The late Prof Ken Edwards alias Joshua Mkhululi

The University of Dar Es Salaam Business School (UDBS) Alumni alias Faculty of Commerce and Management – FCM- Alumni) with deep sympathy would like to announce the death of our founding father and the first dean of the Faculty of Commerce and Management of the University of Dar Es Salaam Prof Ken Edwards alias Joshua Mkhululi.

The legend University don succumbed to death in Arusha on 18th March 2009 and will be laid to rest on Saturday 28th March.

Prof Ken Edwards alias Joshua Mukhululi joined the University of Dar Es Salaam in 1976 after graduating from California State University and Stanford Graduate School of Business. He was born in Jamaica on 22nd of January in 1945. He leaves behind four daughters and two sons. - May his soul rest in eternal PEACE.

The Alumni will be represented by our Chairperson Mr Nehemiah Kyando Mchechu at the burial ceremony in Arusha. We also encourage all alumni residing in Arusha and any other regions in Tanzania and beyond who may have opportunity and honor to be part of this burial ceremony to attend. 

More details please contact 
Fred Moshi 
0787-873-660
Given this day of 21st March 2009 by:
PUBLICITY SECRETARY  
UDSM-FCM ALUMNI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Lo, tumempoteza mtaalam muhimu sana, aliyechangia maendeleo ya nchi yetu kwa moyo moja. Namkumbuka sana, kwani tulifundisha wote pale Chuo Kikuu Dar, kuanzia mwaka huo huo 1976. Alikuwa mtaratibu na mpenda watu. Mungu awape nguvu wanafamilia, ndugu na jamaa, na amweke merehemu mahala Pema Peponi. Amina.

    ReplyDelete
  2. amechangia mengi nchi hii ikiwemo na kujenga kwa chuo cha uhasibu arusha, lakini nchi imemfanyia nini? zaidi ya kumnyima uraia na amekaa nchini hapa kwa miaka mingi tuu ameomba uraia mpaka amekufaa...... mungu ailaze roho yake mahali pema he was something for sure.

    ReplyDelete
  3. Rest in Peace Brother.
    Nelly Temu Williams
    London

    ReplyDelete
  4. hawa waheshimiwa wengine jamani mbona tunakosa habari zao.kimwonekano tu anaonekana mwanamapinduzi hasa aliyetoka cuba na kuamua kufia tanzania. kwa anayefahamu, tupate habari yake kwa undani, alianzaje udsm,alimalizaje,aliishije au aliamuaje kuishi arusha na sio kurudi cuba.mungu ailaze roho yake mahari pema peponi,amina.

    ReplyDelete
  5. munge amempenda kuliko sisi, nikiwa natokea arusha,nimekuwa nikimfahamu kwa miaka mingi,kwa kweli ni mtu wa watu na panafricanism,mind you is jamaican but spend most of his life sharing what god bless him with fellow african,god will rest his soul in peace,amen.

    ReplyDelete
  6. Mwanamapinduzi wakweli ndomaana TZ walimnyima uraia kwakuofia ukweli wa fikra lakini tupo na tunazidi kumwaga cheche ya mapinduzi hipo siku tz patakuwa hakuna ufisadi wala upendeleo.
    Mungu amlaze mahala pema peponi Amina.

    ReplyDelete
  7. RIP Prof Ken,

    Mimi nilibahatika kukutana nae 2005 kwenye seminar moja iliyofanyika chuo cha uhasibu Arusha na yeye alikua mmojawapo wa waandaji wa seminar hiyo. Kweli yule prof ni kichwa ni mwana mapinduzi na ni mpenda maendeleo. Alifanya presenation ambayo wataalam wenzie kwenye hiyo fani wanasema wao wangeumia siku tatu kuelezea, kufafanua lakini mzee alitumia saa moja na nusu. hiyo ni kuonesha livyokua kichwa, lakini pia alikua akisadia baadhi ya wafanya biashara wa kati na wadogo jinsi ya kuendeleza biashara zao (strategic planning & mngt, and corporate Finance). wapo wengi waliokuwepo kwenye hiyo seminar na walitoa ushuhuda wao nisindependa kuwataja majina. Mwisho sitosahau juice yake ya mapera, mapapai, na maembe (zote zikiwa organic) aliyokuwa anagawa bure wakati wa seminar hiyo. Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi, Amina bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

    kichenge@gmail.com

    ReplyDelete
  8. Oh My, sikuwahi kumsikia baba wa watu, Ila tz tuache ubaguzi, tunawapa uraia wahindi/wezi, na kumnyima mweusi mwenzetu, kisa atawakosoa wakubwa.
    Poleni wafiwa, poleni watanzania wote na ndugu zake ndani na nje ya tz.

    ReplyDelete
  9. Kama mtanzania sioni aibu hapa kusema kuwa sijawahi hata siku moja kumsikia huyu mtu. na kama mtanzania na baada ya kusoma maoni ya wale wanaomjua naona aibu kuwa mwanaharakati huyu hakuwa akijulikana na watanzania wengi. naomba wanaomjua watuelimishe na kutujulisha yale aliyoyafanya.

    ReplyDelete
  10. Kuhusu Arusha na watu wa makontineti mengine.

    Arusha kuna wakimbizi wa kisiasa weusi 'Black Panthers'. Walikimbia toka USA baada ya kutumia sera za 'nguvu' kupinga sera za kibaguzi USA ktk miaka ya 1960. Weusi hao toka Marekani sasa ni wazee wa vijiji wilayani Arumeru. Pengine wasomi wanaweza kufanya utafiti kuhusu wakimbizi wa kisiasa walioamua kuishi TZ toka Amerika, Poland, Afrika ya Kusini, Namibia, Mozambique n.k

    Mpaka leo hawa jamaa waliopewa hadhi ya ukimbizi Bongo ni wanted na FBI. Labda Brother Obama anaweza kutoa amri wasamehewe 'makosa' yao.

    Pia Arusha eneo la Usa River, lilikuwa eneo waliokaa wakimbizi toka Poland, waliokimbia vita kuu ya pili ambayo Hitler wa Ujerumani walikuwa anataka kuwamaliza. Baadhi ya wa-Polishi hawa waliamua kubaki Tanzania na wengine waliamua kwenda Amerika baada ya vita kuisha. Maeneo ya Duluti kuna makaburi mengi ya waPoland waliokufa kwa malaria na magonjwa mengine yatokanayo na kuwa wakimbizi.

    Hivyo Prof Mkhululi(Edwards)toka Jamaica, kuchagua kuishi Arusha na kufundisha ESAMI na iliyokuwa Institute of Accountancy Arusha (sasa ni University)ilikuwa ni chaguo muafaka kutokana na historia niliyoeleza hapo juu na hali ya hewa ya eneo hilo.

    Wapo wengi walioishi Tanzania, Kina Prof Walter Rodney, Prof Wamba Dia Wamba, George Garang, Museveni, Frederick Chiluba(Mashamba ya Mkonge), Eduardo Mondlane, Samora na Graca Machel, Mzee na Mtoto Kabila, wanachama wa ANC na PAC Morogoro n.k n.k

    Mdau
    Rocky

    ReplyDelete
  11. MUNGU AMUWEKE PEMA PEPONI, AIMINA - MDAU MMOJA HAPO JUU ANASEMA ALIKUWA ANAFUNDISHA CORPORATE FINANCE KWA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO! HOW? CORPORATE FINANCE! MMMM!

    ReplyDelete
  12. Namimi namkukumbuka nilikutana naye kwa mara ya kwanza nikiwa bado mdogo kwenye miaka ya 97-98 akanipa zawadi ya pera, nikashindwa kumuelewa nikaja kujua baadaye kikwao mtu akikupa tunda ni heshima RIP alikuwa mtu mwema sana

    ReplyDelete
  13. Profesa Mkhulule nilishakutana naye mara mbili Arusha kwenye seminar.Naweza kusema ni mtu mwenye mawazo endelevu.Ni mpole(haongei sana)ila ni msemaji hasa inapokuja kwenye field yake.Nakiri kuwa ni msomi aliyebobea na aliyekuwa akifanya mambo yake.Nachosikitika zaidi ni jinsi nchi yetu inavyonyima haki ya uraia kwa watu ambao wanaweza kuisaidia nchi kwa usomi wao.Nakumbuka mwandishi wa How Europe Underdevelop Africa,Walter Rodney alivyoingia kwenye matatizo na Nyerere baada ya kuandika kwenye kitabu chake jinsi viongozi wa Africa huru wanavyoingilia uhuru wa wananchi kutoa mawazo na kuendesha nchi kidikteta.Baada ya vitisho vingi aliamua kurudi Guyana akauawa na usalama wa Taifa la Guyana baada ya kuhisi kwamba anaweza kugombea urais wa Guyana.Viongozi wa Africa(including African diaspora)badilikeni.

    ReplyDelete
  14. anony wa 10:00pm, usikurupuke, na elimu yako ya kuiga bila kurejesha.soma tena alichokiandika unayemkosoa, kisha changanua senteni ile iliyo aktika mabano,ahalfu ndo kosoa.
    MUNGU AKUREHAMU PROF.MSISAHAU TAREHE 13 APRIL MLIMANI, KUNA VICHWA VYA ZIADA VITAKUWA PALE.

    ReplyDelete
  15. Hivi ni kwa nini watu kama hawa hawajulikani? naamini ni watz wachache waliokuwa wakimfahamu na badala yake ni wanasiasa ambao namini mchango woa kwenye taifa hili ni mdogo sana.Nafikiri ni wakati Watanzania tukaanza kuwaenzi watu kama huyu Prof.May god rest his soul in peace.

    ReplyDelete
  16. Watu kama hawa viongozi wala rushwa wa Tanzania ni vigumu sana kushirikiana nao,maana hawako kama wao na watawakosoa.Nahisi labda alikataliwa uraia sababu alikataa kuonga,maana nchi ya kishenzi kama Tanzania kila kitu ni rushwa rushwa.Watu wengine wanapata uraia 'dakika mbili' uhamiaji kwa kuonga!Daima maendeleo hayatakuja kama hamna mapinduzi ya fikra.
    Mdau Ndoto ya mchana, Sweden.

    ReplyDelete
  17. Mwenye kazi za huyu professor hebu azitundike basi mtandaoni.

    Kama kuna video clips, research papers, published books, etc.. tuwekeeni mtandaoni tujifunze zaidi.

    ReplyDelete
  18. Poleni wote mlioguswa na msiba huu mzito. Sisi tulimpenda bali mwenyezi Mungu amampenda zaidi naye ameamua kumchukua kwake. Binadamu tukumbuke sisi na mavumbi na mavumbini tutarudi. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi AMEN.

    ReplyDelete
  19. Doh! Yaani lazima niseme Prof. Edwards/Mkhululi alikuwa moja wa nyota enzi zile wakati UDSM ni UDSM hasa (thinking pot of Africa).

    Rest in Eternal Peace.

    ReplyDelete
  20. Namkumbuka Prof.Ken nilipokuwa mdogo pale kariakoo alikuwa anakwenda kwa kina Ras makunja,akiwa amefuatana na Ras Bupe Bwakwetesa na ras makunja mwenyewe alikuwa akitupa zawadi ya kalamu na vitabu lakini sijui alikuwa na shughuli gani kule uswahili na kina ras makunja

    ReplyDelete
  21. Prof:Ken Edward aka brother Jushua Mkhululi,naikumbuka sana sura ya marehemu huyu,katika miaka ya 80 nilikuwa namuona akiongozana mara nyingi na ras ebby au ras makunja,mara nyingine walikuwa jogging pamoja kule viwanja vya gymkhana..lakini sijui walikuwa na shughuli gani??lakini mara nyingi tulimjua kwa jina la proffessor Ken.Poleni mlioguswa na msiba huu,yeye katutangulia sisi nyuma yake.

    ReplyDelete
  22. Mwezi uliopita nilikutana naye HAZINA anafuatilia mafao yake. Sijui kama alishalipwa masikini. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...