Bwana arusi aliyeshika kidevu akitafakari gia anazoingilia kwa wakwe zake kuja kupata mwenza wa kwenda kushea nayefunga ya Mwezi Mtukufu na futari
Bwana Nanihii,
Wape michapo wana globu yetu ya jamii, matayarisho ya Ramadhan yamepamba moto hapa Zenj, harusi kila kichochoro hapa kwetu watu wanataka wakapikiwe futari

Wapambe wa Bwana harusi wanaingia kuja kuchukua mwenza wa mwenzao.

Bahatia mbaya hatuna mafunzo ya upigaji picha kwani gari lilishika mwendo wa kasi nasi tumekosa kupata taaswira ya bi arusi ndani ya limo lake (mwenye pink) Msafara unamwaga vumbi tayari kwenda kuanza maisha ya bibi na bwana.
Tuwatakie maisha ya kheri na salama, baraka na furaha tele AMEEEEN
---------------------------
GLOBU YA JAMII INATOA PONGEZI KWA MDAU WA ZENJI KWA TASWIRA HIZI MURUA, NA TUNATARAJIA NYINGI ZAIDI (ZA KIGOMA CHA DAKU NA FUTARI) KUTOKA KILA PEMBE YA DUNIA, KADRI SIKU ZINAVYOKWENDA KWENYE MWEZI HUU MTUKUFU AMBAO PANAPO MAJAALIWA CHUNGU MOJA TWAIANZA KESHO.
GLOBU YA JAMIIU INAWATAKIA WADAU WOTE POPOTE MLIPO DUNIANI RAMADHAN KAREEM NA INSHAALLAH MOLA ATATUAFU TUANZA NA TUMALIZE SALAMA.
-MICHUZI







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Poor Cow , Animal Brutality waswahili bwana.

    ReplyDelete
  2. kaka mambo hayo ya zenji hakika ndoa raha yake siku hizi mambo ya mifugo kutumika kama limo nimeona kwa Iren uwoya lakini sasa hii tamu zaidi nature zaidi mungu awabaliki wote mfungo mwema kwa wale wenye imani ya kiislamu,ahsante kaka

    ReplyDelete
  3. limo ja kimaskini

    ReplyDelete
  4. bibi harusi kanona huyo...mmh ama kweli wakubwa hufaidi...ndio maana huku denmark kumbe wameamua kupiga marufuku vazi la hijab ili watu wasafishe macho

    ReplyDelete
  5. hayo ndio mambo ya kiyakhe harusi kwa n`gombe kama chai kwa haluwa asiule mchana mwezi mtukufu huu

    ReplyDelete
  6. Bro michuzi hii kitu bomba kweli, atleast they'r not ashamed of it. Nawatakia watu wooote popote pale walipo, ramadhan kareem, m/mungu awajalie faraja funga zenu zikubalike inshallah kheri.

    ReplyDelete
  7. wewe mkavirondo huko juu kabisa, huyo ni punda na punda ni mnyama mwenye uwezo wa kufanya kazi za nguvu. Ya waswahili waachie waswahili na sisi waswahili, tutawaachieni yenu ya kikavirondo.

    Kumbuka, limo ni za kidhungu na wala siyo za kikavirondo. jiulize huko kweni ukavirondo (Kilimanjaro, mbeya, iringa, Rukwa, Bukoba, Sinyanga, etc) watu wanaoa kwa limo? au mnajifanya vitu vya wenzenu mmevizoea sana?

    ReplyDelete
  8. Anonymous 10:45:00 AM hapo juu, umeandika kwa jazba namna hiyo na kumbe macho yako hayaoni sawasawa! Una uhakika huyo ni punda? Nadhani hata punda huwajui wakoje!

    ReplyDelete
  9. kaka wa 4 embu kuwa makini kidogo hapo hakuna hijabu kaka naona unasahau mila uku ketu africa mwali ufunikwa na khanga kitambaa ili pale anapokuwa ndani kumfunua lazima umlipe bibi yako au mke wa kaka ako naomba tusisahu mila hata wazungu wana mila zao tusiwe kama wamarekani ambao hawana mila kwasababu wazawa washafukuzwa waliobaki ni wahamiaji tu.

    ReplyDelete
  10. KAKA MICHUZI HII NI RAHA SANA HAO WANAONGEA NEGATIVE INAWATOUCH NA NDIO MAANA WANACHONASANA.
    MAANA WAKIKUMBUKA KUA MIJANA JIKE YAO HAINA REALLUV WAPO KWA AJILI YA VIJISENTI VYAO MBUZI NA VIGARI VYAO MCHWARA WALIVYOVIPATA KWA UFISADI YANI KWA DHURMA YA KUIBA HELA MPAKA ZAWAKULIMA NA WAUZA KARANGA.
    SASA WAKIONA KULE KWENYE MAHABA MTOTO MZURI YUKO RADHI APANDE GARI YA NG'OMBE KAMA TUONAVYO KULIKO KUPANDA BENZI LAKO LA KIFISADI,YANI YEYE ANAFATA REAL LUV,NYINYI WAKWENU VICHUI KAZI YAO KUCHUNA NA KUBABAIKA HAWAJUI UTU WAO.

    KTK HOJA YA KUSEMA KING'OMBE ZAIFU WASWAHILI BWANA HIYO NI WIVU TU MAKWENU HUKO HIVO VIJING'OMBE MNAVILIMISHA EKA MIA NA NYINYI WENYEWE MMECHOKA ILA MNASURUBIKA HATA MAJI SAFI YA KUNYWA HAMNA!!SASA KAMA NYINYI WAZUNGU KWANINI MSINGELIMA KWA KUTUMIA MATREKTA?
    MNAITIKADI ZA KITUMWA WA KIMAWAZO NA MASKINI WA KIFIKRA NA KIROHO!!NDIO MAANA KABLA YA KUINGIA MADARAKANI MAKWENU MASKINI KABISA ILA MKISHAINGIA MNATAKA KUIBA ILI MKAYAONGE HAYO MACHUI!!WENGINE MPAKA LEO HII BADO MWALALIA VIBANDA VYA MAVI YA NG'OMBE.
    WATUMWA WAKIMAWAZO MNAJIONA WAZUNGU WEUSI!!HAYA HUYO MZUNGU ANAUTHAMANI GANI ZAIDI YA KUJIENDELEZA KWA KUTUMIA MABAVU§§YANI HANATOFAUTI NA MTU ALIETAJIRIKA KWA UJAMBAZI AMA UFISADI.
    ACHENI UTUMWA WA KIMAWAZO

    ReplyDelete
  11. hivi rubani anaona mbele kweli? maana kofia imemfunika kabisa uso wake!!

    ReplyDelete
  12. wewe uliyemwita mwengine mkavindoro ni bonge la "K"

    Yaani Kinyesi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...