sehemu ya majengo mapya ya makumbusho na nyumba ya utamaduni dar, zamani makumbusho ya taifa, ambayo inafanyiwa ujenzi pamoja na ukarabati wa nguvu kazi ambayo inategemewa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu na kupafanya mahali hapa sio tu pa kutunzia historia bali pia sehemu ya kukutana na kuburudika kwa muziki, ngoma na vyakula vya asili na mengineyo
tangazo la onesho la kumbukumbu ya soka nchini ambalo tarehe zake zimesogezwa mbele kwa mwezi mzima kutoka na maombi ya wadau

mtaalamu wa utafiti na mtunza historia katika makumbusho na nyumba ya utamaduni B. Margreth M. Mapunda akionesha kitabu chenye historia ya mpira wa miguu ambacho amekiandaa kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu hiyo muhimu. kitabu hicho kinapatikana hapo makumbusho na nyumba ya utamaduni na kina historia ndefu tokea enzi za sunlight na gossage cup, ikiwa ni pamoja na wachezaji wa enzi hizo pamoja na viongozi
mdau akiangalia jezi namba 3 mgongoni iliyovaliwa na beki hatari wa taifa stars enzi hizo mohamed chuma wa mtwara aliyovaa siku anastaafu kuchezea timu ya taifa mwaka 1976.
mdau akiangalia nyota wa zamani wa soka nchini
sehemu ya ukumbi wa maonesho wa makumbusho na nyumba ya utamaduni
wachezaji wa jimbo la nyanda za juu kusini mwaka 1955 katika kombe la sunlight uwanja wa ilala, siku hizi kumbukumbu ya karume
viongozi wetu walikuwa wapenza wakubwa wa michezo. simba wa vita Mzee Rashidi Mfaume Kawawa akiiingia uwanjani kama refa katika mechi ya wabunge na mabalozi miaka ya 70.
Mwalimu Julius Nyerere akiwa na wachezaji na viongozi wa timu ya taifa aliowakaribisha Ikulu baada ya kunyakua kombe la Gossage cup mwaka 1964.
nahodha wa timu ya taifa mbwana abushiri 'director mbwana' akiwa kabebwa juu na wenzie baada ya kunyakua kombe la Gossage cup mwaka 1964.
timu ya taifa wakiwa na kocha wao millan celebic (shoto juu) mwaka 1965
baadhi ya marefa waandamizi miaka ya 1970. hapa namkumbuka manyotto ndimbo (wa sita kulia) na rajabu marijani (wa nane kulia) wadau wenye data tunaomba msaada tutani












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2009

    DUH, NAONA SURA KAMA YA MZEE MARIJANI AU PENGINE NI MACHO YANGU.

    ReplyDelete
  2. Ebana eeh Soksi bila viatu.Kidogo niseme walikuwa wanacheza kick boxing bila gloves.looool

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2009

    Shaaban Marijani

    Marijani Rajab alikuwa ni mwanamuziki

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2009

    Shaban Marijani ni wa sita toka kushoto

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2009

    Mwanzo mzuri, pengine maboresho ya makumbusho ya Taifa yanatakiwa kujengwa hata katika mikoa mbalimbali ambayo yataitwa hifadhi za mikoa.


    Kwa nchi zilizoendelea zinamakumbusho ya Taifa ambayo yamejegwa kwa ustadi mkubwa na kunakila kitu ambazho kimetokea katika nchi nzima. Pengine ni sehemu ya kuongeza pato kwa serkali. Maana watalii wanapotembelea wanajifunza mengi na kulipa kiingilio hata watanzania.

    Bado kazi ni kubwa.

    Eneo la makumbusho ya Taifa ni dogo na linapendeza kama litatengewa kiwanja kikubwa chenye ukubwa wa ekali hata hamsini ambalo linaweza kuwa na zoo za wanyama na kumbukizi zingine kem kem.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2009

    Aisee huyo wa4 kushoto sio gration matovu?
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2009

    hongera Ms Mapunda kwa kazi nzuri uliyo fanya sio kazi ndogo lakini tutafika, hapo kutakuwa na entrance fee?

    ReplyDelete
  8. Al MusomaJuly 24, 2009

    Wa tano toka kushoto ni Kassim Chona toka Mwanza. Ile list ya wachezaji wakongwe imechangawanywa sana. Nafikiri ingekuwa bora kuwaweka kwa vizazi. Juma Pondamali na kina Zimbwe si wa wakati mmoja na kuna wengine sikumbuki hata kuwasikia.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2009

    Duh! Anko Michu!
    Mi sina neno hapo,maana mwaka sabini ndo kwanza Bi mkubwa alikuwa form 3,alikuwa hata hajakutana na mzee.Ruksa kwa wadau endeleeni.By mdau Mbeki 4rm St.Joseph Coet-DSM

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 24, 2009

    Namuona Manyoto Ndimbo

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 24, 2009

    angalau sasa tuna makumbusho

    ila bado sana kwa mikoani jameni

    tuweke historia tulizozimuliana toka enzi za mababu na sio elimu ya wakoloni:sitegemei kukuta apo eti ml.kilimanjaro ulivumbuliwa na mzungu gani au ziwa nyasa lol!!

    nk nk

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 26, 2009

    bwana michuzi asante sana sana kwa kutupa picha kama hizi za wachezaji wetu mabingwa wa soka enzi hizo. hawa ndio walikua mashujaa wetu wa soka enzi hizo. hapo juu ninamuona sharif wa tpc akipeana mkono na mwalim julius nyerere. tafadhali bwana michuzi ninaomba utuonyeshe picha nyingine za hao wachezaji wa gossage. kutufurahisha zaidi please tupe picha na majina yao.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 27, 2009

    Kama tunazungumzia mpira basi ndio kipindi iki. watu walikuwa wanacheza mpira kwelikweli. kulikuwa hakuna kununuliwa kama sasa. kuna mchezaji mmoja aliniambia wakati wake katika miaka ya 1970 hongo kubwa ilikuwa ahadi ya shaba la nguvu(pilau) sana sana totoz kidogo, maana mambo hayo ndio yalikuwa adimu.

    Kama tungekuwa na rais anayependa michezo kama huyu tuliyenaye sasa, naamini kwenye miaka ya 1980 nchi yetu ingekuwa imechukua kombe ka afrika japo kwa mara mbili.wakati ule wakina Peter Tino, Kajole, Thuen Ally, mambo sasa, Jella mtagwa na wengineo walikuwa wanatisha sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...