  18. Na pingana na mdau aliesema bora sindano kuliko vidonge,nasomea unesi na moja katika disadvantage ya sindano ina fanya kazi haraka zaidi kuliko vidonge sasa angechomwa sindano si angeweza kuwa maiti hivi sasa ikiwa kama ana allergy au ni kweli dawa za majaribio tumeletewa sisi watanzania.

    ReplyDelete
  19. minaelewa jamaaa anavyoficha jina anaogopa kibao kinaweza mgeukia nyie simnajua nchi yetu hakuna haki mwenye hela ndo mwenye sheria.wachache ndo wenye ujasiri huo,na nyie mnaomshtumu hivo bila shaka mtakuwa ni wananchi wa ughaibuni ndomana kidogo mko free kwetu hamna hicho kitu unaweza fungwa wakati umeonewa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...