Ndugu michuzi naomba uniwakilishie hili kwa wadau wote ambao wanapenda na wanakumbuka historia za majina yaliyochimbuka hapa na pale kwasababu fulani. Hili litasaidia sana vizazi vyetu, na sijui kama kuna mahala kumbukumbu hizi zimehifadhiwa.
Kwa mfano hapa Dar, Msasani chimbuko lake `tumesikia' kuwa ni Jamaa mmoja alikuwa akiitwa Mussa Hasani, likawa linaitwa kwa MusaHasani na mwishowe kufupishwa kama MSASANI.
Hali kadhalika Kinondoni tumesikia kuwa ni mama mmoja alikuwa amekalia ndoo, na sehemu ya kiuno chake kilikuwa kimezama ndani ya ndoo, akapita mzungu mmoja akawa anashangaa na kumuuliza jamaa aliye naye `unaona yule mama kiuno-ndooni. Watu wakawa wamahadithiana hivyo,na hatimaye ikazoeleka `kiuno-ndooni' na hatimaye Kinondoni.
Zipo kumbukumbu nyingi kwamfano, Mnazimmoja palikuwa na mnazi mmoja, na sijui kwanini wanamazingira msipande mnazi mmoja hapo ili uendeleze hilo jina, magomeni mapipa, pale nakumbuka palikuwa na mapipa, Gongolamboto.
Vile vile Mwananyamala tumeambiwa kulikuwa na simba na mama akipita na mwanae anamwabia 'mwana nyamala' yaani mtoto kaa kimya pana simba hapa. Au Kariakoo ambayo imematumbishwa neno carrier corps ambapo wakati wa vita vya pili vya dunia sehemu hiyo ilikuwa kambi ya jeshi ya kikosi cha magari ya uchukuzi.
je kumbukumbu hizi zimehifadhwa wapi au baadaye vizazi vyetu viwe vinasoma kwenye vitabu vya wazungu ambavyo wataandika kwa kupotosha kama walivyopotosha biashara ya utumwa, au kama walivyoandika mzungu fulani kavumbua mlima kilimanjaro nk.
Mimi nisingependelea ile hali ya kubadili majina ya asili na kubambika majina ya wakubwa fulani.Maraisi watajulikana tu hata wasipopewa majina ya mitaa. Rais wa kwanza, wa pili nk watajulikana, lakini mababu zetu ambao ndio asili ya maeneo hayo watasahaulika tukiwanyima haki yao waliyopewa kuhusiana na eneo hilo.
Kwa hiyo bwana michuzi na wadau wengine tuendeleze hili, kwani tukiwaachia wabunge watataka majina yote wapewe wakubwa, siunajua tena wanapalilia unga, wajisifie kwa raisi ili wapate uwaziri. Tunaomba yule mwenye histroria ya kweli aielezee na isiwe ya uzushi ili vizazi vyetu vifaidike.
Mdau M3

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2009

    Sharifu shamba ilala mwisho wa lami ya amana hospital, ule mtaa unajulikana kama "SHINGOFENI",(muheshimiwa Zungu anakufahamu vizuri sana, alitudanganya atatuletea lami, lakini mpaka leo HOLLA!) asili yake jina hilo nasikia ulikuwa ukipita time yoyote lazima ukute watu nje wanakushangaa/wanakukatia shingo toka unapotoka mpaka unapoishia, yaani pita saa 7 usiku, hata saa 11 alfajiri utakuta watu na mataula na miswaki nje wanashangaa wapita njia. basi wanaokatiza mtaa huo wakaubatiza SHINGOFENI, na mpaka leo unajulikana hivyo, lakini msiogope siku hizi hakuna washangaaji watu wanamaluninga wanajifungia ndani kutwa kucha labda mwenye biashara nje!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2009

    Mdau ameongea point nzito sana. Hili suala halmashauri za miji mbalimbali zilipaswa kulivalia njuga wakati zinaorodhesha vivutio vya miji husika...sema hawakawii kulitengenezea posho za vikao. Nasikia "gongo la mboto" maana yake ni "titi la mama" kwa moja ya lugha za makabila yetu.

    ReplyDelete
  3. Umesahau , Kunduchi, Tandika , Upanga,

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2009

    Asili ya jina Kilimanjaro ni kwamba mzungu alikwenda marangu na akakutana na mzee wa kichaga miaka hiyo ya nyuma na akauliza huu mlima unaitwa nini? mzee wa kichaga akajibu "Kilema Kyaro" akiwa anamaana ni mlima wa ajabu kwa jinsi ulivyokuwa ukichemka volcano. Basi mzungu akapotosha jina na kuuita kilima-njaro! lakini asili yake ni "KILEMA KYARO"
    Mdau you are right we need our natural names back!

    ReplyDelete
  5. Kunduchi.Mzungu alikuwa anaoga ktk bafu lilozungushiwa makuti watoto wa kibongo wakawa wanachungulia wakaimba kund uch.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 07, 2009

    mimi nimefuarahia asili ya kinondoni tu. mdau heko

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 07, 2009

    ngojeeni basi sisi wazanzibari tukupeni yetu: naamnaza na mchamba wima, ohooooo naona mzee michuzi keshakamata shoka anataka kuondoa posti yangu!!!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 07, 2009

    Hii ni hoja nzuri sana na ingejuwa vyema kama tungetengeneza resource yenye majina ya hizi seheme zetu mbali mbali na asili yake.

    Niko tayari kutoa muda wangu juu ya hili, nani mwingine?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 07, 2009

    Nami nipo tayari, wee anon wa 11:36:00. Nipe mawasiliano.

    ati nasikia Iringa, ilikuwa kwa sababu sehemu ina mawe mawe, ikaitwa iliganga = mawe. basi wakasawazisha nengo wakaweka iringa

    P.E.D

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 07, 2009

    ...aisee yan menifanya nitoe chozi la huzuni jinsi tunavosahau ASILI YETU ...

    ivi basata,sijui wizara ya utamaduni nk kwanini hawaweki KUMBUKUMBU ya asili yetu???

    kweli kabisa majina aya ni muhimu kwa vizazi vyetu,sio ivo tu ata ile MICHEZO ya zamani mdako nk,na nyimbo za asili ambazo zimeanza kufa miaka ya 90 mwishoni

    yan now watoto wetu hata hawajui tena,

    HAKUNA KITU KILICHOWEKWA KIMAANDISHI KABISA..utumwa mtupu!!

    shime wadau

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 07, 2009

    KIBO SHOW KIBISHO

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 07, 2009

    mwembe chai hapo palipo jengwa kituo cha super star kulikuwa na bwawa kubwa na mita chache kulikuwa na kinyozi na mzee mmoja majebele alikuwa ana ubao wakuuza chai na ndio kituo cha dmt(uda)basi lakutokea mjini baada ya mapipa ni mwembe chai hongera mdau kwa maada yako ya akili

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 07, 2009

    HAPO MDAU UMSEMA,NASIO ASILI YA MAJINA YA SEHEMU TU HATAMAJINA YETU SISI BINADAMU YA ASILI NAYO INABIDI TUYAENZI MAANA MTU BILA KUITWA KWA JINA LA KIZUNGU AU LA KIARABU HARIDHIKI NAYO TUYAENZI KAMA VILE BATAMWA,MUSHI,RWEIKIZA,MWAKATUMBULA,MWAKAJINGA,CHACHA,WAMBURA.ASANTE MDAU.ILAKINGINE MAMBO YA MAANA WATU SIO WENGI WANAOCHANGIA SIJUI KWANINI

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 07, 2009

    Kuna Mzee mmoja pale karikoo msikiti wa Idrisa huwa anatoa sana historia hizi mbadala.Kwani nyingi huwa hazijulikani kama tujuavyo kwa kuwa aidha tumepotoshwa au kutokuwa na utashi wa kuuliza.Niliwahi kusikia stori mbili tofauti kuwepo kwa Ilala.Moja ni ile isemayo kuwa watu walikuwa wakisikia Adhana ikitokea mitaa hiyo mpaka baadae ikajulikana Ila-Allah(isipokuwa mola wa kweli) na nyingine ni kuwa walikuwepo mama wa Kimanyema wenye asili ya Kiarabu na Kimanyema wakiitwa Mabint Haila-LLah na ndio likatokea jina hili.Kuna mama mmoja mtaa wa Narung'ombe ni mjukuu wa mabibi hawa aweza kutupa dondoo hizi akitembelewa.Mdau ukiwa tayari sema tukupe contacts.
    Kuwepo kwa neno daladala, ni enzi hizo za Julius Nyerere pale gwala km utalikumbuka likiwa na trekta nyuma( ilikuwa sawa na dolar moja ya kimarekani) na wapiga debe enzi hizo walisema dala -dala-dala kumaanisha kuwa bei ni dala moja(gwala/shilingi tano) sina hakika na story hii

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 07, 2009

    Ahsante sana Mdau uliyeleta mada hii ya histora na machimbuko ya majina.

    Majina ya miji ifuatayo inatokana na lugha halisi za watu waliokuwa wakiishi sehemu hiyo.

    MWANZA - Limetokana na neno la Kisukuma, "Nyanza", ikiwa na maana, "Palipotandikwa tambarare"=Ng'wanza, kwa lugha ya Kisukuma. Wakimaanisha utambarare wa Ziwa Victoria.

    SHINYANGA - Limetokana na neno la Kisukuma, "Hinyanga". Sehemu hiyo kabla ya kujengwa nyumba, palikuwa na mti wa Inyanga, uliokuwa na kivuli kizuri. Watu walikuwa wakienda hapo kuuza mazao yao. Walipaita Hinyanga=Kwenye mti wa Inyanga.

    MWADUI - Limetokana na neno la Kisukuma, "Ng'wadubi"=Pale pakutumbukia. Yalipoanzishwa machimbo ya madini, kila mtu alikuwa akienda kutumbukia shimoni, kuchimba madini. Ni Ng'wadubi.

    NZEGA - Limetokana na neno la kisukuma, "Mizega". Kulikuwa na shida ya maji sehemu hiyo, watu walileta maji kwa mizega kuuza, kwa vile sehemu hiyo kulikuwa na shida ya maji, kabla ya kuchimbwa Bwawa la Uchama. Sehemu hii ilikuwa ni muhimu sana kutokana na njia panda zake, kati ya wasafiri waendao Tabora na Singida wakitokea Mwanza na Shinyanga.

    TABORA - Linatokana na neno la Kinyamwezi, "Matoborwa". Viazi vitamu vilivyokaushwa juani. Vilikuwa vikipatikana na kuuzwa kwa wingi katika mji huu.

    Samahani Mzee Michuzi kwa kuandika mambo mengi, ni kwa ajili ya furaha niliyonayo ya kuieleza historia na machimbuko ya miji ya kwetu nyumbani.

    It's Great To Be Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 08, 2009

    Kweli wadau tunapenda wenyewe kusahau/kupoteza asilia yetu.kunasehemu mbili hivi:
    Drive inn zamani kulikuwa kuna sinema watu wanaenda kuangalia picha za kiindi enzi zile za kina mithun chakaraboti bila kusikia sauti lakni nasikitika kwa sasa wanakuita ubalozi wa marekani
    Pia ukisogea mbele ukielekea mikocheni kunasehemu ilikuwa inajulikana kwa jina la kisiwani kwasababu eneo hilo ilikuwa na mabwawa makubwa ya maji yanayoenda baharini(ilipo shoppers plaza,myfair ) na sehemu nyingine walikuwa wanalima chumvi(Palipo tanesco) lakni kwa sasa tumekupachika majina ya hayo majengo(shoppers,My fair Tanesco)tumesahau ya asilia tuzinduke jamani.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 08, 2009

    aise hii Topic imenigusa sana, mimi pia hiki kitu nimekuwa nikifikiria muda mrefu, hasa majina ya watu...
    Juzi juzi nilikutana na rafiki jamaa moja anatoka France, ni mweusi na wazazi wake wanatoka Kongo, eastern Congo,LUBUMBASHI so wanajua kisawahili.jamaa jina lake anaitwa TUZO, Nilishangaa,nikamwambia jina lako ni la kiswahili akasema yes, najua, nikamwambia unajua maana yake akasema ndiyo, akasema na dada yangu pia anaitwa SIFA, mwingine ZAWADI.ingawa wamehamia France for yrs, na watoto wao wamezaliwa France, lakini jamaa wanakeep asili yao...
    Blackmannen naona wewe ni msukuma...Mi nimekaa usukumani na najua maana za majina mengi kidogo ya huko ya watu na maeneo...mfano,
    Madakomlume= ''matako kwenye umande''
    ni jina la mtu.
    Magulumnyanza= ''miguu ziwani'' jina la mtu
    Masangu= makande (nadahani Masangu Matondo Nzunzulima atakubaliana na hilo)
    Misoji= Michuzi, jina la mtu
    Mbitiyaza=fisi mwekundu, jina la mtu
    Ng'holoyapi= roho nyeusi, jina la mtu
    Ng'hoboko= cobra, jina la mtu kuna kamanda wa police anaitwa hivyo sikumbuki wa wapi
    Busulwangili, busulwanhumbili= mahali panapochunguliwa na ngiri, tumbili respectively...jina la mahali
    Maswa=manyasi
    Ndasa= mtamba, jina la mtu, e.g mbunge mmoja anaitwa Richard Ndasa
    Igembe=jembe, e.g Igembe Nkandala(MK5)

    Pia majina kama Songea, mtemi wa wangoni.

    Dar es Salaam= ''Home of peace'', nchi au nyumba ya amani sio bandari ya salama kama watu wanavyoamini,ni neno la kiarabu...walitoa waarabu wa Oman walivyokuja na kukuta bongo kila mtu peace tu...ndo wakaamua kusettle.
    Zanzibar= inatokana na zenj bar, ''the land of black people''-waarabu wa Oman walipofika kisiwani na kukuta watu wa kule ni weusi...
    ingawa hapa sijaelezea chimbuko au historia ya majina hayo, lakini point ni kuwa yana maana fulani ambayo kwa hakika ina-reflect matukio flani yaliyokuwa yanatokea kipindi hicho...na kama umefatilia vizuri wazee wetu wa zamani walikuwa wanapatia watoto wao majina yenye kumaanisha either tukio flani au jambo muhimu la kukumbuka...ndo maana utakuta pia majina kama Shida, Masumbuko, Matata,Matatizo, Tuzo, Faraja, Baraka,Imani,upendo n.k yalikuwepo...sio siku hizi mtu anakurupuka tu na kumwita mtoto majina yasiyo na maana yoyote, alimradi it sounds good.

    N.B: Kwa hiyo michuzi mara nyingine twaweza kumuita ''misoji'' kwa kisukuma....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...