In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.









  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com








msaada tutani

Honda cr-v 2.0 

Wadau naombeni msaada wenu.
Nafahamu ya kwamba hapa ni jungu kuu. Gari aina ya  Honda cr-v 2.0 auto, kwa kiwango gani inafaa kutumika katika nchi zetu za kiafrika. 

Kwa mtu ambaye anatumia  gari ya aina hii au mtu anayeifahamu gari hii anaweza kutoa picha kamili,  kama gharama za uendeshaji na maintainance, uimara wa gari, upatikanaji wa spare, nk. Ushauri wenu utanisaidia sana katika kufanya maamuzi! 
Ahsante 
 
Mdau Dan, Belgium
 Thanks Mr Michuzi in Advance!


Kuna Maoni 27 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Utalia na vipuri!!! Kuna mtu namfahamu analo kama hilo. Ameliegesha kwa sababu mpaka aagize vipuri kutoka ng'ambo.

  2. Anonymous Anasema:

    Tafuta Rav-4 au Harrier. Utalia na spea.

  3. Anonymous Anasema:

    I own a crv since 2005 it had abt 54000km and it is not expensive to maintain. The only major repair i have done to the car is to change stabiliser bushes, stabiliser links..as you know the condition of our roads. The only thing i can advice you is to follow maintance schedule and to use unleaded petrol. You will enjoy it more when you travel long distances..it response to the pedal very well...

  4. Malkiory Anasema:

    Hello, ninapenda kukuambia kuwa HONDA CR-V ni moja ya chaguo langu, kwa maana kuwa inapenda kuwa family car. Japo sina hakika na upatikanaji wa spare parts zake, nimeshawahi kuambiwa kuwa spare parts za HOND CR-V ni kazi kupatikana Tz.

    Pamoja na hayo nimeona watu wengi wakiendasha Honda CR-V sasa sijui wanazipata wapi hizo spare parts.

  5. Anonymous Anasema:

    Kila gari inategemea na matumizi na udereva vyote vinachangia kuwa na gari kwa muda mrefu na ktk ununuzi wa spare pia kwa maana hiyo unakuja kutumia mwenyewe na itakuwa ndio gari mmoja kwa kila safari au?/hapo ukiweza jibu hayo maswali utapata mamna ya kuona gari yako itakuwaje,ila kwa aina ya gari hiyo ni nyanya(kimeo)haifai kwa maana hiyo achana nayo kwa ushauri wa bure.

  6. Anonymous Anasema:

    NDUGU YANGU HIZO HONDA HUKU ZIMEJAA KAMA YEBO YEBO NOW UKIRUDI NA KITU NYUMBANI USIDHANI KAMA UTAKUTA HAKIJAINGIA.
    WEWE RUDI NA GARI LAKO SPEAR PART ZA KUMWAGA TU

  7. Anonymous Anasema:

    spare au spear parts sio kazi. vijana wa kuzichomoa kutoka gari moja na kuwauzia watu wengine au kutoka kwenye gari mwenyewe na kuuziwa sio kazi kubwa hapa kwetu bongo. we leta mchuma tu tuongeze idadi ya kugawana utajiri na umaskini.

  8. Anonymous Anasema:

    Kweli utalia na vipuri LAKINI ukifunga vinachukua muda kabla ya kuchakaa.

    Ushauri: Jaribu TOYOTA, pamoja na kwamba Honda CR-V na Nissan X-Trail ziko daraja moja lakini bei na upatikanaji wa HONDA ni mgumu!

  9. Anonymous Anasema:

    Sasa wadau wenzangu huu ushauri wa upatikanaji wa spare za Honda DR-V ni kwa hiyo model ya 2.0 au ni kwa zote? Kwa kweli mmenifungua macho sana kwani nami nilikuwa na wazo la kuvuta Honda CR-V. Sasa wadau gari gani 4WD ni bora kwa TZ kwa wakati huu. Natanguliza shukurani zangu kwa ushauri wenu.

    Mdau U.S.

  10. Anonymous Anasema:

    Kwa uzoefu wangu mdogo ni kuwa kwa Tanzania bado suala la spare ni tatizo kwa magari ya aina zote ukiachilia mbali TOYOTA. Haya magari ya aina nyingine watu wanaendesha tu kwa ku-"cross fingers" matatizo yasitokee. Na wengine wanayagharamia saana kwa kuagiza spare Japan (Hapa ninamifano ya mtu alieagiza spare Japan za Honda-Odyssey).Na nadhani kinachofanya watu wanunue aina nyingine za gari ni bei zilivyokuwa ndogo ukilinganisha na Toyota makes. Unaweza ukaona aina za mitsubishi,Nissan,SUbaru,Daihatsu, Honda yaana bei ndogo ya kutupa ukilinganisha na Toyota (Hapa nikifananisha model zinazoshabihiana kwa kila manufacturer).
    Ushauri wangu ni nunua Toyota achana na aina nyingine za magari "pasua kichwa" kwa Tanzania. Ukiwa Japan, na nchi nyinginezo hamna tabu gari lolote ni sawa tu.

  11. Anonymous Anasema:

    Umasikini wa akili ni kitu kibaya sana.
    mtu maeuliza upatikanaji wa spea , wewe unajibu honda bongo zipo nyingi sana.
    nijibu swali, spea za honda bongo si nyingi kama toyota .

  12. Anonymous Anasema:

    HAO WOTE WALIOANDIKA KWAMBA SPARE ZA CRV HAZIPATIKANI AU SIO GARI LA UHAKIKA HAWA-OWN CRV...PROBABLY NI MANENO YA MTAANI TU. HUKU BONGO ZIMEJAA KIBAO UKITAKA MPYA NA USED. NA UZURI MPAKA SASA HIVI SPARE ZA CRV HAZIJAWA FAKE ZA KICHINANA KAMA ZILIVYO ZA TOYOTA. MIMI NINA RAV NA PIA CRV...I CAN TELL U RAV4 INAHITAJI MAINTANCE MARA KWA MARA KULIKO CRV...NA SPARE ZAKE FAKE NI NYINGI SANA MPAKA NIMEAMUA NIWE NANUNUA USED TU...

  13. Anonymous Anasema:

    crv siku hizi zinanunuliwa na baadhi ya wizara. hiyo ni indication kwamba ni ya uhakika. Spare zake zipo nyingi tu na kama kuna mtu amekosa spare ya crv aseme ni spare ya chombo gani. Ila ukweli spare zake ni ghari na hasa kwa sababu sio fake kama za magari mengine. Pls bring ur crv we will soon start crv owners club...

  14. Anonymous Anasema:

    Nimekuwa natumia honda miaka minne sasa, Kwa ujumla gari hizi ni nzuri sana hazina matengezo ya mara kwa mara na kama ukitengeneza ni stabilizer tu kwa ajili ya barabara zetu na zenyewe itakuchukua mda kubadilisha tena, Zinakimbia sana na ni stable barabarani nikilinganisha na Toyota rav 4 ambayo pia rafiki yangu anayo. Utumikaji wa mafuta ni wa kawada kwa wastani ni lita 1 kwa km 13. Zina space ya kutosha. Spare parts zipo maeneo ya Kitumbini kuna wataalam kule hawakosi kitu. Na ata hivyo kuagiza Japan kama utalazimika katika nyakati hizi sio jambo gumu kuna wadau wanafanya kazi iyo.

  15. Anonymous Anasema:

    Mimi ninakushauri kama mtumiaji wa Honda. Nimekuwa ninatumia gari za aina ya Honda kwa zaidi ya miaka 18 sasa na ninakuhakikishia kuwa ni gari nzuri yenye low maintenance cost ukilinganisha na ubora wa gari. Nimekuwa na aina tofauti za Honda form Civi to Accord na sasa hivi nina tumia CRV na Odyssey.
    Manunuzi yangu ya spare parts za honda si ya mara kwa mara kwani sifa kubwa ya watengenezaji wa Honda ipo kwenye engine na wanajivunia hilo ingia hapa www.honda.com or www.honda.jp
    Huwa ni rahisi kwangu kununua spare parts online rather than kwenda kununua kariakoo kwani parts za honda zipo Kariakoo mtaa wa Msimbazi na duka lingine lipo mtaa wa Swahili. Lakini kwangu mimi ni convenient kununua online kwani sihitaji kuhangaika na ninapata kile hasa ninachokihitaji na ni Genuine Part.
    Vinginevyo njia nyingiine ya kununua parts unaweza kununua kutoka Nairobi kwa kutuma message kupitia simu yako ya mkononi kwa kuwasiliana na Accord Ltd wa mtaa wa Kirinyaga. Kwa update ya namba zao angalia kwenye Yellow Pages ya Kenya.
    Spare parts nyingi za magari hasa Toyota si genuine parts as a result ukifunga kwenye gari performance inapotea na hazi chukui muda matatizo yanajirudia.

  16. Anonymous Anasema:

    Nunua mawili kabisa, ili moja uwe unachomoa spea! Halafu hizo CRV ni update tu ya 'Kitchen Party', Unazikumbuka? Zilikuwa Bwerere juzi tu, sasa zimekwenda wapi? Nakushauri ununue Toyota.

  17. Anonymous Anasema:

    Honda CRV ni 4WD gari nzuri ambayo hata mimi naitamani, lakini katika kusoma maoni ya watu nimegundua kitu kimoja! Watu ambao wanamiliki CRV maoni yao wote wanaipa credit gari hili! Pengine kutokana na uzoefu halisi wanaoupata, Maoni mengi hasi ni ya watu wasiomiliki CRV. Fuata ushauri wa mtu anayeimiliki gari kuliko ule wa mtu aliyesikia tu. Jamaa yangu aliwahi kuniambia huwezi kusifia iphone wakati wewe unatumia Blackberry! Labda ajitokeze mtu ambaye imewahi kumsumbua gari hii atuambie!

  18. Anonymous Anasema:

    MLETA MADA,NAOMBA UJUE HAKUNA KNACHOKOSEKANA TANZANIA SOEAR PARTS ZIPO,NA HIZO HONDA ZIMEJAA KIBAO KILA AINA YA HONDA,WASIKUTISHE WEWE HATA HAMMER LETE ZIPO TU,

  19. mdau ughaibuni. Anasema:

    JAMANI,na mimi nina swali langu kama la mdau naomba msaada,mimi nipo ughaibuni nataka na mimi nianguke bongo na mchuma na mchuma ninaofikiria ni grand vitara new model 2.0 engine,sasa nayo vipi hapo kuhusu vipuri?

  20. Anonymous Anasema:

    Grand Vitara za kumwaga, gari iko reliable, inadumu, iko economical ila ni target No 1 ya wachomoa spear. As for Honda CRV ni 4X4 nzuri tafuta msaada zaidi kwa watalaamu kama yule jamaa wa top gear BBC, Uki google Honda CRV review BBC top gear jamaa atakupa pro and cons that hiyo gari!

  21. Anonymous Anasema:

    Ulieomba ushauri jaribu kuwasiliana hii blog watakushauri vizuri mimi nilikuwa na tatizo linalofanana na hilo,na walinisaidia

    magaribeipoa.blogspot.com

  22. Anonymous Anasema:

    HAKUNA CHA KUULIZA SPEA PARTS TZ ZIPO ZA KILA AINA NASHANGAA MTU ANAULIZA HATA YA SUZUKI WAKATI KUNA MAGARI YA BEI MBAYA LAKINI SPEA ZIPO,HUKOSI KITU TZ SASA DEALERS WAPO WANAOWAKILISHA MAKAMPUNI MAKUBWA KAMA NISSAN NA SUZUKI AGENT DT DOPBIE,TOYOTA KILA MAHALI ZIPO HIVYO WATANZANIA WALIOUGHAIBUNI TAMBUENI HAPA KUNA KILA KITU SASA TANGU FAKE PARTS UP TO GENUENE,NYINYI LETENI TU MIKOKORO IMEJAA HAPA ILA MAFOLENI TU YANATIHSA

  23. Anonymous Anasema:

    Tabu ya wabongo mnaokwenda nje ya nchi mnaondokaga washamba sana na sijui ni kwanini hamuamini kama Bongo siku hizi kuna changes. Dunia ya huku pia iko kwenye kiganja ni wewe na vijisenti vyako tu. Njoo hata na Hammer Petrol/Diesel mpaka Gas za kumwaga.

    Mtakuwa washamba hata HOME!

    GJK

  24. Anonymous Anasema:

    Mimi ni mtumiaji wa Honda toka 2002 na nina kuhakikishia katika gari ambazo zina space kubwa ndani na unakaa bila shaka ni honda huwezi kulinganisha na ufinyu wa RV4. Kuhusu suala la msingi juu ya spare, Dar spare za kumwaga sio kama zamani tulikuwa tunanunua toka Nairobi "Accord Spare" Nenda Ilala mtaa wa Uhuru kuna duka la wapemba bei yao ni nzuri sana nasikitika jina nimelisahau. Tanzania sio ya Toyota peke yake na mara utakapogundua uzuri wa Honda utajuta kuchelewa kuifahamu.

  25. Anonymous Anasema:

    sorry wadau nami pia napenda kujua kuhusu nissan teana 230jk na series nyingine za teana.sijaziona tz au ni kwamba sijabahatika kuziona.vip kuhusu spare parts,uimara wake nk.
    mdau
    hongkong.

  26. Anonymous Anasema:

    Mie nakushauri achana na honda, ni juzi kati tu nilikuwa naongea na mafundi nikawauliza kuhusu spea zake wakasema zipo ila bei ni kubwa sana hata wao wanapendelea kwenda dukani na mwenye gari akasikilizie mwenyewe bei asije sema anaibiwa, kazi kwako kipato na uwezo wako unaujua mwenyewe.

  27. Anonymous Anasema:

    kwanza angalia unakaa wapi hapo dar....lakini all in all ebwana achana na honda na hata mitsubishi hawa walishashindwa kutengeneza 4WD za ukweli...labda ni Trucks na Meli ndiyo wazuri.....sana sana kama una kahela hiyo CRV mnunulie mkeo manake ni Ladyish car ..awe anaeneda nayo saluni na kwenye kichen parties ,basi.....otherwise utaumia

Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker