dogo mfaume akiibuka baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya msanii bora wa muziki wa asilia katika kili music awards 2009 katika ukumbi wa diamond jubilee hall jijini dar
dogo mfaume akijidai na tuzo yake ya msanii bora wa mwaka wa muziki wa asilia
dogo mfaume akitelemka jukwaani baada ya kupokea tuzo ya mwanamuziki bora wa muziki asilia
mwenyekiti wa yanga imani madega akimpa tuzo dogo mfaume ya muziki bora wa asilia kutokana na kibao chake cha 'kazi ya dukani' kilicho katika mtindo wa mchiriku
ukitaka kusikiliza umahiri wa dogo mfaume katika libeneke la mchiriku



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Woo nimeipenda kazi ya duka natafuta mtaji.

    ReplyDelete
  2. KAZI YA DUKANI,ONGELENI MLIOMCHAGUA KWANI MUZIKI WAKE UMETULIA NA HUYO DADA ANAVYOCHEZA UTASAHAU KAMA ANAMZIGO MKUBWA MGONGONI USHUNGU MTUPU WALLAH NDANI YA BONGO

    ReplyDelete
  3. mmmh yani hapo kama Teja, yani na hisihuyo Azan alikuwa anasikia hiyo fulana ina nuka bangi.

    Kijana hata kuonekana kwake mchafu sijui kwanini na vutiwa naye sana , sija wahi muona ndio nimemuona mara ya kwanz aila nyimbo yake inanisugua roho kw akucheka ilivyo na maneno ya ukweli, halfu hata sura yake inanivutia sana , hongera kijana, jaribu kuvaa vizuri ila hizo nywele ziache zinakupendeza .

    ReplyDelete
  4. Kudadadeki mshkaji anakula ganja hatari,anyway Hongera kaka bora kazi ya duka kuliko ukae maskani...Big Up

    ReplyDelete
  5. Yah ni leo tu nilikuwa nasoma article ya Mchiriku katika website ya Sauti ya Busara. Jinsi mwandishi alivyoelezea ilinivutia sana. Nikatafuta kopi mbili tatu za mchiriku nikaanza kusikiliza kwakweli ilichukua mbali sana yani enzi zile za Uswazi. Yani enzi zile kabla Wagoroko hawajaupiga marufuku Mchiriku. Ndio walidai una asili ya Uhuni uhuni lakini mbona leo tunasikiliza Bongo Flava ambayo kwakweli haina asili ya mwafrika. Minadhani kazi kama hizi za huyu Dogo Mfaume zikiendelezwa zitaleta impact kubwa sana katika muziki wa Kitanzania zaidi ya Bongo Flava. Kwani ikumbukwe Kwaito ya kule South Africa iliianzia kama mchiriku yani muziki wa watu wanyonge wenye mvuto zaidi kwa watoto wa mjini. Kama mchiriku au mnanda kama tuuuitavyo wenyewe watoto wa CDA yani Nyumbani ukiboreshwa na video zake zikiboreshwa basi watanzania tunaweza kutoka kimuziki. Pia mchiriku unajulikana sana katika nchi ya Kongo kwani bila mchiriku klab haichanganyi lakini habo Bongo hata usiku wa mwafrika mchiriku haupigwi. Kazi bora Dogo Mfaume, tunasubiri kazi nyingine za wakongwe kama Omary Omary, Kibaka mdudu, Mudy Kadogo yani wazee wa ATOMIC, 7 Survivals, HISANI. etc. Wazee wa Uswazi nimewakuna hapo au mnasemaje??

    ReplyDelete
  6. WEE 1:27AM 15 APRIL, HUYO DADA ANAYECHEZA YUKO WAPI KWENYE PICHA HIZI MBONA MIMI SIMUONI? AU KOMPYUTA YANGU INAMAKENGEZA? NINAUHAKIKA ULIFELI MTIHANI WA DARASA LA PILI.

    ReplyDelete
  7. wewe anonymous wa April 15 09 8:01 hapoa juu bonyeza pale palipo andikwa BOFYA HAPA alafu toa maelezo kweli vumbi limekulevya usikulupuke tuu na kutoa maelezo au umetoka kubonyezwa na ukasahau kunawa maana uko kama ..........,mdau hata wa 1.27 aplir 15 huo mzigo hata mimi mijicho ilinitoka

    ReplyDelete
  8. we mjomba michu ,nani kasema utumbo utupwe wakati sie twalia ndizi..kudadeki duuh umenikumbuza mabli sana,moody kadogo upo bwana.michuzi nakwambia uwezi kupinga asili ya mbantu,hata kidogo ,manake akuna twanga wala bongo flava mchiriku noma kivyake ,kazi well done bro.nakwambia msondo mchiriku ndo asili yetu sie wabantu.angalia mtoto anavyo kupa hali halisi.michuzi duuh imekolea kinoma yaaani.naudig sana mchiru yaaani.

    ReplyDelete
  9. Big up Dogo Mfaume,achana na wanaosema bangi-Ila umenifurahisha kwa kibwagizo cha Haruna Moshi -Boban - Proffessional prayel- Hakika ni kweli no one like Haruna Moshi kwa ss TZ.

    ReplyDelete
  10. Nakumbuka enzi hizo uswahilini harusi bila mchiriku nikama wali bila pilau.
    Nakumbuka Ilala jamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...