Wadau wa tamthilia ya Lalola najua jana tulikuwa pamoja mbele ya TV kuangalia hitimisho la tamthilia yetu kipenzi.Kila mtu alikuwa anataka kujua je ni nini hatima ya watu tuliokuwa tunawafuatilia kila siku…


Lola, Facundo, Natalia, Grace, Agire, Boogie, Gaston, na timu nzima ya staff wa Hi5.


Baada ya kuona hatima ya tamthilia hii swali linakuja ....

Je umejifunza nini kutoka kwenye tamthilia ya Lalola?

Siku njema,

Wenu Mdau wa Lalola


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Yaani nime miss ile mbaya, msaada katika tuka naomba alieona anihadithi jamani jamani natumai waturudia j'mosi mwe....mpenzi wa kipingi

    ReplyDelete
  2. Yaani jamani tamthilia hii ya LALOLA acha tu...
    offcourse ilikuwa ina viuongo vya hapa na pale like mambo ya witchcraft na nini lakini kwa kweli ilikuwa ni tamthilia iliyoburudisha sana na ilikuwa moja kati ya tamthilia zilizokuwa na visa unique as tumezoea kuona tamthilia katika tv stations mbalimbali zikiwa na visa vinavyojirudia rudia na tamthilia ikianza tu hata wiki haijafika unaweza kupredict nini kitatokea. Hii ilikuwa tofauti sana kwa tamthilia hii ya lalola.... Hopeful tamthilia itakayofuata nayo itatuvutia kama ilivyokuwa kwa lalola....
    Nitammiss sana Gastone na wazimu wake plus handsoome boy Facundo na most of ol Lalola mwenyewe... was a never miss wa hii tamthilia

    ReplyDelete
  3. Anon wa kwanza kabisa hapo juu... pole kwa kukosa sehemu ya mwisho maana ilikuwa ndefu hiyo na yenye msisimko.

    Sidhani kama ITV watairudia tena J'mosi hii hivyo acha nikumegee kwa ufupi.

    1. Boogie si unajua alikuwa anamzimia Grace, lakini akawa ameshushuliwa kuwa asubiri atapata saizi yake? Basi kumbe Grace alikuwa kishamwandalia kifaa ambacho kilikwenda kuchukua nafasi ya Grace kama mtangazaji mpya. Boogie safari hii hajauweka usiku, mtoto aliporipoti tu kazini jamaa kamwaga sera.

    2. Natalie na Gaston uongozi umewashinda. Staff wapya waliowaajiri wameshindwa kutengeneza gazeti. Badala yake wamekwiba kompyuta za Hi5 na vitu vitu vingine vya ofisini na kutokomea. Hi5 na Don Magazine kwishney.

    3. On the other hand wale staff wa Hi5 waliotimuliwa na kina Gastone (yaani Pato, Soledad, Gracileda, Julia na Nicolas) wameanzisha gazeti lao jipya... kituko kilikuwa ni kwamba ishu ya kwanza wameiandaa wakiwa bar... kwenye kale kaclub kao ka siku zote... lakini kikbwa ni kwamba gazeti limetoka na limeingia sokoni. Julia ndio amekuwa kama Meneja wao maana amerithi busara na ucheshi wa Agire ambao umesaidia wengine kufanya kazi kama timu.

    4. Agire na Grace wako honeymoon kwenye lile basi-nyumba lao. Ni mikasi mpaka six in the morning.

    5. Na mwisho kabisa Lola kakutana na Lalo lakini baada ya maongezi marefu kila mmoja akaona bora tu abaki kama alivyo. Hata hivyo mwishoni kulikuwa na suspense kubwa ya Lola kumtafuta Facundo ambaye alikuwa ameshauza nyumba na ameondoka. Ishu ni kwamba kulikuwa na eclipse (yaani kupatwa kwa mwezi) na Lola aliambiwa na mganga kuwa kama eclipse ikipita ilhali hajakutana kimwili na Facundo basi atageuka kuwa kitu kingine... hatarudi kuwa Lalo... atakuwa kitu kingine. Hivyo hiyo possibility ya kugeuka kuwa kitu kingine ndio ikawa imemuogopesha sana Lola akahaha usiku mzima kama fisadi anayekimbia mkono wa sheria kumsaka Facundo.

    Tatizo ni kwamba Facundo alikuwa katupa na simu yake maana ilikuwa inamtia simanzi na kumkumbusha Lola. Alikuwa ameshaamua kutambaa kabisa kutoka kamji kale akaanze maisha mapya mji mwingine... Hivyo kulikuwa hakuna contact.

    Hata hivyo mwisho kabisa akafanikiwa kumpata Facundo ambaye alikuwa bandarini akisubiri boti ije kumchukua.

    Wakakumbatiana.. wakakisi.. maneno ya mwisho ya Lola kwa Facundo ni.. "Facundo... I have been unsure of many things in my life... but one thing I am 100% sure right now is that my life is nothing without you! I love you."

    ReplyDelete
  4. Nilichojifunza ni kwamba Uchawi na imani za kishirikina zipo mpaka huko mbele kwa wenzetu, pia inawafundisha wanaume kuacha kuwa vicheche kama ilivyokuwa kwa Lalo ambaye alijifanya mjuaji, demu akaamua kumtengeneza kivingine.

    Kitu kingine ni kwamba, kumbe umbea ni kawaida ya media house zote duniani? manake Hi5 kulikuwa na wambea balaaa! Na mapenzi ya kuvurugana usiseme kama TSN tu.

    Halafu eti kumbe siku ya kupatwa kwa mwezi kunaweza kubadili maisha ya mtu? hiyo nilikuwa sijui wadau nisaidieni mwenzenu.

    ReplyDelete
  5. Anony no 3 Nakushukuru sana .... umenifanya mwili usisimke kweli nime miss lakini nawe ni msimuliaji mzuri... msg delivered. Once again asante sana. Hivi mtu akitaka kupata epsodes zote zinapatikana wapi ni worth it kuwa nazo home ukiwa bored mtu unajirusha....anony 1

    ReplyDelete
  6. ...My favorite character was...wait for it...GASTON!!! The Guy was simply crazy and always managed to have my ribs in stitches!! Mwehu si mwehu basi ilimradi ujuha mtindo mmoja! I will miss him.

    ReplyDelete
  7. Yes Gaston hata mimi namkubali... the guy knows how to play office politics.

    Mimi nilikuwa naipenda sana tamthilia hii maana inaonesha hali halisi ya maofisini.

    Ukitaka ukubwa ... umeneja ... sometimes you have to play it dirty, otherwise utashangaa walioingia juzi juzi wanakuwa promoted wakati wewe bado unasota!

    Kwa kweli sijawahi kuona tamthilia bomba kama hii ... big UP kwa ITV kwa kutuletea burudani.

    ReplyDelete
  8. Third rate sop opera for bongolanders consumption!! Thanks god the cridpy, dubbed voices are over!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...