rais mstaafu alhaj ali hassan mwinyi akihutubia baraza la maulidi ukumbi wa diamond jubilee hall juzi. kulia kwake ni mzee rashidi mfaume kawawa
alhaji mwinyi akiendelea na hotuba yake
alhaj mwinyi akifafanua jambo
alhaj mwinyi mara baada ya kushambuliwa jukwaani
kama kawaida yake alhaj mwinyi tabasamu halikumtoka pamoja na maswahiba yaliyomsibu
alhaj mwinyi akiondoka ukumbuni huku tabasamu lake likiwaka usoni pake
alhaj mwinyi akiagwa na walohudhuria baraza la maulidi
mara baada ya kumshambulia alhaj mwinyi kijana aliyefanya kituko hicho akigombewa kama mpira wa kona na wadau wenye hasira
maafisa usalama walifanya kazi ya ziada kumuokoa mshambuliaji huyo

ilikuwa patashika na nguo kuchanika. wanausalama walijitolea maisha yao kumuokoa kijana huyu
karibu kila aiyekuwepo alitaka kumuadhibu mshambuliaji huyo
wanausalama walifanya kazi yao kikamilifu kuokoa maisha ya mshambuliaji huyo
haikuwa kazi ndogo kumuokoa
mbinu zote zilitumika kuhakikisha mshambuliaji huyu hapatwi na sheria mkononi
kazi ilikuwa nzito kumuokoa
dakika nne za vurugu hilo zilionekana kama masaa mia nne
hatimaye mshambuliaji aliwekwa kwenye gari na kukimbizwa kituo cha polisi...
Habari ni kwamba mtuhumiwa Ibrahim Said Sultan maarufu kama (Ustaadh) aliyemshambulia Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi kwa kumpiga kofi wakati akitoa hotuba katika Baraza la Maulid katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar juzi atafikishwa mahakamani leo kujibu shtaka la kushambulia hadharani.
Kamanda wa mkoa maalumu wa kipolisi wa dar afande Selemani Kova amesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kupima afya na akili yake pia kujua kama mtuhumiwa ni mwanaharakati na kama alikula njama na watu wengine kufanya kitendo hicho.
Kamanda Kova ameongeza juwa mtuhumiwa amehojiwa na kueleza kuwa hakuwa na nia ya kumdhuru Rais Mstaafu huyo lakini kwa kuwa ni mtu maarufu na anapendwa na watu wengi aliona akimfanyia kituko hicho atakuwa amefikisha ujumbe wake ambapo kijana huyo anapinga waislamu na wakristo kushirikiana katika kusherehekea sikukuu zao.
Kijanan huyo amesema pia kuwa hapendi viongozi wa dini kushawishi jamii kutumia kondom kwani kwa mujibu maelezo yake hiyo ni kahamasisha matendo maovu ya zinaa ambayo hayakubaliki kidini.
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Pole sana mzee wetu Mwinyi kwa matatizo yaliyokukumba

    ReplyDelete
  2. mhhh! yangu macho, maana sijui hata nianzie wapi? ila swala la kupimwa akili ni muhimu naona na pia wangalie kiwango chake cha elimu kimefikia wapi? kama kipo chini sana kinaweza pia kuchangia, maana sioni kama malalamiko yake yanaingiliana kabisa na huyo mzee wa watu aliye jistaafia, hizo ndiyo laana za kujitafutia.

    ReplyDelete
  3. akome kw kweli anadhani yeye ni nani haswa kwa kuanza kumshambulia babu wa watu?
    ndio hivyo tena upumbavu huo

    ReplyDelete
  4. hahaha...hii imenifunja mbavu. Lakini nimefurahi jinsi polisi walivyoitunza. Safi sana jeshi la polisi na raia wema waliomlinda jamaa.
    PS...nadhani kuficha numba za magari katika public imagines ni kitendo muhimu bwana Michuzi, unless kama ni gari la serikali. Inaweza kuleta shida badae.

    mtoto

    ReplyDelete
  5. Watanzania tujivunie kuwa Wakristo na Waislamu wanaweza kusherejea sikuu zao pamoja na kwa Amani! Hayo hayatabadilika ni mila yetu na ni Utanzania! Sisi tunapenda amani. Hebu mlete huyo jamaa tumminye hadharani ashike adhabu! Tena tutapokezanza zamyu za kumminya, waislamu na wakristo! Hebu akome!

    ReplyDelete
  6. Lakini hawa wanofanya ni siasa kali hawana lolote ila ni unafiki tu...Tanzania ni nchi pekee ambayo watu wa dini tofauti wanashirikiana ndo maana kuna amani. Kama anapinga matumizi ya kondomu yeye waaache watu ambao wanatumia. Kwani sasa kila mtu yupo ktk maambukizi.Huyo ni mtu na akili zake ila ni mnafikuna mkubwa naye ataalaania kwa kumpiga babu wa watu asiye na kosa....

    Mijitu mingine bwanaaa...

    ReplyDelete
  7. mambo ya udini hayo, sasa kumzaba kofi mzee mwinyi kaona ni yeye ndo mcha Mungu sana? i hate udini dini na udhehebu dhehebu.maana ukiwa hivyo wewe lazma uwe mbaguzi tu na uchukie wengine. ni umaskini wa mawazo na elimu tu huo.

    Ms GB

    ReplyDelete
  8. Maelezo ya huyo kijana hayakubaliki kabisa kwamba ndiyo sababu tosha iliyomtuma afanye kitendo kile cha fedheha kubwa kwa Taifa na kwa Waislamu wote nchini Tanzania.Kwamba apimwe akili ili kutambua iwapo alikuwa anakijua alichokifanya,hilo nalo pia halina msingi.Kwasababu,angekuwa hana akili timamu au chizi kwa kiasi fualni,basi asingekuwa na ujanja ule au akili zile za kujifanya kaenda mbele jukwaani kwa heshima na unyenyekevu kabisa na kisha kujifanya kama vile anataka kurekebisha mkao na mwelekeo wa Kipaza Sauti(Microphone) na kisha GHAFLA kunyanyua mkono na kumzaba Mzee wa watu kofi ambalo hakulitarajia.Upo uwezekano mkubwa sana kwamba huyo kijana ALITUMWA na waumini wenzake wenye msimamo mkali wa kidini kwa ahadi ya manufaa fualni baada ya kufanikisha kitendo hicho cha aibu kubwa.Waandaaji wa sherehe zile za Maulid pia watabeba lawama kwa kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuendesha shughuli zile katika hali ya usalama mkubwa hususan kwa watu ambao walikuwa Viongozi wa Juu kabisa katika nchi hii ambao maisha yao siku zote yatahitaji ulinzi wa hali ya juu kutokana na sababu mbalimbali.Mathalani,yule kijana angekuwa katayarishwa maalum kwa tendo lile katika sherehe kama zile na kapitia mafunzo ya ugaidi au mambo ya kijeshi kidogo na anajua jinsi ya kutumia silaha mbalimbali,na iwapo siku ile ya tukio angelkuwa na Bomu mwilini au hata Bastora iliyofichika,Madhara yake hii leo yangekuwaje?Tumshukuru Mungu kwamba ametuepusha na Balaa hilo,lakini zaidi ya yote KUTENDA KIASI CHA KUTUPA ISHARA MAPEMA ya yale ambayo pengine ni mabaya zaidi yatakayo weza kutokea siku za mbeleni!Tusijidanganye kwamba Tanzania ni Kisiwa cha amani!Dunia hivi sasa imechafuka mno.Na watu washenzi wasiomjua Mungu hupenda kuitumia mianya ya kidini au mambo yanayo gusa jamii ili kufanikisha maovu yao.Katika tukio hili hakuna haja ya kupoteza muda kufanya Upelelezi!Upelelezi kuhusu nini?Kitu cha kwanza kabisa huyu kijana afikishwe mahakamani na asomewe Kosa lake na kisha aulizwe iwapo na lolote la kujitetea.Baada ya hapo apewe adhabu yake anayostahili.Kusiweko na kuahirisha kesi bila ya sababu za msingi.Hilo likifanyika litapalilia Hasira za watu kujichukulia sheria mikononi mwao pindi tukio lingine la aina hiyo litakapo kuja tokea tena.Tukio hilo liwe fundisho kwa wahusika wote nchini na kwa viongozi wote wa dini.Tumuombe radhi Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa fedheha hii!Kijana yule hawezi kuwa na ujasiri wa kumzaba Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi yeye mwenyewe bila ya msukumo wowote kutoka kwa "hao ambao ndiyo wabaya na hatari zaidi"kwa usalama wa nchi yetu!Haya mambo yasipuuziwe na idara ya usalama wa taifa pamoja na idara ya polisi.Hili ndilo chimbuko la Islamic Fundamentalism and Religious Extremism hapa nchini!Suala hili tutalilani kwa nguvu zetu sote,liwe limetokea Makanisani,au Jamatini au popote pale!Halina nafasi kabisa katika Ustaarabu wa Watanzania wa Leo na hata wa Kesho na KeshoKutwa!Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  9. Huyo kijana ni mtoto wa Marehemu Mazengenuka wa Shinyanga.

    ReplyDelete
  10. Na Ustadh Mwinyi nae kazidi. Vyereje kuzungumzia masuala ya kutumia kondom kwenye kadamnasi ya Waislamu. Kwani kasikia kuwa Waislamu ndio wazinifu. Basi siku ya pili akiitwa kuwa mgeni rasmi atatafuta la maana la kuzungumzia.

    ReplyDelete
  11. Atupishe naye, akaanze kuwachapa vibao walioko karibu yake huko anakotoka! Ovyo......

    ReplyDelete
  12. sijapenda kupigwa kofi kwa mwinyi, mzee wetu mpenda, ila na yeye aangalie hotuba zake aziandae, atofautishe tacaids na maulidi.
    si heshima kabisa, kumpiga mzee, ila kizazi cha kukosa maadili, subira, heshima, uvumilivu, kinachodai kuonekana, kinachodai haki, kinachodai ukweli, kinachodai uwajibikaji ndo kinaindia, yanakuja mengi tu,
    huyu tutasema kakosa akili au adabu, waliomzomea RAIS tunasemaje? wanaotukana tunasemaje, kila mtu anahangaika alipo, ndiomaana mimi naona bora UKWELI TU. mzee kateleza, aombe radhi yaishe, kijana afunguliwe mashtaka afungwe tuendelee na maisha.
    ila kila kiongozi akae sawa, kuanzia kwenye familia hadi kwenye nchi.
    Watu subira siku hizi hailipi.

    ReplyDelete
  13. Kumpima akili ni kupoteza muda tu na matokeo yake makali ya hasira za Watanzania zitapungua. Hili jambo lichunguzwe kwa undani kwani hii tabia ya kuendekeza watu wenye Imani kali wewe Wakristo au Waislamu itakuja kutupeka pabaya, Naomba watanzania kwa pamoja tushirikiane kuondoa huu ujinga wa siasa kali hauna maana TZ

    ReplyDelete
  14. waratakrabu zinaa. wala msiikurubie zinaa. kuwambia waislamu watumie kondom hapo mzee Mwinyi kateleza. Aombe TOBA kwa Mola wake kwanza. Ni siku ya kuzaliwa Mtume halafu unaongela kondom wapi na wapi?
    Kijana naye hakuwa mwenye subira, ni ukosefu wa adabu. Ila ujumbe umefika.

    ReplyDelete
  15. Kila mtu ana dukuduku zake mi naona huyo kijana aulizwe kwanza kwani yaliyoko moyoni kwake hamyajui

    KILI
    Bg

    ReplyDelete
  16. JAMBO MOJA KUBWA NILILOJIFUNZA NA KUTOKANA NA KITENDO HIKI NI KUWA TUNAPOMKAMATA MHALIFU TUNATAKIWA TUMPIGE HAPOHAPO KABLA YA KUMPELEKA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA, KWANI TULISHUHUDIA MHALIFU HUYU AKIPIGWA TEKE KICHWANI NA MIGUMI KIBAO MBELE YA VIONGOZI WANAOTUKATAZA SISI KUJICHUKULIA SHERIA MIKONONI! VINGINEVYO ILI WATUONESHE MFANO BASI WALE WALIOMPIGA MATEKE NA MAGUMI MTU ALIYEKUWA HAPINGI KUKAMATWA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA ILI WATU WAOGOPE KUWAPIGA WAHALIFU.

    ReplyDelete
  17. Ndugu zangu inabidi tuukubali ukweli. Ukimwi upo, dini zipo na zinahubiri watu waache zinaa lakini hadi wakati huu maambukizi yamepungua au yanazidi kuongezeka? Tukiukubali ukweli ndio tutaweza kwa dhati kuudhibiti ukimwi usienee. Watu watake wasitake, wakubali wasikubali, ukweli ni kwamba hao viongozi wa dini wenyewe wanafanya zinaa. Kwa waislamu, utakuta mtu ana wake 3 au wanne lakini bado ana kimada nje. Mtu huyu ukimwambia asitumie kondom eti unahalalisha zinaa, ni kupingana na ukweli. Dini zipo tangu tumezaliwa na zinakataza zinaa na watu hawaachi. Iwapo watu wakielezwa njia za kujikinga waamue wenyewe kama watumie au waache. Kama dini zingekuwa zimeshikwa ipasavyo watu wangeacha zinaa.
    Hao wanaojifanya hawataki kuongelea mambo ya condom ndio wazinzi namba moja. Wanafiki tu. Heri kinga ndugu zangu.
    Pole mzee ruksa, mungu akuzidishie busara zaidi.

    ReplyDelete
  18. Kutumia Condom sikuwambia watu wakimbilie zinaa siuoe basi ubaki namkeo km hutaki kutumia mpira mzee Mwinyi ametaka kuwanusuru watoto wanaobaki yatima na wanaishi wakiwa wameathirika kutoka kwa wazazi wao, hebu tutumie akili hio sio siasa.

    ReplyDelete
  19. huyu kijana kwa kweli anahitaji pongezi za hali ya juu kwa kufanya kile ambacho kila muislamu au mtu yoyote mwenye fuata maamrisho ya dini yake alitakiwa afanye. kazi aliyoifanya huyu kijana ilitakiwa ifanywe na huyu anayejiita shehe mkuu kwani yeye ndiye anayetakiwa kuhakikisha yaale ambayo allah ametuamrisha na mafunzo ya mtume SAW yanafuatwa. SHEKHE MKUU KWA KWELI ALITAKIWA AWE WA KWANZA KUMCHAPA MZEE MWINYI VIBAO KWA KUTUMIA JUKWAA LA WAISLAMU HASWA HASWA KATIKA SIKU YA KUMKUMBUKA MTUME WETU, KIPENZI CHETU MUHAMMAD SAW ANZALIWA KUAMRISHA WATU WATUMIE KONDOMU MAANA YAKE ANAAMRISHA YALE AMBAYO MTUME NA M'MUNGU AMETUKATAZA. JE? YEYE MZEE MWINYI YUKO TAYARI HAO ANAO WAAMRISHA WATUMIE KONDOMU KUMZINI MAMA YAKE, MKE WAKE, MWANAE, SHANGAZI YAKE AU BIBI YAKE? AU ANAJUA KUSEMA TU? JIBU ATAKALOJIBU ATASEMA HAYUKO TAYARI. HIVYO NDIO MAANA ALLAH NA MTUME WAKE WALITUAMRISHA KUTOKUIKARIBIA ZINAAA. HIVYO MZEE MWINYI ALISTAHILI KUPIGWA SI KIBAO KIMOJA TU BALI ZAIDI YA MILIONI ALIPASWA APIGWE KWA KUTAKA KUUPOTOSHA UMMA WA KIISLAMU. SIKU ZOTE MIMI NAJUA MZEE MWINYI SI MUUMINI WA KWELI BALI NI MNAFIKI NA M'MUNGU AMEMUUMBUA. NA KTK UISLAMU AU SHERIA HAKUNA KUSEMA HUYU MZEE AU MTOTO SHRIA NI MSUMENO. ANACHOTAKIWA MZEE MWINYI KWA SASA NI KUTUOMBA WAISLAMU NA WATANZANIA WOTE RADHI KWA KUTAKA DADA ZETU NA MAMA ZETU NA SHANGAZI ZETU WAJE WAZINIWE NA HAO WATUMIAJI WA KONDOMU. KWA UFUPI MZEE MWINYI ALITAKA KUTUPOTOSHA.

    ReplyDelete
  20. nakwawale wanaomlaum alhajj mwinyi kwa kuzungumzia zinaa siku ya maulid,wajiulize swali ikiwa maulidi ni ukumbusho wakuzaliwa mtume sasa kuna ubaya gani wakuendeleza na kushauriana mema aliyokuwa mtume anatufundisha,
    1 tupendane...so mwinyi anawapenda wenzie so anawahusia juu ya ugonjwa ambao upo na si jokes
    2pili kwa waislam wenzangu mtakubaliana kua quraan inasema penyemkusanyiko wa watu basi pasikose kutolewa mafundisho,sasa watu wlitaka azungumzie wali na nyama pale ili wajijue wapo kwenye maulid...siyokiivyo vaeni mipira mkitaka ndiyo hivyo msitake ndio hivyo mtakwisha

    ReplyDelete
  21. nimekukubali anon wa 12:44 na wengine wote wanaokubaliana na hili swala la kutumia condom. inashangaza kwa kweli katika wakati kama huu mtu unashangazwa au unaona kama ni kitu kibaya kwa mzee mwinyi kuongelea maswala ya condom kwenye sherehe za maulid!? tusijikimbie ndugu zangu, ukimwi upo na wengi wameathirika, dini zinapinga zinaa lkn ukweli unabaki palepale ni kwamba watu kwa asilimia kubwa tuu hawafuati hayo yaani wanaendeleza zinaa tuu, sasa mtu kama mzee mwinyi kuongelea hili swala kwenye maulid sioni kabisa kama ameteleza nafikiri ndiyo haswa mahali pake yaani anatakiwa aongelee kuhusu kondom kwenye sherehe za maulid, za chritsmas, za pasaka, za mwaka mpya,na za serikali pia. anayesema mzee kateleza atakuwa na matatizo, maana dini zipo na ukimwi upo.FUATA MAADILI YA DINI UEPUKANE NA UKIMWI,UKIAMUA KUFUATA ZINAA BASI TUMIA CONDOM ITAKUEPUSHA NA UKIMWI.CONDOM KUONGELEWA NI MUHIMU SANA MAHALI POPOTE PALE WANANDUGU, CONDOM KANISANI, CONDOM MSIKITINI, CONDOM SERIKARINI, CONDOM MAKAZINI, CONDOM MASHULENI. NA BINADAMU MUOGOPENI MUNGU ACHANENI NA ZINAA.

    ReplyDelete
  22. Moja; Huyu jamaa nilivyomuona anatembea anad dalili za Bipolar Disorder( currently Depression), ni vyema apimwe akili, isitoshe hata hilo ofi wala hakumpiga amuumize, ni zilezile tabia za wagonjwa wa akili kufanya vituko
    Pili; Hao wanaaonekana ktk picha wanamshambulia mbona hatujasikia wamepandishwa mahakamani kwa kosa la kushambulia?au huyu bwana hana haki?Picha hizi zitumike kuwashtaki hawa jamaa,wafungwe hata kifungo cha nje na faini ili wawe mfano kwa wanaojiita ananchi enye hasira,.ndio hawa waliua wanafunzi mwaka jana bila kosa lolote, wakati mingine wanaua watu kwa kuiba kuku lakini hawawasogelei wale mafisadi walioiba mabilioni ya serikali na wanakesi mahakamani, si wanakutana nao mitaani na kusali nao?mbona hawawashambulii?hata kwa maneno tu,achilia mbali mateke!upuuzi mtupu

    ReplyDelete
  23. Hawa wote wanaotetea kitendo cha Huyo kijana kumpiga kibapo mzee wetu eti kwa sababu anazungumzia mambo ya Kondom kwanini wao wasiwe watu wa kwaza kwenda kufanya hivyo (kumpiga vibao) mzee Mwinyi siku ile? au wanasubiri jambo kama hili litokee halafu waanze kushabikia ujinga? wapi umeona mtu anampiga mzee wake vibao mbele ya hadhara kubwa kama ile?

    ReplyDelete
  24. kondomu ni kinga ya umwi sawa,
    ILA
    hakikisha ni matumizi sahihi,
    Je unajua kuwa hutakiwi muwe mmenyoa karibuni? hamtakiwi muwe na vijiscratch sehemu za around na tukio?
    je lazima contacts ziwe ni sehemu za condom tu? yani mfanye ile missionary style tu, hakuna manjonjo hata chembe, waulize waiopona ukimwi kwa kupima kama wanadhubutu kujaribu kurisk kwa kondomu! lazima watakuwa wachache.
    Hivi wewe mwenyewe unaeshabikia condomu, ukiletewa mtu mwenye uhakika wa kuwa na ukimwi, na wewe una uhakiwa kuwa huna utakubali kwenda na condomu zako unazozitetea?
    Hebu kuweni wa kweli,
    condom is a last resort, kitu ambacho Dini hakizungumzii, dini zinajaribu kukufanya nafsi yako iwe na ujasiri wa kujiamulia mambo mazuri mapema.
    I am against condom and for all the religions to go on improving 'quality of life' and after life.

    ReplyDelete
  25. Ningependa nielezee hii issue ifuatavyo;

    Kwanza nampongeza huyo kijana kwa alichokifanya.Umefika wakati sisi watanzania tuamke na kuacha ujinga unaotumaliza mpaka leo kwa kuogopa kusema au ku act pindi vitu vinavyofanywa sio sawa,kisa na sababu ni kwamba huyo mtu ni kiongozi au sisi watanzania ni wasataarabu..ni wastaarabu wapi walio wapumbavu wa kukubali viongozi na serikali fisadi iendelee kuwa madarakani mpaka leo?
    huu si ustaarabu bali ni ujinga uliokithiri na tusipoangalia ndio tutakuwa hivi hivi maisha yetu yote.

    Pili elimu ni muhimu kwa binadamu wetu wa kitanzania,maana katika maoni yote niliyosoma hapa ni moja au mawili tu ya kumsifia huyu kijana..mengi yao yanamlaani nadhani hata mama yake atamkana si mwanawe.
    sikatai yale mazuri aliyoyafanya,lakini ieleweke kuwa tunastahili zaidi ya hayo,na,akili zetu zibadilike. hatuwezi kufanywa wapumbavu miaka yote hiyo na kundi la watu wachache na tunalielewa kabisa hili halafu tuendelee kukaa kimya,kisa sisi ni wastaarabu au jamaa aliongoza vizuri,au mwacheni mzee wetu apumzike,jamani..hii ni aibu.

    Tatu na hitimisho...nisingependa kusema kuwa nakaa nchi fulani sasa hivi takribani miaka kumi...lakini haya ni machache na mifano ya kuigwa..
    1.South korea-hoja za wabunge na bajeti hazipiti bila ngumi kupigwa bungeni, na polisi hawaruhusiwi kuingilia.huwezi ukasoma bajeti yako na ikapitishwa kwa maswali ya kwa maswali ya kupangiana kama hawa mafisadi wa hicho chama mnachokijua.
    2.Ni bora Waziri akajiua Japan/Korea kuliko kuhojiwa kuhusiana na kuipigia debe kampuni fulani ipate tenda au kujulikana kama alikula rushwa fulani.wanalinda honor and dignity zao.
    3.Waziri mkuu(raisi) wa Norway or Finland anapanda ndege ya abiria ili kupunguza matumizi ya fedha za walipa kodi..

    Hitimisho; sasa nani mstaarabu?
    sisi tulioshindwa kusimamia moja hata ilo la dini kuchanganywa na vitu visivyotakiwa au huyo kijana
    aliyefikisha ujumbe wa kile anachoona sawa na kwa ujasiri mkubwa?? No more time to waste tuamke sisi watanzania kama tunataka tupigana na kupata maisha bora!!!

    ReplyDelete
  26. mh interesting staff. hata roma hawaafiki na condom. .. so ndo kusema papa achapwe?...but ilike the guy kweli bongo ulaya kuna mpaka wana harakati wa jinsi hii? any way inabidi adhabu ilingane na kosa siyo tu kwa sababu ni mwinyi basi sheria zipindwe. kumpiga mtu kofi hadharani naona panishment yake yaweza kuwa community work. hata keko hafiki. kama sheria ni msumeno that is what it should be.

    ReplyDelete
  27. We anon wa March 12, 2009 8:49 AM, huleti suluhisho au ushauri wowote bali unaamsha hisia zako na za watu kama wewe za "secular fundamentalism" na "secular extremism"

    Kama umeamuwa kuwa secular kuwa secular, sio kuwa secular ili dini fulani ikukome. You dont become better than them.

    ReplyDelete
  28. Jamani kama mmeacha dini mkawa masecular basi just be better than religious people. Kama nyie ni secular hasa dont hate religious people otherwise mankuwa sawa nao. Maaana dini zinahubiri upendo lakini kihalisia hawana mapenzi kwa wanadini wengine kutokana na misuguano ya imani.

    ReplyDelete
  29. Mzee usipojifunza kwa fikra utanyooshwa na kofi. Nahisi hamna mtu atarudia kuhubiri kinyume na kitabu cha dini kwenye ibada.

    ReplyDelete
  30. Anon wa March 12, 2009 2:15 PM, kukataza zinaa kungetosha. Maana kwenye maulid watu wanakumbuka mafundisho ya kuacha zinaa. Kama zinaa ainaadhibiwa vikali.. mnajuwa, je kuhubiri kondomu si ni kupinga mafundisho ya mtume huyo? Kwa kisingizio cha ukimwi?

    ReplyDelete
  31. Ahsalaam al khum watanzania washikaji wote wa bongo, kitu kimoja naomba watu mnipe mawazo yenu najua kitendo alichokifanya mswalihina mwenzetu ni kinyume na maadili ya dini yetu, najua Uisilam hautaki vurugu bali unataka amani. Kitu kimoja kinachonisumbua ni kwamba nimeona baadhi ya watu wanachukua sheria mkononi kwa kumwadhibu kijana wa watu bila kumfikisha kwenye sheria aidha ya serikali au kidini kama ipo,pili nilikuwa naomba kama kuna uwezekano huyo jamaa aliyenyanyua mguu kumpiga ustadhi naye apelekwe kwenye sheria navyojua mimi mtu yeyote haruhusiwi kuchukua sheria mkononi tena hadharani kama huyo kijana au ustadhi mwenzetu anavyoonekana, nategemea maswaiba wangu mtakubaliana na mimi katika hilo, namalizia tena kwa kusema ahsalaam al khum (AMANI IWE NASI)

    ReplyDelete
  32. dah naomba atokee mwengine amuwashe kibao amani karume........

    ReplyDelete
  33. Michuzi acha kubania comments zangu..!! Hii yote inanikumbusha mambo ya George Bush kule (Iraq)..na vile viatu...halafu nikakumbuka pia kule Mbeya majuzi walipopiga msafara wa J.K mawe....lakini pia nikakumbuka kuwa raia nao waliwahi kuvamiwa na viongozi..je unakumbuka ya Ditopile?..sasa naona imekuwa tu kama mtindo...nipe nikupe...mbona michuzi unabania hii comment? Itoe basi?

    ReplyDelete
  34. Kuna watu wanasema huenda hotuba yake iliamsha hisia za uchokozi.

    ReplyDelete
  35. HIYO HOTUBA MZEE MWINYI ALIANDALIWA AU ALIANDAA MWENYEWE?
    JE ALIIPITIA KABLA YA KUISOMA. HAPA HAKUNA CHA SIASA KALI WALA NINI UKWELI NI KWAMBA MZEE KAKOSEA. KWA AMBAO HAWAJAOA NA WANASHIKWA NA TAMAA ZA MWILI AMBOZO INABIDI ZIPUNGUZWE MWENYEZIMUNGU MWENYEWE KATOA NJIA NZURI NI KUFUNGA, USILE, IKIWA HULI MWILI UTAKULA NGUVU ZA ZIADA NA HATIMAE TAMAA INASAHUKA. KWELI HILI LA KUFUNGA NI GUMU NA ZITO LAKINI BADO CONDOM HAJAISEMA ALLAH au SWA. HUKU NI KUPOTOSHANA. HATA KAMA MIMI NINAEANDIKA HAPA SIO MSAFI, SINA NDOA NINA MTU AMBAYE NAMWAMINI NA HAKUNA CONDOM KWA KUJIAMINI KWANI CONDOM INAMFANYA MTU KUWA HURU KUFANYA MAPENZI NA YEYETO WAKATI WOWOTE. KWA KWELI TUBADILI TABIA NA TUJITAHIDI KUMCHA ALLAH, KUFUATA YALIYOLETWA NA MITUME? KIJANA ANAONEKANA ANAFUNGA KWA KUANGALIA AFYA YAKE, NA WALA UCHIZI HANA NA SI MTU WA KIJIWENI. UJUMBE UMEFIKA NA MUNGU ATAKUNUSURU NA MATESO. iBRAHIM WALIVYOMTUMBUKIZA KWENYE MOTO ALISEMA EE MOLLA WANGU UFANYE MOTO HUU UWE BARIDI NA SALAMA NA UKAWA.
    pamoja na hayo mzee mwinyi pole na uzee wako wasiutumie vibaya wewe ni muugwana na msomi mzuri hilo kofi likuzindue usiikose pepo.uwi jamani mwenyezimungu tunusuru wengi wana kesi za kutengana shauri ya uzinzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...