kikosi cha timu ya yanga.
Yanga jana ilinyakua kwa mara ya 22 ubingwa wa soka bara kwa kuichapa toto afrika ya mwanza bao 2-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa kirumba na kushuhudia kipa juma kaseja akifunga bao la toka goli hadi goli. Yaani alipiga free-kick toka golini kwake iliyokwenda moja kwa moja kwenye nyavu za toto afrika, jambo ambalo limeingia kwenye historia ya bara
hii inakuwa ni mara ya 22 kwa yanga kuwa mabingwa wa bara


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Issa Michuzi mie siipendi Yanga ila naipa pongezi, sasa kuhusu Juma Kaseja Vitu kama hivyo hamna Clip za Ushahidi basi utuwekee tuone?

    ReplyDelete
  2. PAMOJA NA KASEJA KUWA JUU.BADO MAXIMO ANABANA.KOCHA HUYU AONDOKE.ANATUDANGANYA APETA TIMU SOUTH NANI ATAMCHUKUA LOOSER?
    PIA SOUTH HAWANA MCHEZO AKIPOTEZA MCHEZO HANA KIBARUA SIO KAMA SISI TUNAMUONA KAMA MFALME.
    MDAU KISIJU.

    ReplyDelete
  3. Aaaakkhkhhhh...@#%$**!~ Mabingwa hapa bongo tu, wakivuka mipaka aibu. Yafaa SSC iachiwe ifanye kazi inayoiweza na iliyoizoea ya kuiwakilisha nchi kimataifa. SIMBA OYEE!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Kaseja unatisha Braza...!!!. hiyo ni salamu kwa Maximo........!!!.Kuondoka kwako Simba hakufanyi nikuchukie ,Huko juu....!!!

    ReplyDelete
  5. Teheee teheeeee.... mimi hata msimamo wa ligi yenyewe sijui upo vipi? Zaidi najua Man utd, Inter na Barcelona wanaongoza ligi majuu .....Michuzi naomba uweke pia msimamo wa ligi tujue nani anashuka daraja pia....

    ReplyDelete
  6. HONGERA WAZEE WA TATU BILA (Al alhay wanakuja)

    ReplyDelete
  7. Kwa wasiojua hizo timu mbili ni sawa na mtu na mkewe kwa hiyo goli la Kaseja halishangazi!!!!

    ReplyDelete
  8. jamani yule jamaa Obrein kipa mzungu wa Yanga yuko wapi!mbona hamuwakilishi kwenye picha hii ya magwiji wa Yanga?

    ReplyDelete
  9. tushawazoea yanga wazee wa kununua!!!! tena kwa toto aaah shwari hata kwa mkopo watapewa tu!!!

    ReplyDelete
  10. hatimaye Mh. Balozi umetuwekea habari yetu, tunashukuru sana. Hongereni kwa wanayanga wenzangu wote. Watani acheni kubana, kubalini matokeo; jaribuni mwakani!

    ReplyDelete
  11. YANGA AFRIKA YANGA UMOJA WA MATAIFA!! MABINGWA WA SOKA WA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI NA KATI EEEEE!!!

    Hata mzee mwenyewe Kabasele Yampanya Peple wa Kale kakubali mavituuz yetu. Mlio na wivu kunyweni sumu!!!

    ReplyDelete
  12. Yanga wazee wa majungu na fitina dah siwawezi!!

    ReplyDelete
  13. MTABAKI KUFUNGANA WENYEWE KWA WENYEWE

    ReplyDelete
  14. Nanukuu moja ya rap za marapa wa bendi nguli ya FM Academia,"Yanga Afrika tuna tesa, Yanga Afrika tuna tesaa....."

    Yanga Oyeee....

    Hongereni wana yanga wenzangu kwa ushindi huu...!!

    ReplyDelete
  15. Bahati mmbaya mpira wa miguu siupendi kabisa......Yanga ni timu ya wapi jamani? Mdau MBIJE,A-Kafanabo

    ReplyDelete
  16. hahaha utawajuwa tu watu wanatafuta watu waseme yanga ni YOUNG African Of Dar-es-salaam au Yanga Afrika ni timu mmoja ya mpira au Kandambili za kuendea chooni. Sasa Video ya Kaseja kapiga bao mbona hakuna? yule Mfundishaji wa Yanga mzungu kasema Bao la Kaseja Mguu wa mungu? wazungu vipi hawa? Mpelekeni Elimu ya Dini.

    ReplyDelete
  17. Yanga A imeichapa Yanga B...sio mbaya ushindi wa kupeana!! Tuwasikilizie mashindano ya kimataifa mtakapoishia...Simba oyeee!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...