Makamu mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid akizungumza na wanahabari wakati alipotoa tamko la tume hiyo kulaani kitendo kilichofanywa na mkuu wa Wilaya ya Bukoba cha kuwacharaza viboko walimu wa shule za msingi za Katerero, Kanazi na Kasenene mkoani Kagera kulia ni Bernadeta Gambish Kamisha wa tume hiyo.
picha hii ya mdau ilibandikwa hapa wiki iliyopita kuzungumzia mandhari nzuri ya eneo hilo.

Basi bwana, juzi balaa lilizuka katika shule ya msingi za katerero, kanazi na kasenene mkoani kagera ambapo walimu walichapwa bakola mbele ya wanafunzi wao kwa amri ya mkuu wa wilaya kwa kile kilichodaiwa walimu kushindwa kuwajibika ipaswavyo kiasi cha kushika nafasi ya mkiani katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba.


habari toka mkoani kagera zinasema chama cha walimu kimeamua kumfikisha mkuu huyo wa wilaya mahakamani kwa kitendo hicho ambacho wamekitaja ni kinyume na utawala wa sheria.
wadau hii imekaaje?


TUME YA HAKI ZA BINADAMU YATOA TAMKO!

Tume ya haki za binadamu na utawala bora imeshtushwa na kusikitishwa sana na taarifa kwamba mkuu wa wilaya ya Bukoba Bwana Albert Mnali, amewachapa viboko walimu wa shuli tatu za Katerero, Kanazi na Kasenene katika mkoa wa Kagera.
Kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa mujibu wa sheria za nchi hususan katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na mikataba ya kimataifa inayolinda haki za binadamuna misingi ya utawala bora ambayo tanzania imeridhia.
Ibara ya 13(6) (e) ya inatamka kama ifuatavyo kuhusu adhabu:"ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama wau kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha."
Tume ya haki za binadamu na utawala bora ambayo ina mamlaka ya kikatiba inalaani vikali kitendo hicho kilichofanywa na mkuu huyo wa wilaya ambaye moja ya majukumu yake ni kulinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
Uvunjaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora uliofanywa na mkuu huyo wa wilaya ni pamoja na
- Kutoa adhabu isiyostahili kwani adhabu ya viboko hutolewa na mahakama tu tena kwa kosa la jinailililobainishwa kisheria;
- Kutoa adhabu ya kutweza au kudhalilisha utu ikiwemowalimu wa kike kucharazwa viboko;
-Kuwapa walimu adhabu bila kufuata taratibu za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha maafisa elimu wa Wiliya na Idara ya Utumishi wa Walimu;
Kutumia vibaya madaraka aliyokasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na akala kiapo.
Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora inasema kutokana na kitendo hicho cha aina yake na cha aibu hapa nchini kimeleta athari kubwa kwa walimu ikiwemo kuwavunjia heshima walimu kwa wanafunzi wao, familia zao na jamii kwa ujumla pamoja na kuwavunja moyo katika kazi zao za kila siku.
Hata hivyo ingawa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani kitendi hicho cha Mkuu wa Wilaya, inawataka walimu kuzingatia maadili ya kazi yaoili nao wawatendee haki watoto ya kupata elimu bora badala ya kuwa watoro, wazembe na walevi kama walivyotuhumiwa.
Imetolewa na
Jaji Kiongozi Mstaafu
Amir Ramadhani Manento
Mwenyekiti Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Kwani tunaishi karne gani jamani, na walimu ilikuwaje WAKUBALI KUCHAPWA BAKORA mbele ya watoto wao?Makubwa haya wajameni.Haya BUKOBA HUKOOOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  2. Kanuni za natural justice zinasema huwezi kuhukumiwa pasipo kupewa nafasi ya kujitetea. Walipewa nafasi ya kujitetea? Vilevile huwezi kuwa polisi, mwendesha mashtaka na hakimu katika kesi moja. Mkuu wa wilaya alifanya yote hayo.
    Sijui kwa nini wanaendekeza kupiga Katerero. Zipo njia za kuboresha elimu bila bakora kama vile kuwalipa waalimu haki zao kwa wakati na kuhakikisha shule zote zina vifaa vya kutosha na waalimu wa kutosha.

    ReplyDelete
  3. Siamini kwamba mwalimu anaweza kuchapwa fimbo mbele ya wanafunzi wake. Kuchapwa viboko katerero kunaweza kuwa na maana nyingine. Kama huamini wasiliana na huyu rafiki yangu na mtani wangu wa jadi: l.r.katereric@hotmail.com

    ReplyDelete
  4. Jamani hiyo yenyewe kuwapiga viboko wanafunzi sivema,iwe walimu hakika TANZANIA walimu wanaendeshwa kikondoo,jamani huu UTUMWA bado upo.Nimeona kwa bbc inatia uchungu na kusikitisha mno,hapo si mkuu wa wilaya tu hata waziri wa elimu anatakiwa ajieleze.

    ReplyDelete
  5. teh teh teh, hao walimu kwanini walikubali kuchapwa mbele ya wanafunzi? inaelekea waliridhika na hiyo adhabu,mbona kwenye kudai pesa waligoma iweje wakubali kuchapwa?????
    sisi tunaumiza kichwa walipwe vizuri na wapate vitendea kazi wanaturudisha nyuma tujadili adhabu ya viboko ambayo ilishafutwa mashuleni. kazi kwenu wadau

    ReplyDelete
  6. Nipo huku Iceland tukasikia khabari hii kupitia radio bbcworldservice ndani ya meli, jamaa wananiuliza ikiwa walimu wanacharazwa bakora! Je watoto huko Tanzania wao wanapata adhabu gani?

    Nikajibu wanapata corporal punishment, jamaa mbavu zikawauma maana jibu ni lile lile.

    Mdau
    jijini Reykjavik
    Iceland

    ReplyDelete
  7. sishangai walimu kucharazwa fimbo maana wao ni watanzania kama wengine na wengi tuna 'hulka' ya kuwema 'hewala bwana mkubwa'.

    Waache watiwe adhabu ya mdachi (Jerumani) hamsa kumi papo kwa hapo , mambo ya wizara au DC kupoteza wakati kuandikiana barua za karipio au tume ujieleze ni kupoteza pesa na wakti.

    ReplyDelete
  8. Hao ni watu wazima kelele namna hiyo je sasa kwa watoto wadogo kuanzia darasa la kwanza inakuwaje? Sio jambo zuri lililotendeka hapo lakini na wao wamepata joto ya jiwe hivyo adhabu za fimbo ipigwe marufuku hata kwa wanafunzi pia

    ReplyDelete
  9. Ukweli ni kwamba walimu wengi tanzania wanastahili kuchapwa. Mi ni engineer niko UK nakumbuka nikiwa secondari walimu vijana walikuwa wanapiga wanafunzi bila sababu za msingi. nilihesabu mwanafunzi akichapwa fimbo 30. Nilipoeanda chuo sikuwahi kujiamini wala kuliza swali darasani kutokana na mwalimu kuwa adui wangu. kama wazungu wasemavyo in life self confidency might be the key for you to make it. Kazi ya mwalimu ni kumtayarisha mwanafunzi na dunia na fimbo haisaidii katika hilon ha ndo maana uswahilini watoto wengi wanaishia umasikini kwa sababu ya matusi waambiwayo kwa mfano "wewe taahira mkubwa" utakuwa masikini maishani" "mbumbumbu" Mnategemea lini watoto wataweza kukua na kujitegemea? fimbo shuleni zipigwe marufuku na kabla ya kumchapa mtoto lazima mwalimu apate kibali cha mzazi. hongera mkuu wa wilaya finaly walimu wamepata tamu ya asali yao!!!

    ReplyDelete
  10. Looooo! Salaa-ah la!!! Jamani mambo gani haya tena? TZ kwa vituko!!? Haijambo. Katerero namna gani tena mnachapa waalimu? Hii story imetemwa na BBC-this means Dunia mzima iko jua jabo hii!!!!

    Nakumbuka sana story ya kitabu cha kusoma cha darasa la NNe wakati huo- Story title: "Siku ya Gulio Katerero":

    Poleni sana Watandikwa.

    ReplyDelete
  11. Waache hao Walimu wachapwe bakora tu na tena naomba wawe wanachapwa mbele ya wanafunzi wote, Mbona hao walimu wanapowachapa wanafunzi huwa hawasemi ni ukiukwaji wa haki za binadamu? huyo mkuu wa wilaya nampa hongera sana kwa kuamuru hao walimu wakung'utwe bakora. Mchapa nae Huchapwa na hiyo ndio imewakuta walimu.

    ReplyDelete
  12. Hawa Waalimu walikuwa wanachapwa na koplo wa jeshi kumbe. Waliokuwa wakikataa walikuwa wakipigwa mtama mkali na kurushwa ni, na wanapogusa chini tu, viboko mfululizo! Hongera J.K kwa kumtimua huyo mkuu. Sheria ichukue mkondo wake pia

    ReplyDelete
  13. wadau
    Hiki ni kiwango cha unyonge cha kutisha mno!
    Hapo ndipo unapoweza kuelewa kwa nini taifa la Tanzania kamwe halitaweza kupiga hatua, wananchi wetu ni waoga mno!
    Huu ni urithi tuliorithi kutoka huko tulikotoka, msimu wa chama kimoja wa awamu ya kwanza.
    Lakini cha kujiuliza ni kwamba, ikiwa walimu wa Tz katika karne hii ya milenia ni waoga kiasi cha kushindwa kumfinyanga finyanga huyu mkuu wa wilaya na njagu wake, wanawezaje kuingia darasani na kuwamudu wanafunzi wao?
    Nia yangu si kuwabeza walimu wenzangu hawa (mimi pia ni mwalimu hapa Ukerewe), lakini ukweli ni kuwa mmeidhalilisha fani na [profesheni yetu kwa kukubali kudhalilishwa na mheshimiwa huyu. Poleni sana lakini ni lazmia muwe ngangari otherwise mtakuwa wanyonge maisha!

    ReplyDelete
  14. SERIKALI IME-ACT HARAKA SANA KUHUSU SUALA LA WALIMU KUCHARAZWA VIBOKO.NI SAWA SERIKALI IMEONA HILO JE SUALA LA UFISADI MBONA ILIKAA KIMYA MUDA MREFU BILA KUSEMA CHOCHOTE HADI WAPINZANI WALIPOLITOA BUNGENI NA BADO IKASHINDWA KUAMINI KWA SABABU ZINAZOZIJUA YENYEWE.NASEMA WALIMU HAWAPASWI KUCHARAZWA BAKORA LAKINI WATIMIZE WAJIBU WAO WA KUFUNDISHA SIO KUKIMBIA VIPINDI NA KWENDA KWENYE BUSINESS ZAO.KWA USHAURI WANGU WALIMU HAO WANGEULIZWA IMEKUWAJE SHULE ZAO ZIMESHIKA NAMBA ZA MWISHO HALAFU WAWAJIBISHWE KWA KUONYWA AU KUFUKUZWA KAZI LET THEM BE RESPONSIBLE.

    ReplyDelete
  15. jamani aibu,mwalimu sawa na mama au mzee leo walimu wanapigwa mbele ya wanafunzi tena ni kiongozi katoa amri hio,jamani mbona tanzania inatisha mara mafisadi mara walimu kupigwa bakora hadharani mishahara hamuwapi na fimbo munawapiga.mnadhania watapata moyo tena wa kuwasomesha watoto wetu,kwanza kusomesha jamani kazi sio ndogo walimu wanahitaji kupewa hongera na kushukuriwa sio kudharauliwa.

    ReplyDelete
  16. mdau wa pili umesema vema. Kama vile umesoma sheria. Safi sana

    mtoto

    ReplyDelete
  17. Watu wote ni sawa,kwa nini adhabu ya bakora kwa wanafunzi wote isiangaliwe pia?
    Sam.

    ReplyDelete
  18. Sijawahi kusikia!! Hii ya leo sasa kali duh! eti mwalimu naye anacharazwa enh?

    ReplyDelete
  19. Misingi (principle) narudia MSINGI/PRINCIPLE ya DC kwa wakati (stage of development) tuliopo na hali tuliyonayo (gross bureacracy, lazyness, bribery, fraud, mafisadi, never ending judicial processes, politically tainted judiciary etc)inafaa. Kwa kweli waTz tunahitaji dikteta wa kimaendeleo au (an authoritarian leader) kuweza kupiga hatua hata kidogo.

    ReplyDelete
  20. marafiki zangu wananitania sana na kuniambia hao walimu ni watu waina gani mpaka wakakubali kuchapwa?
    alafu unajua watu wengi wanasikiliza bbc aibu tupu? huyo dc na polisi waliohusika wote wanatakiwa wachukuliwe hatua. maana yake juzijuzi mtu aliogeshwa na wanajeshi kwenye dimbwi, vyombo vya dola vinawanyanyasa sana wananchi

    habari bbc ndio hiyo
    http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/africa/7888158.stm

    ReplyDelete
  21. BUKOBA KUMBE HAKUFAI. WAULIZENI JIRANI ZENU WANYARWANDA WENZENU WANAPIGANA, ETI NYIE MKABAKI MMESIMAMA TU,

    ReplyDelete
  22. Haitoshi kumhachisha kazi tu, mkuu wa wilaya kwani akifika nyumbani kwake atampa kibano hata mke wake.Nafikiri apate adhabu zaidi ya hapo.Kwasababu sisi tuliyo kwenye nchi za wengine ambako hata ukimrushia mbwa jiwe unapewa adhabu,tunajisikia aibu sana na kutaka kujuwa huyu kiongozi alichaguliwa kwa vigezo vipi. Kwani hamna maadili ya viongozi. maana amedhalilisha taifa letu.

    ReplyDelete
  23. HONGERA MKUU WA WILAYA HATA NINGEKUWA MIMI NAWATANDIKA TENA KISASAWA.BILA BAKORA TANZANIA KAMWE HAITAENDELEA.....NA ZOMBE NAYE NINGEMKATA KICHWA KWA WEMBE BUTU.
    LOWASA NA CHENGE NA MAFISADI WAKUBWA WENGINE NINGEWA VUA NGUO NA KUWATUPA KWENYE SIAFU WAFE POLEPOLE KWANI WAMEUA WANACHI WENGI KWA KUWAKOSEHA HUDUMA MUHIMU ZA AFYA....AJABU WATU WAMESHUPALIA TU VIBOKO TUWILI TU,JE HAWA WAUAJI..UNAFIKI TU,HAYA TUONE KAMA TUTAENDELEA KWA MITAJI HII....

    ReplyDelete
  24. SEMENI YOOOOOOOOOOTE LAKINI NAMPONGEZA SAAAAAAAAAAAANA DC. SIO SIRI WALIMU WA TANZANIA NI WACHACHE WANOJITUMA. WENGI KAZI YAO NI KULA VITUMBUA OFISINI NA KUAGIZA WANAFUNZI WAWAUZIE VISHETI, KASHATA, ASHKIRIMU, BISI NK. WAO NI SHUGHUKI HIYO TU HAKUNA NYINGINE. WAKIKAA OFISINI NI GUMZO MPAKA JIONI.

    ReplyDelete
  25. aiseee hii safi saaaaana kumbe DC MJESHI??ndo maana?mana nilishtuka mtu wa kawaida anatoa wapi hii courage?

    wajeshi juuuu,itabidi mpewe vitengo maalumu kwa UFISADI ILI MUWASHUGHULIKIE MAFISADI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...