Mkurugenzi Mkuu wa Zain Tanzania, Khaled Muhtadi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kumpata mshindi wa gari aina ya Toyota Land Cruiser wa promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain Tanzania, Msusa Jaffar wa Tegeta, jijini Dar es Salaam jana (Desemba 31, 2008). Kushoto ni mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain Tanzania Limited leo imemchagua, Msusa Jaffar Msusa mwenye umri wa miaka 32, aliyebahatika kuibuka mshindi wa zawadi ya gari jipya aina la Toyota Land Cruiser jijini Dar es Salaam.

Msusa, mkazi wa Tegeta, Dar es Salaam ambaye ni fundi umeme, aliibuka mshindi katika bahati nasibu iliyochezeshwa Dar es Salaam leo kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski. Ameibuka mshindi wa zawadi kubwa kabisa kwenye promosheni ya Endesha Ndoto 2, akiwa ni mshindi wa 11 kunyakua gari, baada ya wengine 10 kuibuka na magari aina ya Toyota RAV 4 yaliyotolewa na Zain kuanzia Januari 2008.

Zain Tanzania ilitangaza kutoa jumla ya magari 11 katika promosheni yake kubwa kuliko zote ya Endesha Ndoto 2. Pamoja na magari hayo mapya kabisa Zain Tanzania pia imewawezesha wateja wake kujishindia muda wa maongezi na fedha taslimu na kwa wale ambao waliweza kujikusanyia pointi, pia wameweza kushinda simu, ipod na zawadi nyingine nyingi.

“Kama mnavyofahamu Zain Tanzania imekuwa ikiendeleza jitihada zake za kubadilisha maisha ya wateja wake kwa kuwazawadia magari mapya kutoka Toyota Tanzania yakiwa yamesajiliwa kwa jina la mshindi na kulipiwa ushuru na bima zote husika.

“Promosheni ya Endesha Ndoto 2 ya Zain kwa mwaka 2008 imefikia tamati leo, tumekabidhi magari 11 mapya kwa Watanzania waliobahatika kuingia na kujishindia zawadi mbalimbali likiwemo gari jipya la kifahari aina ya Toyota Land Cruizer.

Leo tumemchagua mshindi wa 11 aliyejinyakulia gari hilo la kifahari,” alisema Khaled Muhtadi, Mkurugenzi Mkuu wa Zain Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. JANA TAREHE MOSI JANUARI 2009 NILONA TANGAZO LA ZAIN KUHUSU SARAKASI NA MAZINGAOMBWE (YANAYO)FANYIKA MSASANI NA YATAISHA TAREHE 31 DESEMBA 2008. NI WIZI MTUPU. KUDAI MALIPO KWA KUTANGAZA KITU KILICHOPITWA NA WAKATI NI WIZI MTUPU. ZAIN MSIWALIPE HAO WANAOENDELEA KUTANGAZA TAMASHA LENU KWANI NI WIZI MTUPU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...