Ndugu watanzania wenzangu,

Natumaini wote tunaendelea vema na maandalizi ya mkutano wetu. Kwa niaba ya kamati ya maandalizi nawashukuru kwa ushirikiano wenu mpaka sasa.
Nachukua nafasi hii kuwapa taarifa kuhusu taratibu mbalimbali zinazohusiana na mkutano wetu.

Kama tulivyowaarifu hapo awali tunatarajia wajumbe wote kuwepo Chennai kufikia tarehe 24.

Maandalizi ya tafrija yetu ya krismasi yapo mbioni kukamilika. Napenda kuwataarifu kuwa tutakuwa na ibada ya krismasi tarehe 25 saa 3 (tatu)asubuhi itakayofanyika:
AICUF,
Sterling Road 52,
Nungambakkam,
Chennai 34.
Tutajumumuika baada ya hapo kwa ajili ya sherehe yetu itakayofanyika
Plot no 98,
3rd Main road,
ayyavoo nagar,
Maduravoyal.

Mkutano wetu wa tarehe 26 unatarajwa kuanza saa 3(tatu) asubuhi. Mkutano huu utafanyika
Loyola Institute of Frontier Energy Conference Hall,
Loyola College,
Sterling Road,
Nungambakkam,
Chennai 34.

Tunatarajia kuwa na uchaguzi katika mkutano wetu mkuu wa kwanza. Nawasihi nyote kujitolea kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye jumuiya yetu siku hiyo.
Kutokana na kwamba hatujapitisha katiba mpaka hivi sasa ni vigumu kuwaomba muwasilishe maombi ya kuwania nafasi mbalimbali. Hatahivyo tujiandae kwani fomu za kugombea nafasi mbali mbali zitatolewa siku ya mkutano mkuu baada ya kupitishwa kwa katiba yetu itakayoainisha nafasi za uongozi zitakazokuwepo.

Tafadhali tazameni viambatanisho vya ratiba na muswada wa katiba kwa ajili ya mapitio yenu kabla ya mkutano. Ni imani yangu kwamba tumekuwa tukiujadili muswada huu kwa kipindi cha takribani miezi miwili sasa. Tutapata nafasi ya kutoa mapendekezo kutoka kila mji na watu binafsi wakati wa mkutano.

Ili kuweza kushiriki mkutano huu kikamilifu unaombwa kuhakikisha unatimiza yafuatayo
:wasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na usajili kuhakikisha anacho kitambulisho chako hakikisha unajaza fomu ya uanachama iliyotumwa kupitia barua pepe kwenye ujumbe wa taarifa ya mkutano huu
:hakikisha unabeba picha ya saizi ya pasipoti kwa ajili ya kutengeneza kitambulisho chako cha kudumu
:hakikisha unakuja na ada yako ya ushiriki kama bado haujaiwasilishanaombwa kubeba risiti ya benki kama uliwasilisha ada hiyo kupitia akaunti uliyopewaunaombwa kuja na nakala ya kibali cha ukazi(resident permit) na viza yako kama hukuviambatanisha kwenye barua pepe hapo awali
Mkutano wetu utafatiwa na chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshima ya nchi yetu.
Tutajumuika kwa ajili ya chakula hicho saa 1(moja) jioni katika hoteli ya Aruna, Sterling Road, Nungambakkam, Chennai 34.

Kwa ndugu zetu mtakaoshindwa kushiriki nasi ni imani yetu kwamba tupo pamoja. Tunaahidi kuendelea kufanya mawasiliano yanayohitajika wakati na baada ya mkutano ili kuhakikisha tuna ushiriki sawa.
Nawasihi nanyi muhakikishe mnafanya mawasiliano tuliyowaomba muyafanye.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia:
+91 984 01 23 784
au
+91 984 05 43 985

Nawatakia wote maandalizi mema na natazamia ushirikiano wenu zaidi.
Mungu awabariki.
Karibuni sana tujumuike.

Wenu katika ujenzi wa Junmuiya yetu,
Amonson Asseri,
Mwenyekiti,
Kamati ya Muda,
Jumuiya ya watanzania
Tamil Nadu,
Tawi la Chennai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Michuzi asante sana kwa hizi habari please tu update watakuwa wapi na lini ili tuende kuwaona

    Mdau Slough uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...