WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imethibitisha kuwapo kwa mgonjwa wa kwanza wa homa ya mafua ya nguruwe (H1N1) nchini. Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Aisha Kigoda amesema, mgonjwa huyo amelazwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili jijini Dar.

Dk Kigoda, amewaeleza waandishi wa habari leo, Dar es Salaam kuwa, kijana huyo raia wa Uingereza amelazwa katika wodi maalum, na hali yake inaendelea vizuri. Mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 17 aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam mwanzoni mwa mwezi huu akiwa miongoni mwa wanafunzi 15 na walimu wawili kutoka Uingereza waliokuja nchini kwa ajili ya ziara.

Kwa mujibu wa Dk Kigoda, kundi hilo ni miongoni wa wanafunzi 350 wanaokuja Tanzania kutoka Uingereza kwa ajili ya ziara ya mafunzo kwa kuwa wapo kwenye likizo ya majira ya joto. Kuna taarifa zinazodai kuwa, mgonjwa huyo na wenzake 16 waliwasili nchini Julai 2 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya na watakuwa nchini kwa mwezi mmoja.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili, Profesa Andrew Swai amekaririwa akisema kuwa, kijana huyo amepimwa na kuthibitika kuwa ana homa ya mafua ya nguruwe. Inasemekana kijana huyo alikuwa na homa, mafua, maumivu katika koo, alikuwa akipiga chafya, na pia mwili wake ulikuwa dhaifu.

Mganga Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Deo Mtasiwa amekaririwa akisema, Wizara hiyo hiyo ina dozi 51,283 ya dawa zinazotibu ugonjwa huo ziitwazo tamiflu, na kwamba 1,200 kati ya hizo zimepelekwa Zanzibar.

Mwanafunzi huyo ni mgonjwa wa pili Afrika mashariki kugundulika kuwa na mafua ya nguruwe, wa kwanza alifahamika nchini Kenya, pia ni mwanafunzi, raia wa Uingereza, aliyewasili nchini humo Juni 21 mwaka huu.

Juni 29 mwaka huu, Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Beth Mugo alithibitisha kuwapo kwa mgonjwa huyo aliyekwenda Kenya akiwa na wanafunzi wenzake 33.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO), hadi sasa watu 59,814 wameugua mafua ya nguruwe, 263 kati ya hao wamefariki dunia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2009

    izi ni dili za jamaa kuuza madawa yao,si wakae uko wasiruhusiwe kuingia makwetu?ivi why hawapimwi wanapoingia nchini watu wote wanaotoka nje?

    nyambaf zao,na kufa hatufi ng'o

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2009

    hii iwe fundisho kwa serikali yetu na wahusika wakuu kuruhusu wageni kuingia nchini bila kupimwa afya zao kuthibitisha hawajaathirika na magonjwa ya mlipuko, mbona nchini mwao wako makini sana kuzuia wageni wasiingie iwapo wanakotoka kuna magonjwa? au kwakuwa ni wazungu ruksa kuingia..sisi tunanyanyasika sana kwenda kwao wanatukagua wanatupima wanatumulika kila kona tusiwapelekee maradhi na viambukizo. nchi yetu yenyewe changa uwezo wa matibabu hatuna tutateketea kama kuku ukizingatia tunaishi kwa kubanana mitaani masokoni kwe daladala, jamani pigeni marufuku wageni toka nchi zilizoathirika. gharama ya magonjwa ni kubwa kuliko hizo pesa za kigeni mnazodhani watatuletea

    ReplyDelete
  3. Kaka Michuzi

    Natanguliza salamu za dhati

    Nimeugua flu ya ajabu kwa takriban wiki mbili sasa. Nimetibiwa kwenye hopitali kadhaa bila mafanikio na mbaya zaidi ni kwamba sasa hadi mume wangu na watoto wote tunaumwa, nimejaribu kupita mitandao kadhaa inaonesha nina kila dalili ya "swine flu" cha ajbu ni kwamba nimeenda hospitali za AAR na TMJ kote wanasema hawana reagents za kupima hiyo swine flu na mwisho wananishauri nitumie tangawizi asali na maji moto. Kweli sifanyi utani kwa wiki mbili sasa hata kula siwezi kwa jinsi ninavyoumwa koo na pia watoto wote wanaumwa kama mimi na baba pia (mume wangu) Usiku wa kuamkia leo tumekohoa hadi tunatapika tena ni "dry cough" sasa naomba ushauri wako. Ili kuthibitisha kama ni flu ya kawaida au ni swine flu inabidi nifanye nini? Jamani tuache masihara, serikali inapima wageni watokao nje wakiwa na dalili lakini wale wasiokuwa na dalili wanaingia bila kupima. Mimi asili ya kazi yangu ni kuonana na wageni kwa wingi sana hasa watokao nje. Sasa je serikali inalichukuliaje swala kama langu kwamba hakuna reagents eti mpaka Nairobi hivi si masikini tutakufa hadi tukose wa kutuzika???

    Waosha vinywa na wabeba maboksi tafadhali msinishambulie mwenzenu naumwa kiukweli.

    Ni hayo tu mjomba!!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2009

    Jamani Mungu atuepushe na huu ugonjwa wa mafua ya Nguruwe. Matatizo tuliyonayo yanatutosha sana.

    Mdau Enea

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2009

    Inasikitisha kwani ni ugonjwa unaoogopesha, ila ningependa serikali yetu iwadhibiti hawa raia wa uingereza wanaoingia nchini kwa kuwapima kwanza kabla ya kutoka nje ya airport. Nina uhakika kama ugonjwa huu ungekuwa unatokea afrika sisi wote tungewekwa quarantine pale heathrow!! Miaka kadhaa ya nyuma nilipokwenda uingereza kwa mara ya kwanza tuliwekwa pembeni kupimwa TB. Sasa waliokutwa na TB sijui hatima yao ilikuwa nini. Sasa hawa wazungu watatuletea ugonjwa huu ambao najua sisi tutakufa zaidi kuliko wao kwani huku nje umecontroliwa sana. Kwahiyo nikiwa kama mdau na mpenda nchi yangu na wananchi wangu naomba comments kama hizi zipewe kipaumbele, plz michuzi wajulishe wahusika waliangalie suala hili kwani watu watakufa huko tanzania. Tuna ndugu wengi sana nyumbani.

    Mdau Netherlands

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 10, 2009

    SERIKALI LAIZMA ICHUKUE EMERGENCY MEASURE, PAMOJA NA NGURUWE WOTE WAULIWE HASA WANAOFUGWA KARIBU NA JIJI NA WALA NGURUWE WOTE WA-STOP MARAMOJA. KUTOKANA NA UZEMBE WA SERKALI YETU NAAMINI HUU UGONJWA WA NGURUWE SOON UTAKUA OUT OF CONTROLL VIONGOZI WETU WATALIFANYA DILI LAKUOBAOMBA KWA MADAI NA NGURUWE PENDAMICS

    SIMPLY; CHINJA NGURUE WOTE TUSAVE JAMII YETU.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 10, 2009

    Michuzi mbona kwenye gazeti The sun UK, inaonyesha Tanzania iko kwenye nchi kumi zenye watu wenye swine flu wengi. soma hii link


    http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/news/2527652/UK-swine-flu-toll-third-worst-in-the-world.html

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 10, 2009

    sasa jamani wizara hao wengine aliokuja nao mmewafanya nini? kwa sababu ni ugonjwa unaotambaa haraka,inabidi wenzie wote aliokuwa nao (ikiwezekana ndege nzima) watafutwe na wawe quarantined mpaka vipimo vitakapoonyesha kwamba wako salama! otherwise hao wataingia uswazi na ugonjwa utasambaa (au tayari?) huku ndo wanavyofanya,juzi juzi tumetoka syria kuja UK, kulikuwa na mgonjwa mmoja kwenye ndege, wote tumetafutwa na kupimwa, tumekaa karantini siku 2,wengine waliokuwa dhaifu wamekaa mpaka siku nne ndo wametoka. bahati nzuri hakukuwa na mtu mwingine yoyte aliyeambukizwa!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 10, 2009

    si ugonjwa wa kutisha, kwani unaweza kupona bila hata kutumia dawa unless you have other underlying diseases with you,

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 10, 2009

    Hi flu bana kwa sisi weusi ni kazi kweli kutuua sie hatumoo

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 10, 2009

    Dada Irene pole sana, natumaini mnaendelea vizuri. Nimesikitika kuona kuwa umejitahidi kila njia kujua kama ni flu ya kawaida au la na bado ni tatizo kubwa, ukiachana na matibabu ambayo kwa nchi ya watu zaidi ya Milioni 30 (nadhani zaidi), tuna Dozi elfu 50 (ingawa naelewa khali ya kiuchumi). Na hatuna taratibu nyumbani kwetu za kuweza kuchunguza waingiao nchini kupitia vituo vyote vya anga, barabara na bandari wanaotoka kwenye maeneo yaliyoathirika sana na Swine Flu
    (Kwa jinsi nilivyosoma comments za wadau wengine hapo juu). La kusikitisha zaidi ni kuwa nimetoka kuangalia taarifa ya habari nusu saa iliyopita kuwa kwa mara ya kwanza mgonjwa wa Swine Flu ambaye alikuwa na afya nzuri tu bila 'previous medical conditions/illness' amefariki dunia, ukiachana na watoto, wazee au watu walio 'more vulnarable' waliodhaniwa kuwa ndio wapo hatarini zaidi na ugonjwa huo.

    USHAURI wangu tu kutokana na ombi lako, ni jaribu kwenda Muhimbili kama hospitali za private hawana vipimo vya Swine Flu, au kama unataka kujua dalili tu kama ni Swine Flu au la, angalia kwenye Website ya NHS Direct - link ni http://www.nhs.uk/Conditions/Pandemic-flu/Pages/QA.aspx#diagnosed - au kama link haifanyi kazi, nenda Google search kisha type in NHS direct, halafu utaona maelezo kuhusu Swine Flu.

    Ugua pole.

    Maseke

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 11, 2009

    huwezi kupata swine flu throught kula kiti moto hiyo sayansi umeisomea wapi wewe mtu?alaa?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 11, 2009

    MKUU WA NANII JANA NILICHELEWA KUWEKA COMMENT ZANGU KWA HABARI HII NAJUA MABOX TENA NIMERUDI HOI,TAKWIMU ALIZOTOA WAZIRI NAONA ZINA UTATA,MAGAZETI 10/7/09 SUN,GUARDIN,DAILYMIROR,NA ECHO LA WELS IMETOA TAKWIMU HII YA WATHIRIKA WA MAFUA YA NGURUWE
    US=33,902
    MEXICO=10,262
    UK=10,000
    CANADA=7,983
    CHILE=7,376
    AUSTRALIA=5,298
    ARGENTINA=2,485
    TANZANIA=2,076
    CHINA2,040
    JAPAN=1,790 UK 14 DEAD,43CRITICA.SASA TAKWIMU ZA MUHESHIMIWA WAZIRI ZINAPOTOSHA UKWELI AU NDIO SAHIHI.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 12, 2009

    KUUA NGURUWE SI TIJA TENA KAMA UGONJWA UMESHAINGIA KWA WATU UKIUA NGURUWE NI KUWAONEA KWANI WATU WATAENDELEA KUAMBUKIZANA TU, NA UJUWE HILO NI JINA TU WALA HAUJATOKA KWA NGURUWE SAFARI HII, KAPA UK HATA MAFUA YA KAWAIDA MWANZO MWA WINTER WATU KIBAO WANAKUFA, WA-AFRIKA KIDOGO TUWEZA KUHIMILI KWANI WENZETU WANAKUFA HATA KAJOTO KIDOGO TU AU MAFUA YA KAWAIDA TU AMBAYO SISI WABONGE TUPENGA TU HADI YANAISHA HATA YA KWENDA KWA GP/HOSPITAL

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...