bango
ubwabwa
nyama rosti
andazi
kwa ndani

chiken
pametulia tuliiiii
pasafi ile mbaya
bufee

Ndugu Muhidin Issa Michuzi,

Salamu toka Kijiweni Restaurant.

Tunapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha waTanzania wote kwenye Restaurant ya Kitanzania hapa jijini Dallas, Texas.

Maanjumati ya aina mbali mbali ya Kitanzania na ya Afrika Mashariki yanapatikana hapa kwa bei chee.

Wote mnakaribishwa.
Management,
Kijiweni Swahili Restaurant

125 SOUTH CENTRAL EXPRESSWAY RICHARDSON,
TX 75080
PHONE #S: 972-836-2282
972-310-9701
214-709-4423

HOURS: MON-FRI. 11.00 a.m. - 10.00 p.m.
Weekends: 8.00 a.m. - 11.00 p.m.
KARIBUNI WADAU TUJICHANE KWA MISOSI YA HOMU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. hongera jamani kina rose,sheila,zainabu,habiba,edda, june na wengine Restaurant imetulia haya basi naona hakuna mteja mbona mimi ninatafuta part time job huko dallas simtanipatia jamani.

    ReplyDelete
  2. michuzi na wewe bwana eti chiken ni kicheni au umeona andazi akili imekuruka kidogo, heeeeeee

    ReplyDelete
  3. HONGERA SANA MFANO WA "KUIGWA"

    ReplyDelete
  4. Nimefurahi kusikia kuwa mmefungua Kijiweni-I hope mtafanikiwa sana na biashara yenu na tena nitakuja kuwa support as soon as possible.

    ReplyDelete
  5. imetulia sana hiyo..namissi sana vyakula vya home..mtaniona soon

    ReplyDelete
  6. HÄ°LO NÄ° WAZO ZURÄ° NATAMANÄ° KATÄ°KA NCHÄ° NYÄ°NGÄ°NE Ä°NGEKUWA KAMA HÄ°VÄ°

    ReplyDelete
  7. Evarist Mwakasula hongera sana kwa kufanya mambo haya Mungu akuzidishie na akufanikishe zaidi na zaidi Big up Brother!!

    ReplyDelete
  8. wakuu nikishuka huko south south lazima niwatembelee maana mimate hapa yanidondoka,ushauri wa bure naomba usafi na quality ya msosi viwe number one bila hivyo mtafunga virago mapema...napenda kuona homeboys mkifanikiwa,narudia tena usafi usafi usafi sana sana bathroom...nimeongea kama mtu ninayeelewa hiyo industry kwa saaaaana,good lucky na msituangushe!

    ReplyDelete
  9. wabongo wa dallas mi nawapa hongera sana,i wish we have one like that here in washington dc,huo ni mfano wa kuigwa naamini watanzania watawapa support ya nguvu.

    ReplyDelete
  10. Hongera sana what an accomplishement!!!!!!
    At least mtaajiri wabongo wakiingia tu mjini...Tuliajiriwa na wahindi na wajewish tulipoingia tu huku.....saa hivi ni raha kuona mbongo naye kafanya mavitu yake
    MUNGU AWABARIKI

    ReplyDelete
  11. YAANI WEWE ACHA TU HAPO NDOO MAHALI PA KUWEPO.LAZIMA NISHUKE HAPO TX KIDOGO NIPATE JIBWABWA LA NYUMBANI
    MBOLLO FEZA
    KOLUMBUSI
    OHIO

    ReplyDelete
  12. HONGERA TENA SANA SANA...NI MFANO KWELI WA KUIGWA...MIMI NITAMAKE A SPECIAL VISIT SIYO KAMA NAMISS VYAKULA VYA HOME ILA KUWASUPPORT WATZ WENZANGU JAMANI TUUUNGANIKE KUMSUPPORT HUYU MDAU WATU WA TX NA MIJI MINGINE MAMBO YA KILA SIKU KULA KWA WACHINA (WAHOOHIO) NA WAMAREKANI TUYAACHE IT'S TIME TO SUPPORT OUR OWN ROOTS...

    ReplyDelete
  13. Big up, Dallas! So I guess the saying that everything is big in Texas is proving to be correct!

    Hopefully mtajaribu kuweka vitu fulanifulani vya kiTanzania such as Chai na Kahawa, korosho etc.

    Dallas, making Tanzania proud!

    ReplyDelete
  14. Pametulia.. hongera sana

    ReplyDelete
  15. ....eeehe bwana eehe!!msisahau wali wa nazi,maharahage ya nazi,njegere za nazi,bamia,misumari aka anchovy aka dagaa ,ugali na n.k lazima nishuke dirty south kUwapa support mdau hapa JERSEY CITY.tumechoka kupigwa bao na wakenya hapa state.

    ReplyDelete
  16. Hii ingekuwa bongo mambo yangeenda mswano. Hapo bongo hakuna self-service katika migahawa.
    m3

    ReplyDelete
  17. Safi sana hii. Natumaini huu mfano utaigwa katika miji mingine yenye wabongo wengi.

    ReplyDelete
  18. big up guyz. mnaweza omba ushauri wa customer service kwa mzee gado 79 london road. juu huwa anatufikisha saana. kuanzia ksport channels, fruit shoot kwa watoto, pool table, red wine ugali amarula, na promotion za hapa na pale like happy hour juu wabeba box huwa wanaanza kutoka out kunzia saa tano usiku. unless kuna mpira or... kama nilivosema mtafuteni mzee gado atawapa marizi yote ya kuvuta wateja.chooni usiajiri safisha mwenyewe. ndo siri ya mgahawa good luck guyz

    ReplyDelete
  19. ndugu zangu mnakumbuka ile story ya "cat cat cat" sasa mleta habari za hapa anatupa nyengine chiken badala ya kitchen. safi sana!

    ReplyDelete
  20. Dah!mi nataka ugali na matembeleee vipo hivyooo.

    ReplyDelete
  21. uji jamani upo

    ReplyDelete
  22. Safi sana, pametulia mwanangu, je? kuna ugali, ngogwe na bamia la kupwaza. Nitatia timu washikaji.

    ReplyDelete
  23. Kijiweni big up sana kama wadau waliopita naomba tuwasupport sana hawa kijiweni waweze endelea hasa kwa sasa kwani ndio kwanza wamefungua hii sehemu Pls let surpport our brothers & sisters

    ReplyDelete
  24. hongera sana.

    ReplyDelete
  25. we anony wa saa10:02 unanishangaza
    kwani uko bongo ipi jamani mbona sasa bongo mambo tambarare hebu nenda hapo nyumba ya sanaa au we ndo wale wabeba mabox mlio bobea huko tangu mtoke huku nineteen kweusi unafikiri bado tuko nyuma masehemu kibao kwa kwenda mbele hebu rudi home . na kama uko dar hebu uwe mtokaji during week ends ujionee mwe . no hard feelings

    ReplyDelete
  26. wewe cynthia hao kina rose zainabu eda n.k hawaishi dallas wako houston, usidakiye issue za watu kama hujui

    ReplyDelete
  27. Congratulations!! Sasa basi Waswahili lets make sure tunawasupport wenzetu kwa kwenda na kujichana kwa nguvu. Hope business is good and wishing you luck and much success.

    Akilimali.

    ReplyDelete
  28. Hongera! Umeleta nyumbani karibu.Tutakuja kula nyma ya ku Choma! Ashante.

    Noman Kassam,
    Lewisville, Texas

    ReplyDelete
  29. Hingereni sana na nawatakia kila la heri

    swali moja-nyama munazotumia ni za halali ama za inakuwaje?

    Ambassador

    ReplyDelete
  30. IMETULIA LAKINI UGALI WA MUHOGO NA MCHUNGA UPO PIA MSISAHU KUTUWEKEA MLENDA NA NGURU/PAPA MKAVU NA MAJI YA MADAFU, MIE NAOMBENI TENDA YA KUTENGENEZA TOGWA!!!

    ReplyDelete
  31. Hii ipo shwari si utani.Na inasaidia si tu kwa sisi sote tuliopo maeneo ya karibu (kwa Obama), bali pia kuitangaza nchi yetu kwa vyakula vyetu asilia!!!. Lazima nishuke hapo walau kwa andazi na chapati fulani za kaharage kanazi.
    Juzi tu nilikua hapo DFW nikisubiria connection yangu nikaona tangazo la tourism in Tanzania, nilifurahi sana, hapo nilishaliona kama hilo pia kwenye TV.
    Usikonde mdau, utapata wateja kwani mambo ni polepole tuu.
    Tena ukiweza jitangaze kwenye vijitabu fulani vya mji wa Dallas kwa wageni wote.
    Na ushauri wa bure ndo huu: hapo chini ya Swahili Restaurant Ongezea An East African or Tanzanian Flavor"
    kama ndo moto of your business!!!

    ReplyDelete
  32. Mambo yako safi sana ndani ya Kijiweni. Sisi wakazi wa Dallas twanufaika na Menu hatari kweli kweli. Jana tuu nilitapa pilau kubwa lenye nyama kibao, ndizi za kupikwa, wali wa nazi & nyama rojo, mchicha na mihogo ya kukaanga (chips dume) bila kusahau chachandu. Yote hayo kwa $7 tuu. Hata Mc Donald's Menu got notin' on Kijiweni. Kula kubwa hadi nikasaza. Chapati na maandazi yametulia tuliiiiii. The ONLY challenge I have to all wabongo Dallas na maeneo ya karibu, please tujitokeza kuwasupport wenzetu basi ili nasi tuwe na kitu cha kujivunia. Cha ajabu ni kwamba Wakenya, Waburundi, Wazaire, na Waganda wanatuzidi kwa mahudhurio Kijiweni. Go support mtu wetu wa nyumbani people!

    Merry Christmas and a joyful 2009 to all.

    ReplyDelete
  33. Nimefurahi sana kuona watanzania nasi tuna restaurant yetu.Kila nikipata kideti,nilikuwa nikielekea Ethiopian Restaurant badala ya kwetu Tanzania.Niko mbali na Texas,lakini nitatembelea kwa kupata msosi wa nyumbani sio burgerKing kila wakati.Ongeleeni saaana waanzilishi.Mimi nawa-support asilimia mia moja.
    Chakubanga

    ReplyDelete
  34. Mungu akupeni mafanikio mazuri lakini muandishi kuna kosa na uandikaji katika sehemu moja ya chakula ANDAZI NI MOJA yakiwa mwengi Huitwa MANDAZI huwa sio andazi tena tusaidiane lugha kubwa hii
    By yunus

    ReplyDelete
  35. Hii ni nzuri sana nawapongeza hao watanzania wa Dallas, wengine wafuate huo mfano.Watanzania tuachane na dhana ya kwenda Ulaya au Marekani kutafuta kazi tuende tukaanzishe kazi na kuajiri wengine, namna hiyo tutafanikiwa sana!
    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...