MKUU WA WILAYA YA TEGETA NA BALOZI WA NANIHII.
POLE NA KAZI YA KUTUHABARISHA.
NIMEPITIA MTANDAO WA JAMII FORUMS NA KUONA AMRI YA MASAA 72 ILIYOTOLEWA NA M.M MWANAKIJIJI AMBAYE NI MDAU MKUBWA WA MTANDAO WA JAMII FORUMS NA MITANDAO MINGINE.

AMRI HIYO INASEMA KUWA" TUKO KWENYE MAPAMBANO YA UFISADI HIVYO WATANZANIA WAZALENDO WAACHE KUTUMIA SIMU ZA VODACOM NA KILA MZALENDO MWENYE UCHUNGU NA NCHI YAKE AHAMIE MTANDAO MWINGINE NDANI YA MASAA 72"

MASWALI AMBAYO MWANAKIJIJI AMESHINDWA KUNIPA MAJIBU NI MENGI LAKINI AMESHINDWA KUTIZAMA ATHARI ZITAKAZOWAPATA WATANZANIA, SIJUI KWA VILE YEYE HAISHI TANZANIA HIVYO HAWEZI KUATHIRIKA NA AMRI HII ALIYOITOA KWANI KUTOKUWEPO KWA VODACOM HAKUTAMUATHIRI KITU.

KWANZA NADHANI VODACOM IMESAJILIWA KISHERIA KAMA KAMPUNI HALALI NA VYOMBO HUSIKA TANZANIA, KAMA KUNA MATATIZO YEYOTE KWENYE KAMPUNI HII YA VODACOM, VYOMBO HIVYO VYENYE DHAMANA HIYO VINGETUPA TAARIFA WATANZANIA KAMA ILIVYOTOKEA KWA KAMPUNI YA DECI SERIKALI ILITUAMBIA ATHARI ZA KUWEPO KWA DECI.
KWA MTAZAMO WANGU WATANZANIA WENGI TUTA ATHIRIKA SANA KWA KUTOKUWEPO KWA VODACOM TANZANIA.MOJA- KUNA WATANZANIA WAZALENDO WENGI WAMEPATA AJIRA NA WANAPATA MISHAHARA MIZURI HAPO VODACOM TANZANIA.

PILI-KUNA WATANZANIA WENGI KILA KONA YA NCHI WANAUZA VOCHA AU BIDHAA MBALI MBALI ZA VODACOM WATU KAMA HAWA KUONDOKA KWA VODACOM KWAO NI VILIO NA KUPELEKA NJAA KWENYE FAMILIA ZAO.
TATU-VODACOM INASAIDIA MAMBO YA ELIMU KUPITIA VODACOM FOUNDATION AMBAPO MASHULE YANAPATA COMPUTER NA VITU MBALIMBALI CHINI YA UDHAMINI WA VODACOM.

NNE-HIVI KARIBUNI VODACOM ILIANZISHA TIMU YA WATOTO YA MPIRA NA NILISIKIA VIJANA WATATU WAMEPELKWA UBELGIJI KUPITIA VODACOM ILI WAKACHEZE MPIRA WA KULIPWA MTANIKOSOA KAMA NIMEKOSEA.
TANO-LIGI KUU YA TANZANIA INADHAMINIWA NA VODACOM AMBAPO WATANZANIA TUNAPATA BURUDANI NA TIMU NA WACHEZAJI WANAPATA PESA KUPITIA VODACOM.

SITA-VITU VYA KIJAMII KAMA KUGAWA VYAKULA KWA WATOTO YATIMA,AU SIKUKUU YA IDDI NA KRISMAS, MISS TANZANIA N.K ZIMEKUWA VIKIDHAMINIWA NA VODACOM.

LAKINI MWANAKIJIJI ANGETIZAMA NA UBORA WA HUDUMA YENYEWE MFANO HUDUMA YA INTERNET KWENYE SIMU, MITANDAO MINGINE NADHANI HAINA ILA ZAIN WANAYO, AU UKIWA UGANDA UNAPATA VODACOM KWA GHARAMA ILE ILE KAMA YA TANZANIA, ROAMING UKISAFIRI DUNIANI BADO UNATUMIA NAMBA YAKO YA VODACOM HATA ZAIN INAHUDUMA HIYO PIA KUNA MITANDAO HUWA HAIKO HEWANI KWA MASAA AU MUDA FULANI LAKINI VODA WAKO SAFI KWENYE SMS HASA ZA NJE ZINAFIKA BILA MATATIZO.
YAKO MAMBO MENGI HATA BLOG HII IMEPEWA FURSA YA MTU WA MILIONI SITA KUPATA DOLA ELFU TOKA VODACOM SASA SIJUI ATAKAYEBAHATIKA ASUSE ILI KUONESHA UZALENDO NA KUFUATA AMRI YA MWANAKIJIJI? PIA BLOG HII YA MICHUZI ILIPEWA BLACKBERRY HIVI KARIBUNI ILI KUTURAHISISHIA HABARI ZETU JEE MICHUZI ARUDISHE HIYO SIMU YA KISASA?

LAKINI KUBWA KWANGU NI WATANZANIA WANGAPI WANAFANYA KAZI HUKO KIBAO NA TUKIFUATA AMRI YA MWANAKIJIJI TUTAIUMIZA JAMII YETU.JEE WATANZANIA WAZALENDO WANAVYOJIITA WATAACHA KUTIZAMA MICHUZI BLOG KWA VILE INA NEMBO YA VODACOM HUKO JUU?
LAKINI MWANAKIJIJI HAJATUPA ALTERNATIVE KUWA TUKIONDOKA VODA TUNAENDA ZAIN KWA BALOZI MICHUZI AU ZANTEL,TIGO NA TTCL LABDA ANANUSA KWANZA KUTIZAMA KUWA HAKUNA UFISADI.

MIMI SIDHANI NI BUSARA KUWAAMRISHA WATANZANIA WAACHE KUTUMIA VODACOM HATA KAMA ANA MATATIZO NA WAMILIKI LAKINI SIO BIDHAA AU HUDUMA AMBAYO INA FAIDA KUBWA KWETU KULIKO HASARA.SOMENI WENYEWE LINK YA MADA YA MWANAKIJIJI JAMII
FORUMS.
la-siasa/30198-wanaharakati-
ziachieni-simu-za-vodacom.html
WENU DADA LATIFAH

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2009

    konde "dada akiachwa na wewe kaka ondoka-ushemeji umeisha" naomba wafafanue yaliyowasibu au voda nayo kama mbagala tujihadhali??

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2009

    dada latifah huyo mwanakijiji katoa "amri" yeye ni rais au mtume kuwa huwezi kumpinga?
    mwanakijiji hawezi kukulazimisha wewe wala hata hao wanaotembelea jamboforums.....
    at the end of the day ....mwanakijiji ni nani kwako na kwa watanzania wengine?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2009

    Ni ombi tu na kuwafahamisha ndugu zangu utumiaji wa herufi kubwa katika ulimwengu huu wa internet. utumiaji wa herufi kubwa huwa unaashiria kupiga makele na kwa sababu hiyo ningelipenda kuwashauri ndugu zangu kutoandika ujumbe wote kwa kutumia herufi kubwa. brother michuzi wajibika.

    brother T

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2009

    kwani wewe ratifah tatizo lako nini?? kwani kakulazimisha uache?? wewe ni mtu mzima ukiona inafaa utaacha ukiona haifai haya!!!
    michuzi mwenyewe anafadhiliwa na voda lakini line yake zain!!!
    halafu hao voda unasema wanaleta faida nyingi lakini umesahau kuangalia upande wa pili wa shilingi!! angalia na hasara wanayoiletea nchi. ovyoo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2009

    bado tuna wapumbavu wengi sana wanaodanganywa na peremende, mpira na vi-anasa vidogoooo! wanasahau UZALENDO... wanauza nchi... Mwanakijiji usife moyo... wengine tulisha acha kabisa hiyo mitandao. TUWATOSE MAFISADIIIII, TUACHANE NA BIDHAA ZAO! WAKAWAUZIE MAFISADI WENZAO...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2009

    Mwanakijiji wa JF ameshapoteza uelekeo, hajui asemalo, ametawaliwa na wanaomuongoza, wanamtwist kama kibendera! Hadi anatia huruma, he was so good, lakini sasa hatred ya watu binafsi, imemmaliza, mtazamo wangu ni kuwa amewekwa kibindoni na baadhi ya watu, ndio sababu inabidi ajishaue

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2009

    MHHHHH NDIO MAANA WAKINA DADA TUNAITWA "WAMBEA" KWA KUPINDISHA MANENO
    KU QOUTE ULICHOANDIKA
    ("AMRI HIYO INASEMA KUWA" TUKO KWENYE MAPAMBANO YA UFISADI HIVYO WATANZANIA WAZALENDO WAACHE KUTUMIA SIMU ZA VODACOM NA KILA MZALENDO MWENYE UCHUNGU NA NCHI YAKE AHAMIE MTANDAO MWINGINE NDANI YA MASAA 72")
    YAANI DADA LATIFA HUU NI UONGO..HIVI SIVYO ALIVYOANDIKA MWANAKIJIJI..ULICHOPATIA HAPO NI NENO VODACOM NA 72...KWA NINI LAKINI?????
    MESSAGE YAKE AMELENGA KIKUNDI CHA WATU AMBACHO AMEWAITA WANAHARATI...WALA HAJATUMIA NENO WATANZANIA WAZALENDO.....NA AMESISITIZA KAMA WEWE SI MWANAHARAKATI THEN UJUMBE SIO WAKO NA ENDELEA NA MAISHA KAMA KAWA...
    JAMANI NDO MAANA WANAWAKE HUSUTWA...
    MHHHHHHHHHHHHHH.....NIMENYOSHA MIKONO KWA HILI..

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2009

    Ukusikia mtu kafilisika kiakili ndio huku sasa.
    Sasa hataki watu watumie na kujumuika na vodacom,watakaokosa ajira kule atawalisha yeye?
    mbona hata siku moja hatuja muona akipeleka japo karatasi katika shule zetu za mchangani(primary)huko kijijini anakojidai anatoka?

    Mdau

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2009

    Kwanza wewe dada Latifa ni mnafiki, kwa nini usingejibu hoja huko huko Jamii forums ukaileta huku kama sio umbea??????

    Pili hujasoma hoja ya mwanakijiji vizuri hajasema watanzania wote bali WANAHARAKATI na sababu iko wazi(HAKUNA SIRI YA MAWASILIANO) ingawa kuna sheria imeoanishwa kwenye katiba.

    Mwanakijiji hajasema Vodacom ifungwe bali ametoa pendekezo.

    Kumbuka suala la DECI lilianza kupigiwa kelele mwakajana mwanzoni serikali ilikaa kimya hadi mwezi mmoja uliopita ndio imechukua hatua.

    wakati mwingine tuchukue tahadhari mapema kabla ya kuangukia pua.

    Hoja hujibiwa kwa hoja na sio majungu

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2009

    mimi nadhani mwana kijiji na latifah wote ni wa moja. maoni ya mwanakijiji hayawezilutikisa vodacom. wewe latifah nani alikwambia amrizinatolewa kwenye kurasa za maoni kwenye blog????. siyo mbaya latifah umetoa maoni yako. lakini usiumize kichwa ,amri ya mwanakijiji ni kelele za chura, tembo ataendelea kumywa maji mpaka akate kiu

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2009

    Maskini mwanakijiji box limemuathiri ki - saikolojia tumuombee kwa mungu atapona, tuache mtandao wetu na biashara tutafanyaje wakati ndio contact zinazojulikana, halafu wewe huji ubora wa vodacom ndio maana unasema sema hivyo hawa jamaa wako seroius kwenye mawasiliano

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2009

    We Latifa, achana na Jamii forums, huku kwa Mithupu kwa mambo yetu tu.Ukitaka kujadili ya JamiiF nenda hukohuko.
    Usuruke huku na huko tulia kwenye blogu yetu

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2009

    WEWE DADA UNAMAJUNGU NA MWANA KIJIJI,KAMA KISHAWISHI CHAKE KINAUKWELI TUKUBALI.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2009

    Kwa nini usingemjibia huko huko alikoanzisha agenda? Hapa unasumbua tu..

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 04, 2009

    nataka kufahamu kuhusu mwanakijiji

    1.yeye ni nani?
    2.ana mamlaka gani kwa wananchi ambao wanamiliki simu za mkononi?
    3.anafahamu anachokisema?
    4.anajua mchango wa vodacom katika tanzania?
    5.ana mamlaka gani na jamii forum?

    lakini kila mtu ana mawazo yake, HATA CHIZI NAE ANA MAWAZO japokuwa mie ni mfuasi mkubwa wa kiswahili na huwa sipendi kuchanganya lugha, nitamwambia kifuatacho huyu mwanakijiji kwa lugha tofauti

    "IDEAS ARE LIKE ASSES,EVERYONE HAS GOT ONE"

    Naitwa Swala.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2009

    LATIFAHHHH NA WEWE TUTAKUPA BLUBERRY NINI BACKBERY RIM YA MITHUPU. TUTKUPA BLUEBERRY DADA...TOUCH SCREEN.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2009

    Mwanakijiji anachanganyikiwa sasa.
    Safi latifah kuona ujinga wa jamii Forum.Mwanakijiji maisha kama yamekushinda rudi Bongo.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 05, 2009

    Mada hii angeipeleka Jamii Forum isingekaa ingezuiliwa.pia huwezi kumlazimisha mtu kuweka asikotaka-jamii forums. yeye kapenda kwa balozi michuzi.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 05, 2009

    lakini wewe Dada Latifa uwe mkweli..sio vizuri kupindisha habari wakati umeisoma mwenyewe.
    Nukuu alichoandika Mwanakijiji badala ya kuweka maneno yako unapotosha watu.
    Ulivyonukuu...maneno haya hayajatumika katika maandiko ya mwanakijiji
    - Neno "AMRI" , hajaandika anaamrisha mtu yeyote
    - Neno Watanzania Wazalendo..hajatumia hili neno.
    Naomba tuambie sababu za wewe kupindisha maneno???????

    Yaani wewe ukiwa shahid upande wa utetezi mahakamani..utasababisha unayemtetea afungwe hivi anajiona.
    katika sheria unatakiwa uwe mwangalifu sana na maneno unayotumia..au sivyo yatakuja kukusuta mzima mzima,,,

    please be careful and what you quote kama nia yako ni kufikisha ujumbe

    ReplyDelete
  20. jamani ni kweli tatizo la ufisadi limekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi hii except kwa mafisadi wenyewe. Na kuna kila dalili kwamba serikali imeshindwa kushughulikia suala hili, ama kwa vile inaogopa, au ni sehemu ya maovu hayo

    Alichoshauri mwanakijiji(kama kweli) ni sawa kabisa, silaha pekee ya sisi wanyonge iliyobakia ni kususia Vodacom na bidhaa na huduma zote zinazozalishwa/tolewa na makampuni yenye uhusiano na mafisadi.

    Natoa changamoto kwa wadau kutoa orodha ya makampuni kama hayo na si vodacom peke yake, najua yako mengi sana. KUMBUKA HII NI SILAHA PEKEE. SUSIA BIDHAA HIZO!!!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 05, 2009

    Huyu dada atakuwa ni member huko jamii forums na ana pen name nyingine. Kakutana na vigongo huko kaamua kuleta umbeya huku. Kama walivyoshauri wadau wengine hapo juu haya malizieni huko huko. Siyo kweli kwamba huko jamii forums wote wanakubaliana na mwanakijiji. Nia yako ni ovu na imeonyeshwa na ulivyoweka maneno yako mwenyewe. Halafu mdau aliyesema kuhusu matumizi ya herufi kubwa big up kwa sana. Hiyo ni kupiga makelele ni dhahiri shahiri huyu Latifah anatoka Migomigo hata kwenye maongezi ni mtu wa kupaza sauti hadi anatokwa povu mdomoni.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 05, 2009

    Jee na yule aliyechukua pesa NBC hadi ikafa huduma zake na bidhaa zake anasemaje Mwanakijiji? tususie? mbona anapendelea upande mmoja?

    BRAVO DADA TIFAH.sote tumeona maneno ya kinafiki ya mwanakijiji.

    umemshika pabaya ndio anakuja kujijibia hapa.watanzania wote ni wanaharakati asijefanye kutuzuga.kwanini Vodacom hamchukulii hatua za kisheria?

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 06, 2009

    Mwanakijiji njaa inamsumbua.ameamua kuwa mtumwa wa wachagga ili mkono uende kinywani.njaa mbaya wandugu.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 06, 2009

    Mwanakijiji anaamini kuwa vodacom mmoja wa mashareholders wake ni wale waliomo kwenye list of shame ya akina Slaa. Kwa hiyo vodacom ikinyimwa biashara kwa njia ya sisi kucha kutumia simcard zake basi tutakuwa tumemshikisha adabu huyo shareholder. Lakini anasahau vodacom imetandaa TZ nzima na watz wengi wamepata ajira kutokana na kuweko kwa vodacom.

    Kwa hiyo amri yake Mwanakijiji ni pumba tupu.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 06, 2009

    NYINYI MNAOSOMA HABARI ANAZOANDIKA MWANAKIJIJI WOTE WEHU MAANA SIKU NYINGI WATU NA AKILI ZAO WALISHAONA UTOTO NA UPPUZI ANAOANDIKA MWANAKIJIJI

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 06, 2009

    mwanakijiji ni bingwa wa ukabila?udini?fitna tuwe nae makini jamani hawa ndio watakao ifikisha pabaya nchi yetu,wanajifanya wanapigania maslahi ya TZ;kumbe unafki mtu.
    yani hana tofauti na hao waliomtuma kila siku wanatumia mwamvuli wa uzalendo kujinufaisha binafsi wkt sisi watanzania walendo wa kweli tunaumia.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 06, 2009

    HEE!!HAMJAACHA TU KUSOMA HABARI ZA HUYO MWEHU?ANAEJIITA MWANAKIJIJI?NI MNAFIKI MWENYE NJAA!!UDINI NA UKABILA,MICHUZI UKIBINYA NA WEWE MNAFIKI NA FISADI WA WINO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...