Habari za leo wadau, 'Amakuru yuno munsi'
Mh.Balozi wa Zain mtandao usiopatikana huku Rwanda (Kigali) na mkuu wa wilaya ya nani hii. Najua kipindi kile ulikua huku ulitunyima baadhi ya taswira muhimu ambazo watanzania wanazijua ila tu kwa wale wapenzi wa sinema.

Nakuletea picha za Hotel Des Mille Collines (Hotel Rwanda) kama wengi wajuavyo kutoka katika ile muvi, nilikua huku mdau mwenzenu kuhudhuria Tamasha la Pili la Filamu huku Rwanda (Amani Great Lakes Film Festival) ambalo linamalizika leo.

Katika muvi ya Hotel Rwanda watu wanaweza wakaamini kuwa filamu hiyo imefanywa hapa ila ukweli ni kuwa wajamaa (Wamarekani) walikataliwa kuifanya hapa na hivyo walipiga picha hotel na wakaifanyia muvi hiyo Marekani kwahiyo kila kitu katika muvi hiyo ni cha kutengeneza na hotel ndio hiyo katika taswira hizo. Pia ni ukweli vitu vizungumziwavyo katika muvi hiyo juu ya hotel hiyo vilitokea kweli kabisa.

Hoteli hiyo kwa nje
Pia picha nyingine inaonesha tulipokuwa katika mkutano na vijana wanaochipukia katika sanaa ya filamu kutoka Afrika Mashariki na Kati, Kwa mbali kushoto utamuona mwanamke (Karole Karemera) ambaye amecheza kama muhusika mkuu wa kike katika muvi ya 'Sometimes in April' ambayo kila kitu kimefanyika Rwanda.

Wadau wa filamu hapo Bongo nadhani mtaanza kuamka na kufanya mikutano ya maana kwa wadau na washika dau wa filamu nchini ili kuwasaidia wale wanaochipukia na pia kuelimishana juu ya kiwanda kizima cha filamu na sio kukalia mimi flani nimefanya kitu flani, wengine tunawaona tu ila tunaamini hamjui mfanyacho.

Naomba kuwasilisha Mh.Balozi (Usiyekuwa recharble Kigali, Rwanda)


Mdau Dean
Kigali





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Movie yote haikufanyika rwanda,ila umechemsha ,walishutia south africa sio USA.

    ReplyDelete
  2. Huyu Mdau usianze sasa. Hotel Rwanda ni movie nzuri jamaa katowa hadithi yake yakuwa kilicho tokea si kwamba ni Producer wa movie sio ni katowa hadithi ya kweli Hollywood wamefatilia wameiigiza. ambayo hotel iliyotumiwa ni South Africa. ila ya ukweli Hotel Rwanda Ndio hiyo. sasa kuanza kusema nani kafanya hivi na vile wewe ndio unaanzisha majungu ndugu yangu baada kuwapa moyo. ni kitu kwamba kingetokea TAnzania na mtu angefanya Hotel Arusha basi ingekuwa tu kama hotel Rwanda ila TAnzania hakujatokea balaa hilo na tunaomba mungu kusitokee si tanzania tu dunia yoyote tuna shukuru Rwanda yameisha. kama unawapa Kina Kanumba ushauri wape ushauri mzuri si hapo hapo unatia majungu Ndugu yangu wa RWanda tumewatunza hapa TAnzania wa Rwanda wengi kwa Upole wetu sasa tunawaomba mtuheshimu basi sijawahi hata kuwasikia mkitushukuru Plzzzzzzzzzzzzzzz. from Ndosi.

    ReplyDelete
  3. Asilimia Kubwa katika Movie za RWanda mtazokuja kuona ni kuhusu Matatizo yaliotokea Rwanda. Rwanda wakifanya movie hizo ndio watu nje watatizama yaliyowakuta hiyo movie Somtimes in Rwanda na uhakika itahusu kuhusu wakati ule wa Vita, ndomana itawafanya watu nje watizame ila sizani kama itakuwa movie tu ya kuhusu nje ya matatizo ya vita ilivyokuwa si mtaona. nikama kuandika kitabu sasa Tanzania haiwezekani Rwanda Vita ndio imeiweka kwenye Map kuna anayenikatalia hapa? ila na wasifu kitu kimoja toka vita imepata elimu ya juu sana na watu wameamka vizuri sana. Nigeria wapo mbele ki movie ila haziwezi kuwa kwenye Market ya nje sababu ni movie za kawaida pia kama Tanzania, Ndomana nasema Rwanda Movie zao sababu Ya Vita tizama South Africa zile movie za Freedom Kuhusu mandela au watu wanakufa ndio zilikuwa zikisifika zamani sasa hivi wapi zaidi ya Totsi na Totsi Diractor Mmarekani. kama Hotel Rwanda. sasa sijui chini ya Sometimes April inasaidiwa na nani? tufanye wa Africa wenyewe tuone.

    ReplyDelete
  4. Nakereka sana na mijitu isiyofuatilia vitu halafu ikajifanya inajua. Movie ya Hotel Rwanda ilifanyiwa Afrika Kusini, usifikiri kwa kuwa muigizaji mkuu alikuwa Mmarekani, basi walifanyia Marekani. Tumia akili ya kawaida tu, yake mazingira hayako Marekani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...