Katibu Mkuu wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini,TBF,Lawrence Cheyo (wa pili kushoto) baada ya Vodacom Tanzania kuikomboa kwa kulipia ushuru wa forodha Sh Milioni 1. Shoto ni Simon Msofe na wa pili kulia ni meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Nector Foya na kulia kabisa ni Mbaga Mwamboma.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imekipiga jeki Chama cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kwa kulipia gharama za Ushuru wa Forodha wa mipira 210 iliyoingizwa nchini kama msaada kutoka Shirikisho la Mchezo huo Afrika (FIBA AFRICA).

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mipira hiyo Jijini jana katika viwanja vya Gymkhana, Mkuu wa Kitengo cha Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza, alisema Vodacom imetoa ushirikiano huo ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuendeleza michezo hapa nchini.

“Hafla yetu ya leo ni uthibitisho tosha wa ushirikiano baina yetu na TBF na tunaamini kwamba mipira hii itasaidia kukuza kiwango cha mchezo huu hapa nchini na kulitangaza jina la nchi yetu kupitia mchezo huu,” alisema.

Alisema Vodacom Tanzania inatambua umuhimu wa michezo kwani mbali na kwamba michezo ni afya, pia inatoa ajira kwa vijana wengi hapa nchini.
Naye Katibu Mkuu wa TBF, Lawrence Cheyo aliishukuru Vodacom Tanzania kwa kutoa shilingi milioni moja kulipia ushuru wa mipira hiyo.

Alisema mipira hiyo imeletwa nchini ikiwa ni sehemu ya mpango wa TBF na FIBA AFRICA wa kukuza mchezo huo kwa vijana wa Shule za Msingi na Sekondari hapa nchini.

“Kwa niaba ya TBF ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Vodacom kwani mmeonyesha jitihada zenu za kukuza michezo hapa nchini,” alisema.
Alifafanua kwamba mipira hiyo imetolewa na FIBA AFRICA yenye makao makuu yake nchini Ivory Coast.

Vodacom Tanzania inadhamini michezo mbalimbali kama vile Mpira wa Miguu, Kuogelea, Riadha, mashindano ya Boti na mashindano ya baikeli.
Pia Vodacom inadhamini Ligi Kuu ya Soka ya Vodacom na Vodacom Miss Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. yaani kipindi chote hicho wizara ya michezo lishindwa kutoa hela ya kulipa?

    ReplyDelete
  2. Mipira 210 ni mingi sana, TRA wana haki ya kupiga kodi. Unajua bongo tumejiharibia wenyewe baada ya kuacha kuwa waaminifu kwenye hizi exempt supplies na watu kuchukulia advantage ya kuingiza vifaa wakidai misaada kesho unavikuta vimetundikwa dukani vinauzwa. Kudos TRA- Ila na ninyi muache rushwa mfanye kazi kwa sheria

    ReplyDelete
  3. ASANTENI VODACOM KWA KUWASAIDIA . MICHEZO NI AFYA. JE, MPIRA WA "BASKETBALL" BEI YA WASTANI HAPO DAR ES SALAAM KIASI GANI NA PIA MPIRA WA MIGUU. NAOMBA JIBU NDUGU ZANGU-
    ASANTENI MDAU WA NEW YORK CITY

    ReplyDelete
  4. Kumbe mojawapo ya sababu za michezo kudolola Bongo ni urasimmu kama huu , iweje msaada wa kimataifa kuendeleza michezo mashuleni na kwa vijana ulipiwe ushuru.

    Wakati ni huu vyama vya michezo kupanga mikakati na ku-lobby serikali, ili ushuru kwa vyama vya michezo visivyofanya biashara vipewe support kama kuondolewa ushuru kukuza michezo na afya za watanzania.

    Michezo ni afya njema na afya njema ni sehemu ya kuongeza kasi ya uchumi kupitia nguvu-kazi ya Watanzania wenye afya.

    Mdau
    Rocky.

    ReplyDelete
  5. Nimeshtushwa na gharama za ushuru wa mzigo kidogo kiasi hicho. Vitu vikubwa na vya thamani sana watu si wanakaribia kuvunjika mifupa kwa gharama kubwa? Labda ndoo sababu mizigo ikiletwa inakaa muda mrefu bandarini bila kukombolewa.

    ReplyDelete
  6. aah kudadadeki ifatilieni hiyo mipira kama mtaiona tena! watu watagawana sasa hivi hiyo utaikuta madukani kwa wahindi!! we ngoja tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...