Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. uchafu tu huu...
    from
    KiNg

    ReplyDelete
  2. Ni kweli mwanamke hina lakini yote tisa Kumi mwanamke ni Kanga bila ya kanga anapoteza uzuri wa umbile alilopewa na mola hususan akiwa ndani ya nyumba akivalia kanga na ukiwa mwanamme shababi hapo utafadhaika kanga haimtupi mwanamke katika umbile lolote lile alilo nalo humpendezesha na umbile lake alilonalo kikieleza kizungumzia kivazi cha kanga hapa sio kile unachokiona Mabarabarani.nazungumzia kanga inayovaliwa kiunoni na mwanamke akiwa ndani ya nyuma utafadhaika jinsi utakavyo liona umbile la mwanamke likiwa limevalishwa kanga ni kazi ya Muumba hiyo Mmungu na ndio kule kwetu wazazi wetu kutokea mika ya karne wamekuwa wakitusisitiza Mwanangu we mke ni kanga yaani usije ukafanya kosa lakuto mnunulia mke kanga walikuwa na maana yao (sio matenge ambayo ambayo huvaliwa mabondeni wakati wa kulima au kuwindia ndege);-)

    ReplyDelete
  3. Huu ni urembo si uchafu. Watu wa pwani mpo!

    ReplyDelete
  4. Wafundishwe na matumizi yake hiyo hina sio pambo tu.
    Hii mikono imefanana na ya Mrs.JK!!! Teh!!Teh!!!!!!!!!!!!Teh.....

    ReplyDelete
  5. khaa imezidi imekuwa uchafu mi hata akipika sina hamu ya kula kinyaa,ikipakwa kiasi ndio inapendeza,kazi yake nini tufundisheni jamani sisi wabara hatujui

    ReplyDelete
  6. kapendeza sana!!,hivi lakini mbona wanaopakaga hina sana huwa ni waislamu? je hina inahusiana na dini yani kuna msg yoyote inayotolewa na mpakaji zaidi ya urembo? manake mi sio mwislamu lakini natamani kupaka hina niliambiwa kariakoo kuna watu wanapaka ila naona wanaopaka wote waislamu aidha wanaolewa au kwa raha zao na sherehe za kidini sasa na doubt nisije nikawa navamia mambo ya watu

    ReplyDelete
  7. Kaspersky
    Internet Security 2009
    Access denied
    The requested URL could not be retrieved

    While trying to retrieve the URL:

    http://www.freemedia.co.tz/

    The following error was encountered:

    The requested object is INFECTED with the following viruses: HEUR:Trojan.Script.Iframer


    Please contact your service provider if you consider it incorrect.
    Generated:
    Sat Mar 14 21:24:12 2009
    Kaspersky Internet Security 2009


    HII PAGE VIPI INA VIRUS WAHUSIKA MPO.

    ReplyDelete
  8. This is an Arab inheritance....we should not be influenced by these evil people who barter traded on us black people as potatoes and onions at Tandale!! We can Africanise ourselves rather than copying whatever comes along...

    ReplyDelete
  9. Half time bwawa la maini linaongoza mbili kwa moja la majini wekundu
    Nataka gemu iishe hivi.Ingawaje mimi ni ARSENAL nina furaha hivi sasa

    ReplyDelete
  10. Leo hatutalala bwawa la maini limefunga la 3 tena ndani ya old trafford

    ReplyDelete
  11. mdau wa March 14, 2009 4:34 PM ulieandika kwa kiingilishi je na wewe hayo matumizi ya lugha ya mkoloni ni vipi? sasa si na wewe ujisifie lugha yako ya taifa? kwa nini unatumia lugha ya mkoloni alokuja na kuligawa bara letu? tena kwa nini unatumia lugha ya mkoloni katika blog ambayao asilimia 100 nzima ni waswahili? FATA USHAURI WAKO KWANZA KABLA YA KUANZA KUHUBIRI KWA WENGINE!!!!!
    J M

    ReplyDelete
  12. hinna ni urembo anaweza kupaka mwanamke yoyote kama umependa hina unaweza ukapaka hata wazungu nao wanapenda utawaona wapaka hina.mashallah hina imempendeza sana.

    ReplyDelete
  13. KWA LUGHA YA KIGENI INAITWA TATOO

    ReplyDelete
  14. may be pwani ndo mna-mind hina.....huku kwetu mikoani watakusugua hadi itoke, maana wataiita uchafu. mwanamke jembe!

    ReplyDelete
  15. We unayesema akipika huli, ubara unakusumbua.
    kwani mke kazi yake ni kupika?? tafuta dobi na mpishi , acha mke awe mke.

    Huyu anyezungunzia uarab, rudi kwenu ukaongee kilugha na nduguzo. Utamaduni wa mwambao somehow unafanana duniani koote.
    Honduras kuna hina .

    ReplyDelete
  16. kwa kweli kapendeza

    Ningependa kumueleza anonymous wa no# 6 - 4:17. Hina haiusiani na dini kwani hina inatokana na mti ambao unamea sehemu tofauti, ni moja wapo ya pambo ambalo mwanamke yoyote anaweza akalitumia, ila kwa bahati mbaya watu wanaelewa kuwa hina inausiana na dini ila sivyo kwani ni pambo la asili kama mapambo mengine ya asili. Kwa yule anae sema ni urithi wa kutoka uarabuni wala sio kweli kwani mmea huo unaota sana kwetu bara na visiwani kila mkoa nadhani tz yetu una mme wa aina hiyo. So dear dont worry it you like it just use it like anything else you would like to decorate urself with...

    ReplyDelete
  17. Wewe unejiita marine whatever ni mshamba sana na hapo umewasaidia watu wanaobisha kuwa washahili hawana ubaguzi wa rangi sasa wewe hizo chuki zako binafsi weka pembeni mshamba wewe unaeikataa hina ukenda tumia petrol na diesel toka kwa hao waarabu. Basi hata vitu vingine usitumie na usivae suit maana pia ni mavazi ya wazungu. Kama unanjaa ni bora kula ugali na maharage ulale huma jipya wewe!

    ReplyDelete
  18. huo si uchafu na urembo sio kwa ajili ya waislam tu, kama mumeo anajua mambo utajua hina inaamana gani maana inaraha zake kama unazijua shanga na raha zake basi na hina inamana yake tuulize sie watu wa pwani ndio maana mwanamme akipata mwanamke wa pwani hatoki ulizeni makungwi kwa nini ukipata jibu utajua

    ReplyDelete
  19. too much, to me is a dirtness,

    ReplyDelete
  20. sasa royalmarine unatwambia tuwe wazalendo na kujisifia mila zetu za kiafrika, sawa nakuunga mkono, lakini mbona we unatumia lugha ya kigeni hapa, tumia lugha yako tukujue kama mzalendo kweli, kujua kiengereza si usomi! na hata hao wazungu pia wametutesa (na wanaendelea) na kutufanya watumwa vilevile

    ReplyDelete
  21. HINA ilikuwa inatumiwa na wake wa mitume na watu wa kale kwakuwa.
    (1) inaruhusiwa kuswali nayo sio kama rangi ya kucha inaziba kucha kiasis hata ukiji andaa kuwasli yani kushika udhu langi inakuwa imezuia maji kusafisha kucha ipasavo.

    (2)ina ilikuwa inatumiwa mpaka kwenye ndevu za wanaume na nywele za wanake kwakuwa enzi hizo ilikuwa hamna hair dye .na inasaidia kuzuia nywele zinazokatika kuto kukatika.nywele zinakuwa ngumu na hafya hina ni bonge la arb.

    (3)inanukia vizuri na harufu yake uchukuwa hata wk kuisha hata ukiosha viombo hina inanukia tu,

    pia ni sunna kupaka hina.ni kati ya vitendo vilivokuwa vinatumiwa na wake wa mitume.pia ni halal.

    ReplyDelete
  22. HiNA haiitwi TATTOO kwa kiinglish ni Henna ni vitu viwili tofauti jinsi ya kupakaa ina ni tofauti na kutengeneza tattoo ingawa the end result is the same that una mchoro au michoro mwilini.

    ReplyDelete
  23. anon wa11:15 unajidanganya wanawake wa pwani wanaachwa vibaya mno tatizo lenu mnatembea na waume za watu ,wenzenu wa wachaga tuna tesa coz tunaleta maendeleo ndani ya nyumba

    ReplyDelete
  24. AKA MIE NAPENDA RANGI YANGU NATURAL YA MIKONO, INAVUTIA HIVYO HALISI ILIVYO..mICHORO MICHORO YA KUFUNIKA UHALISIA WANGU..NAONA NI UCHAFU TU

    ReplyDelete
  25. SUGGESTION TO HATERS LIVE YOUR LIFE!!! STOP DEPRESSING YOURSELF, YOU WILL END UP HARMING YOUR CONSCIOUS, YOUR MIND, YOUR LIFE, ULTIMATELY TAKE YOUR LIFE, GET A LIFE GUYS!....

    Mtu akitia hina, akitia mamwele ya wafu, kuvaaa vimini, nk, thats their own choice, they live their life SO DO YOU I GUESS!

    ReplyDelete
  26. Anon wa 434am nakuunga mkono Sisi sote ni ndugu; watoto wa Baba mmoja.

    ReplyDelete
  27. we unayejiita royalmarine huna lolote na kiingereza chako cha kuokota,ushamba na ulimbukeni ndo unaokusumbua. kama umeenda shule bila shaka ulipata zero,0,SIFURI FORM FOUR na ukaishia hapohapo. unadhani wanaosoma blog hii hawana akili kama wewe?? we teja nini!!!
    uarabu na mapambo kwa mwanamke vina uhusiano gani!!how about kuhusu wazungu waliowafanyisha babu zetu kazi ngumu bila ujira na wanatutawala hadi leo hii,still mnaiga culture yao kama kutoga masikio kwa wanaume na kutembea nusu uchi,,hayo huoni?au wewe ni kipofu?? fikiri kabla ya kuandika uchafu,matope na pumba zilizojaa kwenye akili yako,sawa??emeelewa??

    ReplyDelete
  28. unayesema mke mchagga analeta maendeleo, mbona hujasema maendelo ya aina gani. maana mamilionea ndo zao zinavunjika kila kukicha. mapenzi si pesa, wewe kweli bwege.

    wanaume wa pwani hatuachi mke, ukileta matata naongeza wa pili, talaka sitoi.
    Mke ni pambo la nyumba, si house maid.

    ReplyDelete
  29. Kweli mwanamke Jembe, nakumbuka kule kwetu wanawake wa Kinyamwezi ndio huwa wanatulimia.

    ReplyDelete
  30. Oh asanteni mliotoa majibu kuhusu hina, got the picture.

    ReplyDelete
  31. ndugu marine, mbona huna point???
    haya hizo rangi za kucha ndo hatujaiga au...? get a life!

    ReplyDelete
  32. WEWE UNAYESEMA KUPAKA HINA NI KUIGA MAMBO YA WAARABU WALIOTULETEA UTUMWA. SIDHANI UMESOMA YA KUTOSHA. MBONA TUNAIGA MAMBO YA WAZUNGU AMBAPO WAO WALIWAFUNGA CHAINS MIGUUNI NA MIKONONI NA KUWAFANYA WATUMWA NDUGU ZETU WA WEST AFRIKA. TAFADHALI CHUNGUZA UONE JINSI WAZUNGU WALIVYO WAFANYA WATUMWA NA KUWATESA NDUGU ZETU WA WEST AFRIKA. FOR YOUR INFORMATION WAKATI WAARABU WANAFANYA BIASHARA ZA UTUMWA EAST AFRICA WAZUNGU WALIKUA WANAFANYA THE SAME WEST AFRICA. WAZUNGU WALIIENDELEA NA KUWAUWA RED INDIANS IN AMERICA WAKIJISINGIZIA WALIKUWA WANAFANYA HIVYO KWA SABABU YA CHURCH. KABLA HUJAROPOKA PLEASE FANYA UCHUNGUZI. SOMA HISTORIA YA BLACK AMERICANS JINSI WALIVYO TOLEWA WEST AFRIKA NA KUFANYWA WATUMWA AMERICA.

    ReplyDelete
  33. kazi kuiga mila za mashariki tu,hina hina nini!? Jivunieni uafrika wenu sio kuiga mila za kivivu-vivu hizo za kupaka mi-hina mwili mzima badala ya kufanya kazi! Arabic culture hiyo tena iliyokomaa na reference unapewa kama anon hapo juu alivyochambua!!! wabongo wengi hasa wa pwani wanaiga sana tamaduni za kiarabu!!! Arabic culture (Eastern culture)= Western Culture vyote uchafu mtupu maadili ovyoooo.Tujivunie African Culture

    ReplyDelete
  34. Nakumbuka kuna kipindi Bablii alitoa darsa juu ya huu urembo, nachelea labda somo halikueleweka vizuri kwa wale waliouliza maswali mengi hapa jamvini, Ni hivi enyi wanawake wenzangu, hasa wale wenye ndoa mpya waanze mapema kutumia huu uerembo ili kumzoesha habibi wako aweze kukufurahia zaidi , una raha zake ambazo ni katika jumla ya mautundu ya kwenye sita kwa sita inapendeza zaidi kutofautisha mwili wa mme na mke, ukweli mikono yenye mapambo ya hina inaleta sana ashki kwa wanaume hasa kwa wale wanaoijua, narudia tena enyi wanawake urembo katika majamboz ni lazima ili kuongeza ladha, mfano shanga zimezoeleka sana machoni kwa wanaume wa pwani na bara, ili kuleta vitu/ladha tofauti weka na hina kidogo kisha weka vikuku pete na bangili utizame kazi kuchikuchi kuchaeeee.

    Hii hina hapo juu ni nzuri sana na ina wakati wake, kuna ile ya kuhanikiza ambayo inafanana na hii hapa inafaa kwenye maharusi na kuna ile ya kutupia kwa kiasi zote ni raha tu na mapendekezo yako waweza weka kiasi iwe kiunoni au kifuani nyuma au mbele mikononi au miguuni kisha mautundu kwa sana inaleta burudani sana kwa aliyewekewa na kuijua inaleta gumzo la mahaba wakati mwanamme anapoiona na kuisifia naamini hapa naeleweka na wanaume watundu wenye utani wa kimapenzi, inaongeza mvuto na hisia kwa rijali yeyote inapopakwa kwa umakini. Hapa nakusudia kusema si mambo ya dini ni urembo kama urembo mwengine wa asili, kipindi hicho kabla ya mambo ya rangi za kucha zilikuwa hazijaanzishwa ilitumika sana na hasa kwa watu wa mwambao, nawashauri na watu wa bara waitumie tu haina ubaya ila inabidi na huyo unaekuwa nae aizoee mapema kwanza ili isilete maswali au karaha .

    ReplyDelete
  35. HINNA sio uchafu wee mshamba nini "watakucheka" waulize wanaume wenzio wanaojua nini maana ya hina, HINA ni urembo kwa wanaume wanaojua nini maana ya hina kwa taarifa yako anaejua huwa hatoki ndani mpaka hina iishe kabisaa na hina mwenziwe udi upo!

    ReplyDelete
  36. Mikono ya bi9 salha mrisho sengo siku ya harusi yake!! Umependeza dada.

    ReplyDelete
  37. Kwa kweli kila kitu ni mazoea na kama haujui kitu uliza upate kueleweshwa hinna ni sehemu ya mapambo ya kumfurahisha mwanaume ambaye anajua nn maana ya kupaka hinna na hinna sio uchafu na wala haikuzuii kufanya kazi nyingine acheni kulumbana bila sababu wote ni ndugu moja.

    ReplyDelete
  38. we mwanamke wa kichagga acha ushamba ungejua hao wanaume zenu huwafata wanawake wa pwani kutafuta mapenzi, mapenzi sio pesa mwanamke pwani we acha tu mambo yote anayajua na ukimpata hutoki kwa marembo sio kuwa za pesa time zote, na wewe unaesema mwanamke jembe umekosea mwanamke ni urembo sio utumishi ndi maana wanawake waaina hiyo huwa hawana mapenzi kwa saabu ya kuchoka, mwanamke sio mtumwa wako mwanamke ni pambo lako oooohoooo ulizenu wanaojua zaid watu wa pwani

    ReplyDelete
  39. huyu aliyemenshen african culture na kusema culture ya kiarab ni ya kivivu anafanya nini kwenye kompyuta?????
    saa hizi alitakiwa awe shambani, shambani toka saa kumi na moja asubihi, unarudi nyumbani saa kumi na moja jioni.
    kwa maoni yangu uvivu ni silika ya kibinadamu , kulima siku nzima ni matatizo tu, si jambo la kijivunia .
    wazungu wanatumia mashine na kabla ya hapo walituchukua utumwa ili wao wasifanye kazi ya kulima.

    ReplyDelete
  40. Kwa kuongezea maoni yako mbwegele, haya mambo ya kujishughulisha ni kila mtu na mazoea na uwezo wako waweza piga hilo jembe tangu subhi mpaka magharib ukapata chakula cha kulisha familia yako tu bado matumizi mengine zaidi ukaishia umaskini, na waweza fanya biashara za hao walowaita wavivu. a.k.a waarabu na wakatoka, sasa hapa swala la hina ni burudani kama burdani nyengine zile kama kwenda mziki au kutembea jioni ufukweni bila kazi maalum yaani ni kupumzika. Tena kwa kukukhabarisha zaidi wanaume zetu wanoijua hii hina hukuenzi ili isifutike haraka aendelee kuiona, na baadhi ya kazi za kushika maji sana mf kufua unapewa likizo kidogo, nataka nikupe thamani yake kwa wanaoijua na kuithamini we kalaga baho tu ukidhani kufurahia maisha na kazi kulima pekee.

    ReplyDelete
  41. Binadamu ni mtu wa ajabu sana inapofikia mahali pa kuchagua, `ubinafsi' unatawalana na kiwingu kinaugubika utashi wa kufikiri.
    `Eti watu wanaiga utamaduni wa Kiarabu, kwa kupaka hina, huku yeye kavaa tai, anaongea Kiingereza...'
    `Eti, Waarabu ni `evil people' kwasababu waliendesha biashara ya utumwa, huku anajua kuna Waamerika weusi huko Marekani, walitoka wapi, Afrika magharibi,sijui kule walichukuliwa na Waarabu...
    Sawa, kuna mfano wa vidole, ukimnyoshea mwenzako kidole, ujue na wewe unajinyoshea mwenyewe vidole, sijui vingapi.Cha muhimu kila tunachoiga tujaribu kuangalia uzuri na ubaya wake, faida na hasara zake...
    M3

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...