HABARI ZA HUZUNI ZINAWAKILISHA KUWA NDUGU YETU PETER ANG'IELA OWINO ALIYEKUWA ANASAFIRI BARABARA KUU YA KATI AMEVAMIWA NA MAJAMBAZI MAENEO YA NZEGA AKIWA NA MKE NA WATOTO WAWILI WA MIAKA MIWILI NA MWINGINE MIEZI TISA NA WOTE KUKATWA NA MAPANGA VIBAYA NA YEYE YUKO MAHTUTI HOSPITALI YA BUGANDO, MWANZA.
NDUGU OWINO ANAISHI UINGEREZA NA AMEWASILI JUZI AKIWA LIKIZO FUPI KUELEKEA NYUMBANI SHIRATI, RORYA.
MAJAMBAZI HAO WAMEWANYANG'ANYA KILA KITU WALICHOKUA NACHO HADI LISHE ZA WATOTO HAO WADOGO WALIOJERUHIWA PIA. POLISI NZEGA WAMETHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILO LA HUZUNI, NA HABARI ZAIDI ZINAFUATA.
PETER OWINO NI MMOJA WA WATU WALIOTOA MAPOKEZI NA HIFADHI KWA WATANZANIA WENGI WALIOKWENDA KUSOMA UINGEREZA TOKA MIAKA YA 1990
TUMWOMBEE NAFUU YA HARAKA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. Dah aisee inasikitisha sana...
    This is one of the reasons i dont want to come back home.

    ReplyDelete
  2. Ndugu yetu OWINO pole sanaaa, mungu awajalie afya njema na uponyaji wa haraka, nitawakumbuka katika sala.
    KWA ushauri tuuu kwa wale ambao si wenyeji wa kusafiri kila mara kwa kupitia njia za sengerema, biharamulo, nyakaura, nyakanazi, ngara, bukoba, shinyanga, na nzega,tabora, ni vizuri sana kupata au kuwasilia na Polisi kwanza kwa kupitia vituo vilivyo njiani vya polisi ilikujua hali halisi ya usalama kwa wakati huo.
    Bado wizi wa uvamizi upo, sii wakimbizi tena hata sisi raia tafadhali msijidanyanye kwamba wizi wa uporaji ilikuwa ni wakimbizi siiii kweli.

    POLENI SANA UGUA POLE,

    ReplyDelete
  3. Pole sana kwake na familia yake, inasikitisha sana ukizingatia alikua mbali na nyumbani kwa muda mrefu. Njia ya kati si salama sana siku hizi, ujambazi umezidi na wanausalama wanazidiwa nguvu kwani wana silaha kali hata mabomu. ushauri wa bure kwa wenzetu mlio nje ya nchi mnapotaka kuja nyumbani baada ya muda mrefu, muwe mnauliza juu ya nyia mbalimbali zenye usalama za kufika kwenu, maisha yamebadilika sikuhizi bongo.

    ReplyDelete
  4. Mungu awape nguvu wanafamilia wote wapone haraka.

    Pole nyingi kwa familia ya Owino kwa janga hili.

    ReplyDelete
  5. Yani hawa wakikamatwa wanatakiwa wasitoke jela hadi kiama. Hawana huruma kabisa. Kwakweli wamezidi hii imekuwa kama kawaida katika hizo njia zakuelekea kanda ya ziwa.

    Tutapoteza watu muhimu katika jamii zetu, maendeleo yetu yanarudishwa nyuma kila leo kwasababu ya majambazi.

    Tunaomba jeshi la polisi liwemakini katika hili. Mimi ni mmoja wa mkereketwa mkubwa wa hili kwani ni msafiri wakutumia njia hizi sana. Nikiwa nasafiri nakuwa sina amani ya maisha yangu na mali zangu kwani nakuwa nahisi tuu kuvamiwa. Tunaomba kilio hiki kiwe kimesikika.

    ReplyDelete
  6. Jamani, this is so sad. Hapo mtu mpaka anajuta kurudi nyumbani kwake mwenyewe. Our prayers are with them.

    ReplyDelete
  7. Poleni sana Nd. Uwino and family. Tunakuombea nafuu ya haraka. Hali hii inasikitisha sana kwa kweli. Haya ni matokeo ya nchi kufukarishwa na mafisadi. Juhudi tunazofanya za kuvutia utalii na uwekezaji kwa wazawa na kwa wageni hazitazaa matunda yeyote kwa mtindo huu. Unaporwa Bandarini, airport, mitaani na barabarani! Wizi gani huu paka uji wa mtoto?

    ReplyDelete
  8. Habari hii ni ya kusikitisha sana...napena kutoa ushauri kwa wote wanaotumia usafiri kibafsi kwenda safari za mbali hasa wakiwa na familia zao nyakati za usiku ni mbaya sana kusafiri hasa kwenye barabara zenye mapori makubwa kwasababu majambazi wengi hutumia muda huo na hiyo hali

    ReplyDelete
  9. Wadau jueeni ukijulikana umetoka ulaya au uzunguni!! hata pale Dar waweza kuvamiwa sio ndani ya balabala za mapoli tuu..Ushauri wa bure mtu anaye toka ulaya au nchi nyingine ya uzunguni ajue kwamba akisha ingia Tanzania ajue ameingia ndani ya nchi isiyo na amani ,watakiwa kutembea na skot wengi sio lazima wawe mapolis,,hata familia tu.Tanzania hata maisha mtapoteza huko..mimi sirudi kabisaaaa!!!!Ila poleeni sana ndugu zetu.

    ReplyDelete
  10. Hii nchi hovyo kabisa..
    WaTZ hatuna maana.
    Polisi,Serikali na raia kwa ujumla...Kila siku Ujambazi na Ajali Barabarani,Raia hata hatupigi kelele.

    Kibaya zaidi,ila power yetu ya voting hata hatuitumii..
    Amkeni waTZ wenzangu,muanze kuwatishia walio madarakani kwa kutumia voting power ili waongeze juhudi.

    ReplyDelete
  11. Hivi watu kama hawa ni azabu gani inaweza kuwafaa? Yaani kitendo wachokifanya ni cha unyama, kuwakata mapanga hata watoto??? Wangechukua mali na kuondoka bila kuwajeruhi.

    Poleni sana, Mwenyezi Mungu awajalie mpone haraka.

    ReplyDelete
  12. Kwa kweli swala la majambazi linaudhi sana, hata angewataarifu hao polisi, wangefanya nini? polisi nao ndio hao hao, kwanza wanazidiwa na majambazi, patafutwe suluhisho lingine kwa mfano kuhamasisha watu kutaja majina ya hao majambazi, kwani wanajulikana na jamii, ila woga umekithiri kwa wananchi. Pole sana Peter na mkeo na watoto, twakuombea upone haraka, poleni kina Maria,Akinyi na wa mwisho, kwa Tully.

    jamani tunapoandika tuwe na ukweli na uhakikia na kile tunachoandika Peter amesaidia wajaluo wenzake kwa hifadhi mara wajapo kwa mara ya kwanza hapa UK, na si kwamaba ni mtz yeyote yule, ni ki-group cha yeye na wajaluo wenzake hapa UK, na si vibaya kwani mtu unaanzia nyumbani kwako.

    ReplyDelete
  13. Pole Mr Peter na familia yako.

    lakini mbona watoaji wengine wa maoni wana mambo ya ajabu? Kwamba eti ndo maana hawataki kurudi nyumbani Tanzania kwa sababu ya mambo kama haya! Ina maana huko juu kakuna uhalifu ila ni huku tu Tz? Basi endeleeni kukaa huko huko majuu.

    ReplyDelete
  14. pOLENI SANA KWA KUVAMIWA NA HIYO MIJAMBAZI. MUNGU NI MWEMA SANA ATAWASAIDIA KUPATA NAFUU YA HARAKA. USAURI WA BURE, SIYO VIZURI KUSAFIRI NA FAMILIA HASA WAKATI WA USIKU HASA MIKOA YA KUPITA MAPORINI.

    ReplyDelete
  15. Poleni sana!!
    Samahani hivi huyu OWINO ni yule mw/kiti wa CCM tawi la London? Tafadhali mwenye taarifa sahihi anifahamishe!

    ReplyDelete
  16. Kwa sisi ambao tunauzoefu na hiyo njia ya kati na kanda ya ziwa kwa ujumla kuanzia shelui,igunga,nzega,tinde,isaka,kahama,bukombe,nyakanazi(njia panda ya kwenda kigoma),nyakahura,ngazi saba(balaa tupu hapo),zero zero(njia panda ya kwenda Ngara na Rusumo Rwanda)yaani hata ukiwa na escort ya polisi hawa jamaa majambazi wakiamua kufanya unyama wanafanya tu kama wao ndo wenye nchi,nimepita hizo njia takribani miaka 10 sasa sijaona mabadiliko makubwa yenye matumaini zaidi ya ahadi kibao toka jeshi la polisi ktk kuimarisha ulinzi,imefika hatua unaposafiri atleast lazima uwe na kiasi fulani cha pesa ili mkisimamishwa uwe na cha kutoa ili usipate adhabu toka kwa mafirauni haya ambayo kukutoa uhai kwao ni kitu kidogo sana.kuna umuhimu nadhani sasa kwa nchi hii kugawa madaraka kwa kanda ama state kama USA ili kila state iwe na utawala wake kamili nadhani unaweza kusaidia kiasi kwani kila kitu kutika Dar tu huku mbali na Dar inakuwa shida sana katika utekelezaji,kwani pesa zote inaonyesha kama ziko Dar.kwahiyo mikoani hali ni mbaya sana na ndo maana maasi hayapungui hata kidogo,Nawapa pole sana hii familia kwa janga hilo lakini Mungu yupo pamoja na wewe ktk maisha yako,tunakuombea upone haraka na familia yako.ushauri tuulize tukifika TZ toka majuu hasa ktk usalama na namna ya kufika ktk vijiji vyetu kwa usalama.mdau wa glob ya bro mich Dar

    ReplyDelete
  17. hao wasiorudi wanategemea nani ataisaidia nchi yao?
    mwaka juzi nilikua uk na kuna group la watu walikua wanavamia vijana na kuwaumiza, uhalifu mbona hata ulaya upo ,ajali za matreni mbona na ulaya zipo kule underground tena london,na kuna rafiki yangu mmoja alipata ajali ufaransa?,nyie wachache malimbukeni wa ulaya msiopenda kurudi kwenu mnaropoka tu,nchi yetu itajengwa na sisi wenyewe,kama wenyewe ndio mko huko mnategemea nani awarekebishie nchi

    ReplyDelete
  18. mwezi ulipita nilikuwa Bongo, wakati natokea maeneo ya kiwalani ndani ndani usiku nikakutana na tuseme maharamia sijui majambazi wenye mapanga wakasema toa ulichonacho nacho, kwa haraka nikatoa bunduki ndogo nikampiga ya mguu liyenikaribia nikamtandika ya pili mwingine aliekuwa karibu anashangaa shangaana panga kwenye mguu. wengine kuona hivyo wakaagusha mapanga yako, wakatawanyika. na mimi nikaondoka taratiibu. unajua saa nyingine inabidi uwe na mguu wa kuku(bunduki) kwa selfdefence na uisajili kihalali.

    ReplyDelete
  19. Ni kweli hata wananchi nao wanachangia, utakuta mtu anamuona mwenzake anaibiwa na hawa wezi wa mfukoni kwenye madaladala, hasemi kitu, au baadae ndio anamwambia kuwa umeibiwa na yule jamaa aliyeshuka.
    Mimi nina imani kuwa sisi raia tukiamua ni rahisi kuwathibiti hawa wezi wa kawaida kuacha hiyo mijambazi inayotumia silaha, au mafisadi wanaiba kitaalamu, kwasababu hawo wezi tunaishi nao na wengine ni watoto wetu na tunajua tabia zao kwanini hatuisaidii polisi wakaswekwa ndani?
    M3

    ReplyDelete
  20. Huyu Peter ni kaka wa Maina M/kiti wa CCM UK.Tunamtakia kheri njema.

    We anony 11:53:00 huu ni wakati wa huzuni kwa familia hii,kama una Beef na mtu subiri saa nyingine.Mie sio mjaluo na kwetu ni Mtwara,mwaka 1997 nyumba YA Huyu bwana London ilijaa makabila tofauti ilimradi ni Wa TZ,hakukua hata na mjaluo wakati huo sasa wewe hako ka group unakokaongelea ni make up facts!!! Roho ya Uasi imekujaa.

    ReplyDelete
  21. Poleeni sana.Pona haraka. Jamaa aliwahi nipokea Readig mwaka 2000 na kunisaidia kununua malori na trekta.Mungu akusaidie haraka.
    Mambo ya makabila yanatoka wapi enyi wa Bongo?

    ABDALLAH JECHA

    ReplyDelete
  22. Mkuu Abdallah Jecha

    Huyo uliyemtaja ndio Peter Owino ninayemjua mimi tangu mwaka 1992.

    Hawa wanaoleta mambo ya ukabila kwenye habari hii wanahitaji maombi na sala.

    ReplyDelete
  23. Pole sana Mungu awalinde, so sad especially watoto..

    Sasa wadau kwanini tunashindwa kuwa na serious discussion. What's the role of the government on this. Wizara ya mambo ya ndani inafanya nini? Polisi na waziri wao Masha wako wapi???
    Yule anayesema kwamba hataki kurudi nyumbani ana point. Kwasababu hali kama hii inatisha na inasikitisha sana.
    Tunahitaji comprehensive solution on this issue, tatizo hili limeanza nikiwa na mdogo na sasa niko 35. Kwahiyo kwenye vikao vya Polisi ina maana haliongelewi???
    This is compteletly BS

    ReplyDelete
  24. Anony 01:54:00 PM ahsante sana kwa taarifa hiyo, Mungu awape wanafamilia hao nguvu na uzima pia wakati huu wa kuuguza majeraha!!

    ReplyDelete
  25. MPENI POLE KWA YALIYOMKUTA, BASI. SIYO KULETA SIASA ZA SIJUI ANASAIDIA MAGROUP YA WATANZZANIA UK. KWANI YEYE AMEKUWA UN? YAANI UKISAIDIA WATU 4, 5 AU HATA 10, TAYARI MNASEMA ANASAIDIA WATANZANIA KWA MAKUNDI? UK IMEKUWA NCHI NDOGO KIASI HICHO HADI MNAKUZA KANAKWAMBA YEYE NDIO KITUO CHA KUPOKEA WATANZANIA? WENGI TU HUSAIDIA WATANZANIA WENZAO, NA HAPA SI PA KUONGELEA.

    PILI, MIE NAKAA USA, UJAMBAZI UKO KILA MAHALI, HUWEZI KUSEMA TANZANIA TU NDIYO INATISHA. UNAYEJIFANYA HUPENDI KURUDI TANZANIA SABABU YA UJAMBAZI, MSHAMBA, HUNA NAULI, NA LABDA ULIKIMBIA TZ MATATIZO FULANI AU ULIFANYA UOVU UKAENDA NJE YA NCHI YAKO.

    ReplyDelete
  26. Familia ya Owino poleni sana. Nitawaombea daima.Bila hata kunifahamu mlinichangia karo ya mwaka wa mwisho form six ilimradi dada yenu rafiki yangu Martha Owino aliwaomba na nilikua nimefukuzwa shule.Nilijifunza utii kwa makaka za Martha waliokuanao kwa kaka yao huyu Peter.Mungu akuponye haraka. Marafiki Martha ameingia Mwanza asubuhi na yuko na mgonjwa.Salaam za kheri simu 0786 200611
    na 0754 302048

    Rahel Msamba

    ReplyDelete
  27. DUH!Kweli inasikitisha! Hata watoto waliumizwa! Bongo tunaelekea wapi?!!! Ninawaombea wapate nafuu.

    ReplyDelete
  28. KILA SIKU TUNASIKIA WANAJESHI WAKIPATA KAMISHENI HUKO MONDULI AU KUMALIZA MAFUNZO YA ULENGAJI SHABAHA KUNDUCHI, KWA NINI BASI WASIPELEKWE KWENYE PORI HILO LA BIHARAMULO / NZEGA WAKAKABIRIANE NA HAO WEHU MAHAYAWANI AMBAO KILA KUKICHA WANAVUA WATU NGUO, KUKATA WATU MAPANGA, NA KUWAIBIA MALI ZAO INASEMEKANA KAMA HUNA KITU UNALAWITIWA HATA KAMA WAKO 20.

    KILA SIKU WATALII WANAIBIWA CAMERA ZAO SAMORA POLISI WAKICHEKELEA HAO WEZI NDIO WANAPANDA DARANA NA KUHAMA SAMORA NA WANAINGIA MAJUMBANI HATIMAYE BIHARAMULO.

    ReplyDelete
  29. Poleni sana , tena natoa pole zaidi kwa watoto na mke, wewe akak Msaidia waTZ umejitakia na nime chukizwa sana na huyu Mr mhanga wa hili shambulio kwa kuhatarisha maisha ya watoto wake na mkewe kwa kusafiri na gari , ni ubahili au ni nini?.kwani lazima watoto waone kijiji ulicho kulia,wakati hali ya usalama hairuhusu?

    Usafiri wa barabara tuu si salama tanzania haswa ukizingatia hizo ajali za kila siku na ujambazi ulio kithiri.
    Kwanini angalau asinge chukua ndege mbaka Mwanza na labda kuchukua usafiri mwingine wa bara bara toka Mwanza?
    Hu ni uzembe na kuto fikiria na kujifanya eti unafurahia road trip wakati mazingira ni ya hatari , utakuta mtu ana safiri kwa basi ndio wa kwanza kuka mbele ya basi kunye seat mabayo ni hatari zaidi, (sisemi kukaa mbele tu ndio hari) lakini ina saidia kupunguza majeraha au kifo,
    Watu muwe makini kabla ya kuamiua jambo haswa unapo husisha fammilia yako ,fanya research hali ikoje sio unajipandia tuu basi or una endesha gari cross country huku hujui kama kuna mazingira gani barabarani, kweli huu ni uzembe na usababishaji w amajeraha na maumivu ya kisaikolojia kwa watoto kusiko kuwa na sababu kweli na hasira na huyu aka Msaidia waTanzania.

    ReplyDelete
  30. JembeulayaAugust 12, 2009

    Nampa pole ndugu Peter na familia Mungu atamsaidia.
    Kwa kweli hii hali inatisha lakini kwa wale wanaosema eti ndio sababu sirudi Bongo ambapo wengi wao wako Ulaya ninawashangaa, pengine ndio kujikomba ama wamelewa na 'mataa'
    Sehemu nyingi za Ulaya na America crime ipo juu kushinda Bongo, Wazungu wana tabia ya kuzibania crime figures zisiingie kwenye national or international mainstream news, kwa sababu wanaelewa zinatoa sura mbaya kwa nchi, ukweli ni kwamba nchi hizi mfano hapa nilipo UK kwa siku wanajeruhiwa ama kuuliwa zaidi ya watu 10 kutokana na vitendo vya uhalifu ila kama wanavyosema wenyewe "those news will never grab the front pages or headlines" kwa sababu zinaleta picha mbaya kwa nchi, utaziona kwnye local news tu.
    Kwa hio tujaribu kuwa na balance na tuwe wakweli.Hivi kwa siku matukio kama haya mangapi yanatokea Bongo?
    Personally I can walk the streets of Dar at late night but I can't walk the streets of Peckham or Hackney in London at night.

    ReplyDelete
  31. Kama tungekuwa na sheria uiuwa nawe uliwe basi ingekuwa salama tupu hakuna muda wa kusubiri imebainika umeuwa kwakukusudia basi na wewe hakuna haja kuwepo kwani kupelekwa jela ni sawa na kuzidisha machungu kwa wapenzi wa aliyetoweka kutokana na wao wanatakiwa kumlipia mfungwa ambae amemtowa roho kipenzi wao akiwa jela kwa mana nyingine ni tax yako inamhudumia yeyey kuwa kule jela.

    ReplyDelete
  32. Pole bwana Peter Mungu awape uponyaji.

    Anon wa 11.53 binadamu ni binadamu. Alieandika ujumbe hakusema mambo ya kabila hapa. Na wenye kuelewa wameelewa.

    ReplyDelete
  33. Jamani kwanini mnatumia magari kusafiri usiku wakati ndege siku hizi zinatua mikoa yote mikubwa.Hata kama haitui kijijini kwenu ukishatua mkoa wa karibu halafu utafanya mpango ufike kijijini kwenu. Msijidanganye ooh mimi m/kiti CCM ulaya hawatanifanya kitu, watu wana njaa wako tayari hata kumuharibia JK kama akikaa vibaya. Ajira hamna watu wanataka mambo makubwa wakae bar wanywe kila jioni sasa unazani hata ukiwa kwenye system ukikaa vibaya watakuacha. Cheap is expensive. Tumieni usafiri uliosalama

    ReplyDelete
  34. Mungu awaponye Inshaalah!

    ReplyDelete
  35. Muuza sura aache kuwa mgeni wa heshima kwenye u-miss huko na kupiga konozz na vimwana mnamwambia wizara yake ikashugulike na majambazi huko nyie MMEROGWA NINI!!!??Tena majambazi yenyewe mkoani sio dar hehehe......ALAHUAKBALU

    ReplyDelete
  36. I think there is a need to Airlift Owino, if necessary, to South Africa, Nairobi or back to UK for immediate medical attention.

    The family may need to think about that, at the moment!

    US

    ReplyDelete
  37. Ni kweli ina katisha tamaa sana kwa mtu aliyeko nje ya nchi kuona unyama kama huu waweza kumkuta akirudi home. Wabongo tujitahidi kuelewa na kutambua fikra za watu wengine, mpo mnaoona kuwa suala kama hili kumtokea mtu ni jambo la kawaida na haliwezi kuwafanya mkate tamaa ya kurudi home na vilevile wapo wanaoona kuwa hii ni issue ya hatari kwa maisha yao na kuingiwa na woga kabisa wa kurudi home.

    Nyumbani kweli ni nyumbani lakini si lazima iwe nyumbani daima hasa mtu unapokuwa mtu mzima na una uwezo wa kuchagua wapi panakufaa kuishi na wapi hapakufai, sababu zipo nyingi zinazoweza kumfanya mtu akajisikia salama zaidi mahali fulani na si pengine.

    Tusipende kutukana watu wengine kwa kuwa tu hawana fikra kama zetu au hawawezi kung'ang'ania kujifanya wanaipenda bongo ili hali nchi yenyewe inawachefua tu. Si lazima pia kwa kuwa ulizaliwa Mtanzania basi ubaki kuwa mtanzania daima, una uhuru wa kuamua kuwa raia wa nchi nyingine yeyote ile hapa duniani unapoona panakufaa na si vizuri kulable mtu kuwa ni mpumbavu kwa kuwa eti anaeleza ni kitu gani kinamfanya aamue kutorudi Tanzania. Kama nchi inanuka inanuka tu hata muwalazimishe watu waone nzuri kwa kuwatukana na kuwapa majina yasiyofaa, bado inanuka tu. La msingi ninyi mlio bado na usongo sana na Bongo, irekebisheni ili ivutie na wengine wasio wabongo waone ni nchi safi na yenye usalama na inayojali wananchi wake.

    Watanzania acheni unafiki na longo longo, muda wa kuficha ficha mambo umeisha hakuna anayenufaika na nchi hii zaidi ya baadhi ya viongozi wa serikali na mafisadi wao, hakuna, wengi wetu ni vidampa tu wa hao niliowataja.

    ReplyDelete
  38. loh Jamani mliosaidiwa na PETER OWINO sioni hata mmoja akiulizia namba ya account ya benki kwa ajili ya msaada kwa majeruhi maneno meengi!!!
    eti mungu awajalie wapone haraka wakati mmeambiwa kaibiwa kila kitu mpaka lishe za watoto!!!

    ReplyDelete
  39. Ni kweli kama wanavyosema baadhi ya wadau kuwa ujambazi upo kila mahari duniani, lakini kwa njia ya hii ya kati,kuanzia pale manyoni, kahama , mpaka biharamulo haa ni balaa kabisa. ukiwa ni msafiri wa mara kwa mara nadhani utaelewa ninachokisema. hari ni mbaya sana.
    Uwa nakosa raha kabisa kuanzia kahama kuelekea biharamulo,hakuna usalama wala amani. muda wowote mnaweza kuvamiwa na kuporwa vitu na mali mbalimbali na fedha na kibaya zaidi ni kupigwa kwa mapanga na mbaya zaidizaidi ni kuvuliwa nguo na watu kufanyiwa matendo yasiyofaa.
    Kamanda Tossi alipokuwa mkuu wa polisi mkoa wa kagera alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matendo haya lakini tangu kuhamishwa kwake hari bado ni tete.

    ReplyDelete
  40. Anony 10:20:00 AM umeongea jambo la mbolea kweli ambalo wengi wetu tumekuwa tukilizungukazunguka. Si wale tu waliosaidiwa na OWINO bali pia kila mwenye kuguswa na jambo hili linalotia simanzi kwa wote wapenda mema.
    Ningependa basi jambo hili kwa wale mlio UK msilichukulie ki-CCM, bali kijamii ili watu wote tupate kushiriki kutoa michango yetu. Kwa walio-TZ hao sina shaka nao hasa JALUOs (Watani zangu) nawaaminia watawajibika vilivyo na kutimiza wajibu wao.

    ReplyDelete
  41. kumi ishirini (10:20)umeongea neno la maana owino anahitaji msaada wa hali na mali watanzania kila mwenye nacho kitu kidogo asaidie

    ReplyDelete
  42. TUTAKUJA KUJENGA KIKUNDI CHETU BINAFSI TUPAMBANE NA HIYO MIJAMBAZI, KWA KWELI INAUMA SANA KWANI UKIANGALIA HUKO UPANDE WA WA POLISI TUNAOTEGEMEA KWA ULINZI NDIO KUNAONGOZA KWA UJAMBAZI SASA TUKIMBILIE WAPIIII????? KILA MKOA UNA KAMBI ZA JESHI SI CHINI YA 5 MNASUBIRI NINIIII????? MNASUBIRI VITA MKAPIGANE???? MNAKAA KAZINI MPAKA MNAZEEKA HAMJAWAHI KUPAMBANA VITA KWANZA FANYENI MPAMBANO NA MAJAMBAZI JAMANI AU VITA HII HAMUIONI?????? MNASUBIRI VITA GANI TENA????? MBONA RAIA HAWANA AMANI KUTWA TUNATANGAZA NCHI YETU INA AMANI AMANI HIYO NI IPI MBONA SIWAELEWIII????? WATU WANAPIGWA MAPANGA NA WENGINE RISASI NA MALI ZINAIBIWA WAKUU MATUMBO JUUU HATA KUKIMBIA HAMUWEZI TULETEENI AMANI YA KWELI TUNAWAOMBA AU KWAKUWA NYIE MPO NA AMANI NA FAMILIA ZENU NDIO HAMJALI YA WENGINE???? MUNGU AWAPATIE UZIMA NA UVUMILIVU MLIOATHIRIKA SIKU MOJA ATAWALIPIA KWA HAO MAJOKA WATU....mdau uholanzi

    ReplyDelete
  43. Pole sana ndugu owino na familia yako , Mungu awajalie mpone haraka. Jamani nyumbani kunatisha kiasi kwamba mtu unaogopa hata ukianza kufikiria kuja likizo. Kusema kweli pamoja na wadau kusema uhalifu uko kote duniani tena labda ughaibuni ni mwingi zaidi, lakini kuna tofauti kubwa bado mtu unaweza kujisikia salama zaidi huku, sababu kuna polisi wanaofanya kazi zao, while huko nyumbani polisi kujakuwaokoa sahau. Pili uwezekano wa wahalifu kukamatwa na kutiwa mikonononi mwa sheria ni mkubwa kompea na nyumbani, na hilo la kuwa huku na kujua polisi watakuja any minute kukuokoa linakupa hata nguvu ya kupigania uhai wako ukiwa na mwanya cause unajua help is on the way right away, huko jaribu uone, ndo maana hata magari mengine au hata kama ni basi watu wanashindwa cha kufanya zaidi ya kukaa na kusubiri zam yako ya kukatwa mapanga kama nyama buchani ifike.
    sasa kwa vile serikali yetu haijihusishi tena na usalama wetu, labda ni wakati wananchi wenyewe tuwe na mikakati ya nini cha kufanya tukisafiri kwa mabasi kina kaka na kina baba bebeni pocket knives, au hata visu vikubwa uwe benet nacho, na hata kina mama pia, bebeni hata pilipili ya unga ya kuwamwagia osoni hata mchanga! seriously, inasikitisha kuona basi lenye abiria 60 wanatekwa na majambazi 6 au hata kama 10, may be wana bunduki au ni mapanga tuu, na watu wanashindwa kabisa kufait back, this is a matter of life and death either ufe wewe au afe yeye, msikubali roho zenu kuondolewa kirahisi hivihivi, hata ukifa katk kujipigania uhai wenu ondoka na mmoja wao! u will be a hero na utakumbukwa 4rever kwa ushujaa wako.
    Ingefaa pia kabla basi halijaanza safari kuwe na tangazo kwa abiria wakishakaa kwamba jamani in case of this hapning to us, we must fight for our lives! Manake serikali haijihusishi tena sory 2 say that but we hav to find our own solutions, cause this is sickening now!!!
    New York NY

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...