leo nimebahatika kugongana na mmoja wa wadau waandamizi wa globu ya jamii, dennis londa, anayepiga kitabu na boxi huko helsinki, finland.
Mdau Dennis alikuwa vekesheni bongo na mchana huu kapaa kurejea ughaibuni kuendeleza libeneke.
Huyu mdau pamoja na fide mtimkubwa walikuwa mashuhuda wakati globu ya jamii ilipokuwa leba ikizaliwa huko helsinki septemba 8, 2005 (bofya hapa) , chini ya maelekezo ya mkuu wa wadau, mkombozi na mwanzilishi wa globu za kiswahili kaka ndesanjo macha (bofya na hapa). Wote hawa pamoja na wengine kibao nawashukuru kwa ushauri wanaonipa katika kuendeleza libeneke. Ndesanjo, Mtimkubwa, Dennis Mbarikiwe!
nyuma yetu ni club billicanas ambayo baada ya ukarabati na ukarafati wa takriban mwaka mmoja, sasa iko katika hatua za nchani kabla ya kufunguliwa rasmi. redio mbao zimesema ilikuwa ifunguliwe kesho lakini hatua hiyo imesitishwa kwa sababu ambazo hazijaelezwa na kwamba sasa itafunguliwa januari 8, 2009.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. KUFUNGUA CLUB ALHAMISI! THATS ODD!!..

    ReplyDelete
  2. Oya Denis Londo inakuwaje mdau wako nipo Dallas-Texas hapa, nipe issue tangu Jitegemee kwa Masawe naona jii. Poa mpe Hi Kirita ukikutananaye hapo Ma-Finlii.....!

    ReplyDelete
  3. Duh..ebwana bills ina mvuta mzuri kwa nje..natumaini na ndani mambo yatakuwa makubwa.


    Michu nimependa hiyo stahili ya kuweka mkono mfukoni nafikiri inaitwa "mfukozi"..aaa aa

    ReplyDelete
  4. inapendeza,sasa nimefahamu kwa nini hupost maoni yanayowaponda walionje ya nchi au kushawishi utanzania zaidi kuliko kuendekeza uzungu,blog ilizaliwa huku.ka michuzi mi nipo denmark lakini nasisitiza uzalendo.
    Pia hongera kwa kutozeeka.kwani tangu miaka hiyo hadi leo bado wafanana vilevile,mafikiri unakula vizuri,unalala vizuri na unzshiriki mazoezi,HONGERA,

    ReplyDelete
  5. sante kutujulisha maendeleo ya billicana, sasa tunaomba utujulishe maendeleo ya Forodhani, mlitujulisha mwezi wa kumi itakuwa tayari wameshafanyia ukarabati auuuu!! Plse tujulishe maana tunataka tukienda huko tuhiji hapo maana kwenda zenjy bila kipita Foro abaaa! bado huja enjoy sawasawa utamaduni wa wazenjibari alooo!

    ReplyDelete
  6. kaka mambo vipi
    aisee kumbe upo bongo mzee londo
    salaam sasa

    ReplyDelete
  7. We Ndau wa Tarehe December 31, 2008 4:08 AM, Get your life man, kama mzalendo pekeyako, hukumleta mtu ulaya huku wala hutujui hatukujui, hutulipii bili wala hutusaidii kulisha nyumbani, unaacha kutuambia tuswali tuingie peponi unatuambia upuuzi gai sijui... sio kazi yako kuomba na kubembeleza watu warudi kwao, kwani we baba yao mzazi??
    Ebo....wee vipi .. michu usibanie mshamba huyu apate vidonge vyake..



    Mdau Ulaya

    ReplyDelete
  8. Duu!Mr. Misifa akiwa bongo blog zote lazima zimtangaze!Vipi bado yupo na ushabibiki wa Mch. Mtikila na SIASA ZA MAJI TAKA au?Mnafiki mkubwa!

    ReplyDelete
  9. Duu!Tambi la ufagio! Someni lugha za watu na kutafuta kazi za heshima!Mzee una miaka zaidi ya saba Ufini!

    ReplyDelete
  10. Karibu tena Denis tulifurahi kuwa na wewe hapa Moshi. Wasalimie wote huko

    ReplyDelete
  11. Babu piga life kwa kwenda mbele, achana na hao wazushi wanaoishia social, kutwa hawaishi kushinda kwenye internet kuponda wenzao. Watakufa na vijiba vya rohoo. Haoo wakubwa wazima roho mbaya tu.

    ReplyDelete
  12. Londo tumekuona mjomba. Michuzi huyo jamaa kashaacha Ice Hockey long time, sasa hivi anapiga kazi yenye akili huku. Kwa kifupi jamaa ni mmoja vijana wachache wa mifano ya kuigwa hapa Ufini, huyo anony wa juu ana lake jambo na huyu kijana, kwa kifupi hapa loosers wapo wengi na kwa kuwa wanashindwa kusolve life problems zao, huwa wanaishia kutoa flustrations za maisha yao kwa vijana innocent kama kijana wetu huyu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...