Huyu ndiye jabali la muziki marijani rajabu katika enzi za uhai wake akiwa kijana mdogo bado na kabla ya kuanza shughuli za muziki. Alianzia bendi ya stc na baadaye safari trippers kisha dar international, akifuatia na Afriso kabla ya kuaga dunia. Alifariki March 25, 1995 na kuacha kumbukumbu isiyofutika miongoni mwa wapenzi wa muziki

kaka habari za mihangaiko?
nimekutana na link hii

ambayo nikiwa kama mpenzi wa muziki wa dansi wa enzi za kina mzee Maneti kwa kweli imenigusa sana, pamoja na kwamba ni mashairi peke yake.ningependa kuiweka hapa ili na wadau waweze kujikumbusha kidogo.

Ama kweli za kale ni dhahabu..

MdauThessaloniki

----------------------------------------------------


Georgina - Safari Trippers (Marijani)]

[Wote]
Ooo Georginaaaa....
Siku uliyoondoka

uliniacha nalia na machozi
Umekwenda kuishi mbali nami

Georgina wa mamaaaa
Sipati usingizi

nikikumbuka

tulivyoishi mimi nawe Georginaaaaa
Ooo Georgina.......
(repeat Wote)

(Chorus)
[Wote]
Umeondoka Georgina

umeniachia masikitiko
Georgina Georgina oooo
(repeat)

[Marijani]
Nauliza Georgina oooo
Ni lini utarudi? oooooo
Uniondoe wasiwasi...oooooooo
Georgina wa mama aaa
Georgina Georgina oooo

(Repeat Chorus)


(Gita) Tatilalala

titiliilitiliiiiilii

tatilalaaa titilaaaa...

tititutiliiii talialaa

tititutililaaaalliaa

tilililililililiiiii

tatitalaaaa...


(Rudi mwanzo)

---------------------

Dah! hadi raha manaake. Asante mdau kwa kutupa link hii. Ingependeza kuwepo na siku ya kukumbuka wanamuziki kama hawa kwa shoo moja kali itayojumuisha waliofanya naye kazi na kizazi kipya.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Hivi huu mwimbo aliimbiwa nani haswa? maana nakumbuka kuna fammily moja ilikua inaishi Hill Road,Oysterbay , wanasema aliimbiwa binti wa mzee wa nyumba hiyo ambaye naitwa Gergina nikweli? huyo mzee anaitwa Mahiga , msaada tafadhali

    ReplyDelete
  2. Asante mdau kwa kweli lyrics ya nguvu hasa hizo za mwisho mwisho sijui ndio trumpet zenyewe, asante kwa kunifurahisha asubuhi.

    ReplyDelete
  3. jamani is it true that marijani kafariki 1995?

    ReplyDelete
  4. hivi wadau mi nimshamba kidogo kwenye swala hili .et ni nani anaye tunza nyimbo za vijana wa zamani ? kama hamna je hazitzpotea na kusahaulika . na sijawa kusikia hiyo taadisis ikizitangaza kuwa inauziuza. tuwaenzi basi hawa kwani wana vitu vizuri sana mi navizimia sana . wale basi matunda yao watoto au ndugu zao. asante michuzi umetukumbusha mbali sana

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli nimefalijika sana kwa kuona picha ya jabali la muziki hapa tanzania, japo kuwa inaonekana ni ujana mno lakini inapendeza kuiona.
    jabali la muziki marijani shaaban.tutamkumbuka sana kwa tungo za maana na zilizokwenda shule. huo ulikuwa ni wakati wa muziki kweli wa bongo. kuhusu huu wimbo wa gergina, ni historia ya kweli. huyo dada alikuwa ni miongoni mwa wasichana warembo sana kwa wakati ule na inasemekani ni kweli marijani alikuwa na uhusiano wa kimapenzi. mimi nilisimuliwa na rafiki yangu mmoja ambaye kwa sasa ni lecture wa chuo fulani.aliniambia kuwa alikuwa karibu na marijani na alikuwepo hiyo siku geogina alipokuwa akiondoka kwenda chuo fulani cha uhazili. ilikuwa ni masikitiko kwenda mbele.

    ReplyDelete
  6. Dah Georgina naupenda sana mwimbo safi kabisaaa, hata nikiwaga mitaa ya Lion pale weekend kwa wazee wa TANGO, burdaniiiiiiiiiiiii!!!!

    Baunsa mwenyewe!!!!

    ReplyDelete
  7. Yes zinatukumbusha mbali, but mie ningefaidi kama nigepata kuzisikia zaidi, any one knows ntazipata wapi?

    ReplyDelete
  8. TAMBAZA BOY HUYO

    ReplyDelete
  9. Marijani Rajab alikuwa mwanamuziki hodari mwenye kipaji sana cha kutunga na sauti nzuri!Hata mimi huwa nazikumbuka nyimbo zake ukiwemo ule wa "Mkuki Moyoni" bado unavutia sana masikioni kuusikiliza.Imenikumbusha mbali sana wakati ule bado tukiwa wanafunzi wa chuo kikuu dar es salaam miaka ya 1973 na 1974 na tulipenda sana kwenda hoteli ya Forodhani ambayo sasa imegeuzwa chuo cha utalii pale karibu na jengo la NDC au wizara za Nje kama sikosei,wakati huo Marijani akipiga na bendi ya safari trippers ikiongozwa na Mussa mpiga solo mahiri sana sana !Zile siku hazitasahaulika.Utacheza dansi hadi saa tisa usiku kisha utarudi kwa mabasi ya UDA toka Posta hadi Chuo Kikuu,fikiria,siku hizi itawezekana?Na pesa yenyewe ilikuwa kidogo sana.Ukimwi wakati huo hakuna,mechi zilikuwa kali sana !Mungu amlaze pema peponi Marijani Rajab,jabali la muziki tanzania!Kwa wale waliomjua toka utotoni,alijitahidi sana na kuwaacha wenzake kwa mbali sana!

    ReplyDelete
  10. HILO NDILO JABALI LA MUZIKI HAKUNA MWANAMZIKI YEYOTE TANZANIA ALIYEFIKIA KIWANGO CHAKE
    HATA MBARAKA MWISHEHE NI CHA MTOTO.
    KATUNGA NYIMBO LUKUKI ZA AKILI

    ReplyDelete
  11. Ahhh bro Michu hii ni noma, wadau wekeni na sauti zake kabisa

    ReplyDelete
  12. Mbaraka Mwaruka Mwinshehe naye alikuwa katika enzi zake alikuwa Moto wa Kuotea mbali!Alikuwa mahiri sana katika kutunga,kuimba na huku alipiga solo!Na ni mwanamuziki pekee hapa nchini aliyeweza kupiga gitaa la nyuzi muki na mbili la "Hawaian Guitar" ambalo kwa wakati huo ni Dokta Nicco Kasanda,mpiga solo mashuhuri bara zima la Afrika akiwa na bendi ya Afrisa International ya Congo Kinhasa enzi hizo!Mbaraka Mwinshehe ni mwanamuziki wa kwanza hapa Tanzania aliyeweza Kulimudu gitaa la Solo na wakati huo huo akiimba kwa hisia kali bila kupoteza mwelekeo!Tungo zake zilikuwa Tamu sana na za kuvutia kwa wale wazee wenzangu waliokuwa wakitinga katika kumbi za maonesho yake.Mbaraka alikuwa "role model" ya wanamuziki makinda hapa Tanzania.Tuliweza kumfananisha wakati huo kwa upigaji wake na Franco Makanda Makiadi wa Le TP ok jazz pia ya Congo Kinshasa!Wakati uimbaji na upigaji wake Mbaraka ulielekea kwa Franco wa OK Jazz,uimbaji na upigaji wa Marijan uliekea zaidi kwa kina Joseph Kabaselle Ya Npanya,Peppe Kalle na kiasi fulani kwa Rochereou Tabu Ley MAJABALI YA MUZIKI BARANI AFRIKA!Kwa bahati mbaya sana Mbaraka muziki wake ulithaminiwa sana nchini Kenya na hata Congo kuliko hapa kwetu Tanzania.Muziki wa Marijani ulikuja tukuka sana na watu kutambua kwamba kumbe Marijan alikuwa mwanamuziki mahiri na aliyekamilika kila idara BAADA YA KIFO CHAKE.Lakini alipokuwa hai watanzania hawakumpa ile support tunayoiona kwa wenzetu BanaCongo kwa wanamuziki wao!Bongo bado tuna matatizo sana ya kuwanyanyapaa masupa staa wetu hadi pale mtu atakapo tutoka duniani ndipo shamra shamra zitakapo anza kwa vifijo na nderemo!----tonnie pappaa--

    ReplyDelete
  13. Mi nakumbuka niliona na kusikia ktk kile kipindi cha usiku ITV wanawekaga mizilki ya kitanzania nakumbuka siku moja wakaweka hiyo ya marijani lakini yeye alishafariki, wakawa wanamuhoji mmoja wao kuhusu wimbo huu.Yeye akasema huyo dada alikuwa mshikaji wake kweli na sio wa Marijani na walipendana sana, lakini wazazi wa yule dada wakaona ule uhusiano kama no uhuni, si unajua tena kizamani...wakamchukua binti yao na kumpeleka mikoani, yule kaka akaumia sana na ndo akatunga ule wimbo kwa masikitiko makubwa kwa kunyang'anywa tonge mdomon...lakini na yeye alifariki baadaye kidogo siku zilipoenda mbele...na wla hakuwa mchuchu wa Marijani..Pia unaweza kuwauliza nadhanii ITV au nadhani Television ya Taifa siku zile watakuwa na kumbukumbu hiyo naamini

    ReplyDelete
  14. Marijani Rajabu hana mfano wake. Alikuwa jabali la kweli la Muziki. nani ana habari za yule mpiga solo wake mashuhuri David Mussa??

    ReplyDelete
  15. tatilalalalaa lililili
    tallalaaaa oooooooo

    jamani!!wee mdau Thessaloniki nataka tukutane basi mana siNAAAAA mbaVUUUUUUU,,,khaaa

    nyimbo za zamani bwana sio now,adi gospel ni kituko

    ReplyDelete
  16. AMA KWA HAKIKA MICHU UDONGO UMECHUKUA WATU!KUNA SIKU PALE PRINCESS BAR UWANJA WA NYUMBANI WA SOKOMOKO MPIGA BESI CHRISTIAN KAZINDUKI HAKUTOKEA ALIPATA AJALI YA PIKIPIKI,DANSI LIKAWA NA HATIHATI KUPIGWA TUKATOKA MASHABIKI MPAKA GETAWAYS KWENDA KUMUIBA MPIGA BASS WA TP SANTAFE KIJANA WA KIZAMBIA JOSEPH MULENGA AKA KING SPOILER NAKUMUKA TIMU NZIMA YA TRIPERS IKIONGOWA NA,DAVID MUSA,SELEMANI KILINGO,MAHDI TUMBO,MSIBA ABDALA,ALLY RAJABU,JOJO,MOHAMEDI KASIM,MAKATA,MWARAMI NA MZEE MZIMA VULY HEND MSAUZI AMBAE AMEMALIZIA KUPIGA SAX NA LUCKY DUBE,WAKATI HUO MBUNGE WA TAGETA NAKUMBUKA ULKUA NYANDA KWENYE MECHI ZA CHANDIMU MITAA YA AGREY,OH!MY GOD THOSE DAYS WE ACHA TU.

    ReplyDelete
  17. Dozza (Doser) Marijani Rajabu Mwana wa Manyema Jabari la Muziki toka enzi za SOKOMOKO na vibao moto moto:

    "..Yule mwanamwali hanifai mwenzenu.."

    "..Sauti yako nyororo naipenda unapoimba, inanikumbusha mbali sana. Hebu wee Kaka imba.."

    "..Niliporudi rafiki sikumkuta na vitu vyangu nyumbani vimeondoka. Oooh kumbe rafiki si mtu mwema. Kwa majirani wote nimeulizia. kaondoka siku nyingi wamenambia, kaondoka yapata wiki ya piliii.."

    "..Juzi juzi walikuja wazee na mengi mengi kunieleza, Ooh Maria Umenishinda.."

    "..Mwanipa mume haraka haraka masomo jee? Samahani, samahani, samahani Baba na Mama sitaweza kuolewa na miaka kuminambili.."

    "..Habari zako nimezipata kutoka kwa walimu zako kwamba siku nyingi zimepita na wewe shule mbona huonekani.."

    "..Hekoo Ndugu Nyerere, Hekoo Ndugu Kawawa..Heko Sheikh Abeid karume hatutakusahau kamwe mawazo yako na vitendo bado vipo.."

    "..Oooh Georgina siku uliyoondoka uliniwacha nalia na machozi. Umekwenda kuishi mbali nami Georgina wa Mamaa. Sipati usingizi nikikumbuka tulivyoishi mimi nawe Georgina..ahh.."

    "Mpenzi wangu nakueleza, uaminifu wako waupoteza..Unanitesa, unaniumiza unanichoma mkuki moyoni.."

    "..Khanifa maisha yamekushinda tazama unavyoishi sasa.."

    "..Ukweli Dada husemwa. Nimeona leo nikuambie kweli. Nimeona watu wavivu sana lakini uvivu wakoo wee Dada umezidi..Mi nakuomba tafadhali mi nakuomba hebu fanyafanya dada tukacheze sokomokooo.."

    "..Dada Mathilda punguza nyendo za usiku na mchanaa aah..Mathilda ooh mtunze mwanao Mama. Uhuni wako hauna faida Mathilda utaua.."

    "..Chanzo cha nyumba nzuri na gari uwe na pesa ooh..Nazo pesa utapata wapi kazi huna? Alinacha mbaya hizoo.."

    "..Inakuwaje Bibi na Bwana hamkai vizuri ooh? Munawaacha watoto wenu wakivunja milango na madirisha! Nikisema munasema mi na mudomo.."

    "..Kwa jina Salama, Salama nakuomba Salama nakuita Mama. Poa kaka poa. Poa Salama.."
    Wimbo huu ndiyo unaotuthibitishia kwamba kweli Dozza na Pepe Kalle walikuwa wakimzimina. Ukisikiliza ule wimbo wa Nazoki wa Empire Bakuba utasikia ghani ya wimbo na uimbaji wa nyimbo huo utaamini Salama na Nazoki zilivyofanana ni kama Kulwa na Doto.

    Baada ya SOKOMOKO likaja SUPER BOMBOKA na;

    "..Kweli sikitiko sikitikooo.. kuona wale wenzetu wanateseka Mamaa wapo katika makucha ya watu weupe wachache, watu makatili wa wa roho za watu, watu wasiothamini utu wa mtu..Witoo! Witooo yoyo witoo Afrika lazima tuikomboa jamaa.."

    "..Zuwena.."

    "..Vicky.."

    "..Siwema.."

    "..Kristina.."

    "..Mayasa.."

    "..Usia wa Baba.."

    "..Masudi.."

    "..Mzee Gerald na Mzee Said.."

    "..Ndoa ya lazima.."

    "..Pombe siyo chai.."

    "..Dunia imani imekwisha.."

    Halafu na Tanzania All Stars

    "..Samora / Rambirambi kwa ndugu zetu wa Msumbiji.."

    Etcetera, etcetera, hits upon upon hits. Vigongo juu ya vigongo. Moto juu ya moto

    Namkumbuka mara ya mwisho nilipomuona Mbowe Hotel (Bilicanas) wakati wa Tanzania All Stars. Ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kumuona. Mwaka 1995 nikawa napanga kuandika makala juu ya hayati Dozza Mwana Manyema yenye kichwa cha habari Kumomonyoka kwa Jabari. Azima yangu haikutimia. Sikumuwahi akafariki mwezi Machi nami nikawa Dar mwezi Juni. Nikasikitika kwa nini sikupiga naye picha alipokuja chumba cha The Tanzanites Band pale Kilimanjaro Hotel siku chache kabla ya tukio la Mbowe Hotel. Nakumbuka alipiga picha na Marehemu William "Kizibo" Chiduo. Namkumbuka Marehemu Madi "Babu" Tumbo na masihara na kicheko chake.

    Mwenyezi Mungu awarehemu Marehemu wote kwa amani. Amen.

    PS/ Nina miziki mingi sana ya Marehemu ambayo ninahitaji sana msaada wa kuihamisha toka kwenye kaseti kwenda kwenye cd. Pia ninamjua mtu ambaye ana miziki mingi zaidi yangu ya kuanzia STC, Trippers mpaka Dar International. Zaidi namjua mtu ambaye ana video ya Marehemu akiwa na Super Bomboka.

    Ukiwa na nia ya kweli ya kushirikiana nami wasiliana na Muhidin Michuzi halafu Muhidin atauunganisha. Asante.

    ReplyDelete
  18. Anon 6:42

    Umekitaja kikosi cha Trippers na kunikumbusha Vuli. Bendi ya mwisho Vuli kuipigia hapa Bongo nadhani ilikuwa wana Njenje enzi za Revolutions. Kuna wimbo mmoja sijui kama ulikuwa orijino wa kwake au vipi lakini ulikuwa unaitwa Lonely Child. Ule wimbo Vuli alikuwa akiuimba alikuwa anavuta hisia mpaka unaweza kulia. Kumbe alirudi kwao na akaendeleza libeneke na Marehemu Lucky Dube?
    Hii ndiyo raha ya globu ya jamii lakini ina karaha zake pia.

    ReplyDelete
  19. Jamani kwani Marijani alifariki lini, mbona nakumbuka sio miaka ya 90 ? nakumbuka kama ni nyuma zaidi.

    Jamani kuna mtu anaye jua hii story ya Georgina? kwani nilipata habari ya huyo Georgina ni msichana alikua ana ishi Hill road ,Oysterbay ,miaka ya 80 , baba yake naitwa Mahiga na mama yake alikua ni naibu Meya wa Jiji naitwa Consolata Mahiga , je ni kweli ndio yeye aliye imbwa?

    Habari niliisikia zamani sana wakti tunaishi jirani na Hao Mahigas , jamani hebu anaye jua atoe jibu tafadhali , Asante

    ReplyDelete
  20. sio wa zamani sana lakini namzimia na nimecheka saana manake huo uandikaji kama vile nausikiliza wimbo.
    vijana wa zamani nanayi na story zenu nimecheka saaana.

    ReplyDelete
  21. Jamani Kaka michuzi na wengine mmenikuna sana na kunikumbusha mbali sana enzi za Marijani. Mtu ulikuwa ukipika jikoni na kuburudishwa na nyimbo zake kwenye kipindi cha mchana mwema. Yaani acha tu basi ukamsikiliza live jamaa alikuwa anaimba sana. Enzi zile Dar pametulia kama maji baridi hamna vurugu vurugu Unatembea toka shuleni kama ni zanaki au jangwani raha mstarehe unavuta hewa yenye amani. Mweeeeeeeeee. Pumzika vema Marijani. Nyimbo zako tutazienzi milele- UNANICHOMA MKUKI MOYONI!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  22. sitaki kuongea mengi,ila ukweli huyu jamaa,kwanza mwenyezi mungu aiweke mahali pema peponi roho yake.alikuwa kweli ni jabali la muziki.ila waungwanakama kuna mtu yeyote mwenye link ambayo tunaweza kusikiliza nyimbo zake ,basi atusaidie,au mkulu,wewe utusaidie kupata link hii tule maana ya ZILIPENDWA,maana bila watu kama yeye huwezi kusema neno ILIPENDWA
    Yasser

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 19, 2009

    mimi ndiyye tizedboy. Huo ukurasa uliounukuu hapo juu nimeuondoa kwa vile watu wnatumia vibaya kazi zilizofanywa na wengine.

    tizedboy

    ReplyDelete
  24. Marijani alikuwa msanii kweli kweli kioo cha jamii kionacho mbali kuliko macho ya kawaida. Ukiusikiliza wimbo unahisi kama uliimbwa mapema wakati imani ipo ipo. Sasa hivi ndoo imani imekwisha. watu wanachuna ngozi za wenzao ili wapate hela.........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...