Kikosi cha kwanza KCSC
Kikosi cha pili KCSC
Uongozi na Wachezaji wa Kijitonyama Chipukizi Sports Centre unatoa shukurani kwa wadau wote wa michezo hususani mpira wa miguu kwa misaada ya hali na mali waliyotupatia katika mwaka huu wa 2008 unaomalizika leo.
Tunapenda kuwataja wafuatao:-
Wakazi wa Kijitonyama,Uongozi wa Shule ya Msingi Kijitonyama,Uongozi wa Kata ya Kijitonyama,Uongozi wa Kifa,Uongozi wa Kidiyosa, Mh.Iddi Azzan Mbunge wa Kinondoni, Mwenyekiti serikali ya mtaa Bwawani, na Balozi Issa Michuzi(blogu ya jamii).
Wengine ni Bw. Prince Tumaini wa Bongosoccer,Bw F.Mressa wa CRDB, Sheikh Issa Kamtande,bw,J.Makongo(Mlezi wa KCSC). Bw Esmail Mwenda Mwenyekiti wa CCM Vijana Kata ya Kijitonyama, Bw Hussein Sapi,Bw Kaijage waTanzania soccer academy, Uongozi wa Mwiba F.C .

MAFANIKIO YA KCSC KWA MWAKA 2008.
Timu A(U-17) imetwaa mataji mawili yaani Kombe la Sinza 2008,Kombe La Upendo Na hatua ya nusu fainali kombe la Copa CocaCola Ngazi ya Wilaya.Hatua Nusu Fainali Kombe La Pasaka.
Timu B (U-14)Ubingwa wa Kombe La Idd 2008
MALENGO YA KCSC KWA MWAKA 2009.
Kijitonyama Chipukizi tunatarajia kushiriki ligi mbalimbali mpira wa miguu ngazi ya kata na wilaya kwa timu zote mbili yaani timu A na Timu B na ifikapo mwezi wa Oktoba, Timu A itaingia kwa mara ya kwanza katika ligi ya TFF ikiwa na lengo la kuuza wachezaji kwa timu kubwa, kuendelea kutafuta wadhamini mbalimbali wa vifaa vya michezo.

Pia kutafuta wadhamini watakaotudhamini katika ushiriki wa ligi mbalimbali tulizozitaja hasa kwa mfano gharama za ,chakula,maji ya kunywa,usafiri wa kwenda na kurudi katika mechi,posho za wachezaji na viongozi N.k .

Kuwa karibu na Timu kubwa kwa kucheza mechi za Kirafiki na timu zao za kikosi cha pili na kupata ushauri mbali utakaotolewa na Walimu wa timu hizo.
Kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na wakala wanaotafuta wachezaji ndani na nje ya nchi.
Ni matarajio yetu kuwa mtazidi kutuunga mkono katika kukuza vipaji
Tunawatakia kila la Heri ya Mwaka Mpya wa 2009
CHRIS FIDELIS
kny KCSC


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...