dege la KLM likimwaga wese ili kupunguza uzito na kuiwezesha kurudi na kutua uwanja wa schiphol jijini amdsterdam mchana huu kufutia hitilafu za kiufundi mara tu ilipopaa kuelekea san francisco, marekani
dege likitua schiphol ambapo abiria walitelemka na kupewa ndege ingine iliyowafikisha mwisho wa safari yao salama salimini
dege la KLM likitua uwanja wa ndege wa san francisco, baada ya iliyoanza safari kurejeshwa amsterdam kwa ajili ya matengenezo
nanihii akikaribishwa na mdau alipowasili jioni hii hapa san francisco, california, kwa vekesheni fupi ambayo ilianza kwa kimbembe cha hewani ambao baada ya dege kupiga chafya ikabidi inadilishwe. nanihii anamshukuru Mungu kwa kuwafikisha salama salimini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 55 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2009

    du pole sana ukikutana na kimbembe cha angani kila unapoingia ndani ya pipa lazima uombe manake kuna ile moja Air chine inaonyeshwa ktk natgeoq tv ni noma tupu kosa dogo tu la pilot linge sababisha kifo cha watu kibao sababu ya fatiki likizo njema mkuu wa kijiji hiki

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2009

    DEAR MICHUZI AND COLLEAGUES,
    WELCOME TO THE STATES. I KNOW IT'S NOT EASY TO SEE YOU, BUT GLAD THAT YOU ARE WITH US IN OBAMA'S. GLAD YOU LANDED SAFELY. SOMETHING BAD WOULD HAPPEN, IF THE PLANE WAS NOT CHANGED. WHO KNOWS!

    MMEKUJA MSIMU MZURI, USA HAKUNA BARIDI SASA. NA MIEZI YA 6, 7, 8, 9 ITAKUWA NA JOTO ZAIDI.
    ASANTE SANA.

    Marko.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2009

    mkuu wa wilaya ya Tegeta huko San Francisco itabidi ununue ze fulans nyingine maana hiyo imekuwa kauka nikuvae wadau tumeichoka kuiona

    ReplyDelete
  4. Mdau, SoharMay 18, 2009

    Tatizo ni kuwa nanihii longi taimu hujaenda vekesheni, yaani hadi ndege ilipata mshituko kukuona umo pipani!
    enewei, vekesheni njema, ukiwa unarudi pitia basi na huku Omani ule tende yahe!

    ReplyDelete
  5. Mdau, SoharMay 18, 2009

    Halafu mkuu wa nanihii, pamoja na kuchapa koti, kwa ndani naiona ze fulanaaaaz ile ile!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 18, 2009

    mdau Marko siyo lazima kuandika kiingereza kibovu. kwani ukiandika kiswahili kitaharibika nini? eti'something bad would happen' jamani hicho kiingereza mie hoi.na hapo uko Marekani.kazi kweli kweli.Michuzi nakutakia mapumziko mema na UK unakaribishwa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 18, 2009

    duh pole sana,walitaka kukatisha koromeo lako kupokea mpunga na tamutamu za bongo?au uliwashtua km we mtu muhimu bongo wajitahidi kurekebisha ufike salama nini?anyway umepona kaka endeleza libeneke

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 18, 2009

    Michuzi I'm sure list ya mafisadi dagaa ikitoka na wewe utakuwemo tu bila shaka. Maana hizi si kodi kweli zinakupeleka huko vacation? Anyway hamna mbaya lakini kula maisha kufa kwaja.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 18, 2009

    We Michuzi mbona nimesikia uko kwenye delegation ya JK Marekani? Naona umeukata haya balozi au mkuu wa wilaya?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 18, 2009

    Ukirudi mjini mjomba utuletee zawadi...

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 18, 2009

    hahahaaa huhu huu
    yani naona picha #1 ulilenga kikweliii
    ayo mambo ya kawaida sana babu,midege km kawa tu.

    aya mkuu wetu kula raha kwa raha zako,ila mboni pekee ivo mamsapu wapiiiii???
    ze fulanazz km kawa!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 18, 2009

    ma-engineerz wenye akili zao na kujua kazi zao...dege likabadilishwa kuepusha kero kwa wasafiri waliojikunja vijisent vyao kwenda vekesheni km wewe misupu!!

    sio bongo adi mwa-wehuka ndani ya ndege na bado si pilot wala wahudumu ataetoa japo maelezo km sii kuwatia moyo nk nk...huduma F

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 18, 2009

    Nanihii nawewe kwa kujifagilia...mpaka tujue upo Marekani!! Haya ni Vekesheni kweli au umekuja kupiga box?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 18, 2009

    mkipita silicon valley waambieni hao magwiji wa teknohama tunawahitaji waje bongo kuwekeza na sio kutupiga mchanga wa macho na vimisaada vyao...

    siye sio akina matonya!!

    ReplyDelete
  15. TVZ KicartoonMay 18, 2009

    Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyeezi Mungu kwa kuwajaalieni wewe na abiria wenzio kufika salama salimini safari yenu.

    Pili namshukuru tena Mwenyeezi Mungu kwa kurenew visa yako ya kuishi hapa duniani maana hapo ilikuwa almanusra globu ya jamii kwishney!

    Tatu, sku ingine uagage! siku zote si unaagaga oh, naenda vekesheni! vipi leo? au wewe siku hizi unaamini juju uliogopa ukiaga, safari haita onja mwanga wa jua?!

    Nne, au wewe umekimbia simba jimboni kwako twambie kweli bwana!

    Enewey mwisho pole sana Bwana Michuzi kwa mtikisiko ulioupata maana kama nakuona vile ulivyokuwa juu ya kiti unasali rakaa mia bila udhu wala nia!
    Hiyo yote ni mitihani ya Mwenyeezi Mungu ya kukukumbusha kumcha siku zote siyo unapopata matatizo tu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 18, 2009

    I hope kuna tamaduni mtakazo geza na kuwapelekea ndugu zetu Tanzania. Karibuni Texas, nilisikia mnatapita Texas mara mkabadilisha.... sisi tupo

    Mchumi wa Texas

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 18, 2009

    Huyu mkuu wa nani hii muacheni tuu na kazi zake za nani hii!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 18, 2009

    Hello mkuu wa wilaya ya nanihii, karibu sana huku kwa watu!- Kwa wenzetu. Natumai fulanazz umekuja nayo!! hahaha

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 18, 2009

    Michuzi umeenda na tubegi tuwili tudogo, ukirudi tutumie picha ukiwa unawasili pale Dar es Salaam airport, I am 100% sure utakuwa umerudi na masanduku 6 na carry on moja. Naomba usinikose ka-fulana walao ka Ross dress for less. Enjoy mtu wangu na umeenda wakati mzuri, sale za sping kwenda summer

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 18, 2009

    Ni kweli nanihii, mkuu wa wilaya ya nanihii amekuja na fulanazz yake, nilikuwa naangalia hiyo picha kwa makini ndani anayo ile fulanazzz, Maisha mema na BOX jema

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 18, 2009

    Mkuu wa Wilaya walikuweka third class kama kwenye gari moshi la kwenda Mpanda

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 18, 2009

    Ebwana hiyo t-shirt waipenda sana au ulinunua nyingi saaaanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa-mdau MBIJE,A-Kafanabo

    ReplyDelete
  23. Mr Ze Fulana cheats death! God is good.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 18, 2009

    michuzi, haya ndo matatizo ya tiketi za bure, utapandaje klm bwana?

    kadida

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 18, 2009

    MICHUZI TUACHE UTANI USIONDOKE BILA KUJA CAPITOL CITY MUHESHIMIWA.TAFADHALI SANA NINA JEZI YAKO YA LIVERPOOL NYUMA NIMEANDIKA MAN UNITED NA NAMBA 1 ,NAMBA YAKO UNAYOPENDA KWENYE JEZI ZAKO ZA LIVERPOOL.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 18, 2009

    Naona Fulana zzz....kama kawadia inawakalisha. Mpe hi Mr. President ukonana naye Ijumaa.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 18, 2009

    Tulikwambia upitie Bagamoyo ukakataa.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 18, 2009

    Kweli michuzi mungu ana mpango nawe maana angkupenda mkafa wote ingekuwa hadthi nyengine ntaniii wangu

    ReplyDelete
  29. Swine fluMay 18, 2009

    Mh michuzi karibu sana state but mind you that mikono huko San fransisco ni noma so no mikonozz please.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 18, 2009

    Why you like wearing that same T- shirt in many of the time i see you?????????

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 18, 2009

    Michuzi atakuwa mhaya. Mpaka dunia nzima ijue kuwa umeenda marekani.
    Mdau Ubena Zamosi.

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 18, 2009

    Nanihii fuatilia onyo la Swine Flu kwa karibu. San Francisco inafahamika kwa jinsia moja na kinyume na maumbile.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 18, 2009

    Ebanaaeee..mkuu wa nanihii ndani ya Frisco, si mchezo, karibu mkuu, naona mijihela ya chama wewe wajua kuitafuna..tehe

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 18, 2009

    Mh! Issa upaparazi mbaka angani!!! keli iko damuni

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 18, 2009

    michuziumekuja huku kuonana na john mashaka nini? i bet we will see a picture of and john mashaka together no no no its not good its smell fish!!ufisadi mtupu!!!!

    ReplyDelete
  36. DUH! Pole sana kaka Michuzi. I'm glad you arrived safely and WELCOME TO THE USA!

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 18, 2009

    Michuzi acha uchoyo hata kutuletea tuzawadi. Jamani tubegi huto tuu unakuja nacho USA? Jamani zile tumlenda kweli hukuuona mweee

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 18, 2009

    BRO KARIBU NAJUA UTATUPA STORY BWEE BWEE SASA HIVI USIJE UKASINGIZIA MTANDAO MANAKE MTANDAO HUKU NI CHAGUO LAKO TU WENYEWE UNAPOTAKA.

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 18, 2009

    Msije mlimpandisha raisi wetu KLM. Kwiii kwiii
    au ni kuwa mmekwenda wengi marekani na lindege letu la raisi halikutosha ikabidi wengine mbane kwenye klm?

    ReplyDelete
  40. Ni kweli ndg Balozi, SAN Fransisco ukiweka mikonoz kwa mwanaume mwenzio tayari unasikia vigeregere na wimbo wa iyena iyena au mwansomaso mwanangu msimuoneh...you know the rest !!
    Be careful

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 18, 2009

    Hicho kingekuwa kimbembe! Angani hakuna simile! Pole na mshituko!

    ReplyDelete
  42. PhatlorenzoMay 18, 2009

    Michuzi karibu sana U.S. na pia Minnesota ukipata muda. By the way nina ka fulana ka Minnesota Twins hapa kana rangi nzuri tu.

    Phatlorenzo-MN

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 18, 2009

    mkuu ni shujaa sana maana kama ingelikuwa mimi hata hiyo picha isingepigika kwa woga!

    ReplyDelete
  44. Kweli mkuu wewe mtu wa habari, ndege imepata msukosuko angani bado unapiga picha!!!!!!!!!!. Wewe ni noma. Siku simba wakivamia tuna uhakika tutapata ushahidi kwenye camera yako jinsi tukio lilivyokuwa.

    ReplyDelete
  45. SICENGA KOKUMay 19, 2009

    watu kwa kusema, wahaya wachaga wa nini na nini ni watu kama wewe, acheni hizo, Mungu alipomuumba adam hakumawmbia kuwa yeye ni Mhaya wala mjaruo, punguzeni hadithi zenu zinaboa mhaya mhaya mhaya.......... fungeni midogo mnaboa saaaaaaaaana.

    Michuzi anasafiri sana, kukushirikisheni ni kwasababu ndege yake ilipata matatizo, alipoenda uswede alikwambia? je alipokuwa ujerumani na nchi nyingine mlijua?? acheni hizi, unganeni naye KUMSHUKURU MUNGU KWA KUMFIKISHA SALAMA SIYO KULETA WAHAYA WAHAYA MNACHOSHA NA MIMANENO YENU KAMA HAMNA YAKUONGEA KAENI KIMYA KHA!

    MICHUZI MUNGU YUKO NAWE, KWA JINSI ULIVYOSAIDIA WATOTO KIBAO NA WATU KUPONA KUPITIA JITIHADA ZAKO MUNGU HAWEZI KUKUACHA, TUTAZIDI KUKUOMBEA TULIO NA MOYO WA UPENDO KWAKO. MUNGU AKUBARIKI

    ReplyDelete
  46. Michu' welcome to Los Angeles as well... upate your Oscar!

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 19, 2009

    HONGERA KWA WALIOSAFIRI NA NDEGE WANAJU KASHESHE KIDOGO TU UNAANZA KUSALI, ILA KWELI MICHUZI NAKUAMINIA, HUKU UNATAKA KUDEDI HUKU UNATAKE PICHA--HONGERA SANA NIMKUBALI, WE MDUME.THANKS GOD U R SAFE AND SOUND.

    ReplyDelete
  48. Karibu the US mkuu wa nanii, jihisi uko nyumbani, we appreciate the work you do michu.

    Lini mtakujua, Atlanta... black americans mecca.karibu sana. Home of Dr. Martin Luther King.

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 19, 2009

    Mkuu karibu sana Texas, will be happy to have u. Fulanas ziko nyingi

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 19, 2009

    kama huku chukua namba ya simu utakua umechemsha LONNY anataka kurudisha fadhila
    ulizo muenzi ndani ya Njenje kaka yako hapa

    ReplyDelete
  51. Hii kaka inatisha, pole sana, safari njema na urudi salama.
    /Maggid
    Iringa.

    ReplyDelete
  52. We Michuzi we.

    Hiyo picha ya tatu kutoka juu mbona kama hilo bawa la ndege limetoboka hapo!?!

    Au ndo hicho kimbembe kimesababisha bawa la ndege kutoboka?

    Duh! Poleni sana.

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 19, 2009

    Hi! ZE FULANAZI !NAYO ON TOUR
    Kwikwik kwikw!!!!!!!!!!
    ZE FULANAZIII HOYE EEEEE!!!!!!

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 20, 2009

    tuambie huyo aliyekupokea anaitwa nani, nimemind

    Nay
    CA

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 20, 2009

    ebu nikuchunguza

    huna pete ya ndoa pia uku,why??

    ivi nyie wanaume mliooa kwanini hamvai pete zenu??

    au mko ktk imani zile??za akina kakobe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...