hii ni taswira ya jinsi mambo yanavyokuwa barabara ya bagamoyo kati ya mwenge na makutano ya barabara ya morocco jijini dar ambayo imejengwa na kuwekwa mistari ya kuonesha ni njia tatu.

watuamiaji wa barabara hii wamekuwa wakilalama kwamba badala ya kuleta ahueni ya foleni sasa imekuwa 'machinjioni' kwani kila kukicha ajali mbaya kibao (majuzi tumempoteza mwenzetu hamidu bisanga) hutokea kutokana na komfyusheni iliyopo hapo na wahusika wako kimya tu, japo kila kukicha wanalalamikiwa na  pia wanaliona.

utafiti wa globu hii ya jamii umeonesha kuwa mmiliki wa barabara hii ni wakala wa barabara, yaani Tanroads, kwa vile ni njia kuu. ombi la watumiaji wengi ni kwamba yawekwe matuta ili kuzuia ama kupunguz mizinga sehemu hiyo.  wadau mnasemaje?


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Asante mdau kwa kulileta suala hili. Kwa maoni yangu ni vema mabmo ya njia tatu yaondolewe kabisa. Michoro ya mistari ionyeshe njia mbili tu. Hali ilivyo sasa badala ya kupunguza foleni, ajali zinazidi. Madereva nao wanatumia ubabe kupita nafasi sio yao. TANROADS waondoe mistari ya njia tatu zibakie mbili tu. TANROADS washirikiane na Traffic Police kuondoa kero hii.

    ReplyDelete
  2. hii nchi imejaa upumbavu wa kutia machozi ,kila siku nalia na hawa watu na uvunjaji wa sheria za barabarani hio njia haina matatizo yeyote na alama za barabarani ziko wazi katika hio njia, ila madereva hawaoni kama hio inajalisha sasa wewe utengeneza barabara nzuri kisha kesho unaweka matuta kama vile ile njia ya kimara high way imejaa matuta kwa sababu watu hawajali sheria za kutumia barabara hii inauzi sana, tunakua tunapiga hatua mbili mbela tunarudi tatu nyuma, hii inakera sana,cha muhimu boresheni sheria za barabarani, the president na watendaji wake wa polisi lazima watafute tough measures kurudisha sheria za barabarani hata kama ikihitaji zero tolorence on traffic rules.hii swala la matuta linanikera sana, serikali lazima iwe na nguvu katika hili swala jamani hii nhi itakua wapi baada ya miaka hamsini? watu wanataka magari kila kukicha, usafiri wa public hauboreshwi,njia haziongezwi in the same rate as cars and people increases. hi nini? je sisi ni watu au mbwa? au nguruwe? lazima tukatae kua nguruwe tuwe na utaratibu, na suluhisho lisifanywe na watumishi wa serekali kama vile lowassa alivyoamka asubui baada ya kushauriana na mkewe eti wakati wa rush hour barabara zitumike hivi, watu walipoteza sana maisha wakati ule na alietoa hilo tamko bila kujali ushauri wa kitaalam au kufanya research yupo anakula nchi tu, hii nini watanzania? aaaaaaaaaaah inakera sana, acheni kutoa masuluhisho ya kujiiba kwa kukosa kauli kwa wavunja sheria.
    we need tough measures, including zero tolerance on law breakers, here get their cars out of the roads take their driving licenses and lets wait and see who's tougher. wala hutaitaji hao matuta ila tu kuongeza alama za barabarani na kutoa mafunzo mazuri ya barabarani, hizi shule zote zimejaa ulughai mtupu nazo ziboreshwe udereve sio kukanyaga mafuta tu ila madereva hawa wanachofundishwa ni kuchomekea na kukanyaga mafuta na break, nchi hii inakua watu wanaongezeka basi watake wasitake lazima sheria zitawale ila vinginevyo tutakufa wote kabla ya siku halali. aksanteni ni hasira sana wadau na hili swala

    ReplyDelete
  3. Hiyo mistari ya njia 3 ifutwe tu hamna haja ya kuweka matuta wewe uliona wapi hiyo njia ya3 asubuhi inatumiwa na waendao mjini jioni inabadilika inatumika kwa wanaotoka mjini sasa huoni huko ni kuchangany'ana madereva wangine wanakuwa wamekuja mara moja tu toka mikoani watajuaje kama asubuhi hivi jioni hivi huyu ruassa sijui aliona wapi barabara za aina hiyo.
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  4. I hate watu wanaofikiria matuta ndio njia ya kupunguza ajali. Huku mnalalama foleni, then bado mnataka matuta. Lipi jema kwenu? Suala la ajali halipunguzwi kwa kuweka matuta barabara zote. Naamini itafika siku barabara zote za Tanzania zitakuwa na matuta kila baada ya nusu kilometa. Hii ni kwasababu ya fikra finyu. Tujiulize, mbona wenzetu hawana matuta na magari yanakimbia sana tu, na ajali ni chache? Tatizo la kwanza ni madereva kutokuwa na elimu ya udereva na kupatiwa leseni feki. Na pili ni ubovu wa magari yenyewe. Magari mengi ni vimeo. Na tatu ni ubovu wa barabara zenyewe. Barabara nyingi ni substandard.

    Matuta sio suluhisho la kupunguza ajali.

    ReplyDelete
  5. Hakuna sheria kama hii duniani. Njia tatu ni hatari kwa maisha ya wenda kwa miguu na wenye magari. Hivi tujiulize, mwenda kwa miguu anapotaka kuvuka njia tatu atafanyeje? Tunapotaka kuimplement vitu kama hivi tuwe na resources za kutosha kama madaraja ya kuvushia wenda kwa miguu na wenye magari wapewa elimu tosha na sheria kali zitungwe. Kama hoja ni kupunguza foleni; sidhani kama huu ufumbuzi sahihi.

    ReplyDelete
  6. Tanroads wangetupa mifano ya utaratibu kwenye nchi nyingine duniani, maana tembeatembea yangu huko duniani sijawahi kuona utaratibu kama huu. utaratibu wa kuweka matuta ni mzuri kwetu sisi wenyeji lakini ni picha mbaya kwa wageni wanaokuja nchini.inaonyesha ni jinsi gani madereva wa tanzania ambavyo wana akili kama za wanyama (samahani lakini) mpaka kutokujua alama za barabarani na kuzifuata. iko siku matuta yakishindwa kutoa suluhu ya tatizo tutaanza kufikiria kuweka mashimo (drifts kama njia ya kwenda mto wa mbu), kwa hali hii wakijitokeza wazungu saba kama Dr James Watson na kutoa sentensi zinazofanana kuhusu uwezo wetu waafrica huku upstairs (ubongoni) tusilalamike maana mambo mengine yapo wazi kabisa. ni hayo tu

    ReplyDelete
  7. Mdau LubidaApril 02, 2009

    Kwa njia kama ile matuta hayafai kwani yataleta shida zaidi, hawa TANROADS waipanue ile barabara (nimesikia mradi wa upanuzi umekwishaanza morocco mpaka TEGETA) msaada toka JAPAN hivyo wafanye jitihada kuelimisha wananchi wakisadiana na matrafiki ili kupunguza ajari.
    ila kwa sasa madeleva wazembe wanazidi kuongezeka, kuna lika la vijana/watoto labda wadau na hili tuliongelee

    ReplyDelete
  8. Kama kawaida yetu bongo mpaka watu wafe ndio tunashtuka. Tuliliona hili toka mwanzo wengine infact baadhi yetu hatukuelewa mantiki ya kuongeza lane ya tatu. Kwa hulka yetu ya ubinafsi uliokithiri lane tatu ni ngumu sana kuzicontrol jamani. Mswahili gani atakubali apite lane moja na kuziacha zingine mbili eti za waendao mjini nani thubutu yako. N hawa ndugu zetu wa daladala ndio kabisaaaaa!

    Sijuwi kama mmelinotice hili, kwa kuwa na lane 3 almost tumeua kabisa njia za baiskeli na waendao kwa miguu sasa sijuwi hao TANROADS huu utaalamu walijifunzia wapi kwa kweli. Haya mambo ya kienyeji kinenyeji yana gharimu sana infact kama serikali inapaswa kuwa na mipango mizuri ya muda mfupi na mrefu huu ukienyeji enyeji ni aibu kwa serikali na inawagharimu maisha ya watz yasiyo na hatia. Mimi hii njia kwa sasa ninaiogopa kama ukoma maana naona kama tunayachezea maisha ambao ni ya thamani kubwa. Yaani ni kama vile tunatengeneza sinema vile kumbe ndio maisha yanaenda, bongo noma.

    ReplyDelete
  9. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  10. Kama kawaida ya vitu vingi TZ, hii barabara imejengwa kwa mtazamo kuwa wanachi watakuwa wabusara na kufuata sheria. Hii dhana ni potofu na haifai kwa nchi yeyote, iwe Sweden, USA, Japan, Italy au hata Cayman Islands.

    Watu watakuwa watu tu. Wana haraka zao, wengine wana pombe zao, wengine ni waoga. kila mtu ni complex na atafanya maamuzi ya namna ya kuendesha kutokana na hulka aliyonayo wakati husika.

    Hivyo basi, inabidi Tanroads wanapojenga barabara wajenge kwa namna ambayo italazimisha watu waendeshe kwa namna fulani - na siyo kutegemea busara za dereva.

    Solution ya hii kitu inayoitwa njia tatu, kwa sasa ni kujenga Island - au tuta, la kutenganisha wanaoenda mwenge na wanaotoka mjini.

    Kujenga matuta ya kupunguza mwendo ni mwendelezo wa tatizo. Naomba tuache kufikiri kuwa matuta ya kupunguza mwendo ndiyo solution ya kila kitu.

    ReplyDelete
  11. Mbona hiyo barabara ina mapungufu makubwa tuu. Hizo njia tatu mbaona hazipo hapo. Kwa sheria za kimataifa ninazozifahamu mimi hiyo daladala hairuhusiwi kabisa kupita huko kwenye mstari wa njano. Kwanza naomba niulize kwanini huo mstari wa njano upo hapo na uliwekwa kwasababu gani. Mbona hakuna vibao vyovyote vile vinavyoweza kumfanya mtu yeyeote mgeni kutumia hiyo barabara hiyo bila kusababbisha ajali. Sijaona vibao vinavyo ruhusu au kukataza kiwango cha speed hakuna alama zozote zile. Hapo moja kwa moja mbona ujenzi haujaisha jamani au ndio ujenzi umeisha?. Kama umeisha basi tume ifanyekazi yake hao wakandarasi na mainjinia waliohusika wakamtwe na waulizwe kwanini na kwasababu gani kujenga kisu cha kutolea roho zetu. Kingine bado haijaingia kichwani njia tatu kivipi ukisema njia tatu mimi naelewa kuna njia tatu kuelekea na kurudi Bwagamoyo yaani jumla pawe na upana njia sita. Yaani magari sita yaweze kuendeshwa sambamba mbona hapoa sioni. Michuzi ninachokiona hapo ni njia moja na nusu hata mbili hazijafika naomba msaada mimi bado haijaelewekw hapo vipi?.

    ReplyDelete
  12. Napenda kuchangia kidogo bwana michuzi na wadau wengine. Mimi naona dawa ni kuboresha sheria za usalama barabarani kama wadau wengi wanavyosema. mafunzo ya udereva yatolewe ya kutosha na mitihani iwe ya kweli kweli. Wakitaka mifano wasafirishe wadau wachache kwenda Marekani waangalie shughuli ilivyo pevu kwenye baadhi ya States, (usiku hakuna magari lakini red light means YOU HAVE TO STOP, pita uone ukikamatwa) kila kosa lina adhabu yake kuanzia fines kubwa, kupoteza leseni kwa muda mpaka kifungo cha jela, usipolipa fine unaweza enda jela! na hakuna utani. Kwa msingi huu watu wangekuwa wastaarab na watumiaji wazuri wa barabara

    ReplyDelete
  13. Wanaochangi na kusema eti shida ni madereva; sijui hawajui kuendesha, sijui wameletewa leseni bar, sijui marekani inabidi dereva asomee chuo kikuu - wote wametoka kwenye point.

    Shida ya hii barabara, au "KISU", kama alivyokiita mdau mmoja hapo juu, ni kwamba kimejengwa vibaya. Hauwezi ukajenga kitu ambacho kitaweza kufanya kazi kwa usalama kama tu watumiaji wake wote ni walokole.

    Kwanza ni asilimia ngapi ya wana Darisalama wameokoka - je walifanya hiyo tathmini? Na hata kama ni asilimia 100%, je kila siku wanavyotumia hicho KISU, wako under controll? Hakuna siku ambapo wanakimbiza watu hospitali? Au wanawahi ndge Air port? Je siku wanapokwenda kufumania, wanakuwa wako under controll? Kama engineer, ni sharti uzingatie vyote hivi.

    Afazali waJapani wameahidi kuibomolea mbali. Tuombe tu Mungu kuwa hu mdororo wa uchumi duniani usilete kiwingu.

    ReplyDelete
  14. Bwana Michuzi tafadhali tupia jicho na hapa!
    Hi wanandugu.
    Wazo langu kuhusu hii barabara ya Bagamoyo Road ni kuwaomba wamiliki TANROAD kuchukua hatua za dharura kuongeza barabara ya nne hata kama kwa kuanza na ya kifusi. Hapo usumbufu utapungua pia wasisahau kuweka matuta sehemu zote zenye vivuko vya watu wengi.
    Ningeshauri pia jicho la kuchukua tahadhari lione OLD Bagamoyo tatizo Roundabout ya Kawe kuelekea Daraja la Mlalakuwa, wakati wowote kuanzia sasa patakuwa na maafa makubwa kutokana na msongamano mkubwa wa magari yatokayo Tegeta, Boko, Kunduchi na vitongoji vyake.
    Nawasilisha kwa utafiti wa kina.
    Mpenda Taifa hili.

    ReplyDelete
  15. Mimi nafikili barabara aina makosa yoyote,tatizo lipo kwa watumiaji. kwa kweli inaitajika elimu mpya hapa tanzania hasa kwa madereva.hakuna sababu kwa dereva kuendesha gari kana kwamba unakwenda mwanza. kila asubuhi pale victoria ni kasheshe kuvuka barabara.magari yanayotoka mwenge yanakimbizwa utafikili kuna mashindano. pamoja na kuwa kuna alama ya pundamilia lakini si ajabu kwa dereva kumpigia honi mwenzie eti kwa kuwa amesimama na kupisha wenda kwa miguu.
    Leo asubuhi kamanda wa kikosi cha usalama barabarani oysterbay, amesema kuwa matumizi ya barabara hiyo ni njia mbili kutoka mwenge hadi morocco, na moja morocc hadi mwenge. lakini utakuta mwingiliano usio na lazima watu wazima wanafanya vitu vya ajabu barabarani.

    Ila naunga mkono hoja ya matuta, maana kwa uendeshaji huu wa kitanzania, bila matuta tutauana sana ama kutiana vilema.

    ReplyDelete
  16. MATUTA SIO NJIA YA KUTATUA AJALI,HUWEZI KUWEKA MATATU KILA KONA YA JIJI.NJIA NZURI NI FAINI KALI KWA MADEREVA NA KIFUNGO KAMA AJALI NI MBAYA ZAIDI.WATU WANAOWEZA KUPUNGUZA AJALI NI POLISI WA BARABARANI KAMA WATAWEZA KUACHA KUCHUKUA RUSHWA.RUSHWA INAWAFANYA WATU WASIJALI SHERIA ZA BARABARANI KWANI WANAJUA WAKIFANYA KOSA NI RAHISI KUACHIWA.FAINI KALI KWA MADEREVA PAMOJA NA KIFUNGO KILA MTU ATAKUWA MTIIFU BARABARANI.FAINI ZIWE KUBWA NA KAMA MTU HANA HELA APIGWE KIFUNGO JELA.SIO MTU ANAUWA WATU WAWILI KWENYE AJALI ANAPEWA DHAMANA YA MILIONI MOJA.
    "CHA MTU MAVI"

    ReplyDelete
  17. Njia tatu sizioni hapo juu, bali njia mbili (two lanes each direction). Kuna umuhimu wa kuwapeleka shule madreva bongo especially wa daladala i.e. kuwe na mandatory training kwa kila dreva ili wafundishwe alama za barabarani. mfano: Dreva wa daladala anaendesha kwenye shoulder ambayo is meant for pull over hasa kwa magari madogo. kawaida upana wa lane unatakiwa uwe 11 - 12 feet kutegemeana na aina ya barabara (type of the road). pia upana wa shoulder unatofautiana e.g kwa highway ambapo shoulder inatumiwa kama bus lane during rush hrs inakuwa 12ft otherwise from 4 - 10 ft kulingana na aina ya barabara. Kuweka matuta siyo solution kabisa bado yanaweza kuhatarisha usalama wa wasafiri.

    ReplyDelete
  18. Tujifunze kuendesha magari kwa staha barabarani. Mbongo mtaani hana haraka. Mpe gari umwone. Kuchomekea, mibio, haraka, kukosa heshima kwa yeyote mwenye gari dogo zaidi yake na mwenda kwa miguu. Nakuhakikishia tukianza kuendesha magari kwa kuheshimiana, hata bila kufuata sheria ajali zitapungua. Tukiongezea na kufuata sheria inaweza kutokea ajali moja ndogo kila miaka kumi, ajali iliyotokana na tairi bovu kutoka China kupasuka baada ya kukanyaga kokoto. Waziri wa mambo ya ndani waagize kikosi cha usalama barabarani wakusanye faini za kuchomekea, kuendesha kupita taa nyekundu, mwendo wa kasi, kuendesha na kileo kichwani nk. Ukishapigwa 20,000/= mara mbili tatu utatia adabu tu.

    ReplyDelete
  19. USHAURI WA NINI NA WEWE NA WALIO HUKO NKIPITA NKITAMBA, "BONGO TAMBARARE".
    MTU AKIUA, AKIFA TENA ANAYEKUGUSA KAMA RAFIKI NDIYO UNAKUJA NA HOJA ZA KUCHANGIWA. MBONA ZA CHENGE HUKUWEKA HAPA UKAOMBA WATU WACHANGIE? HII NI BLOG NA SIYO NEWSPAPER KUDHANI UTASHTAKIWA KWA KUTOA HUKUMU DHIDI YA CHENGE.
    MADEREVA WOTE BONGO PENGINE HATA WEWE MICHUZI HUNA LESENI. NA KAMA UNAYO BASI YA KUPITA KWA AFANDE "NIPELEKEE KITOWEO NYUMBANI" LESENI NJOO CHUKUE BAADAYE.
    HIYO BIMA NDIYO USISEME. ASILIMIA 80 YA MADEREVA WA BONGO HAWANA. DEREVA WA DALADALA HANA BIMA KWA VILE MMILIKI WA GARI AMEKATAIA GARI YAKE TU NA HAIMGUSI ABIRIA SEMBUSE DEREVA NA WAPIGA DEBE WENZAKE.
    HATUWEZI KUENDELEA WAKATI NCHI IMEKALIA RUSHWA, WIZI, UNYANG'NG'ANYI NA UDANGANYIFU USIO NA KICHWA WALA MIGUU.
    VYUO VYA UFUNDI VIPO, MAGARI YANAYOFUNSHIA WATU UDEREVA (WEKA PICHA ZA MAGARI TUNAYONE HAYO HAPA), YAPO HOI TAABAN NA HAYAKAMWTI KISA....YANA LESENI YA LENA! UNATEGEMEA DEREVA ATAJUA ANACHOFANYA.
    KWA UJUMLA, KAMA MNATAKA KULINDA USALAMA WA WATU, MADEREVA LAZIMA WAJUE BARABARA SI MAGARI PEKE YAO BALI NI ZA WATUMIAO BARABARA WAKIWAMO WATEMBEAO KWA MIGUU, BASIKELI (BYCICLE) ETC.
    LESENI ZIWE ZINATOLEWA KWA UMRI UNAOSTAHILI ANGALAU MIAKA 18 NA KUENDELEA. WANAOTAKA LESENI LAZIMA WAHITIMU MITIHANI YA UDEREVA YA DARASANI NA VITENDO HALISI NA LAZIMA KUWE NA MAKSI KUBWA.
    MITIHANI YA UDEREVA MAJUU HUNA HAJA YA KUIBA KWA KILA KITU KINAUZWA MADUKANI KWENYE CD NA DVD ROM. UNACHOTAKIWA KUSOMA MASWALI HAYO (ZAIDI YA 2000) NA HUJUI UTALETEWA SWALI GANI SIKU YA MTIHANI.
    KAMA CHENGE ALIDAI ALIKUWA ANAENDESHA GARI KATI YA SPIDI 80-100 KWA SAA, SIJUI SHERIA GANI INAYOMLINDA KUENDESHA GARI KWA KASI KIASI HICHO NA AMEKIRI KUFANYA HIVYO LAKINI KOSA HILO HALIPO KWENYE MASHTAKA YAKE. UNATEGEMEA KUTAKUWA SHERIA WAKATI MWANASHERIA MKUU ANAVUNJA HADHARANI. ACHENI KUPOTEZA MUDA WATU KUJADILI MASUALA HAYO.
    TUNA USONGO NA JINSI MAMBO YANAVYOEDESHWA KIENYEJI HUKO BONGO. ILA TUKIGUSIA TU, TUNAAMBIWA WABEBA MABOSKI HATA KAMA MTU HUFANYI KAZI HIYO, LAKINI UTASHAMBULIWA. WACHE WAFE NA HATA NDUGU ZANGU PIA NI MIONGONI MWA WAFAJI KWANI NCHI INAONGOZWA KIENYEJI MNOOOOOOOOOOOOOOOOOO. DAMN IT.

    ReplyDelete
  20. matuta kwenye highway si ndio kutakua machinjioni zaidi? mimi naona kama alama zote (signs) za barabara ziko sawa ni kuweka kamera na mtu anayevunja sheria kufuatwa na kutozwa faini. Hizo hela zitasaidia kuimarisha kuitunza hiyo barabara.

    Na mbona sioni lane tatu? na huyo mwenye van mbona kama anaendesha kwenye lane mbili?

    ReplyDelete
  21. Hiyo gari inavunja sheria...hiyo sio yellow line kweli? hiyo sehemu inatakiwa iwe ya emergency parking. hao watu wanapata kuendesha gari bila kujifunza sheria za barabarani taaabu kweli...leseni za mwanerumango hizo

    ReplyDelete
  22. jamani serikali kilio chetu mkisikie hizo njia tatu wekeni ulaya watu wanofuata sheria sio TZ nilikuwa huku last year kwakweli niliona hiyo barabara haina tofauti na 'SUCIDAL" plase jamani something needs to be done

    ReplyDelete
  23. Shukran Brother Michuzi kwa kuileta hoja hii mezani.
    Kwa kweli kama kuna kitu kinanikera, au kinawakera watanzania wengi waishio jijini Dar es salaam na wenye machungu na maisha ya watanzania wenzao ni hizi barabara 3, kwani kama kuna takwimu zimehifadhiwa kuhusiana na ajali za barabara tatu,,,basi hatitakua zinamvutia mtu yeyote kuzisoma au kuziona. Kwa macho yangu nilishuhudia mtu akigongwa ubungo karibu na tanesco, tena wala si kwa uzembe wake,,,bali ni kwa uzembe wa viongozi wenye uvivu wa kufikiri na uzito wa kutoa maamuzi sahihi. Huyu mtu alikua anavuka akitokea upande wa ubungo maji, na kuelekea tanesco,,,ilikua ni asubuhi, muda ambao barabara tatu zilikua zikielekea mjini. kwa kweli iliniuma na mpaka leo picha hii hua hainitoki kichwani.
    nirudi Bagamoyo road, barabara ambayo "desishem mekaz" wengi hupita kwa kwenda kazini na kurudi majumbani kwao...hivi kweli, waliweza kukubaliana na hali hii ya kujenga barabara 3? nini kilikua kina harakisha? leo tena tunasikia kuna utanuzi wa barabara nne mpaka kule tegeta! sasa jamani ni nini hiki kama sio wizi mtupu? wanaokufa wengi, si wale ambao wanahusika na maamuzi haya,,,kwani wengi wao, hua wanapita na misafara,,,kwa hiyo hili hawalioni. mimi ninakua na wasiwasi juu ya taaluma ya ujenzi na mipango iliyopo hapo TANROADS,,,waliwezaje kukubaliana au kuushauri uongozi wa juu, kuhusiana na utanuzi wa barabara wa namna hii?,,,,hebu nenda pale njiapanda ya sayansi au pale bamaga(pamoja na kuepo kwa taa) ukaone magari yanavyo umana. Watanzania wengi bado hatuja staarabika kiasi ambacho tukaweza kujiendesha kwa kutumia akili mara mbili zaidi ya kawaida. Nasema hivi, kwa kuzingatia mambo yanavyokua magumu kwetu, kwenye hali nyepesi na za kawaida tu, mfano kuheshimu vitu kama vivuko na taa za barabarani. Sasa leo unatuwekea barabara 3, tutumie akili kichwani kufanya maamuzi? litawezekana hilo? mara mishale ioneshe mwenye haki ni yule atokaye mwenge, mara matangazo redioni yaseme asubuhi ni haki kwa anayetoka mwenge,,,na jioni ni haki kwa anayetoka mjini. Sasa jamani hili kweli ni sahihi? na vipi kwa wageni,,,ambao udereva wao, ungetegemea zaidi alama za barabarani? kuhusu matuta hiyo ndio kero nyingine ambayo sipendi hata kuizungumzia....maana kuna mengine hata alama za kuonesha kama yapo, hakuna. Ni bora kutokufanya kitu kama huna hela ya kutosha, kuliko kufanya kitu kwa mapungufu, na mwisho wa siku ikapelekea vifo vya watu wasiokua na hatia. hata kama maendeleo yanakuja taratibu, basi kwa hili la kuongeza lane "njia" moja moja kwenye barabara kubwa, tumechemsha. tusifananishe ujenzi wa barabara nyeti kama hii na ujenzi wa nyumba ya kuishi mtu binafi (ambayo unaweza ukaezeka upande mmoja ukaanza kukaa, au ukahamia, ndio ukajenga fensi).

    ReplyDelete
  24. Najaribu kum-picture huyu engineer aliyechora hii barabara....

    ... baada ya kukesha usiku mzima anachora, mhandisi anaamka kwenye kiti. Anachukua ile chupa tupu ya Teachers aliyokuwa anakunywa staili ya "kazi na dawa" na kupeleka jikoni. Anaangalia mchoro wake na kujisifu "Yes, kitu hicho. Bei poa kujenga na magari mengi zaidi yatapita. Mimi ni Genious... Lazima hapa niukwae uwaziri"

    ReplyDelete
  25. Hili tatizo lina sura nyingi mno.
    1. Askari wa usalama(hatari) barabarani hawajui sheria kabisa. Ukiwa unasubiri taa(kijani) ikuruhusu daladala inaweza kukupita na kwenda kufanya miujiza kule kunako taa nyekuku mbele ya macho ya askari wa hatari barabarani.
    2. Matumizi ya barabara dar es Salaam ni mabaya kuliko sehemu nyingine nyingi za ulimwengu.
    Hakuna jambo la kishenzi zaidi kuliko kujenga kilometa moja ya barabara kwa TAS 0.5bn halafu unaweka matuta yanayoruhusu MATIPA ya mchanga kuruka kwa spidi wanayoitaka bila kujali, wakati sisi (walipa kodi wakubwa) ambao ndiyo kodi zetu (kubwa) ndiyo zinazojenga hizo barabara magari yetu kwa kuwa ni mafupi na aghali yakiharibika kabisa. Bahati mbaya hatuwezi kwenda kwenye shughli zetu za biashara kwa Matipa. Hata Rais haendi kazini kwa Tiiiiiiiiiiiiipa.
    3. Barabara ya Morogoro ina askari wa hatari barabarani na matuta mengi /km kuliko baraba zote Tanzania nzima, lakini vile vile ina ajali na mauji mengi kuliko barabara zote Tanzania kwa mujibu wa taarifa za afande Kombe. Matuta barabarani hayasaidii kumgeuza dereva shenzi kuwa mwerevu ghafla. Kwani huko kwingine kwenye magari mengi zaidi saaana kuliko hapa (k.m. Dubai, China, AbuDhabi, Hong Kong) wanafanya je? Trafiki wa hapa kashindwa kazi 100%. Wakati umefika wa kuwabinafsihsa na kuleta vijana kutoka hapo Rwanda, au sehemu nyingine. Faini watakazokukusanyia kutoka kwa madereva shenzi wale ambao wasiyojua tofautu ya kushoto na kulia lakini wanaweza kumhonga trafiki wa pale Ubungo buku mbili tu wapite faulo, zitawalipa mishahara hao wazungu na faida mlima kwa serekali.Sisi tutapata faida kuweza kusafiri kwa usalama hasa ukizingatia ukweli kwamba magari yetu ni ya bei mbaya sana.
    4. Huo mDCM uaonafanya fujo hapo kwenye picha ambao hata afande mwema, kombe, manumbu, wanauona,,, nani kafanya au kasema nini???
    5. Madereva waangalifu ni wengi dar es slaam. Akifanyiwa fujo anende wapi ambapo hatageuziwa kibao? Tutakapofika huko tutamwuuliza mzee DITO yaliyomfikisha pa kumwadhibu Yule kijana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...