Jambo Kaka michuzi,
Mimi naitwa mama Mekere. Ninaomba unitangazie tangazo langu. Ninauza nyumba au ninapangisha. Nyumba iko Tegeta Block G. Ina vyumba vitatu vya kulala,master bedroom 1,sitting room, choo/ bafu na jiko. Imezungushiwa ukuta wa tofali, bati la kisasa na vioo vya aluminium, tiles kila mahali toka sitting, dinning, jikoni, koridoni, vyooni na bafuni. maji, umeme na tenki la maji la akiba.
Ninapangisha laki 3 kwa mwezi malipo kwa mwaka. Na kama kuiuza naiuza kwa bei poa ya mil 100 tu.

Tafadhali naomba msaada kwenye tuta. ninaambatanisha baadhi ya picha ukiweza unitolee kwenye blog yetu ya jamii.
Kwa mawasiliani namba za simu ni
0745088610,
0715088610,
07873030997,
0754303997

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 55 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2009

    Kaka Michuzi, mbona hukuniambia kua bongo siku hizi kila mtu ni fisadi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2009

    Tangazo limekaa vizuri lazima tukusifie siyo watu wanaotoa matangazo yao yasiyo na kichwa na mguu. Na wewe mdau wa kwanza ufidani wewe unauelewaje?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2009

    TAFADHALI HII NYUMBA HAIJAISHA HAPO NJE INAHITAJI SI CHINI YA MILIONI 4 KUTENGEZA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2009

    Mbona tunaonyeshwa nyumba kuibapa ubapa? Toa picha kamili na tuonyeshe ndani kila siku.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2009

    Maza acha tambaa! Niandikie email mkunjob@hotmail.com na nitakusikisha $ 35000. Sitaki ku negoshieti.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2009

    Landscaping haijatulia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2009

    Mtoa mada hapo juu 2.15am huna akili. Ina maana kila nyumba iliyojengwa bongo ni ya kifisadi? Au hujaona mahekalu ya kifisadi -- kashangae feri mshamba wee

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2009

    Millioni mia moja! Kweli bongo tambarare!!!!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2009

    Yaani nilikuwa nimenuna sijacheka siku nzima nilipo fungua blog ya jamii nikakutana na nyumba kilichonifanya nicheke ni bei inayouzwa nyumba sasa nilipotaka nitoe comment zangu nikajikuta sina mbavu kwa comment ya mdau wa kwanza, naona huyo ni mmoja wao

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2009

    kwa nini anaiuza hiyo nyumba?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2009

    pole yako anonymous 2.15am june 9 nataka nikuulize kaka michuzi kwani kazi yake ni kupasha watu kama bongo kuna mafisadi.naona fisadi wa kwanza uliye letwa duniani ni wewe uliye kosewa njia ukaletwa aridhini ulitakiwa uingie shimoni siku ulipo umbwa.michuzi kazi yake kutuletea habari za nchini na dunia mambo yenye busara na kimaisha siyo kutuletea ufisadi tafuta jengine ujibiwe.mdau toronto.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 09, 2009

    haki ya mama

    shilling ngapi??toa basi view zima mayb house ni kubwa saaana,na finishingi umo ndani nk nk

    hahahahaaaaa

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 09, 2009

    milioni mia moja????

    ndo nini

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 09, 2009

    annon #1
    tutake radhi kabisa,usifikiri kujilipua uko ndo dili
    mkimbizi-misarable wa nchi za watu

    an alien mkubwa wee

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 09, 2009

    Wabeba BOX tunajisahau sana , Bongo kuna ufisadi bwana,Sisi tukichanga viDollas 7,000 tunafikili tumemaliza,Bongo watu mafisadi bwana.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 09, 2009

    Kweli watu hamjui gharama za ujenzi kabisa. Milioni 100 mnashangaa? Kiwanja tu eneo hilo kwa sasa ni mpaka milioni 30 bado gharama za ujenzi, kuweka umeme, maji nk. Hii wala haichelewi nyie bakieni na mawazo yenu ya pesa za zamani. TZ is a changed place now!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 09, 2009

    Pole sana mama maana kuna comments za ajabu ajabu huko juu. Please tuambie ukubwa wa kiwanja kilichotumika na kilichobaki. Na kama nyumba imejengwa katikati au pembeni, maybe picha kutoka juu itasaidia so utakaposema uwanja uliobaki ni kadhaa mtu ata-relate na picha.
    Ahsante

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 09, 2009

    kweli kuna watu mmeondoka dar es salaam zamani mbona viwanja siku hizi ni milioni 30 tegeta na mbezi beach milioni 80 sasaunashangaa nyumba milioni 100?mbona tunauza sana hizi nyumba na tunapata commission kama kawaida.kariakoo tunauza bilioni moja mpaka mbili au na hiyo manabisha.nyie bebeni box bwana haya

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 09, 2009

    waoshavinywa mnajua bei ya kiwanja dar? mfuko mmoja wa cement ni bei gani? lori moja la mchanga/mawe kiasi gani? kokoto dar debe kiasi gani? siomnakurupuka tu..

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 09, 2009

    wabeba mabox msijishau, kama mnafikiri mnaweza kumiliki nyumba kwa dola elfu ishirini basi mbadidimia
    mbatakiwa kujua dunia inavyo zunguka.nyumba ya mill 100. ni ya kawaida na ya kichovu, kama walivyosema wadau, kiwanja mil 30, kuingiza umeme application ni mil3.5, sasa jiulize mill 100 ni kitu gani???. mnashauriwa mrudi nyumbani mlijenge taifa. uchumi ukiwa imara mfumuko huu usingetoka. washurini na hawa madokta uchwara akina shayo na mashaka. wakati wasomi wenzao wanqtoa maoni ktk majukwaa ya kiutendaji wao kazi yao kuingilia blog yetu, watuachie wenyewe tunaongea lugha tunayoelewana ( kama wao ni njiwa kweli waache kujitapa mbele yetu sisi makinda wapambane na njiwa wendao)

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 09, 2009

    maskinii nyumba nzurii lakini hela sinaa!
    lakini milioni 100 si bora nikanunue kariakoo kisha niingie ubia na fisadi mmoja ashushe gorofa nipate flat moja na maduka chini 1 au mawili maelewano kisha nilale tu niwe nakula pensheni! huko tegeta itabidi niingie gharama nyingine ya kuweka ultimet security kulinda wezi na simba wanaozurura ovyo huko!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 09, 2009

    Mie nawashangaa wale wote wanaostaajabu na kuponda bei ya hiyo nyumba, kimsingi hiyo ni bei ya kawaida kabisa kwa nyumba za maeneo hayo iliyopo. Kiwanja tupu kupata mitaa hiyo ni fweza ndefu mno, ukichanganya na gharama za ujenzi siku hizi, pamoja na kwamba ameionyesha portion ndogo tu lakini hiyo aliyoonyesha inatosha kureflect aina ya nyumba kwamba ni ya kisasa kwelikweli. ukichanganya na faida kidogo aliyojiwekea lazima itafika 100M. cha msingi mtu aliyekuwa interested na mwenye nazo ajitose, wenzangu na mimi tubakie kupiga domo na kustaajabu.
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 09, 2009

    Nimefurahishwa sana na wale wanaonekna wana ina na kutoa ushauri.Mama wa watu ametoa tangazo la kuuza nyumba yake kw nia njema lakini watu sio na heshima wala adabu wanaanza kukebehi na kuonyesha kila mtu atakayetoa tangazo lake ni fisadi.Mi nafikiri watu hao wanahitaji kupewa ushauri nasaha.Ndio maana ametoa namba za simu namichuzi bila hiana ameziweka ili kama kweli unania basi umtafute muhusika uione na kununua au kupanga,sio kutoa lugha za ajabu ajabu.Tunaomba msituharibie blog yetu kwa lugha za ajabu ajabu.Blog hii inaheshimiwa sana duniani na inasomwa na watu wa rika zote.Kama unlugha za ajabu ajabu basi ningekushauri tafuta blog nyingine

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 09, 2009

    Nadhani kuna watu hobby zao ni kukosoa kosoa. Kama huna hela tulia. Kwa bei hiyo ni fair. Haijalishi kiwanja ni low density au high density. Nyumba ni nzuri na ina eneo la kutosha kabisa.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 09, 2009

    jamani embu tusaidieni tuemieni ni kiasi gani kwa pounds,?

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 09, 2009

    Hivi kutanganza kwenye hii blog ni bure,du,kumbe bongo bado kuna vitu vingi vya bure.
    bomba.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 09, 2009

    Nyie mnaoshangaa nyumba kuuzwa milioni 100 mmepitwasana na wakati,mjipange sawa sawa! mbona nyumba hiyo ni nzuri sana,kule maeneo ya Sinza ukitaka kupata banda bovu si chini ya milioni 200,mimi nakaa nyumba ya kupanga just chumba na sebule selfcontained iko fenced na ina tiles nalipa 250,00/= kwa mwezi na mwenye nyumba anataka utoe ya mwaka mzima na ninitoa bila shida na ndio kwanza nina 2yrs kazini,sasa nyie mnaoshangaa hiyo milioni 100 sijui tuwaelewe vipi? Amkeni sasaaaa!!!

    ReplyDelete
  28. Nakushauri weka Fanicha halafu kodisha.Hata mtu akitaka wiki moja kodisha.Ndio biashara nzuri kwa sasa.Kuuza ni hasara.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 09, 2009

    nyie mnaosema bongo kuna ufisadi kwa ajili ya nyumba ya milioni 100 mnachekesha saaana,tena msiseme tena mbele ya Mtanzania aliyetoka Bongo miezi 6 iliyopita atawashangaa sana!Hivyo vi dolla sijui vipound mnavyovipata mkirudi navyo bongo vyote vitaishia kwenye chips! Watu wana magari ya milioni 50 na wamemaliza chuo kikuu mwaka jana nao utaesema mafisadi,salary slip inasoma 2.5mil kwa mwezi,bongo maisha bomba sana nyie endeleeni kubenba mabox!!!!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 09, 2009

    HIVI HII IDEA YA WATU KUTAKA KODI YOTE YA MWAKA WAMEITOA WAPI? NA JE HAWAJUI KWAMBA MTEJA ANAPOLIPA KWA MWEZI NI NAFUU ZAIDI KWA MTEJA WAO ? AU KWNAINI WASIOMBE HELA MWEZI MMOJA KWANZA HIWEKWE CHINI ALAFU MTU ALIPE KWA MWEZI NA SIKU AKISHINDWA KULIPA NDIO MWISHO WA MWEZI UNAMFUKUZA NA HIO HELA ALIOWEKA CHINI MWANZO INAKUWA IMEKAVA RENT YA MWEZI HUO ALIOSHINDWA KULIPA.MAISHA MAGUMU TANZANIA WATU WABADIRISHE AKILI YA KUFANYA BIASHARA SIO MNAKAA NA MAWAZO YALE YALE.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 09, 2009

    Annon wa kwanza kabisa inaonyesha ana akili sana, maana wooote waliofuatia wamekua wakifafanua alichokisema kwa ufupi.

    Kwa hiyo nyie mnaona kwamba kulipa milioni 3 na nusu kufanya application ya kuweka umeme ni kitu cha sawa kabisa? Oh my god!!! Sasa hizo kodi zenu mnazozilipa kila siku zinakwenda wapi? Kuwekewa umeme kwenye nyumba kwani ni favour ama ni wajibu wa serikali kufanya hilo jambo kwa kua nyinyi mnalipa kodi? Hivi mmeshaangalia kwenye payslips zenu jinsi mnavyokatwa mapesa kibao kama kodi? Mmeshaangalia kwenye risiti za mauzo pesa zinazokatwa kama VAT.. Hivi hamjiulizi pesa zote hizo zinakwenda wapi? Je hamjiulizi pia na utajiri wetu wa natural resources ambao haujifichi na ambao inafahamika kua serikali yetu inapata mabilioni kibao kutoka humo.. Bado hamjiulizi why pesa hizo zisitumike kuendeleza infrastructures, TANESCO ikiwa included? Watanzania bwana tuna uwezo mdogo mno wa kufikiri. Mungu tusaidie..........

    Na hizo gharama za kuleta lori la mchanga... Nyie mnaona ni saaawa kabisa eeh? Nyie maannon mnaokaa mtandaoni na kuchangia je mishahara yenu inawawezesha kufanya mambo ya ujenzi wa nyumba ya milioni mia moja bila ya kutumia kaufisadi kidogo? Mngefikiria kabla ya kum-crash annon wa kwanza nafikiri mngekubali kwamba bongo "KARIBIA" kila mtu ni fisadi maana kila mtu anakula kivyake kulingana na nafasi yake. Kama tusingekua na lawless society na kama kila mtu, including serikali yetu, wangekuwa wanafanya mambo kwa kufuata sheria na kanuni basi tusingekua na situation tuliyonayo sasa. Tusingekuwa MASIKINI WA KUTUPWA MIAKA ZAIDI YA 40 BAADA YA UHURU.

    Niambieni, ni asilimia ngapi ya watu hapa bongo kwa mishahara yao wanaweza nunua nyumba ya milioni 100 cash bila ya kufanya ufisadi? Sijazungumza kuhusu wafanyabiashara, ila hata hao wafanyabiashara.. Je ni asilimia ngapi ya wafanya biashara wa bongo wanaweza nunua kiurahisi bila maumivu nyumba ya milioni 100 bila ya kukwepa kulipa kodi ama bila ya kufanya ufisadi mwingine wa aina yoyote... Give me the answer..

    Halafu, nyie mnafikiri nyumba hiyo ilivyokaa designless na bila mvuto wowote (in my opinion - sorry, no offense intended) je inastahili kweli kuuuzwa kwa milioni 100? Kama Tanesco wasingekua mafisadi kubambika charges zisizo na msingi, Twiga Cement wasingebambika raia bei za cement ku-cover ongezeko la allowances na mishahara yao, wauza mchanga wasingechukua advantage ya Tanganyika kuwa lawless society na kubambika bei zisizo-make sense, architect ange-design jengo kwa kutumia elimu aliyoipata shuleni ili jengo liendane na wakati na bei kusudiwa, kamwe bei ya nyumba kama hiyo isingefika hata milioni 20.

    Open your eyes people...

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 09, 2009

    Maza acha tambaa! Niandikie email mkunjob@hotmail.com na nitakusikisha $ 35000. Sitaki ku negoshieti,YAANI WEWE KAKA MKUNJO UNA HALI MBAYA SAAAANA,HIZO DOLA $35000UKIZIBADILISHA HATA MILIONI 50,000Tshs hazifiki! Kaka kazana kubeba maboxi au rudi nyumbani ufanye business nyinine,hiyo ni pesa ya kununulia kiwanja bunju na kujenga nyumba mgongo wa Tembo bila tiles wala vigae! Jitahidi angalau zifike $1,000.00 kidogo bila hivyo wale rafiki zako utakuta wamekupiga bonge la gepu!!! Pole sana ndugu yangu!!!

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 09, 2009

    Nakushukuru sana Michuzi kutuondolea shida ya madalali.Ninachoomba huyo mama apige picha nadni na nje ya nyumba hiyo akiwa juu na chini ikiwezekana na nje ya geti ili iwe rahisi kujua picha halisi.Sio lazima twende huko Tegeta.Ninaomba ajibu kabla ya alhamisi.Na je nyumba hiyo in hati?na je muuzaji ndio mwenyenyumba?au anafanyakazi ya udalali?Nitashukuru kupata majibu haya kwenye ukurasa huu mapema.Michuzi bigup sana.Wewe ni mbunifu nakushauri gombea ubunge wa viti maalum wa vijana kwa chama chochote kile sisi tutakupa kura.maana hapa umenitatulia shida yangu niliokuwa nayo kwa muda mrefu

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 09, 2009

    Ndo maana ikaitwa BONGO wengi wanajua ila wamesahau maana ya asili ya kuitwa bongo.neno hili lilianzia kwa mtu kuishi kwa mshahara wa kitabu moja kwa mwezi hapa Dar, sasa hivi ni nchi nzima ni Ubongo wako tu.na sio mafisadi.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 09, 2009

    Acheni kudanganyana,
    a) naomba nifahamu kama eneo limepimwa surveyed area na kama una title deed
    b) ukubwa wa kiwaja nusu ekari, 30 x 30 or what details?
    c) Kiwanja bunju..ni kati ya Tsh mil. 5-6, kujenga nyumba yote kama hiyo Tsh.mil 50 inatosha. kwa hiyo 70 mil. inakutosha acha kugonga watu kama details above zipo
    mdau wizara ya ardhi.

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 09, 2009

    anony# hapo Juu pay slip zinasoma 2.2mil kwa mwezi mshahara wa mwaka utakuwa 30mil. Kazi mwaka mmoja na gari la 50mil kama si ufisadi ni nini?

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 09, 2009

    Ukweli ni kwamba kama unabeba box huwezi kununua nyumba kwa bei hiyo ya mil 100 hata siku moja,wabeba box viwanja vyao Segerea, Kigilagila, Mbagala, Tuwangoma na sehemu za bei powa,Bei kama hizi ni za Mazungu ya Ungu, Mafisadi au wafanyabishara wakubwa, Bongo pesa ipo,ila ujue jinsi ya kujipangilia, tuna hangaika tu na mabox na mabaridi bure.Bongo shwari.Mwinyi Mpeku.

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 10, 2009

    WATU WANA UWEZO WA KUNUNUA NYUMBA UGHAIBUNI HATA KWA $200K AU $300k NA UNAPEWA MKOPO WA MIAKA 25 HADI 30 KULINGANA NA KIPATO CHAKO.
    BONGO NHC INAJENGA NYUMBAA INAUZA MILIONI 75-150 NA WANATAKA ULIPE KWA MUDA WA MIEZI 12-18. NDO MAANA WATU WIZI NA UFISADI HAUKOMI. JENGENI MJIIBIE WENYEWE, MLALE WENYEWE SISI TUTABAKI HUKU HUKU WEZI WAKUBWA WASIO NA HAYA HATA KIDOGO.

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 10, 2009

    Bahati nzuri Tanzania hakuna mabenki wanaoweza kukupa mikopo mikubwa ya kununua au kujenga nyumba kwa wingi. Uchumi wetu hauruhusu. Watu wengi wangefilisika na kufilisi benki na serikali kama wananchi wa Marekani.

    Hii ni uchumi wa bubble, utapasuka na bei ya nyumba itashuka tu. Hamna kazi nyingi inayoweza kutupa mishahara cash ya kununua nyumba ya milioni 100. Ilikuwa hivi hivi Iceland, Ireland, UK, Spain na Marekani. Watu walikuwa hawaulizi bei, wananunua tu kwa kukopa, mpaka wakafilisi benki na serikali zao.

    Hata hapa Marekani, sasa ni vigumu kupata mkopo mkubwa na lazima uwe na kazi nzuri yenye mshahara mzuri ili ukopeshwe.

    Mdau anayesema kuna kazi za milioni mbili au tatu kwa mwezi, naomba data za makampuni ili niombe hio kazi. Nina B.Sc., na MBA hapa ya marekani(Boston University). Nilivyoenda nyumbani mwaka jana makampuni walitaka kunipa dola 500 tu kwa mwezi.

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 10, 2009

    annon June 10, 2009 12:00 AM umesema kweli,nyie walioko nje nunueni nyumba huko huko,bongo tamaa tu mshahara wa mfanyakazi serikalini laki 2 ,cement inapanda,hiyo nyumba ataijenga lini kama sio kuendelea kufanya watu tuzidi kuwa maskini,Nunue huko huko zinazobakia watumieni ndugu zenu.

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 10, 2009

    Nyie watoaji maoni karibu wote inaelekea ni watoto au bado mmezoea nyumba za kupanga ndio maana hamuelewi bei za kununua nyumba na kujenga. Wewe uliosema bora ukanunue Kariakoo badi ujue kariakoo hupati kiwanja (nyumba mbovu ambayo ukinunua inabidi ubomoe) chini ya Milioni mia mbili.

    Kumbukeni gharama za ujenzi sasahivi zimekuwa kubwa sana pia viwanja ni bei ghali sana.

    Tegeta angalao muda kidogo uliopita viwanja vilikuwa rahisi lakini sasahivi havishikiki, hata Bunju sasahivi pia viwanja vimepanda sana.

    Kumbukeni miji inavyotanuka kama wewe unahitaji nyumba za bei rahisi au kiwanja labda ukimbilie maeneo ya kibaha mbele kabisa but no near Dar es Salaam.

    ReplyDelete
  42. AnonymousJune 10, 2009

    Hivi nyinyi mnashangaa nyumba kupangishwa laki nne nzuri kama hiyo au kuuzwa milioni mia 100?

    Fikiria nyumba za hapa town zinazopangishwa laki nne mandhari yake ndipo ufikirie uzuri wa nyumba hiyo.

    Mimi sioni ajabu nyumba kuuzwa bei hiyo. Ni gharama sana kujenga na kununua viwanja sasahivi ndio maana kinasisi tutaishilia kupanga na kuwa masikini.

    ReplyDelete
  43. AnonymousJune 10, 2009

    asante

    ila izo windows ni njia laiiini ya jambazzz

    asante sana

    ReplyDelete
  44. AnonymousJune 10, 2009

    sasa watu wanashangaa nyuma hii kuuzwa Tshs. 100m?! Nyumba bongo bei mbaya sana.

    Hamjaona kibanda cha Ray C kwenye magazeti ya udaku kajenga huko huko Tegeta. Nyumba yenyewe vyumba viwili, na sebule, chini bado mavumbi, madirisha wazi, juu bati la kawaida jekundu la ALAF. Hata ripu bado, yeye anakwambia ameshatumia Tshs.30m.

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 10, 2009

    Wewe anon wa 10 june 2009 06:28 am, hapa bongo kuna baadhi ya industry zina mishahara minono kama Mil 2 na zaidi, jaribu kwenye Telecom, huku kuna mishahara mizuri tuu, kwa MBA yako ukipata kamoubi kama Vodacom, Tigo, Zantel, Zain, Hits,Dovetel, Ericsom n.k unaweza kupata mshahara huo na zaidi, ila ufanisi ni muhimu sana kaka lazima udeliver mkuu, mie nipo kwenye hii sector hivyo ninafahamu vizuri kuhusu malipo

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 10, 2009

    Wewe annon June 10, 2009 4:17 PM kweli mbumbumbu wa economics,yaani unaona mshahara wa Tshs.mil 2 kwa mwezi utakuwezesha kununua nyumba Tsh.mil 100,hujatulia. Hapo huli,hulipi kodi ya kiota chako,huvai, huugui,watoto hawaendi shule n.k .Mbali na hayo ni watu wangapi wanafanya kazi vodacom,tigo?mtanzania hali mf.mwalimu mkuu huko kiteto au muuguzi hapa Dar anamshahara gani?Tatizo letu watanzania sisi wabinafsi na malimbukeni ndio maana hatuendelei watu wabinafsi hawana uzalendo akipata mshahara eti mil. 2 (kumbuka hiyo sio $ ni Tshs)eti anaridhika kabisa na kujisifia wa kati hela hiyo bado ni ndogo na waliomzunguka wote wanashida tu, na limbukeni kwa sababu tunadhani kununua kitu gharama ni sifa.Nchi za wenzetu watu wanataka watu wote wainuke na kila mtu akiwa na uwezo wa kupata mahitaji muhimu kwa bei inayoendana na kipato chake,lakini mtanzania ni kinyume.Tutabadilika lini?

    ReplyDelete
  47. AnonymousJune 10, 2009

    Marekani ambako mfanyakazi kiwanda cha cement analipwa dola 10 kwa saa moja (dola 80 kwa siku 1) mfuko wa portland cement wa pounds 94 (kilo 50) unauzwa dola 10. Tanzania ambako mfanyakazi wa Tiga cement ambaye yuko mtamboni kutengeneza Twiga Cement na analipwa less than dola 100 kwa mwezi (sio kwa siku 1) mfuko wa cement unauzwa kwa bei kubwa zaidi ya Marekani. Mind you, huyo mfanyakazi wa kiwanda cha cement cha Portland analipwa vitu kama health insurance na kadhalika. Mimi sipati jibu kwanini mfuko wa cement Tanzania uwe na bei kubwa kuliko Marekani. Sipati jibu kwa kweli.

    Hapa Texas tunanunua gallon moja ya petroli kwa dola 2. Kumbuka kwamba gallon moja ni almost 4 liters. Haya jiulizeni Tanzania mnalipa bei gani kwa lita moja ya petroli. Je wafanyakazi wa petrol stations Tanzania wanalipwa mishahara mikubwa compared to wale wa USA?

    Yote haya yanasababisha kama annon wa hapo juu alivosema kuongezeka kwa gharama kwa watanzania kusiko make any sense. Ndio maana nyumba zinachapwa bei za ajabu kwa kua kila mtu anakua alishakula kulingana na nafasi yake kabla ya muuza nyumba hajaamua kujenga hiyo nyumba.

    Uongezekaji wa gharama (bei) za mafuta nma kadhalika unatokana na Serikali kutoza kodi nyingi kwa viwanda halafu izo kodi haziji kunufaisha raia kwa kuwawekea infrastructures kama jamaa wa apo juu alivosema. Wenye viwanda vya cement nao wanachukua advantage of the situation nao wanawabambikia bei wananchi. Matokeo yake anayekuja kuumia ni mwananchi wa kawaida ambaye anakuja shindwa kuafford gharama ya final product.

    Sijui wahusika wanasomaga vitu hivi? Inaboa sana.

    ReplyDelete
  48. Nafikiri hapa si kwamba watu hawaelewi nyumba kuuzwa mil 100 ila watu wanashindwa kuelewa mtu ataweza vipi kupata hela hiyo kwa mkupuo kwa mshahara wa mtanzania wa kawaida ukizingatia kuwa hatuna system nyingi ya kupata mikopo ya kujenga au kununua nyumba kutoka mabenki.Harafu mwenye comment eti watu wanapata mishahara mil. 2 ni wangapi jamani hao? mie mwenyewe nimefanya kazi serikalini na ni Graduate lakini mshahara wangu na marupurupu yoote yasingeniwezesha kujenga au kununua nyumba bei hii.Ndio maana watu wana maswali,mwenye jibu ni jinsi gani hii inavyowezekana hebu afafanue atakuwa amejibu utata na pia utatusaidia maana naamini kila mmoja anataka nyumba nzuri na hii yavutia kweli kweli.

    ReplyDelete
  49. AnonymousJune 11, 2009

    Bongo kazi za mishahara mizuri zipo kibao sema huku tofauti na huko kwenu ughaibuni huku hazitangazwi sana ni connection na network ya marafiki na wadau ndio itakuwezesha kupata kazi ya maana. Ila kwa sababu kampuni nyingi ni za kigeni ku-survive lazima u-deliver watu hawajali vyeti vyako wanajali performance yako. Kuna magabacholi kibao kutoka Udosini wanapiga kazi kwenye kampuni za wadosi wanakula mikwanja ya maana kwa vyeti vya kughushi coz matajiri sometimes wanakosa wabongo qualified wanaamua kwenda kuzoa magabacholi udosini kumbe ndugu zetu qualified wamejazana Ulaya wanabeba boksi na kuishi kwa kujifichaficha kama panya kwenye nyumba ya mtu asiyependa uchafu!

    ReplyDelete
  50. AnonymousJune 11, 2009

    Nyoe mnaosema wabeba mabox tunashangaa na kutuona tuwajinga nyie ndio haoa hao mnaoliwa. Siku hizi sio zile za zamani mababa zetu walikuja huku barua ni mwezi mmoja ndo ifike bongo. Siku hizi communication ni mweeee. na Tukishangaaa hiyo millioni moja si ajabu. Hebu yuonyeshwe hiyo nyumba humo ndani kwa vile nje hailipi millioni moja bado.

    Msituone makasem ahtujui thamni ya viwanja...welll maybe kiwanja nighali hapo lakini cost ya hiyo nyumba haipay kabisa.

    Mimi nina nyumba nimejenga mwenyewe from scratch kiwanja nilipewa na wazazi kwa hiyo price ya kiwanja ondoa na ni kubwa saaana saaana tu zaidi ya hiyo na ilicost sio zaidi ya million 25. Sasa ukisema millioni mia moja labda kuwapata matuarist ambao utawala mark up 100%.

    Msizanie hatujui ndio maana nilikataa kaka yangu asisismamie nyumba yangu kabisa. Mwanzoni alikua ananilangua bei ya cement ananipa price tofauti nikamtimua

    ReplyDelete
  51. AnonymousJune 11, 2009

    Da Sophie, nakubaliana nawe kuwa Tanzania kuna watu wachache wenye uwezo wa kulipa milioni 100 au zaidi Cash. Nadhani Mama anawatafuta wateja hao na gumzo limekwenda kwingine. Sasa tunazungumzia ufisadi, mishahara ya Bongo v/s Marekani na kadhalika. Ukizingatia kuwa kuna nyumba chache na watu wengi Bongo, ni rahisi kuona kwa nini bei ni kubwa. Mama ameweza kujenga na anataka apate faida yake kama wafanyabiashara wengine.

    Kuna Wadau pia wanalinganisha bei. Hatuwezi kulinganisha bei ya vitu Marekani na Tanzania kwa kuwa Tanzania ni nchi masikini na haizalishi vitu vingi (GDP UD$20 Billion v/s $1 trillion ya India au Brazil. Ndio maana vitu ni ghali Tanzania kwa kuwa kila kitu kinaletwa kutoka nje. Hio simenti peke yake ya Bongo haiwezi kuzalisha nyumba. Bei ya petroli ni ndogo Marekani kwa kuwa wanazalisha wenyewe na wananunua kwa wingi. Serikali yao pia inatoza ushuru mdogo kuliko Ulaya katika petroli yao. Hapa Tanzania tunategemea makampuni ya nje na wafanyabiashara wadogo waagize mafuta ulaya, wengi wao wanakopa. Ni muhimu kujua uchumi kidogo ili uelewe.

    Mdau aliyenipa data za Makampuni asante sana. Nashukuru kwa msaada wako. Amini sana kwamba kama unaishi Ulaya au Marekani, ku deliver ni kitu cha kawaida au hutakaa sana kazini. Uzalishaji wako unapimwa kila miezi sita. Kwa sasa naona nitakaa hapa kutokana na mishahara bora lakini nina hamu ya kurudi nyumbani na kuendeleza libeneke.

    ReplyDelete
  52. AnonymousJune 11, 2009

    Anony wa June 09, 2009 7:27 PM (Mdau wizara ya ardhi),

    Tafadhali nifahamishe hivyo viwanja vya bunju vinapatikana vipi, nami nijitose na tudollar twangu twa boksi.

    -- Proud Tanzanian.

    ReplyDelete
  53. AnonymousJune 17, 2009

    Akili ni mali. Wenzetu India sasa hivi wanajenga nyumba kwa bei nafuu kwa kuwa wanatumia vifaa vya bei rahisi. Kotokana na habari ya gazeti maarufu la Kiingereza, The Economist la wiki hii, inasema kuwa Wahindi sasa wanaweza kununua vyumba viwili katika fleti kwa peza zetu milioni tano (USD 4500)hapo Mumbai. Kampuni kama TATA na wenginewe wanatumia vifaa vya bei rahisi kujenga nyumba ili wananchi wao wanaofanya kazi za mishahara midogo waweze kununua nyumba. Pia, serikali yao inatumia benki zake kuwakopesha wafanyabiashara na wanunuzi. Kwa nini sisi hatuwezi kujenga nyumba za bei rahisi?

    Si lazima uweke zege kote. Ukuta wa nyumba hizi za bei rahisi za India inasemekana unajengwa kwa kutumia makaratasi,mbao na plastiki na ni imara bila ya kuhatarisha maisha ya watu. Pia gorofa ni moja ili vyuma vingi visitumike kupunguza gharama. Nyumba zinajengwa kwa upana sio urefu. Wajenzi mpo?

    ReplyDelete
  54. Huko juu kuna watu wanatoa lugha chafu na maneno yasio na busara! na katika hao hakuna mnunuzi, basi tu kutia ufirauni wao kwenye biashara za watu!! na wajomba msiwashangae hawa wabeba mabox wanaofikiri bongo bado sh. 5 inatumika!! hawa mafala( kumradhi lugha hii) hata kwao hawana, kwa hiyo msione ajabu kwamba hawajatokea hata kutembea. wengine huku wapo kazi kuchafulia wabongo majina. hata hayo mabox wakibeba wanataka na kuiba. sasa unafikiri pimbi kama huyo atakuwa na uwezo wa kununua nyumba!! huko walipo hata baiskeli zinawashinda basi tu wanataka wasifiwe eti wanaishi nje!! **&¤`"*#"¤"¤"" wakubwa. mwana mama wa watu anajaribu kutangaza nyumba yake wanakuja kutia lugha chafu. Mi ningeshauri humu ndani kusiwe na uwezoekano wa kuacha maoni ya mtindo wowote bila LOG IN. ili mimtu kama hiyo iwekwe hadharani na kupigwa marufuku kuingia humu.
    inawachafulia majina wale wachache walio na nia za maendeleo. na hao wengine wanasema tu huku marekani!! huku uingereza, huku ......!! kumbe kapata access ya computer kutoka kinyelezi na hakuwa na la kufanya. AIBU sisi wabongo tunajua kuaribu. nna mengi lakini acheni tu.

    ReplyDelete
  55. AnonymousJuly 30, 2012

    MAMA YUKO SAHIHI KWA KUZINGATIA GHARAMA ZA UJENZI ZA SASA.TATIZO NI KUWA WASWAHILI HUWA HATUELEWI KUWA HATUELEWI!MAMA KATANGAZA BIASHARA YA KUPANGISHA AU KUUZA NI JUU YAKO MSWAHILI KUCHAGUA KIMOJA AU KUACHA VYOTE.ANAPANGISHA SHILINGI NGAPI AU ANAUZA SHILINGI NGAPI NI JUU YAKE NA MNUNUNZI AU MPANGAJI.OTHERWISE ZIPO NYUMBA MPAKA ZA LAKI 6 DSM HII HII.MAISHA NI KUPANGA NA KUPANGA NI KUCHAGUA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...