Arnold Chiwalala mwanamuziki/mwalimu wa Kitanzania (katikati, akiwa na watunukwa wenzie) anayechukua Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu Cha Muziki Cha Sibelius (Sibelius Academy) ametunukiwa Tuzo ya Dhahabu ya muziki wa Ala ya Kantele 2008. Kantele ni ala ya kiasili ya Finland.
Tuzo hii hutolewa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni ya Finland kwa mwanamuziki bora ambaye amechangia katika utunzi(composition) na uendelezaji (promotion) wa ala ya Kantele ndani na nje ya Finland.

Arnold Chiwalala ni muhitimu na mwalimu kutokea Chuo cha Sanaa Bagamoyo. Vile vile ni mwanamuziki, mtunzi, muandishi wa nyimbo na mbunifu wa miondoko (choreographer).
Kazi za Mwalimu Chiwalala zinatambulika kimataifa ambapo ameshiriki katika warsha, matamasha na makongamano sehemu mbali mbali ulimwenguni ikiwemo Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Uingereza, Ujerumani, Marekani, Urusi, Norway, Denmark,Sweden,Finland, Estonia na Yugoslavia.
Mpe pongezi Arnold Chiwalala kupitia email:
ama Simu
+358405290622
tuzo aliyopewa Arnold Chiwalala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hongera kwa tuzo hilo

    Naomba kuuliza shahada ya uzamifu ndio nini?

    ReplyDelete
  2. hakika ni faraja kuona kazi za mwalimu chiwalala zina tambulika na kuheshimika.

    Nakumbuka pia ni chuo hicho hicho ndio kilimpatia "nondo ya heshima" marehemu ZAWOSE.

    Tuna kila sababu ya kujifunza nyumbani kuthamini na kutambua mchango wa wadau kutoka sekta mbalimbali.

    hongera sana mwalimu CHIWALALA..

    ReplyDelete
  3. Big thumb teacher!!

    ReplyDelete
  4. Hongera sana mwalimu lakini kitendo cha kupewa tuzo kwa kubobea ktk ala za miziki ya nje na siyo ya tanzania huoni kwamba utamaduni wetu utakufa wakati tamaduni za wenzetu zinasonga mbele? Huoni kwamba tunashiriki kutambulisha tamaduni za wenzetu wakati zetu zinakufa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...