August 2008
no image
KAKA MICHUZI LEO NILIKUA MSAFIRI WA NDEGE YA AIR TANZANIA TC 100 IENDAYO DAR/MWZ.
NIMEFEDHEHESHWA SANA NA DADA ALIYE KUWA KWENYE UKAGUZI WA USALAMA WA MWISHO ( LAST SECURITY CHECK POINT ) UNAPOINGIA DEPARTURE LOUNGE ( DOMESTIC) KWA KUTUMIA LUGHA ZA FEDHULI SANA KWA WATEJA BAADA YA KUWAPEKUA.
MIMI ALINIKUTA NIMEBEBA VIMIMINIKA (LIQUID) AMBAZO NI UTURI (PERFUME) NA LOTION ANAZODAI ZIMEZIDI UJAZO WA ML 100 KILA MOJA KAMA TARATIBU ZA USAFIRI WA ANGA ZINAVYO SEMA,SINA TATIZO NA HILO.
CHA KUSIKITISHA NI KWAMBA YULE DADA WA USALAMA ALIPONIAMBIA KWA FEDHULI KWA KUNIFOKEA KUWA SIRUHUSIWI KUSAFIRI NAZO,AU KAMA UNAZIMIND JIPULIZIE HIYO PARFUME YAKO MPAKA IISHE NA LOTION JIPAKE MPAKA UIMALIZE KABLA HUJAPANDA NDEGE.
JE MHESHIMIWA TEMU WEWE UNAWEZA JIPULIZIA PERFUME ILIYOZIDI 100ML NDANI YA DAKIKA 5 UKAIMALIZA AU NI KEJELI NA KUDHALILISHANA?
AU BWANA TEMU NIKULETEE LOTION ILIOZIDI 100ML UJIPAKE NDANI YA DAKIKA 5 UIMALIZE?
TEMU ONDOA UWOZO AIRPORT,UNAWALEA SANA!!!
UTANISAMEHE KAMA MUHUSIKA WA KUMFUNDA HUYU DADA SI WAKO NI WA DADA MAGRETH MUNYAGI.
NAOMBA RADHI KWA LUGHA KALI NILIYOTUMIA.
SIKU NJEMA
STAKE HOLDER
JK na mama Salma Kikwete wakiwa kwenye game ya Wnba kati ya washington mystics(75) vs chicago sky(79) ilofanyikia verizon center downtown dc.chini mdau wakila snepu la kishikaji na jamaa kabla ya gemu hilo
MAREKANI YATANGAZA DIPLOMASIA YA
MPIRA WA KIKAPU KWA TANZANIA
Na Mwandishi Maalum

Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ijumaa, Agosti 29, 2008 alimaliza ziara ya kikazi ya siku tatu yenye mafanikio makubwa katika Marekani kwa kuhudhuria mchezo wa mpira wa kikapu wa ligi ya Marekani ya wanawake ya WNBA kati ya timu za Washington Mystics na Chicago Sky.

Kabla ya mchezo huo kwenye uwanja wa kisasa wa Verizon Center katikati ya jiji la Washington, Rais Kikwete alihudhuria shughuli fupi ya kutangazwa kwa “Diplomasia ya Mpira wa Kikapu” kwa Tanzania kwenye uwanja huo huo.

Katika shughuli hiyo ambako Rais Kikwete alifuatana na Mama Salma Kikwete, Balozi wa Marekani katika Tanzania, Mark Green, alitangaza ujio wa nyota wawili wa mpira wa kikapu katika Tanzania mwezi huu wa Septemba.

Rais Kikwete na Mama Salma wote walipata kuwa wachezaji wa mpira wa kiapu katika ujana wao.

Chini ya diplomasia hiyo, wachezaji wawili nyota wa mpira wa kikapu, watatemblea Tanzania kati ya Septemba 8 na 11 kuendesha mafunzo ya mchezo huo kwa vijana.

Shughuli hiyo inadhaminiwa na Ofisi ya Michezo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ya Sports United.

Wachezaji hao watakaotembelea Tanzania ni Jennifer Azzi, mchezaji wa zamani wa kike wa WNBA ambaye alicheza katika ligi ya NBA kwa miaka mitano akiwa na timu ya Utah Starzz.

Mama huyo, ambaye alipata shahada yake katika Chuo Kikuu cha Stanford, pia alishinda Medali ya Olimpiki ya Dhahabu akiwa na timu ya taifa ya Marekani.

Mwingine ni Matt Bonner, aliyepata shahada yake katika Chuo Kikuu cha Florida na ambaye amekuwa anacheza katika ligi ya NBA tokea mwaka 2003. Kwa sasa anachezea klabu ya San Antonio Spurs.

“Diplomasia ya Mpira wa Kikapu” inalenga kuimarisha uhusiano kati ya wananchi wa Marekani na wale wa nchi nyingine, na hasa vijana.

Mpango wa “Diplomasia ya Mpira wa Kikapu” ulianza mwaka jana kwa kuhusisha nchi ya Congo na mji wa Jerusalem.

Mwaka huu, mbali na Tanzania. wachezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani watatembelea nchi za Saudi Arabia, Thailand, Kazakhstan na Kyrgyzstan chini ya mpango huo.

Katika mechi hiyo kali ya juzi kwenye uwanja wa Verizon Center, timu wenyeji ya Washington Mystics ilishindwa kwa vikapu 76-73.

Mbali na timu ya Mystics, uwanja huo pia hutumiwa na timu ya mpira wa kikapu ya wanaume ya Washington Wizards, timu ya mpira wa magongo ya Capitals, timu ya mpira wa kikapu ya Chuo Kikuu cha Georgetown na una uwezo wa kuingiza watazamaji 20,000 kwa wakati mmoja.




no image
Kaka habari za kazi iliyo bomba sana. Kazi yako naifagilia kaka hongera sana Naomba msaada kwenye tuta kaka.
Mi ni kijana mkiristo miaka 36 nimejikuta nimejichimbia zaidi shule namalizia Masters. Naitwa James, ni kijana mpole, mchapakazi, Mtanzania. Kwa blog yako kaka naomba kutafuta dada aliye SERIOUS TU tutakayeishi kama my waifu wangu.
Atakuwa na uchaguzi wa kunichagua kama mimi nitakavyomchagua kwamba halazimishwa kunipenda kama hatanipenda.
Na endapo atakubaliana na hilo awe tayari kupima afya zetu zaidi ya mara mbili kwa muda muafaka kabla ya kuendelea na mambo mengine.Awe na elimu ya kidato cha sita na zaidi ya hapo ni nzuri zaidi.
Awe mrefu si mnene (unene wa kawaida ni bomba), mwenye tabia mzuri, talkative, cheerful na mwenye sura ya nzuri na mkiristo Asiye na makuu anayetarajia mambo ya juu.
Mi ni mtoto tu wa mkulima ninayetafuta maisha wala si wa matawi ya juu.
Anayekubaliana na ombi langu akina dada please niandikie ndatangule@yahoo.com
na akituma picha ya full ingekuwa poa zaidi


Be Brave use MOTOFLOW today and you could benefit from a REDUCTION IN FUEL CONSUMPTION.


Over Millions of satisfied customers around Europe and Australia are using MOTOFLOW today.
MOTOFLOW is going to be available in Tanzania for the First time in Africa.


For more information click on http://www.bewithusonline.com/ or here.

Or Phone +44 (0) 778 552 8468.

JK akioneshwa na Rais George Bush wa Marekani mandhari ya ikulu ya Marekani,White House, wakati Rais Kikwete alipomtembelea Rais Bush Ijumaa asubuhi jijini Washington D.C.Rais Kikwete yupo nchini Marekani kwa mwaliko wa Rais Bush
JK na mwenyeji wake Rais George Bush wa Marekani wakiwa katika mazungumzo ofisini kwa Rais Bush,Oval office iliyopo ikulu ya Marekani White house jijini Washington D.C Ijumaa asubuhi. picha na mdau Freddy Maro wa ikulu


May Allah shower his blessings on all fasting wadaus and their families during the holy month of Ramadhan and beyond.


May HE accept our Duas and good deeds and forgive all our transgressions


I wish you all a successful month and life

Ameen
rais wa zanzibar mh. amani abeid karume na mkewe mama shadya katika picha ya pamoja na will smith na mai waifu wake jada pinckett smith ikulu zenji
rais wa zanzibar mh. amani abeid karume akipiga stori na will smith
rais amani abeid karume akipokea zawadi ya sovenia toka kwa will smith aliyemtembelea ikulu ya zenj ijumaa hii, kwa mujibu wa mdau othman maulidi wa zanzibar leo aliyetuletea picha hizi
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisoma hotuba ya kuahirisha kikao cha bunge mjini Dodoma jana
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (kushoto ) na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Karatu, Dr. Wilbrod Slaa (katikati) baada ya kusoma hotuba yake ya Kuahirisha bunge

wah. wabunge toka shoto dk. harrison mwakyembe (kyela), dk. raphael chegeni (busega), beatrice shelukindo (kilindi) na anna kilango malecela (same mashariki) wakijadiliana nje ya ukumbi wa bunge baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho kilichodumu kwa muda wa siku 80. msikilize dk. mwakyembe na wah. wengine wakiongelea ripoti ya serikali juu ya mkataba wa umeme wa richmond na tanesco kwa kutembelea
Mmoja wa wazazi waliofika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, akitoa msaada wa kushikilia kwa chupa ya dripu ya dawa kwa mwanafunzi aliyedhurika na dawa ya chanjo ya Kichocho na Minyoo iliyofanyika jana
Mmoja wa mzazi wa mwanafunzi anayeelezwa kuathiriwa na dawa za kichocho na minyoo akiwa amembeba mtoto wake kumpelekwa wodini kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wakisaidiana na wazazi wa wenye watoto walioelezwa kuwathiriwa baada ya kupata chanjo ya dawa za kichocho na minyoo jana katika Shule mbalimbali za Msingi za Manispaa ya Morogoro.

ZAIDI ya wanafunzi 363 wa shule za msingi mkoani Rukwa na Morogoro leo walikimbizwa katika hospitali mbalimbali baada ya kuanguka na kupoteza fahamu muda mfupi baada ya kupewa dawa za kinga ya kichocho na minyoo katika mikoa hiyo.

Kutokana na hali hiyo utoaji wa chanjo katika mikoa hiyo ulilazimika kusimamishwa kwa muda usiojulikana.

Tafrani kubwa ilizuka baada ya watoto hao kupoteza fahamu mara tu baada ya kunywa dawa hizo.

Habari kutoka Rukwa zinasema kuwa utoaji chanjo hiyo ulisimamishwa baada ya wanafunzi wa shule za msingi kuanguka na kutoa povu mdomoni huku baadhi yao wakitapika na kupoteza fahamu.

Kutokana na hali hiyo wazazi wa wanafunzi hao walivamia shule hizo katika Manispaa ya Sumbawanga hususan shule za msingi Chemchem, Katandala, Mwenge, Malangali na Jangwani wakitishia kuwapiga walimu kwa kile walichodai kuwa wamesababisha hali hiyo.

Hali ilizidi kuwa mbaya wakati wazazi wa wanafunzi hao walipofika hatika hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga na kukataliwa kuingia wodini wakiwa na lengo la kuwaona watoto wao waliokuwa wamefikishwa hospitalini hapo kupatiwa matibabu.
Wazazi wa watoto hao waliwapiga mawe madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo huku wakilia kitendo kilichosababisha polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia wapelekwe hospitalini kuwatawanya wananchi zaidi ya 600 kwa kutumia mabomu ya machozi.
Mabomu hayo yalipigwa kwa zaidi ya saa tatu na kuweza kuwatawanya wananchi hao waliokaa umbali wa mita 500 ingawa baadhi yao wakiendelea kulia wakidhani watoto wao wamekufa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk. Saduni Kabuma alisema wanafunzi wote waliofikishwa katika hospitali hiyo wamepatiwa matibabu na wengi wao wameruhusiwa.
Alisema hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyefariki dunia kwa tukio hilo au aliyekuwa mahututi baada ya kumeza dawa hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Daniel Ole Njoolay aliwataka wazazi wa wanafunzi hao kutokuwa na uamuzi wa kukurupuka katika kukabiliana na matatizo badala yake wawe wasikivu kwani serikali kamwe haiwezi ikawapa sumu raia wake.
Mh. Njoolay amewataka wazazi mkoani Rukwa kuwapeleka watoto wao kesho kuendelea na chanjo ya surua na polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwani ni salama na wala hakuna madhara yatakayotokea.
Huko Morogoro chanjo ya kichocho na minyoo imekwama kutolewa baada ya kuzuka vurugu katika shule mbili ulipoenea uvumi wa kufariki dunia kwa mwanafunzi baada ya kupewa chanjo hiyo.
Katika utoaji wa chanjo hiyo wanafunzi 63 walizirai na kufikishwa katika hospitali ya mkoa kwa matibabu.
Vurugu zilizozuka zilisababisha polisi kutumia mabomu ya kutokwa na machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika maeneo ambako chanjo hiyo ilikuwa ikitolewa huku wakiwarushia mawe wahudumu na walimu kuwalazimisha wawaachie watoto wao warudi majumbani.
Polisi inawashikilia watu 25 wakiwamo wanawake wawili kutokana na vurugu hizo, zilizoanza jana saa tano asubuhi katika shule za msingi Mafisa A na B, katika Kata ya Mwembesongo hali iliyowalazimu walimu kupiga simu Kituo cha Polisi kuomba msaada wa ulinzi.
Katika vurugu hizo polisi mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Clemence Bazo, alijeruhiwa kwa kupigwa jiwe chini ya jicho lake moja na kupelekwa kwenye Hospitali ya Mkoa kwa matibabu ambako alishonwa nyuzi sita.
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, afande Thobias Andengenye alisema jeshi hilo lilikuwa halijapokea taarifa ya mtoto aliyekufa kufuatia chanjo hiyo.
Wakati huohuo, Mganga Mkuu wa mkoani Morogoro, Dk. Frida Mokiti amesimamisha utoaji wa chanjo hiyo ya kichocho na minyoo hadi itakapotangazwa tena kwa mkoa huu.

Picha hizi za matukio mbalimbali mkoani Morogoro ni kwa hisani ya Mdau John Nditi wa Morogoro na habari ni kutoka kwa mdau Gurian Adolf akiwa Rukwa na John nditi ambao wote ni watendaji wa gazeti la HabariLeo






BBC confirms commitment to Africa with launch of new branded channels

BBC Worldwide Channels pledged its commitment to the African market recently as plans were announced to launch a suite of BBC-branded thematic channels into the region. The channels will be available via MultiChoice’s DStv platform, Africa’s leading television provider, from 1 September 2008*

The new thematic channels - BBC Entertainment, BBC Knowledge, BBC Lifestyle and CBeebies - will replace and build on the success of existing channels BBC Food and BBC Prime, enabling viewers to access even more of the award-winning and high-quality programming from the BBC.

Darren Childs, Managing Director, BBC Worldwide Channels, said: “Today’s announcement builds on BBC Worldwide channel’s long-term relationship with MultiChoice. In asking us to provide more channels for the platform is testimony to the BBC brand and the quality of our content.”

MultiChoice Africa CEO Eben Greyling says “MultiChoice welcomes the four BBC channels which we believe will contribute to our ongoing commitment of ensuring our customers receive high quality channels from a variety of different genres.”

Dean Possenniskie, General Manager and SVP EMEA, BBC Worldwide Channels, adds: “Africa has always been of great importance to us, and we are now making a significant investment as we launch four dedicated channel feeds for Africa. This new deal with MultiChoice confirms our commitment to the territory, and allows us to deliver a greater range of contemporary, award-winning programming across all four channel genres to loyal BBC viewers in addition to attracting new ones.”

The new BBC channels:

BBC Entertainment showcases the very best comedy, drama and light entertainment programming from the BBC and other UK production houses. The channel launched first in Asia in October 2006, and most recently in Poland, to critical acclaim. The South Morning Post (Hong Kong) hailed the arrival of BBC Entertainment as “the TV success story of [2006]. Having changed its name from BBC Prime and concentrating on the best of British comedy and drama, this channel now boasts the most consistently watchable primetime line-up on Hong Kong screens, and offers a welcome alternative to the monopoly American shows.” BBC Entertainment will be on channel number 120 and will launch on 1 September.*

BBC Lifestyle is an inimitable destination offering inspiration for home, family and life. The channel dishes up six tasty strands to entertain engage and inspire viewers. Favourite African series, once on BBC Food, will now broadcast in the Food strand. Serving up the best food and cookery shows with world-famous chefs, it promises enticing gastronomic journeys around the world. The other Lifestyle strands include: Home & Design, offering expert advice and design knowledge to help viewers transform houses into perfect homes; Fashion & Style, bringing honest, practical advice and fashion tips from some of the world’s top style gurus; Health, helping to improve diet and nutrition with expert advice; Parenting, providing child psychologists and advisors to help with busy or stressful family life; Personal Development, helping enrich mental wellbeing and achieve inspiration in all aspects of life.
BBC Lifestyle will be on channel number 180 and will launch on 2 September*.

BBC Knowledge showcases the best of the BBC’s award-winning factual and non-fiction entertainment programming, The channel provides five key strands enabling simple appointment viewing: The World delves and explores new cultures around the world; Science & Technology explores new frontiers, from space to motoring; People explores aspects of the human body and mind; The Past brings historical events, places and people back to life; Business offers advice on how to stay on top of today’s challenging business world. BBC Knowledge will be on channel number 251 and will launch on 3 September*.

CBeebies is a pre-school channel for children aged six years and under with a programme schedule that has an emphasis on educational entertainment and supported by the core BBC values that make the channel trustworthy, reliable, informative and educational. CBeebies offers a mix of new and landmark, high-quality programmes to educate and entertain the BBC's youngest audiences. The service provides a range of pre-school programming designed to encourage learning through play in a consistently safe environment. CBeebies will be on channel number 306 and will launch on 4 September*

no image
Kaka Michuzi Kwanza nakupa hongera sana kwa besidei yako ya kutimiza miaka kadhaa uliyoiadhimisha ukiwa Dodoma.
Pili naomba kupitia blog yetu hii ya jamii kumtafuta ndugu yangu aitwaye DEUSDEDIT TIRUMANYWA IZUMBA ambaye nimepotezana naye kwa muda mrefu sasa.
Mara ya mwisho alikuwa anafanya kazi Idara ya Mifugo akiwa Same. Yeyote aliye na habari zake naomba tafadhali anijulishe kupitia blog hii au tuwasiliane.
Mimi naitwa Switbert Msoga na
email yangu ni
no image
Habari Mkubwa,

Naitwa Francis, nafanya kazi hapa Music Mayday kama Program Assistant. Pia nafanya kazi kama reporter wa website ya Ghetto Radio ambayo inaendeshwa na Ghetto Radio Foundation iliyoko Uholanzi.

Nahitaji Msaada wako ili kuweza kutangaza website ya
Ghetto Radio
iweze kufahamika na watu wengi zaidi wanaotembelea blog yako ndani na nje ya nchi.

Naomba ui-publish newslater ambayo nimeambatanisha pamoja na e-mail hii. Pia naomba uiweke link ya website ya Ghetto Radio katika list ya link zilizoko kwenye blog yako.

Ghetto radio Mtandao ambao unalenga kuonesha utajiri wa utamaduni wa kisasa wa kiafrika wa watu wanaoishi ghetto tofauti na ilivyozoeleka kuoneshwa na vyombo vingine vya habari vya Ulaya na Marekani.

Tovuti ya Ghetto radio imesheheni habari kutoka majiji saba katika Afrika ambayo ni Dar es Salaam, Nairobi, Kampala, Harare, Johannesburg, Lagos na Dakar.

Natanguliza Shukrani.
Francis Moris Sampa

Wadau tangu jana ninaigiza katika sinema, Edge of Darkness, hapa Boston. Stelingi wake ni Mel Gibson na Robert DeNiro.

Ninacheza kama askari polisi wa kike (background). Nitaitwa mara kwa mara kuigiza kwenye background hadi wanapomaliza ku-shuti mwezi Desemba.

Nilipatwa na butwaa nilipopigiwa simu wiki mbili zilizoipita na kuambiwa kuwa nimechaguliwa na mwongoza sinema, kuwa askari kanzu wa kike. Na tena si kwa siku moja tu.Haturuhusiwi kupiga picha kwenye set hii nimepiga mwenyewe Dressing Room.

Ninavaa bastola bandia na madude mengine wanaovaa polisi wa Boston.Mel Gibson mtu poa sana, jana alikuwa anatuchekesha kwenye set, leo alikuja kula lunch kwenye meza tuliyokuwa tunakula. Kaongea vizuri tu na sisi. Tulishangaa kuona mtu "A" list kama yeye anafanya hivyo. Mara nyingi wanaenda kula kwenye trela au hoteli lakini siyo na extras.

Haya nitawapa updates.

Mcheza sinema, Gbenga Akkinabe (The Wire) mwenye asili ya Nigeria anaigiza kwenye hiyo sinema kama mpelelezi. Nimeongea naye kidogo, alisema kuwa ana marafiki wengi kutoka Tanzania huko New York.

Habari na picha kutoka:
-------------------------------------------------------
Hongera sana da'chemi kwa mafanikio yako ambayo yanakuja taratiiiiiiiibu. iko siku tutasikia wewe ndiye stelingi. ukija bongo tutakuwa tunakugombea kama kina will smith. he, mbona watani wa jadi watatukoma! iko siku dada, kaza buti tu
-michuzi
Bosi wa masoko wa Vodacom akimkabidhi rasmi zawadi ya gari kwa mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2008 Nasreem Kalim .Gari hilo jipya aina ya Suzuki Garnd Vitara lina thamani ya sh Millioni 42 limekabidhiwa kwa mrembo huyo aliyenyakua taji hilo mwaka huu



JK akilakiwa na bosi wa kitengo cha elimu cha shirika la misaada ya kimataifa la marekani USAID Dr.Sarah Moten alipotembelea jana. katika mkutano wao Dr Moten alitangaza msaada mpya kusaidia ununuzi wa vitabu vya sayansi kwa shule za sekondari nchini wenye thamani ya dola milioni 1.5 za kimarekani
JK akihutubia katika makao makuu ya shirika la misaada la marekani USAID huko washington
waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh. bernard membe na mkurugenzi wa wakala wa biashara na ushirikiano wa kimataifa wa marekani (USTDA) mama leocadia zak wakimwaga wino wa mkataba wa makubaliano ambapo wakala huo utaipatia bongo dola 600,000 za kimarekani kuipiga tafu sekta za umeme, mafuta na gesi huko washington, kwa mujibu wa mdau freddy maro aliyeleta picha na habari hizi
Mwimbaji wa bongo flava Ali Kiba ambae alitua Marekani wiki iliyopita kwa kishindo kwa maonyesho mbali mbali hapa Marekani,atafanya onyesho lake la kwanza kwenye bashi la ubwete la Watanzania Washington Dc jumapili august 31 kwenye ukumbi wa
Mirage,
4401 university blvd,
Hyattsville Md 20783.

Onyesho litaanza saa 4 usiku.

Ali Kiba ameahidi kufanya mambo makubwa,wapenzi wa Washington Dc na vitongoji nyake kaeni chonjo,usingoje kuhadithiwa,njoo kwenye onyesho la kwanza na uwe wa kwanza kucheze CINDERELLA.
waziri mkuu mh. mizengo pinda na mai waifu wake mama tunu pinda wakiongoza mduara katika hafla ya kumalizika kikao cha bunge usiku huu hapa dodoma. nyuma ya mama tunu pinda ni mh. spika samwel sitta akifuatiwa na naibu wake mama anna makinda na waziri wa nchi ofisi ya rais mh. philip marmo. bunge linaahirishwa rasmi leo baada ya kudumu kwa takriba miezi mitatu ya bajeti na mijadala mizito
dj too short wa clouds 88.4fm alikuwemo ndani ya nyumba na malavi davi yake
mama tunu pinda na mh. martha mlatta wakicheza twisti
mh. spika samwel sitta akiongozana na mh. al-shaymaa kwegir kwenda kuchukua zawadi yao kwa kuibuka washindi wa kucheza bongo fleva katika hafla hiyo
wah. wabunge wakiserebuka
mkuu wa wilaya ya tegeta ambaye amesherehekea besdei yake ya kuzaliwa hakujivunga kwani aliunganisha sherehe yake na hafla hiyo na akisaidiwa na wadau athumani hamisi, juma dihule na selemani mpochi
mkuu wa wilaya ya nanihii akiwa na kikosi kizima cha wana njenje ambao walikubali kuja dodoma kusherehekea besdei yake ya kuzaliwa
wah. na wafanyakazi wa bungeni wakiyarudi mambo
babu njenje (shoto) na keppy kiombile wakiwa na mc wa shughuli hiyo sakina wa lyoka toka clouds 88.4fm
"walumba mpoooo...." anaimba nyota waziri wakati njenje walipoduarisha wah. wabunge usiku huu
--------------------------------------
Happy birthday to you*2
Happy birthday dear Issaaaaaaaaaaa
happy birthday to you!
How old are you now*2
Happy birthday dear Michuziiiiiiiiiiiiiiiii
happy birthday to you!
Sasa mkuu wa wilaya ya nanihiiiiiii ndio nn cku ya besdei kuvaa suti na t-shirt?? Mi naona hiyo haijakaa vizuri.Au ndio umetufanyia sapraizi?????????????????????????????
Mdau Naomi
----------------------------------------------
asante mdau naomi na wengine wote mlionitakia besdei njema. shati lilikuwa halijakauka ikabidi nipige ze fulanzzzzz. si unajua tena?
-michuzi

Pichani ni Kondakta wa Basi linalofanya safari zake jijini Dar es Salaam akiongoza magari baada ya foleni kubwa ya kwenye makutano ya barabara ya Lumumba na Uhuru.


Kujitolea kwa kondakta huyo kati ya Makondakta wote waliokuwapo hapo, ni moja ya kazi ya kila raia wa nchi kujitolea wakati jambo au mambo yoyote yanayojitokeza aidha kwa bahati mbaya, bila ya makusudio au kwa makusudio.


Kujitolea kusawazisha ya wenzako au kusawazisha kwenye kila jambo linaloelekea pabaya ni haki ya kila raia kumshauri raia mwenzako ili ndugu au jamii au kijiji au nchi isielekee pabaya.


Kwa nchi kama Uingereza wanaita "Duty of Care".


Je, huyu ni wewe?Kwa yeyote anayemjua kijana huyo (pichani) atume namba yake ya simu,



tuna zawadi ndogo tu ya kumpa ndugu yetu huyo mwenye mfano mzuri, ahsante.Na aliyepiga picha hii wa gazeti la This Day, tunampa ahsante.
Na Kaka Issa Michuzi (Happy Birthday on the 28th August 2008).
Zenjydar Community Association inawatakia Watanzania wote duniani, RAMADHAN KAREEM.
Mhariri,
Zenjydar Community Association
no image
Biashara na Ajira mtandaooniNdugu watanzania wenzangu vijana kwa wazee, mlioajiriwa na mnaofikiria kujiajiri, part-time ama full-time, ninayofuraha kuwafahamisha habari ya ajira na biashara mtandaoni.
Unachotakiwa kufanya ni ku sign-up
zoezi hilo fupi ni mkataba kamili wa ajira

Ukweli na undani kuhusu biashara hii Kampuni ya Carsons Services,Inc ins duka mtandaoni(Veriuni Stores) ambapo wanatumia online network marketing kupromote bidhaa zao ambapo wao hawa-advertise bidhaa zao moja kwa moja bali kazi hii wanaiacha kwa jamiiUnapo sign-up
www.cashinjectionstratergy.com
tayari unakuwa umejiajiri kama online sales representative(affiliate) wa SFI Marketing Group shughuli inakuwa ni kupromote bidhaa mtandaoni kwanjia tofautitofauti ambazo nyingi utajifunza kwa kusoma kupitia site yao.
Katika utaratibu huo inapotokea bidhaa uliyopromote ikanunuliwa unapata camission 30%-80% ya bidhaa itakayonunuliwaMantiki ni kwamba commission unayoipata ndicho kiasi ambacho wangekitumia kupromote biashara lakini badala yake hiyo kazi unaifanya wewe na kupata hizo fedha
Faida za ajira/biashara hii
Huhitaji kuzunguka(machinga) kama biashara nyingine za promosheni hapa mambo yote yanaishia mtandaoni
Hakuna kubahatisha mana soko la bidhaa ni ulimwengu mzima(world-wide customer-base)lenye utajiri wa wateja wenye hulka za kila aina(diversity)Huhitaji kutengeneza matangazo kwani mengi yameshatengenezwa kazi inakuwa kuya distribute kwenye site mbalimbali (online classified)
Huhitaji kutengeneza website kwani mara unapo sign-up tovuti yao inakupa account ambayo inakuwezesha kumanage mapato na mauzo yako yote mambo yote(mengi utajifunza taratibu kwa kusoma kwenye hiyo site)

Jinsi ya kupata mapato yako
Njia rahisi SFI Marketing Group wanayoitumia wa kulipa affiliates wao ni debit card (bank card) Pindi affiliate anapofikisha mauzo ya US$20 basi anatumiwa kadi hiyo,kadi hii inaweza kutumika katika ATM system nyingi hapa nchini na popote pale dunianiPia zipo njia nyingine kama cheque, ni chaguo la affiate mwenyewe

DokezoWengi wanakata tamaa mapema kwa kukosa subira kutaka kujua mambo yote kwa siku moja,kuepuka hilo soma/fuatilia maelezo kwa taratibu uyaelewe

Kwa msaada zaidiWasiliana na bw.Tonny Namata kupitia
va@thecashaccount.co.uk
huyu bwana ndo alileta hili wazo huku tanzania, ana uelewa mpana wa hii biashara, mwepesi kutoa msaada mengi utayapata kwake kutokana na uzoefu na exposure aliyonayo
Wasiliana na mimi
Martin Elisante
kupitia
m_elisante@yahoo.com
Sasa hakutakuwa na anayesema hajui kufanya biashara wala atakaye lia njaa wala mwenye juhudi za kusaka chapaa akazikosa.www.freewebs.com/ajiramtandaoni.comIts up to you!

Kwanza kabisa nakutakia Happy birthday mkuu wa nanihii,

pili mimi ni mkazi wa hapa washington, d.c nilikuwa nawatangazia wakazi wa dc na suburbs zake kuwa nina ticket za game ya wnba kati ya washington mystics v Chicago sky ambayo iko kesho ijumaa game ambayo mhe.

JK atakuwa ndani ya nyumba hapo Verizon center, seat ziko nyuma ya watangazaji (Floor seat).

Kama kuna mtu angependa kununua awasiliane na mi kwa machimu3@gmail.com

au text

@ 301 787-5390

ama piga simu

(240) 582 - 0057.
no image
TAARIFA YA WAZIRI MKUU, MHE. MIZENGO P. PINDA, (MB.), KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BUNGE YA MKATABA BAINA YA TANESCO NA RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY LLC
28 AGOSTI 2008
(VIDEO ZA MH. PINDA AKISOMA TAARIFA HII ITAPATIKANA KUPITIA www.dailynews-tsn.com kwenye milango ya saa sita usiku saa za Bongo )


UTANGULIZI:

1. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 37(1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007), naomba kuwasilisha Taarifa ya Serikali kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge ya Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond Development Company LLC.

2. Mheshimiwa Spika, Katika Mkutano wa Kumi wa Bunge tarehe 15 Februari 2008, Bunge lako Tukufu lilipitisha Maazimio 23 baada ya mjadala wa Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa mwezi Novemba 2007 ili kuchunguza mchakato wa Zabuni ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC wa kuzalisha umeme wa dharura Nchini mwaka 2006. Kwa kuzingatia uzito wa suala hili, wakati nilipotoa Hotuba yangu ya kuahirisha Mkutano wa Kumi wa Bunge nilieleza kuwa Serikali itaunda Timu ndogo ya Wataalam ili kuchambua kwa makini na kupendekeza namna ya kutekeleza Maazimio hayo 23 yaliyopitishwa na Bunge. Vilevile, niliahidi kuwa Kamati hiyo itazingatia mambo yote muhimu yaliyomo kwenye Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge na Taarifa za majadiliano zilizoingizwa kwenye kumbukumbu za Bunge (HANSARD).

3. Mheshimiwa Spika, tarehe 25 Aprili 2008 wakati nikitoa Hotuba yangu ya kuahirisha Mkutano wa Kumi na moja wa Bunge lako Tukufu, niliwasilisha Taarifa ya Awali ya hatua zilizochukuliwa na Serikali katika utekelezaji wa Maazimio hayo.

Aidha, niliahidi pia kuwa Serikali itajitahidi kuharakisha utekelezaji wa Maazimio hayo kwa kadri itakavyowezekana na Taarifa rasmi itawasilishwa katika Mkutano huu wa Kumi na Mbili wa Bunge, jambo ambalo linafanyika leo.

4. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2008 Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikubali kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Edward Lowassa (Mb.). Aidha, Mawaziri wawili, Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha, (Mb.), na Mheshimiwa Nazir Karamagi (Mb.), nao kwa wakati mmoja walijiuzulu kwa kuwajibika kwao kisiasa kwa Maslahi ya Taifa. Kutokana na uamuzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu kujiuzulu, Kikatiba kulisababisha Baraza zima la Mawaziri kuvunjwa, jambo ambalo lilikuwa ni uamuzi mkubwa kwa Serikali. Hatua hii inaonyesha kiwango kikubwa cha usikivu wa Serikali yetu. Hasa kwa kuzingatia kwamba, hatua hii ilichukuliwa mapema mara tu baada ya Taarifa ya Kamati Teule kuwasilishwa katika Bunge lako Tukufu.

5. Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hiyo, napenda kueleza hatua nyingine muhimu zilizochukuliwa na Serikali hadi hivi sasa:-

Kwanza, Serikali imekwishapeleka maelekezo kwa kila Wizara na Taasisi zinazohusika na utekelezaji wa Maazimio haya na hatua za utekelezaji zinaendelea kuchukuliwa na Vyombo hivyo;

Pili, Kufuatia utata uliojitokeza kuhusu uhalali wa Mkataba baina ya TANESCO na Richmond Development Company LLC uliorithiwa na Dowans S.A, Serikali imechukua hatua ya kusitisha Mkataba huo kuanzia tarehe 1 Agosti 2008.

Tatu, Serikali imesitisha malipo yote ya fedha zinazohusiana na Mkataba baina ya TANESCO na Richmond Development Company LLC uliorithiwa na Kampuni ya Dowans S.A.;

Nne, Watumishi wote wa Umma waliohusika katika mchakato wa kuandaa na kutoa Zabuni ya Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND wameandikiwa barua za kujieleza kama hatua za awali za Kinidhamu kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma. Aidha, kwa wale watakaoonekana kuwa wamefanya makosa ya jinai, hatua stahiki za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

6. Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo sasa ningependa kueleza kipengele kwa kipengele kuhusu hatua za utekelezaji wa Maazimio yote kama yalivyorekebishwa tarehe 15 Februari 2008 na Mtoa Hoja wakati akihitimisha hoja yake.


AZIMIO NAMBA 1:
“ Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2004 (Public Procurement Act, 2004) haina nguvu ya kutosha. Sheria ipitiwe upya ili kuiboresha kwa kuipa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) nguvu zaidi za udhibiti na uwezo wa kuchukua hatua pale Sheria na Kanuni zinapokiukwa, badala ya kutoa ushauri tu kama ilivyo sasa.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Wizara ya Fedha na Uchumi ikishirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), wamekwishaainisha maeneo yote yenye mapungufu na yanayohitaji marekebisho kwenye Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004.

Baada ya zoezi hilo kufanyika, Serikali itawasilisha katika Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge lako Tukufu, Mapendekezo ya kufanya Marekebisho katika Sheria hiyo. Maeneo yatakayozingatiwa ni yafuatayo:

(i) Kuipa uwezo PPRA kusitisha Zabuni yoyote pale itakapobainika kuwepo kwa ukiukwaji wa Sheria na Kanuni zinazosimamia Manunuzi ya Umma.
(ii) Kuipa nguvu PPRA kutoa maelekezo kwa Mamlaka zinazohusika na ununuzi, (yaani Procuring Entities) kuchukua hatua kwa watakaokiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.

(iii) Kuifanya PPRA kuwa Taasisi Huru inayojitegemea ikiwa na Muundo sawa na ule wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

(iv) Kufanya marekebisho yatakayowezesha Sheria kutoa adhabu kali kwa Viongozi na Watumishi wa Umma watakaobainika kujihusisha na ukiukwaji wa Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.

(v) Kufanya marekebisho ya kuzitaka Mamlaka zenye dhamana zitakazopokea hoja za ukiukwaji wa Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka PPRA, kutoa taarifa kuhusu hoja hizo katika kipindi maalum, na ikibidi kuchukua hatua zaidi kwa Taasisi au Mtu atakayekiuka Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.

(vi) Kuweka utaratibu mzuri wa namna ya kushughulikia masuala ya Ununuzi wa Dharura yanapotokea.

(vii) Kuweka utaratibu wa kuwezesha kufanyika uchunguzi wa kina (due deligence) kwa Wazabuni wa ndani na nje ya Nchi wanaoomba kuingia Mikataba na Serikali.

(viii) Kuweka Utaratibu wa kutumia Kamati Huru ya Wataalam itakayofanya uchunguzi wa kina pale itakapobidi.


AZIMIO NAMBA 2:
“Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) isiwajibike Wizara ya Fedha ambayo nayo ni Taasisi ya Ununuzi (Procuring Entity) badala yake iwe chombo huru kinachowajibika Ofisi ya Rais na Taarifa zake kuwasilishwa Bungeni.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
(i) Kulingana na Sheria ilivyo hivi sasa, PPRA ni Taasisi Huru inayojitegemea nje ya Muundo wa Wizara ya Fedha na Uchumi. Aidha, PPRA ina Bajeti yake inayojitegemea na pia ina Chombo chake Maalum cha Usimamizi, (yaani Bodi ya Wakurugenzi). Hata hivyo, katika Marekebisho ya Sheria yanayotarajiwa kufanyika, Serikali inakusudia kuwasilisha pendekezo la kufanya PPRA iwe na Muundo sawa na ule wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG) ambapo utatoa uhuru kwa Chombo hicho kutoa maamuzi ya kila siku bila kuingiliwa na Chombo chochote, ingawa Kisera itaendelea kuwa chini ya usimamizi wa HAZINA kama ilivyo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

(ii) Kuhusu Taarifa za mwaka za PPRA kuwasilishwa Bungeni, suala hili limezingatiwa katika Kifungu cha 26 (2) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004, inayotumika hivi sasa. Chini ya Sheria hiyo, Waziri wa Fedha na Uchumi huwasilisha Bungeni Taarifa ya kila mwaka ya utendaji wa PPRA.


AZIMIO NAMBA 3:
“Mikataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC (uliyorithiwa Dowans Holdings S.A) na ile kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo Mikataba ya Madini ilivyopitiwa upya na Serikali. Bila kufanya hivyo, mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea Wananchi na kushindwa kufikia azma ya Serikali ya maisha bora kwa kila Mtanzania”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Pamoja na kutoa Taarifa ya utekelezaji wa Azimio hili, napenda kueleza kuhusu hali ilivyo sasa kwa Mikataba baina ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals.

(i) Mkataba baina ya TANESCO na IPTL

§ Mgogoro uliopo sasa kati ya TANESCO na IPTL unatokana na kutokubaliana kwa pande zote mbili kuhusu kiwango cha capacity charge kinachotozwa na IPTL.

§ Kwa mujibu wa Mkataba wa kuuziana Umeme kati ya IPTL na TANESCO, capacity charge inapaswa kukokotolewa kwa kuzingatia mtaji (equity) wa asilimia 30 na faida ya asilimia 22.31 uliopaswa kuwa umewekezwa (ambao ni US$ 36.54 milioni) wakati IPTL wanaanza kuzalisha Umeme na kuiuzia TANESCO tarehe 15 Januari, 2002. Hata hivyo, kufuatia uchunguzi uliofanywa na TANESCO imegundulika kwamba mtaji halisi wakati IPTL inaanza kuzalisha Umeme ulikuwa Shilingi Hamsini Elfu tu (50,000/=). Hivyo, mtaji huu ndiyo unaostahili kutumika kukokotoa capacity charge inayolipwa IPTL na si vinginevyo.

§ Kwa mantiki hiyo, madai ya TANESCO na Serikali katika Mradi huu ni kuwa, capacity charge inayotozwa na IPTL izingatie kiwango halisi cha mtaji (equity) uliowekezwa na IPTL, na si zaidi ya hapo. Aidha, Serikali na TANESCO inadai kutoka IPTL kiasi chote cha malipo kilichofanywa kimakosa kama capacity charge ambacho hakikustahili kulipwa kwa IPTL.

§ Kutokana Serikali kutoridhika na kiwango cha malipo ya capacity charge chini ya Mradi huu wa IPTL, ilisitisha malipo kwa IPTL; jambo ambalo lilipelekea IPTL kufungua Shauri la Madai dhidi ya TANESCO kwenye Mahakama ya New York Nchini Marekani mwezi Novemba 2007. Mnamo mwezi Aprili 2008 Serikali ilishinda Shauri hilo baada ya Mahakama hiyo kutupilia mbali shauri hilo na kuelekeza kwamba mgogoro huo uwasilishwe kwenye Baraza la Usuluhishi (Arbitration) kama Mkataba baina ya pande mbili unavyoelekeza.

§ Tarehe 9 Julai, 2008 IPTL iliwasilisha mgogoro huu kwenye International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID). Kwa sasa shauri hili bado halijatolewa uamuzi.

§ Hata hivyo, Serikali imejiandaa ipasavyo kutetea na kulinda haki zake chini ya Kamati Maalum ya Serikali iliyoundwa kushughulikia mgogoro huu. Mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo Maalum, ni Wakili mzoefu wa Kujitegemea Mheshimiwa Nimrod Elirehema Mkono, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

§ Hivyo, Mkataba huu tayari umekwishapitiwa na Kamati husika na mapungufu yake yaliyobainika ndiyo yamepelekea kuwepo kwa Shauri hili.

(ii) Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND (uliorithiwa na DOWANS)

Kutokana na utata uliojitokeza katika mchakato mzima kuhusu Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND uliotiwa saini tarehe 23 Juni 2006, Serikali kupitia TANESCO iliamua kufanyike mapitio ya Mkataba huo na kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa Wanasheria waliobobea katika masuala ya Mikataba ya Kimataifa wa Kampuni ya REX ATTORNEYS. Uchunguzi wa REX ATTORNEYS ulibaini pamoja na mambo mengine kwamba:-

(a) Utaratibu mzima wa manunuzi ya huduma ya umeme na kuingia Mkataba na Richmond Development Company LLC ulikiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004;

(b) Kutokana na ukiukwaji huo, Mkataba baina ya TANESCO na Richmond Development Company LLC haukuwa halali na hauna nguvu ya Kisheria; na,

(c) Vilevile, hata kama Mkataba husika ungekuwa halali, uhamishaji (assignment) wa Mkataba huo kutoka RDEVCO badala ya Richmond Development Company LLC kwenda DOWANS HOLDINGS S.A. na hatimaye Dowans Tanzania Limited haukuwa halali.

Kwa kuzingatia mapungufu hayo yaliyobainishwa katika Mkataba huo, Serikali iliamua kusitisha huduma za Dowans Tanzania Limited kuanzia tarehe 1 Agosti 2008.


(iii) Mkataba baina ya TANESCO na Alstom Power Rentals (APR)

Kama ilivyoelezwa na Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja (Mb.) wakati akiwasilisha Hotuba yake hapa Bungeni, tarehe 8 Julai 2008, katika Mkutano huu wa Bunge lako Tukufu, alifafanua kuwa, mitambo ya Alstom Power Rentals ilikodishwa na TANESCO kwa kipindi cha miezi 12 kuanzia tarehe 20 Machi, 2007 hadi tarehe 19 Machi, 2008. Baada ya muda wa Mkataba huo kumalizika, Serikali haikuhuisha Mkataba huo, licha ya jitihada za Wahusika kutaka uhuishwe.

(iv) Mkataba baina ya TANESCO na AGGREKO

Mkataba baina ya TANESCO na AGGREKO ulianza kutekelezwa mwezi Desemba 2006 na unatarajiwa kumalizika mwezi Novemba 2008. Kamati ya Serikali ya Wataalam inapitia Mkataba huu ili kujiridhisha kama upo kwa maslahi ya Taifa na kuchukua hatua kadri itakavyoonekana inafaa.

(v) Mkataba baina ya TANESCO na SONGAS

Kwa sasa Mkataba mkubwa wa Sekta ya Nishati ambao unapaswa kupitiwa upya ni baina ya TANESCO na SONGAS. Mkataba wa SONGAS unahusisha Wadau wengi na unajumuisha Mikataba midogo mbalimbali ipatayo ishirini na moja inayohusu masuala ya utafutaji, usambazaji, ununuzi na mikopo ya uendelezaji wa Gesi Asilia na hivyo kuwa na uzito wa aina yake, (complex). Ili kuwa na tija katika mapitio ya Mikataba hiyo na kupata ushauri mzuri, Serikali inaendelea kushauriana na Wataalam Washauri waliobobea katika Sekta hii ya Gesi Asilia wakiwemo Wanasheria, ambao wataweza kushauri ipasavyo iwapo kuna mapungufu yoyote yanayostahili kufanyiwa marekebisho kwa maslahi ya Taifa.


AZIMIO NAMBA 4:
“Serikali itathmini upya uhalali wa kuwepo Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC (sasa Dowans Holdings S.A.) kwa lengo la kusitisha malipo kwa Dowans Holdings S.A. na kuvunja Mkataba huo haraka iwezekanavyo.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Kama nilivyoeleza awali, kufuatia utata ulijitokeza kuhusu uhalali wa Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND uliorithiwa na Dowans, Serikali imesitisha Mkataba huo kuanzia tarehe 1 Agosti 2008. Vilevile, Serikali imesitisha malipo yote ya fedha zinazohusiana na Mkataba huo.


AZIMIO NAMBA 5:
“Kwa kuwa Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC (sasa Dowans Holdings S.A) umesheheni makosa mengi ya kisheria yanayoashiria udhaifu mkubwa wa kitaalam katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au ukosefu wa umakini katika kuiwakilisha Serikali; Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili wa Serikali Donald Chidowu ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yoyote, wawajibishwe na Mamlaka ya juu ya Nchi kwa kuchangia kuiingiza Nchi katika Mkataba wa aibu.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
(i) Kikatiba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri Mkuu wa Serikali katika masuala yote ya Sheria za Nchi. Hivyo, ana wajibu mkubwa wa kuishauri Serikali katika maeneo ambayo anaona yanakiuka Sheria, Taratibu na Kanuni za Nchi.

Kutokana na nafasi yake Kikatiba, Mamlaka yake ya Nidhamu ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa miongoni mwa Watendaji Wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali, suala lake la kuhusishwa kwake katika Mchakato mzima wa Mkataba huo linashughulikiwa na Ofisi ya Rais, IKULU.

(ii) Kuhusu Wakili wa Serikali Bw. Donald Chidowu ambaye alikuwa ni miongoni mwa Wajumbe wa Kamati ya Majadiliano (GNT), akimwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amepelekewa barua ya kutakiwa ajieleze kwa kuzingatia Misingi ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice) na kuzingatia Sheria za Utumishi wa Umma. Mtumishi huyu amewasilisha utetezi wake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba ambaye ndiye Mamlaka yake ya Nidhamu katika muda wa siku kumi na nne zilizotakiwa. Hivi sasa, maelezo ya utetezi wake yanafanyiwa uchambuzi na Mamlaka yake ya Nidhamu ili hatimaye maamuzi yatolewe kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.


AZIMIO NAMBA 6:
“Katika kushughulikia Mikataba yote na Makampuni ya Nje, Serikali ihakikishe kuwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inatumika kikamilifu kupata Taarifa kamili za Makampuni haya. Aidha, Ofisi zetu za Ubalozi zilizo sehemu mbalimbali Duniani zihusishwe katika majadiliano na Makampuni yanayotoka nje ya Nchi, na vilevile katika kuyachunguza Makampuni hayo kwa lengo la kupata Taarifa zao za msingi na kuboresha nguvu ya hoja ya Serikali, kabla ya kuingia Mikataba husika.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Serikali imetafakari na kuzingatia kwa makini pendekezo hili. Hatua zilizoanza kuchukuliwa ni pamoja na zifuatazo:

(i) Kuanzia sasa, Balozi zetu zote za nje zitakuwa zinashirikishwa kikamilifu katika kufanya uchunguzi wa kina (due diligence) kwa Makampuni ya nje ambayo Serikali inatarajia kuingia nayo Mikataba katika manunuzi au katika miradi mikubwa. Serikali imeshatoa maelekezo haya kwenye Wizara zote. Aidha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nayo imetoa maelekezo kwa Balozi zetu zote ili zizingatie uamuzi huu.

(ii) Kama ilivyoelezwa katika Azimio Na. 1, Serikali itawasilisha mapendekezo kuhusu marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ili kuongeza Kifungu kinachohusu kufanya uchunguzi wa kina (due deligence) wa Wazabuni wa ndani na nje ya Nchi wanaoomba kuingia Mikataba na Serikali. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kuwa na Kamati Huru ya Wataalam itakayofanya uchunguzi huu wa kina, pale itakapobidi.

(iii) Katika kuhakikisha kuwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inatumika ipasavyo katika masuala ya Manunuzi ya Umma, PPRA tayari imeanzisha Mfumo wa Habari na Mawasiliano katika Manunuzi ya Umma ujulikanao kama “Procurement Management Information System”. Ni matumaini ya Serikali kuwa, Mfumo huu utatumika kurahisisha upatikanaji wa Taarifa mbalimbali za Manunuzi kati ya Mamlaka (yaani PPRA) na Taasisi za Ununuzi.


AZIMIO NAMBA 7:
“Wajumbe wote wa Kamati ya Serikali ya Majadiliano (Government Negotiation Team – GNT) ambao ni Maofisa Waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya Umma kwa kulitia hasara Taifa kutokana na kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya Taifa”.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Katika kushughulikia suala hili, (yaani katika mchakato mzima wa Zabuni pamoja na majadiliano ya Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND), kulikuwa na Kamati za aina tatu.

Kwanza, ni Kamati iliyokuwa inaundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mheshimiwa Johnson Mwanyika (Mb.), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Arthur Mwakapugi pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Uchumi Bw. Gray Mgonja. Kamati hii ilikuwa na jukumu la kutoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini na Serikali kwa ujumla.

Kamati ya pili, ilikuwa ni Timu ya Wataalam (Expert Team) iliyokuwa na Wajumbe kutoka Wizara na Taasisi zifuatazo:

1. Bw. Singi Madata - Fedha na Uchumi (Mwenyekiti);
2. Dkt. Lutengano Mwakahesya-Nishati na Madini (Mjumbe);
3. Bw. Theophilo Bwakea-Nishati na Madini, (Mjumbe);
4. Bw. Stephen Mabada - TANESCO (Mjumbe);
5. Bw. Athanas Mbawala - TANESCO (Mjumbe);
6. Bw. James Mwalilimo - TANESCO (Mjumbe);
7. Bw. Julius Sarota - Nishati na Madini (Sekretarieti).

Kamati hii ilikuwa na jukumu la kutathmini Wazabuni wote waliokuwa wameomba Zabuni ya mitambo ya kukodi ya dharura ya kufua umeme wa Megawati 105.6.

Kamati ya tatu ni ile ya Majadiliano baina ya Serikali na Wawakilishi wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC. Wajumbe wa Kamati hii ni wafuatao:-

1. Bw. Singi Madata - Fedha na Uchumi (Mwenyekiti);
2. Bw. Theophilo Bwakea- Nishati na Madini (Mjumbe);
3. Bw. Stephen Mabada - TANESCO (Mjumbe);
4. Bw. Godson Makia - TANESCO (Mjumbe);
5. Bw.Donald Chidowu-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (Mjumbe);
6. Bw. Dick Thewa – Benki Kuu ya Tanzania (Mjumbe);
7. Bw. Gideon Nassari – CTI (Mjumbe);
8. Bw. Julius Sarota - Nishati na Madini (Sekretarieti);
9. Bw. Mwita Wangwe – TANESCO (Sekretarieti).

Kamati mbili za Wataalam (yaani Kamati ya pili na ya tatu) zote zilikuwa zinaripoti na kutoa ushauri kwa Kamati ya Makatibu Wakuu wawili wa Hazina, na Nishati na Madini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa madhumuni ya utekelezaji wa Azimio hili, Wajumbe wote wa Kamati hizi tatu wamepelekewa barua za kutakiwa watoe maelezo kwa mujibu wa Sheria zinazohusu nidhamu katika Utumishi wao. Hatua hii inazingatia Misingi ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice), kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Miongoni mwa maeneo ambayo Watumishi hawa wametakiwa kutoa maelezo ni jinsi walivyohusika katika mchakato mzima na kuiingiza Serikali katika Mkataba unaoonekana kutokuwa na Maslahi kwa Taifa. Maeneo hayo ni pamoja na:

(i) Kutotumia utaalam na uzoefu wao kikamilifu ili kutambua mapema kuwa Richmond Development Company LLC haikuwa na uwezo kitaalam, kifedha na kiuzoefu na hivyo kutokidhi matakwa ya Zabuni.

(ii) Kutozingatia kikamilifu Sheria ya Manunuzi ya Umma, ya mwaka 2004 katika mchakato mzima wa kutoa Zabuni hii.

(iii) Wajumbe kushindwa kuishauri Serikali kuhusu kuifanyia Kampuni ya Richmond Development Company LLC uchunguzi wa awali (due diligence) pamoja na ukaguzi baada ya tathmini ya Zabuni (post qualification);
(iv) Kutokuwa makini na hivyo kushindwa kutambua udanganyifu wa ubia/uhusiano wa kibiashara kati ya Richmond Development Company LLC na Kampuni ya Kimataifa ya Pratt & Whitney;

Watumishi wote wameshawasilisha utetezi wao katika muda wa siku kumi na nne zilizopangwa. Aidha, hivi sasa utetezi wao unafanyiwa uchambuzi wa kina na Mamlaka zao za nidhamu ili hatua muafaka zichukuliwe kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotawala utumishi wao.

Kwa upande wa Watumishi wa TANESCO ambao ni Bw. Stephen Mabada, Bw. Athanas Mbawala, Bw. James Mwalilimo, Bw. Godson Makia na Bw. Mwita Wangwe, Kamati Ndogo ya Nidhamu ya Bodi ya TANESCO tayari imekwishapitia maelezo ya Watumishi wao wote na mapendekezo ya Kamati hiyo yamewasilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO ambayo itatoa maamuzi yake na kuiarifu Serikali.


AZIMIO NAMBA 8:
“Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Nazir Karamagi (Mb.), aliyeshabikia sana uhaulishaji wa Mkataba kutoka kwa Richmond Develeopment Company LLC kwenda kwa Dowans Holdings S.A. awajibishwe”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Mheshimiwa Nazir Karamagi (Mb.), aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini alijiuzulu mwezi Februari 2008 kwa kuwajibika kutokana na suala hili. Hata hivyo, kwa lengo la Serikali kujiridhisha kuhusu ushiriki na ushauri wake katika suala hili, Vyombo vya Dola vinaendelea na uchunguzi wa kina kwa lengo la kutaka kujua kama kuna rushwa yoyote ambayo ilijitokeza katika mchakato huu inayomhusisha Mheshimiwa Nazir Karamagi (Mb.), katika suala hili. Taarifa ya uchunguzi huo itawezesha Serikali kuamua juu ya hatua zaidi zinazostahili kuchukuliwa dhidi yake.


AZIMIO NAMBA 9:
“Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU awajibishwe kwa manufaa ya Umma na Maofisa wa TAKUKURU walioshiriki katika zoezi la uchunguzi na kuandaa Taarifa ya Richmond Development Company LLC iliyoficha ukweli nao pia wawajibishwe kwa manufaa ya Umma.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Zoezi la kufanya uchunguzi lililofanywa na TAKUKURU lilihusisha Watumishi wafuatao:

(i) Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Edward Hosea akiwa ndiye Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), iliyohusika na uchunguzi wa mchakato mzima wa Zabuni ya umeme wa dharura, ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC.

(ii) Mkurugenzi wa Upelelezi Bw. Alex Mfungo ambaye ndiye aliyesimamia zoezi zima la uchunguzi na kuandaa Ripoti ya Uchunguzi ya TAKUKURU kuhusu suala hili.

(iii) Maofisa wanane wa TAKUKURU walioshiriki katika zoezi la uchunguzi na kuandaa Taarifa katika maeneo yao ya utaalam katika mchakato mzima wa Zabuni ya Ununuzi wa mitambo ya umeme wa dharura ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Develeopment Company LLC.

Ili kutekeleza Azimio hili, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amepelekewa barua ya kutakiwa kujieleza na Mamlaka yake ya Nidhamu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi. Vilevile, Wasaidizi walio chini yake walioshiriki katika zoezi la uchunguzi, nao wametakiwa kutoa maelezo yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ambaye ndiye Mamlaka yao ya Nidhamu. Hii ni kwa kuzingatia Misingi ile ile ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice).

Hata hivyo, kwa kuzingatia mazingira ya shauri hili, Katibu Mkuu Kiongozi ataamua juu ya utaratibu mzuri wa hatua za nidhamu dhidi ya Wasaidizi wote wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU waliohusika katika suala hili.

Baadhi ya maeneo ambayo Mkurugenzi Mkuu na Wasaidizi wake wamepelekewa barua wajieleze ni yafuatayo:

(i) Kushindwa kuona kuwa Taarifa ya Uchunguzi iliyofanywa na Wataalam wa Taasisi yake haikubainisha kuwepo kwa kasoro nyingi zilizokuwepo katika Zabuni hiyo kama zilivyoainishwa katika Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, badala yake Taasisi iliona kwamba:-

§ Mchakato mzima ulizingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali;

§ Hayakuwepo mapungufu makubwa katika Zabuni hii;

§ Hakukuwa na hasara kwa Taifa kutokana na Zabuni hii.

(ii) Kushindwa kuona kuwa ushauri uliotolewa na PPRA kwa TANESCO kuhusu muda wa kutangaza Zabuni Kimataifa ulipuuzwa na hivyo kuvunjwa kwa Taratibu za Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004, na hivyo kutia shaka.
Hivi sasa, Watumishi wote tisa wameshawasilisha utetezi wao katika muda uliopangwa. Aidha, kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Utaratibu wa Utumishi wa Umma, Mamlaka yao ya Nidhamu inapitia utetezi wao ili kutoa uamuzi unaostahili.


AZIMIO NAMBA 10:
“Gavana wa Benki Kuu pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wachunguze kwa makini uhalali wa malipo ya ziada (US$ 4,865,000) yaliyofanywa kwa Dowans Holdings A.S iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company na kuwachukulia hatua waliohusika na uzembe huo.”
HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Wizara ya Fedha na Uchumi na Benki Kuu ya Tanzania wamechunguza na kuona kuwa malipo ya US$ 4,865,000 yaliyolipwa kwa Kampuni ya Dowans Holdings S.A. iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company LLC ni halali. Malipo hayo yalilipwa tarehe 2 Februari 2007 ikiwa ni gharama za ndege za usafirishaji wa mitambo ya kukodi ya umeme wa dharura, baada ya kupokea Invoice Na. EFD786675. Uchunguzi unaonyesha kuwa, taratibu zote za malipo zilifuatwa na malipo yalifanywa baada ya kuhakikiwa na TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini na HAZINA baada ya kupata ushauri wa Kisheria kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba yanawiana na Mkataba husika.


AZIMIO NAMBA 11:
“Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995 (The Public Leadership Code of Ethics Act) ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaoonekana wa kawaida sasa wa Viongozi Waandamizi wenye dhamana ya kisiasa kuendelea na biashara zao binafsi wakiwa madarakani, jambo ambalo lina mgongano wa kimaslahi. Serikali ianze rasmi maandalizi ya majadiliano ya kina kuhusu suala hili ndani na nje ya Bunge kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
(i) Kama alivyoeleza Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Hotuba yake ya terehe 21 Agosti 2008 wakati akilihutubia Bunge lako Tukufu kwamba, Serikali inayo dhamira ya dhati ya kuangalia namna ya kutenganisha shughuli za biashara na uongozi katika Utumishi wa Umma katika ngazi za juu za Viongozi na Watendaji Waandamizi. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imeanza mchakato wa kushughulikia suala hili na tayari wamewasilisha mapendekezo yao ya awali Serikalini.

(ii) Hivi sasa Serikali imeunda Timu inayojumuisha Wajumbe kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Uchaguzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na TAKUKURU ili kufanya uchambuzi zaidi wa Mapendekezo hayo. Aidha, Timu hiyo itafanya uchambuzi wa Sheria za Nchi zilizofanikiwa kuweka utaratibu wa Viongozi wa Umma kuweza kutenganisha shughuli za biashara zao na Uongozi ili kuondoa mgongano wa kimaslahi.

(iii) Katika zoezi hili, Wananchi na Wadau mbalimbali watashirikishwa kikamilifu ili kupata maoni yao.

(iv) Baada ya hatua hizo, Serikali inatarajia kuwasilisha hapa Bungeni marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma mwezi Aprili 2009.



AZIMIO NAMBA 12:
“Serikali ijiepushe kadri inavyowezekana na utaratibu wa kutumia Mawakala katika ununuzi wa Umma na kuhakikisha kuwa Wizara zote zina taarifa za bei halisi za mahitaji yao kila wakati ili kujiepusha na mchezo wa kawaida wa Mawakala kupandisha bei mara mbili au zaidi ya bei halisi.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Katika utekelezaji wa Azimio hili, Wizara zote, Wakala na Idara za Serikali Zinazojitegemea, Mikoa pamoja na Mashirika ya Umma zimeagizwa kuzingatia kikamilifu Taratibu za Manunuzi na Ugavi kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004. Pamoja na maelekezo hayo, hatua zifuatazo zitachukuliwa:

(i) Serikali imeamua kuwa, kila inapowezekana, Taasisi za Ununuzi zinunue vifaa moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wa bidhaa hizo. Ikibidi kununua kutoka kwa Wakala walioidhinishwa, ni lazima Taratibu za Manunuzi ya Umma zizingatiwe kikamilifu.

(ii) Katika hatua za awali, Wizara ya Fedha na Uchumi inaandaa Utaratibu wa kufanya Ununuzi wa pamoja wa bidhaa zinazoweza kutumika na Taasisi zaidi ya moja (Common use items). Utaratibu huo utakapokamilika, utawezesha bidhaa hizo kuagizwa kwa pamoja kupitia Wakala wa Serikali wa Huduma za Ununuzi na endapo itabidi, kununua moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji kwa lengo la kupata unafuu wa bei.

(iii) Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma tangu mwezi Juni 2008, imempata Mtaalam Mwelekezi wa kuandaa Mfumo wa ununuzi wa pamoja na kupata takwimu za Bei Dira za bidhaa mbalimbali (Indicative Price) kutoka kwa Wazalishaji wa bidhaa na huduma. Kazi hiyo itakamilika mwezi Septemba 2008. Takwimu hizo zitawekwa katika mtandao wa Mamlaka na kwenye matoleo ya Jarida la Masuala ya Ununuzi Tanzania ili ziweze kutumiwa na Taasisi za Ununuzi pamoja na Wazabuni. Bei hizo zitafanyiwa mapitio ya mara kwa mara na PPRA.


AZIMIO NAMBA 13:
“Serikali izihusishe Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya Mikataba mikubwa ya kibiashara na ya muda mrefu ili kuondokana na utaratibu uliopitwa na wakati kwamba Mikataba ya Kibiashara ni siri, hata kwa walipa kodi wenyewe. Aidha, Serikali ihakikishe kuwa, Kamati zote za Bunge zinapitia Mikataba mikubwa ya kibiashara na ya muda mrefu chini ya Sekta zao ili kuliondolea Taifa mizigo isiyo ya lazima.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Tarehe 24 Aprili 2008, Ofisi ya Waziri Mkuu ilimwandikia barua Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumfahamisha kuhusu utekelezaji wa awali wa baadhi ya Maazimio ya Kamati Teule yaliyopitishwa na Bunge. Katika barua hiyo, utekelezaji wa Maazimio Namba 13, 15, 16, 21 na 23 yalitolewa taarifa. Hata hivyo, kwa madhumuni ya Taarifa hii, ninapenda kurejea kwa muhtasari maelezo kuhusu utekelezaji wa Maazimio hayo.

Kuhusu Azimio Na. 13, Serikali imechambua Azimio hili kwa kina na imekubali kimsingi kwamba, Mikataba yote muhimu ya Serikali itakuwa inawekwa kwenye Maktaba Maalum ya Bunge ili Kamati za Bunge lako Tukufu ziweze kupata nafasi ya kupitia Mikataba mikubwa ya Kibiashara na ya muda mrefu chini ya Sekta zao na kushauri ipasavyo.

Kuhusu kuzihusisha Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya Mikataba mikubwa ya Kibiashara na ya muda mrefu, Serikali imeanza kufanya tafiti katika Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola ili kupata uzoefu zaidi utakaosaidia katika utekelezaji wa suala hili.


AZIMIO NAMBA 14:
“Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), na Katibu Mkuu, Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni. Aidha, Kamishna wa Nishati, Ndugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara mwaka 2004 kwenye Mradi wa bomba la mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua Kampuni hiyo kusitisha Mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa Zabuni ya umeme wa dharura haujaanza.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
a) Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki alijiuzulu mwezi Februari 2008 kwa kuwajibika kutokana na suala hili. Hata hivyo, kwa lengo la Serikali kujiridhisha zaidi kuhusu ushiriki na ushauri wake katika suala hili, Vyombo vya Dola vinaendelea kuendesha uchunguzi wa kina. Lengo ni kutaka kujua kama kuna rushwa yoyote inayomhusisha Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), ambayo ilijitokeza katika mchakato huu, ili hatimaye uamuzi stahiki dhidi yake uweze kuchukuliwa.

b) Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Arthur Mwakapugi ambaye alikuwa miongoni mwa Wajumbe watatu wa Kamati iliyoundwa na Makatibu Wakuu wa Fedha na Uchumi, Nishati na Madini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, naye amepelekewa barua ya kutakiwa ajieleze katika maeneo ambayo Kamati Teule ya Bunge ilibaini kuwa hakuyazingatia kwa maslahi ya Taifa. Hatua hii imechukuliwa kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Nidhamu katika Utumishi wa Umma na Misingi ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice), kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Bwana Mwakapugi amekwishawasilisha maelezo yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ndiye Mamlaka yake ya Nidhamu katika muda uliotakiwa.

Baadhi ya maeneo ambayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ametakiwa kujieleza ni yafuatayo:

(i) Kutozingatia maagizo ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na suala la ununuzi wa mitambo ya umeme wa dharura.

(ii) Kutozingatia ushauri wa kitaalam uliotolewa na PPRA kuhusu kufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 na Kanuni zake za mwaka 2005.

(iii) Kutoishauri Serikali ipasavyo kuhusu umuhimu wa kuifanyia uchunguzi zaidi Kampuni ya Richmond Development Company LLC ili kujiridhisha na uwezo wake kifedha, kiutendaji, kiutaalam na kiuzoefu ili kulinda maslahi ya Taifa.
Hivi sasa, Mamlaka yake ya Nidhamu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi, inafanya uchambuzi wa maelezo yake aliyoyawasilisha ili hatimaye maamuzi yatolewe kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.

c) Kwa upande wa Kamishna wa Nishati Bw. Bashir Mrindoko ingawa hayupo kwenye Kamati zote tatu zilizotajwa awali, Kamati Teule iliona kuwa, Bw. Mrindoko kwa kuzingatia nafasi yake kama Kamishna wa Nishati, naye achukuliwe hatua za nidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC. Kwa kuzingatia Azimio hili la Kamati Teule, Bw. Mrindoko amepelekewa barua ya kutakiwa ajieleze kwa kuzingatia Misingi ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice) na pia kulingana na Kanuni za Nidhamu katika Utumishi wa Umma.

Miongoni mwa maeneo ambayo Kamishna wa Nishati ametakiwa kujieleza ni kushindwa kutumia utaalam na uzoefu wake kumshauri ipasavyo Katibu Mkuu wake kuhusu uwezo wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC. Hii ni kwa kuzingatia kuwa, Kamishna huyu ndiye aliyehusika kuandika barua ya kusitisha Mkataba uliosainiwa tarehe 30 Juni 2004 baina ya Wizara na Kampuni ya Richmond Development Company LLC wa ujenzi wa bomba la mafuta la km. 1,150 kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, kutokana na Kampuni hiyo kukosa uwezo wa kifedha.
Bw. Mrindoko amewasilisha maelezo ya utetezi wake kwa Mamlaka yake ya Nidhamu katika muda wa siku kumi na nne uliotakiwa. Hivi sasa, Mamlaka yake ya Nidhamu inayafanyia uchambuzi maelezo yake ili hatimaye maamuzi yatolewe kwa mujibu wa Taratibu, Kanuni na Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002.


AZIMIO NAMBA 15:
“Utaratibu wa kuteua Wakurugenzi na Makamishna katika Wizara kuwa Wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi wa Mashirika yaliyo chini ya Wizara zao unazua mgongano wa kimaslahi na kudhoofisha usimamizi pamoja na uwajibikaji, hivyo Serikali iupige marufuku mara moja.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Ni kweli kuwa huenda katika baadhi ya maeneo, mfumo huu wa uteuzi wa Wakurugenzi au Makamishna kuwa Wajumbe wa Bodi za Mashirika ya Umma unaweza kuwa na matatizo. Hata hivyo, baada ya Serikali kuzingatia Azimio hili, imeona pia kwamba, zipo pia faida za baadhi ya Wakurugenzi au Makamishna kuwa Wajumbe wa Bodi hasa katika kusaidia kutoa msimamo na ufafanuzi wa Sera na Mipango mbalimbali ya Serikali. Kwa kuzingatia umuhimu huo, Serikali inaona ni vyema utaratibu huo uendelee lakini kila Bodi itaangaliwa kipekee. Pale itakapodhihirika kuwa ni kwa maslahi ya Taifa kuwateua baadhi ya Wakurugenzi au Makamishna kuwa Wajumbe katika baadhi ya Bodi, Serikali itafanya hivyo kwa maslahi ya Taifa letu.


AZIMIO NAMBA 16:
“Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mheshimiwa Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na Uongozi wa Nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake Kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vilevile, ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 ya Katiba kuangalia kama matokeo ya uchunguzi huu hayataathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge”.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Azimio hili lilitekelezwa mwezi Februari 2008 kwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu aliamua kujiuzulu kwa kuwajibika kisiasa kwa maslahi ya Taifa.


AZIMIO NAMBA 17:
“Msajili wa Makampuni (BRELA) aifute Kampuni ya Richmond Development Company (T) Ltd. mara moja kutoka kwenye orodha ya Makampuni halali Nchini.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Serikali imefanya uchunguzi juu ya Usajili wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC pamoja na Richmond Development Company (T) Limited ili kubaini uhalali wake na kutaka kujiridhisha kama usajili wake uliofanywa na BRELA ulikuwa kinyume cha Sheria za Nchi. Uchunguzi huo umebaini yafuatayo:

(i) Kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited ni Kampuni iliyosajiliwa na BRELA hapa Tanzania tarehe 12 Julai 2006 na kupewa Certificate of Incorporation Namba 57014 ili kuiwezesha kupatiwa leseni ya biashara ya uzalishaji wa umeme. Hata hivyo, uchunguzi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko unaonyesha kuwa Richmond Development Company LLC haikuwa imesajiliwa na BRELA.

(ii) Hakuna taarifa ndani ya BRELA zinazoonyesha kuwa, Richmond Development Company LLC iliyoshinda Zabuni husika, ilikasimu jukumu lake la kuzalisha umeme wa dharura kwa Richmond Development Company (T) Limited ambayo ndiyo ilisajiliwa Nchini kwa kusudio hilo.

(iii) Kutokana na utata huo uliojitokeza, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametoa ushauri juu ya Mamlaka ya BRELA ya kuifuta Kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited kwa kuzingatia Sheria ya Makampuni (Sura ya 212). Hivyo, kwa mujibu wa kifungu cha 215 cha Sheria hiyo, BRELA imekwishatoa notisi ya siku thelathini kwa Kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited kuwasilisha utetezi wake kabla ya hatua za kuifuta kampuni hiyo kuchukuliwa. Taarifa hiyo ya notisi iliyotolewa na BRELA haijajibiwa.


AZIMIO NAMBA 18:
“Wamiliki wa Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd wafunguliwe kesi ya jinai mara moja kwa udanganyifu na ujanja wa kuiibia Serikali”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Awali, Serikali ilimuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia kwa makini Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge; pamoja na kumbukumbu zote za Mjadala wa suala hili Bungeni, ili kubaini maeneo yenye Makosa ya Jinai ambayo yangewezesha Serikali kuwafungulia mashtaka Wamiliki wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd na Wawakilishi wao.

Baadhi ya maeneo ambayo yaliangaliwa ni pamoja na yafuatayo:
(a) Kampuni ya Richmond Development Company LLC kuwasilisha Taarifa za udanganyifu Serikalini kwamba wana uwezo wa kifedha, kiutendaji na utaalam katika kuzalisha umeme, jambo ambalo halikuwa kweli.

(b) Kuwasilisha Hati na Vielelezo vya udanganyifu kwa Kamati ya Serikali ya Majadiliano kuwa Kampuni ya Richmond Development Company LLC ina Mkataba wa Ubia (Consortium Agreement) baina yake na Kampuni ya Pratt & Whitney ambayo inajulikana kuwa na uwezo mkubwa Kimataifa.

Baada ya zoezi hilo kufanyika, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alishauri kuwa, pamoja na mambo mengine ipo haja kwa Serikali:

(i) Kufanya uchunguzi wa kina ili kuthibitisha kuwa Kampuni ya Richmond Development Company LLC haina uhai wa Kikampuni (Corporate Personality) na hivyo kujiridhisha kuwa, mambo yote yaliyofanywa kwa jina la Kampuni hii, yalikuwa batili. Hii ni kwa kuzingatia fungu la 320 la Sheria ya Makampuni (Sura ya 212).

(ii) Kufanya uchunguzi wa kina katika makosa yanayoonekana kuwa ya jinai kwa watu waliohusika katika uwasilishaji wa baadhi ya nyaraka na vielelezo vingine vya udanganyifu vilivyowezesha Kampuni ya RICHMOND kupata ushindi wa Zabuni hii.

(iii) Kwa kuwa Makosa ya Jinai hupelelezwa na Polisi, TAKUKURU, Mamlaka ya Mapato na Vyombo vingine ambavyo vimepewa Mamlaka hayo Kisheria, Serikali iagize Vyombo hivyo vya Dola vilivyopewa Mamlaka ya kufanya upelelezi na kukusanya ushahidi vifanye kazi hiyo. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka ya Jinai - (The Criminal Procedure Act Cap. 20 R.E. 2002);
Lengo la zoezi hili ni kujiridhisha na kupata ukweli na ushahidi wa kutosha unaoweza kupokelewa na kukubalika Mahakamani kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Ushahidi (The Evidence Act, Cap 6. R.E.2002).

Hivyo, hivi sasa Vyombo vya Dola ikiwemo Idara ya Polisi vimepewa kazi hiyo na vinaendelea kufanya upelelezi na uchunguzi wa kina wa nyaraka na hati mbalimbali zilizowasilishwa na Wahusika kabla ya kuchukua hatua nyingine dhidi ya Wamiliki wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd na Wawakilishi wao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.


AZIMIO NAMBA 19:
“Serikali ichukue hatua za kuviboresha na kuvitumia ipasavyo Vitengo vya Utabiri wa Hali ya Hewa na Kitengo cha Maji - TANESCO ili kuiepusha Nchi na Maamuzi ya zimamoto, ambayo uzoefu unaonyesha yanaiingiza Nchi kwenye hasara kubwa.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Hatua zifuatazo zinaendelea kuchukuliwa na Serikali kama mkakati wa utekelezaji wa Azimio hili:

(i) Serikali imeanza kuimarisha Wakala wa Hali ya Hewa Nchini kwa kutoa mafunzo na kuwapatia vifaa vya kisasa kama kompyuta, vifaa vya kupimia mvua na ununuzi wa mitambo ya kisasa ya mawasiliano na ya kuchambua takwimu za hali ya hewa. Mfano, hadi sasa Serikali imekwishanunua mitambo ya mawasiliano ya kisasa iitwayo Retin 4 na Snergie kwa ajili ya kuimarisha Utabiri wa Hali ya Hewa nchini.

(ii) Kuhusu ushirikiano baina ya Kitengo cha Utabiri wa Hali ya Hewa na TANESCO pamoja na Mabonde ya Maji ni mzuri, kwani kila siku TANESCO inapokea Taarifa za utabiri wa hali ya mvua na kuziingiza katika Takwimu za Msingi (data base) zinazoonyesha Mfumo wa uzalishaji umeme wa kila siku.

(iii) Vilevile, Serikali kupitia Mradi wa Maendeleo ya Sekta ya Maji (Water Sector Development Program) itaimarisha Ofisi za Mabonde ya Maji ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa Vitengo vya Maji vya TANESCO. Hii ni pamoja na kutoa mafunzo kwa Watumishi na kununua zana za kufanyia kazi kama vile magari na vifaa vya kupima kina cha maji, na wingi wa maji kwenye mito na mabwawa. Vifaa vingine ni vya kupimia mvua, maji chini ya ardhi, kupima ardhi na kuanzisha Mtandao wa Mawasiliano kwa njia ya kompyuta.


AZIMIO NAMBA 20:
“Serikali iendeshe uchunguzi maalum ili kubaini ukweli kama Taarifa rasmi ya TAKUKURU iliyotoa matokeo ya uchunguzi kuhusu mchakato wa Richmond ilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine na kama jalada halisi linalohusu Kampuni ya Richmond lililokuwa BRELA liliharibiwa na kuwekwa lingine kwa lengo la kuficha ukweli”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Dola wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu suala hili.


AZIMIO NAMBA 21:
“Ofisi ya Bunge ianzishe Maktaba Maalum itakayohusika na utunzaji wa Mikataba yote inayoingiwa na Serikali.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Serikali inakubali utaratibu huo na itatoa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa Azimio hili kama nilivyoeleza katika Azimio Na. 13.


AZIMIO NAMBA 22:
“Miswada yote inayowasilishwa Bungeni hasa Miswada ya Umeme na Mafuta, (The Electricity Bill, 2007 na Petroleum Supply Bill, 2007) izingatie changamoto zilizoonekana wakati wa mjadala wa Taarifa ya Kamati Teule”.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Miswada ya Sheria ya Umeme na ule wa Sheria ya Mafuta ilijadiliwa Bungeni mwezi Aprili 2008 na kupitishwa. Wakati wa Mjadala huo, ushauri uliopo katika Azimio hili ulizingatiwa kikamilifu.


AZIMIO NAMBA 23:
“Serikali iyafanyie kazi Mapendekezo ya Kamati Teule na kuliarifu Bunge kuhusu utekelezaji wake ndani ya miezi mitatu kuanzia tarehe 15/2/2008.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Hali halisi inaonyesha kuwa, jitihada zimefanywa na Serikali kuhakikisha Maazimio ya Bunge yanatekelezwa ndani ya miezi mitatu kuanzia tarehe 15 Februari 2008. Muda huo uliisha tarehe 14 Mei 2008. Hata hivyo, katika utekelezaji, imedhihirika kuwa, baadhi ya Maazimio yanahitaji muda mrefu kukamilisha mchakato wake wa utekelezaji hasa yale yanayohusu marekebisho ya Sheria na Mifumo mbalimbali ndani ya Serikali; na pia yale yanayohitaji kufungua mashtaka ya jinai au mashtaka ya makosa ya nidhamu.


HATUA ZA NIDHAMU KWA WATUMISHI:

7. Mheshimiwa Spika, kabla ya kumalizia naomba kutoa angalizo kwamba, katika kushughulikia suala hili, Kamati Teule ya Bunge katika baadhi ya Maazimio yake yanayohusiana na kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya Watumishi wa Umma waliohusika katika mchakato mzima wa Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND, imetumia maneno mbalimbali kama ifuatavyo:

Azimio Namba 5:
“………wawajibishwe na Mamlaka ya juu ya Nchi kwa kuchangia kuiingiza Nchi katika Mkataba wa aibu.”

Azimio Namba 7:
“……Maofisa Waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya Umma…..”.

Azimio Namba 9:
“…….wawajibishwe kwa manufaa ya Umma.”

Azimio Namba 14:
“……. wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni”.


8. Mheshimiwa Spika, Katika kutafsiri maana ya maelekezo haya, Serikali imeona kwamba, yanaweza kuwa na maana ya kushtakiwa Mahakamani kwa Makosa ya Jinai; ama kutumia Mamlaka ya Rais ya kuwastaafisha kwa manufaa ya Umma; ama kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Kanuni zake.

Serikali baada ya kutafakari kwa kina suala hili, imeona kuwa, katika mazingira ya suala hili, ni busara kutumia utaratibu wa hatua za mashtaka ya Nidhamu chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma. Utaratibu huu ni mwepesi na unaweza kusimamiwa kwa haraka zaidi, lakini bila ya kuathiri Misingi ya Haki Asilia (Natural Justice) ya Mtu Kupewa Haki ya Kusikilizwa Kwanza. Hii ni hatua muhimu sana kwani hata chini ya Mamlaka ya Rais ya kumstaafisha Mtumishi kwa manufaa ya Umma, taratibu zinataka Mtumishi apewe fursa ya kutoa maelezo ya kujitetea kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa. Hii inatuondolea hatari ya Serikali kushtakiwa kwa kutofuata Sheria, Kanuni na Taratibu kama ilivyowahi kutokea huko nyuma, ambapo baadhi ya Viongozi na Watendaji walistaafishwa kwa manufaa ya Umma kimakosa, na baadaye Serikali ikalazimika kuingia gharama kubwa ya kuwalipa fidia. Vilevile, hatua hii inaipa nafasi Serikali kupitia utetezi utakaotolewa kuona ni Watumishi gani wanaoweza kustahili kushtakiwa kwa Makosa ya Jinai kwa mujibu wa Sheria za Nchi.


HITIMISHO:

9. Mheshimiwa Spika, napenda kusema kuwa, yapo mambo mengi ambayo sisi kama Taifa tumejifunza kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mchakato wa Zabuni ya Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND, lakini pia na Mikataba mingine. Kwa kuzingatia hali hiyo, Serikali imeanza kulifanyia kazi suala la kuimarisha Mfumo na Uwezo wetu wa ndani wa Majadiliano ya Mikataba hasa ile mikubwa ya Kibiashara na Kiuchumi na ya muda mrefu yenye maslahi makubwa kwa Taifa letu kwa kuchukua hatua mbalimbali. Ofisi yangu tayari imepata maoni ya Wanasheria mbalimbali wakiwemo Mheshimiwa Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu; Mheshimiwa Johnson Mwanyika - Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na Mheshimiwa Nimrod Mkono Mbunge wa Musoma Vijijini. Maoni yao yatatusaidia sana katika kuimarisha Mfumo wetu wa Majadiliano ya Mikataba. Naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge hawa kwa maoni na ushauri wao mzuri sana.

Vilevile, nimepata nafasi ya kuzungumza na Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela, ambaye pia alinipa ushauri mzuri kuhusu namna mbalimbali za kuimarisha majadiliano katika Mikataba baina ya Serikali na Vyombo vingine vya Uwekezaji. Naomba kutumia fursa hii naye kumshukuru sana kwa mawazo yake.

Aidha, Ofisi yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria na Katiba kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), tunaendelea kulifanyia kazi jambo hili. Serikali inatarajia kwamba, jitihada hizi zitatuwezesha kubaini kwa kina mapungufu yaliyopo na kushauri njia bora zaidi za kuimarisha majadiliano yanayohusu Mikataba.

10. Mheshimiwa Spika, mwisho, natoa Wito kwa Watumishi wote wa Umma kufanya kazi kwa Uadilifu, Bidii, Uzalendo na kuwa makini katika kila kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali. Kwa upande wake, Serikali itajitahidi kuhakikisha kuwa Viongozi na Watendaji wote katika ngazi zote za Utumishi wa Umma wanafanya kazi kwa umakini na kuwatumikia Wananchi kwa kutanguliza mbele Maslahi ya Taifa letu.


11. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.