Hi! Kaka Michuzi,
Wakati Dar mnasherehekea sikuu ya xmas kwa kulikabili joto wadau wako tulioko Harbin Uchina tuliamua kushehereka kwa kuutembelea mji wa muda hapa kasikazini mashariki mwa China katika mji wenye baridi sana wa Harbin ambako wameandaa mji wa muda ambao umetengenezwa kwa barafu. Inategemewa huu mji kuishi kwa miezi kama mitatu tu hivi. Kaka wakati sie tunaandaa SABASABA kwa ajili ya maonyesho wenzetu wakati wao unapofika hujenga nyumba na kutengeza mitaa mingi na mizuri yenye urembo wa kila aina kwa kutumia maji (barafu/ice). Mlango wa kuingia msikitini

Waweza kuona wanavyotengeza nguzo na hiyo arch kwa barafu


Wazee wa feki hupendelea sana decorations na hiyo ilikutwa kwenye mtaa wa barafu.

Mjengo huo ni maji (ice) tu hapo


















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Naomba nianze kwa kuwapongeza kwanza wadau wachina, na wengineo ambao mara kadhaa wamekuwa wakituekea kwenye blog hii picha mbali mbali za mambo ama matukio ya kuajabisha yanayofanywa na binaadam wenzetu katika pande mbalimbali za dunia.
    Isipokuwa tu ningewaomba watanzania wenzangu tulioko nyumbani na ughaibuni tuwe washangaaji makini zaidi kuliko tulivyo sasa, nafikiri ili kufikia hapo tunatakiwa tushangae means not end result. Mengi ya tunayoonesha hayahitaji superman kuyafanya na mara kadhaa huwa si technology ambayo labda kwetu haipo; dunia ni kijiji sasa. Lakini kama utafikiri sana tunachokosa ni dedicated and committed individuals in our nation. Ili kuweza nasi kupata kama au zaidi ya hivyo tunavyopita na kushangaa. Hivi tuulizane kwanini mpaka leo mmoja wetu anapochaguliwa nafasi ya juu katika serikali neno la mwanzo tunalosema au kufikiri ni "sasa amepata ulaji" yaani katika majukumu yote yanayohusiana na cheo hicho tunachokiona sisi ni ulaji tu!!! Kwa kadri akili zetu zimeelemea zaidi kwenye ulaji basi tusitegemee any commitment or dedication tutayokuwa nayo kwenye nafasi mbali mbali za kijamii na kiserikali tunazopewa kwenye taifa letu. Na hii hasa ndio tofauti kubwa ya sisi na wao, kwa sababu chukua mfano wa huo mji wa barafu ulionyeshwa hapo na wadau, unaweza kukisia ni bilioni ngapi ya shilingi zinahitajika kufanya kitu kama hicho? Tujaalie tunazohizo pesa, unadhani tutaujenga mji kama huo ikiwa kuanzia project manager mpaka chini na walioko juu yake wote wanachojali ni "ulaji" badala ya kuona fahari kwamba project muhimu kama hiyo anaiongoza na kuifanikisha kama ilivyopangwa. Kwa hiyo watanzania wenzangu popote mlipo let us from now on not surprised by the result but by the means, tujiulize hivi ni kitu gani hasa ambacho kimemfanya let say huyo project manager wa kichina kuhakikisha kwamba project yake hiyo inakamilika kwa mafanikio wakati kwetu sisi ni bahati nasibu? hawa wenzetu all over the world wanaamini nini mpaka ikawa wanapoendesha project muhimu kama hizi hawashindani kuiba wakati sisi ndio tunaloonea fahari kufanya.
    Once we manage to imulate them in this respect we shall stop all together going around and suprised with their results since now we know the means.

    ReplyDelete
  2. duh! wachina kweli nuksi

    ReplyDelete
  3. Ahh...lakini sasa mkiganda je?

    ReplyDelete
  4. Mh.Balozi
    Mie nilikuwa nasikia usemi 'Tofali la Barafu' halijengi nyumba!

    Kumbe usemi huu ni kweli kwa TZ lakini si kweli kwa Greenland na hata huko kaskazini ya Uchina.

    Soma: lisemwalo ulaya au sehemu nyingine ya dunia sio lazima liwe kweli kwetu mfano 'Tanzania ni nchi ''masikini' kama vile hatuna ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora'.

    ReplyDelete
  5. Acheni kutuzuga! Hata kama kwetu kuna joto kama la jehanamu hapo mnatudanganya!! Europe kwenyewe kuna baridi la kufa mtu na technologia ya juu bado hawajatengeneza hizo nyumba za barafu!! UONGO MTUPUUUUU!!!!!

    ReplyDelete
  6. khe wadau wachina mmechoka utadhani mmetoka usambaani kule lushoto.
    watanzania jitaidini kwa pamba mnaniangusha.
    mwanamitindo

    ReplyDelete
  7. Mdau uliotoa comment wa kwanza nakupa tano. Ulichoelezea kuhusu ulaji ni kweli kabisa. Watu kufikiria matumbo yao na kupata hele za chap chap(short cut) ndo kinacho ua nchi hii. Bila kusort out this mentality we bound to fail as a nation.

    Mdau wa Nkwenda
    RAF

    ReplyDelete
  8. wewe unayesema ni uongo hakuna nyumba za barafu europe, fanya research yako vizuri. zipo kibao russia, sweden, finland n.k.

    ReplyDelete
  9. Wadau tayari tu kwa jinsi tunavyo changia comments unaona tu tayari ambavyo wachache wetu wanapungua jinsia ya kufikiri anonimosu mwana mitindo hapo juu badala ya kuongelea jinsi ya nasi tufanye nini unaongelea kuwa wadau wa china hawajapiga pamba ulitaka wavae suti kwenye hilo baridi!
    Naona unahitaji kufungua macho na kuachana na udosi. Tuko hapa Tz nasi tuangalie jinsi ya kuyatumia mawe ya mkoa wa mwanza sio kuangalia wadau wa uchina kuwa hawajavaa suti. Kwani wako huko kwa kujua wanachokifanya ndo maana wameshirikiane nasi kwa hayo wanayokutana nayo.

    ReplyDelete
  10. maendeleo gani bwana.maendeleo kaongelee bungeni,or maendeleo yanafanywa na citizens wenyewe.then who told u kuwa kupiga suit ni pamba?kupiga suit co pamba bwana
    acha ushamba anonymous uliepost on the 30/12/2008

    ReplyDelete
  11. unaesema uongo mtupu tembea uone. Zipo hizo ila season house na watu wanakwenda kulala huko kama vile hotel. na kuna watu walishafungia ndoa yao kwenye one of these lakini ilikua Canada

    ReplyDelete
  12. Nyie mna hatari sana. natembelea kaburi? Barafu ukiyeyuka mko nayo

    ReplyDelete
  13. Maonyesho makubwa kwa hapa Marekani yapo Minnesota lakini kwa wale walio Texas nenda Dallas (The Gaylord Texan).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...