Unajua kaka Michuzi sisi watanzania tumezidi kunyanyasana wenyewe kwa wenyewe!! Majuzi nililalamikia utaraytibu mbaya pale DIA (Mwalimu JK Nyerere Airport), then nilichangia kuhusu matatizo yanayotokea Bandarini Dar, hivi ninavyoongea nimeagiza gari kwa ajili ya matumizi ya familia, for my poor mother, gari lenyewe thamani yake ni dola 4000 (CIF) hadi Dar, wajapani wamenitumia invoice (tena zimetumwa moja kwa moja Dar, nimeshtuka sana na taarifa toka TRA, wansema eti documents ni feki!! KENI YUU IMAJINI ZISI???
Naambiwa gari ya dola 4000 (mwaka 2001, cc 1500) natakiwa nilipe MILIONI TANO!!...Sababu ni kwamba documents ni feki!!! Sasa jamani twende wapi?? Kama nimetumiwa invoices toka kampuni iliyouza gari yenyewe kwa nini Watanzania wenzangu wanalazimisha kuwa hiyo gari siyo bei yake??
Huu si ni wizi mtupu jamani?? Mimi nipo tayari kuwapa hao TRA na wengine wanaohusika contacts za kampuni, wao wenyewe wafuatilie, kama kweli ni feki mimi nitalipa hat amilioni 10 kutoa gari bandarini, lakini nasangaa sana kuona unalipia gari almost zaidi au sawa na bei ya kununulia??
Hapa watanzania tunaumizana wenyewe kwa wenyewe na kwa kweli mimi naona si haki!!
Kaka michuzi hebu naomba msaada tutani, nirushie hii kwa wanaohusika, lakini to be honest sasa hivi nitahakikisha kilio cha wengi kinafika kwa mheshimiwa JK, ama sivyo wanyonge tumekwisha dunia ya leo! KHA!!!-
Mdau Selu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 64 mpaka sasa

  1. Miaka mingi iliyopita kulikuwa na Mr. Mchata kama mkuu wa Anti Corruption. Ulikuwa unapeleka kesi kwao, wanakupatia cha mbele na unawapa hao watakao rushwa. Wakistuka wako OB (lupango). Siku hizi hakuna mpango kama hii? Mie nitakufa na mtu. Na msidai kuwa namzibia mtu ridhiki yake: unajua nilivyupata hii pesa?
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  2. Pole sana kwa mazabahu yalikukuta,kuna namba ya Kawambwa pale wizarani kam iko ngumu au upendi ukifanikisha yako tumia bandari ya Mombasa

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu pole sana, nalia na wewe.
    I am not surprised at all, yaani hiyo ndo Tanzania yetu. Kama hutoi rushwa basi utapigwa namba za ajabu ajabu mpaka ukimbie.
    Mwaka 2007 niliagiza vifaa vya ujenzi ya nyumba na vitu vingine vya kutumia ndani kama friji na majiko. Gharama ya kila kitu ilikuwa kama milioni saba.
    Nakwamba vilivyofika, nikaenda ofisini TRA. Kwanza nikazungushwa zungushwa, nikiingia ofisi wanasema ingia ofisi ile.
    Baadae ofisa akakaaa kwenye computer muda mrefu, akasema wameshindwa kupata originality ya vitu vyangu. Kwanza sikuelewa, nikasema nina original receipt. Na I swear to God, nothing was forged.
    Baadae akaingia ofisini kwa mkuu....nafikiri ni menaja. Alivyotoka akasema natakiwa kulipa million kumi.....nilipe million kumi kwa vitu vya milion 7.
    Niliwatupia makaratasi nikasema vitu watavitoa na milion kumi silipi.
    Nikaandika barua kwa mkuu wa TRA...nilikuwa napiga simu almost everyday...Baadae wakaniita nikaripa milioni moja na..
    Kwahiyo itabidi ukomae nao....don't let them get away with it.

    ReplyDelete
  4. Mdau pole sana , hiyo ndiyo Tanzania nchi ambayo Mheshimiwa sana Michuzi anaisifia ya kuwa mambo tambarare! Inasikitisha sana , Rushwa imekuwa ni part and parcel ya maisha ya mtanzania.

    Watanzania wengi siku hizi wanapitisha magari au mizigo yao Mombasa, kwani hawawezi uswahili wa hapo Dar. Lakini hata hao nao cha moto wanakipata wanapofikisha mizigo hapo horo horo , kwani kuna urasimu wa ajabu.

    Mungu tuu atunusuru , ila kama serikali aitalitatua hili la rushwa basi...

    ReplyDelete
  5. KAMA SIJAKOSEA
    SI ULISHAURIWA UTUMIE PORT YA MOMBASA? NINI TENA UNALALAMIKA NA HAUNA MTU UMJUAE AKUSAIDIE HUKO TRA MAMBO YAENDE KIKAWAIDA?

    HIVYO NDIVYO WANAVYOKULA PESA ZA WATU

    SASA ITABIDI UWASILIANE NA KAMPUNI YAKO UWAAMBIE WALICHOKUAMBIA TRA AS WAO BUSINESS MBELE WANAWEZA INGILIA ILI WASIARIBU JINA LAO LA KAMPUNI NA SIDHANI KAMA WATATAKA TRA KUWAARIBIA JINA

    HAYA TUAMBIE INAVYOENDELEA NAO NA WENGINE WAJISAIDIE

    ReplyDelete
  6. TRA WANAMATATIZO SANA HAPO KAMA UNAWEZA HAKIKISHA UNARUDISHIWA DOCUMENT WANAZOSEMA NI FEKI PIA UWAOMBE WAKUANDIKIE KIMAANDISHI KUWA DOCUMENT HIZO NI FEKI, KISHA COPY MFIKISHIE RAIS NA NYINGINE FUNGULIA KESI MAHAKAMANI UTARUDISHIWA PESA YAKO.NA HAKI ITAPATIKANA NI HIVYO NDIVYO WAGHANA WALIPIGANIA HAKI YAO SASA MAMBO KWAO NI MSWANO TU.

    ReplyDelete
  7. MAMBO MZEE HAYA MAMBO KWELI YANAFANYIKA PALE DAR MIMI MWENYEWE NILISHAWAHI KUAGIZA GARI IKALETWA UBABAISHAJI WA KIAINA WAKAJA BAADA YA KUTOA GARI WAKA REISSUE INVOICE ETI GARI ULIYOTOA ILIKUWA NA THAMANI KUBWA ZAIDI NIKAIPELEKA HIYO INVOICE PALE KWAO WAKAIFUTA WAKA KAA KIMYA LIKAISHA,HAPO NILITUMIA CLEARING AND FORWADING,SASA UCHUNGUZI WANGU HAWA JAMAA WA CLEARING NDIO WABABAISHAJI WAKUBWA WANASHIRIKIANA NA WATU WASIO WAAMINIFU PALE TRA WANAKUSUMBUA HIVYO ILI UTOE RUSHWA WAO WAFAIDIKE ZAIDI,SASA NIKUPE USHAURI KAMA UNATAKA KUWA NGANGARI KAMA INVOICE YAKO NI HALALI HUNA HAJA YA KUONGEZA HATA CENT MMOJA KWENYE HIYO OVERPRICED INVOICE,CHA KUFANYA WEWE WAAMBIE HULIPI KAMA WANATAKA WA PROOF NA KAMA NI KWELI WAKUPELEKE MAHAKAMANI KWA FRAUD HIYO CRIMINAL CASE,HALAFU KIUTATARATIBU COMMISSIONER ATAKUWA RESPONSIBLE KWA GHARAMA ZOTE ZITAKAZO ONGEZEKA KAMA ITAONEKANA YEYE NDO MWENYE MAKOSA,AU MBADALA WEWE UNAWEZA KUONGEA NA MWANASHERIA PALE DAR WAAMBIE JAMAA WAKUPE BARUA YA MAANDISHI KUWA INVOICE YAKO NI FAKE,KAMA UKIOGOPA USUMBUFU WEWE WAWEZA LIPA UNDERPROTEST HALAFU UNAKUJA KU CLAIM ILA HIYO NDO INABIDI UMTAFUTE MTAALAMU WA SHERIA ILI AKUPE NAMNA YA KUPATA VIAMBATANISHO VYA KUJA KULALAMIKA KWA COMMISSIONER,ILA KOTE HUKO NI MBALI SANA WEWE KAMA UPO DAR AU KAMA KUNA MTU YUPO PALE DAR UNAENDA PALE KUMWONA COMMISSIONER KWANZA,AU BOSI WAO PALE ITAKUWA NJIA RAHISI ZAIDI IKISHINDIKANA NDO UJARIBU HIZO PROCESS ZA JUU HAPO WAKUPE BARUA YA MAANDISHI UWAELEZE KWANZA NI DEFAMATION KWAKO KWA AGENT KWAMBA WEWE UNA FANYA FRAUD KWA KWELI KUNA USUMBUFU MKUBWA PALE

    ReplyDelete
  8. Pole mdau Selu ila huo ni utaratibu wa kawaida kutathmini thamani halisi ya gari hata kama uligaiwa bure huko japani basi inabidi wapige hesabu. Siseme kwamba hiyo milioni tano ulioambiwa ulipe ndio kiwango sahihi kwa vile sielewi wanacalculate kwa kutumia vigezo gani. Its unfortunate kwamba wewe umepeleka document halisi na wamekwambia ni fake, ila hii inachangiwa na jamii yenyewe kutokua na uaminifu hadi sasa kila mtu anakuwa doubted.

    Binafsi nishaenda kununua gari dubai mara mbili, bila kuomba unapewa risiti moja inaoyoonesha bei halisi na nyengine unapewa haijajazwa bei ila ina stamp tu ya showroom ulinunulia. Hiyo ya mwisho vijana wanaitumia kama changa la macho hapo TRA au kama mtu aliagizwa hilo gari na mtu mwengine ndio anapatia ulaji hapo kwa kuongeza tu dola twa juu.Sina uzoeefu wa huko japani ila inawezekana sana huu mchezo upo ndio maana hao TRA wanashindwa kutambua nani mkweli nani muongo.

    Hizi tabia mbaya tunazilea sisi wenyewe kwenye jamii na mwisho wake ndio huu wanachanganywa waliomo na wasiokuwemo. Nisawa sawa na hii kasumba ya al qaeda au terrorism na uislam, unatusababishia inconvenience waislam wengi sana tukipita airports za kimataifa, especially kwa wale wenye asili ya kiarabu wanatiliwa shaka sana.

    Ila kwa upande mwengine, hao jamaa wa TRA au mamlaka kama hizo wanautamaduni wa kubambikiza watu hizo bei za ajabu ili ushindwe kulipa kihalali ulazimike kwenda chini ya meza ufisidiwe mradi utapata nafuu. Ni dillema kwa kweli, hebu niambie wangapi watamudu na kuwa tayari kulipa viwango vya juu kama hivo kama kuna option ya kupewa unafuu, tutaishia kuliwa tu.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  9. iI HAVE BEEN A FUN OF THIS BLOG FOR A WHILE EVEN THO' I DONT REALLY GET TO GIVE MY OPINIONS ALL THE TIME I FIND IT INTERESTING THAT AS TANZANIAN LIVING OVERSEAS OR NYUMBANI WE ALL ARE FACING THE SAME PROBLEM 'WAFANYAKAZI WA SEREKALI' POLISI POSTA ,BANDARINI UHAMIAJI KILA MAHALI NI SHIDA TUPU HAWA WATU WANALIPWA JUST LIKE MKULIMA AKIUZA KAHAWA OR MFANYAKAZI WA BENKI BUT HUKO BENK UKIENDA KILA KITU NI RAHISI HAKUNA CHA NIPE POSHO ETC THE POINT IS KAMA HUYU KAKA KANUNUA GARI YAKE $4000 THEM HE SHOULD ONLY HAVE TO PAY TAX ON IT NO MATTER WHAT THOSE GUYS BANDARINI THINKS IT COSTS ITS NONE OF BIASHARA YAO KUMWAMBIA YEYE HAKULIPIA THAT MUCH ...KAMA WANATAKA HELA ZAIDI WAFANYE KAZI YAO LABDA WATAPEWA RAISE...... ONCE AGAIN KAMA WATU SISI WATU WADOGO NDIO TUNAZIDI KUNYANYASWA...IM SO SICK OF IT AND YOU SHOULD TOO..... WHAT ARE WE GOING TO DO TO STOP THIS ?!

    ReplyDelete
  10. Once and for all lazima huu ufisadi uishe na ndugu sio peke yako wengi tumefanyiwa sana huo mchezo na cha ajabu hapo wanataka kitu kidogo,hawa wapuuzi hawana clear standard ya kufanya kazi zao zaidi ya ubabaishaji tuu,hii issue tunaomba mlio karibu na JK au Waziri mkuu mkisoma humu wapelekeeni moja kwa moja na huu uwe mfano wa hawa mafisadi wala rushwa..pole sana yaani natetemeka hapa kwa hasira maana hii game ya kila siku hapo bandarini,Michuzi tunajua unaweza kuongea hata na Raisi au wasaidizi wake wampe hii issue aiangalie mwenyewe.

    ReplyDelete
  11. Msanga LupaloteAugust 18, 2009

    Haya si ndio yayale aloyosema mzungu...wizi mtupu Bongo...Tatizo ni kuwa na watumishi wa umma wanaoona kama vile kufanya kazi yao ni kukusaidia...na wanataka uwakisi matako ili wafanye kazi zao. Huu ni ujinga kabisa...kama hawaamini hizo risiti si wawapigie simu wajapani...Aaaahhhh...bongo.

    ReplyDelete
  12. Gari unanunua mnadani hao TRA wanapanga bei yao utafikiri walikuwepo wakati unabid. Hayo yalinipata hata mie.

    ReplyDelete
  13. Pole Mdau!

    Usidhani Wakuu hawafahamu hayo. Wanafahau sana, tena siku nyingi. Kuna Kampuni kubwa za kuuza magari kukuu Japan zimewahi kutoa tamko na kufuatilia kuhusu suala hilo mwaka 2007, lakini wapi. Tatizo nadhani ni hayo makampuni ya kifisadi yaliyopewa tenda za ku 'process' sijui na TRA au na nani, na nadhani hupata percentage ya makusanyo! Pia pale Longroom, mpaka JK aliwahi kupiga mkwara pale, nadhani 2008 katikati. Sasa kama mkuu wa INJI anaweza kupiga mkwara wa kufa mtu, kusiwe na mabadiliko, wewe ni nani? Chelewachelewa na uone 'storage charges' zinavyo 'accumulate'. Tena unaweza kutoa gari haina hata tairi na...

    ReplyDelete
  14. isije ikawa kampuni kweli iko japan lakini ni ya wanaijeria kama richmond ilikuwa iko marekani lkn wamiliki ni watanzania pyuaa mmoja toka arusha na mwenzake twammezea..ila pole dada nchi nayo ina laana hii bongo

    ReplyDelete
  15. Ndugu yangu utahangaika bure tu,hata JK ukimwambia haisaidii,nina uhakika anajua kila kitu,haiwezekani institution kama TRA wanafanya mambo yao kisanii sanii tu,hakuna uwazi,haiwezani raia mpaka unaagizia gari wala hujui unatakiwa ulipe kiasi gani,unabakia kuomba mungu gari lifike ili ulipuliwe ndo uanze kupalangana kulitoa,ya nini yote hayo,weka flat rate,na ukifika pale looooong room unakuta kila kitu kiwe wazi,waandike kwenye notice board kama ni gari lenye ukubwa flan na la mwaka flan ni shs flan za kitanzania,kwishaa,mambo yangekua poa,lakini tunabakia kuishi kwa kubahatisha bahatisha tu,hii sijui mpaka lini wallah,haya MANYANG'AU haya yatatumaliza kabisa.

    ReplyDelete
  16. Kweli TRA na bandarini kwa uzima wamezidi. Hata mimi yamenipata kama hayo hayo hivi karibuni. Kweli kama malalamiko haya yatafikia wahusika wakubwa - (Rais JK's goverment), na wakashughulika, italeta picha ya maendeleo na mabadiliko sana nchini kwetu. Otherwise neighbouring countries watazidi kufaidika.

    ReplyDelete
  17. We kwanini ununue vitu nje ukiijua nchi yetu ilivyo? Wengi ukiwaambia huwa tunanunua magari $1000 wanashangaa na hawaamini.

    Kama ulitaka gari ungenunua ndani au achana na masuala hayo kabisa.

    Hata ulalamike mpaka kwa JK haisaidii.

    Na bado 50%.

    Hivi bado kuna watu wanatuma magari bongo pamoja na lawama nyingi hivyo za wadau waliolizwa mamilioni ya kugomboa na rushwa juu?

    ReplyDelete
  18. Mwishimwa Michuzi sasa nnaomba kuuuliza kama huyo naye ni Mzungu !! kwa sababu yule Mzungu alipolalamika Watanzania wengine wanasema oooh mbona hata JFK mizigo inapotea !! Sikatai mizigo kupotea, mizigo hupotea makhali popote pale lakini JFK HAWAIBI NA POLISI HAKUOMBI DOLLARI MIA TANO ILI WAFUATILIE VITU VYAKO. !! Na hata hivyo huyo Ray alisema walimwimbia vitu vyake ndani ya begi na si begi lote.

    Na hata mambo ya Forodha pia ni kweli alivyokuwa anasema hasingeweza kubuni vitu vyote hivyo ! Haya na huyu sasa naye ni mbongo atakuwa anaisingizia TANZANIA ??
    Haya ni mambo yanayokera sana na yanatakiwa kupatiwa UFUMBUZI.

    Haya Mr. Michuzi weye upo kwenye magazeti ya serekali haya malalmiko myaweke ili hao wanaojiita wakhshimiwa wayasome.

    Kila la kheri na ni AIBU SANA.

    ReplyDelete
  19. WADAU HUKU NILIPO NI SAA TISA USIKU NAFUATAILIA MAONI YA WAZALENDO WENZANGU!! ASANTENI SANA; MAPAMBANO NDIYO YAMEANZA SASA, HII ITAKUWA NDIYO LANDMARK NA KIKOMO CHA WIZI HUU NA UNYANYASAJI ULIOKITHIRI. NSAHUKURU KWA MAONI, SASA NAANZA KAZI RASMI YA KUKOMAA KWA KUFUATA UTARATIBU!! KWA KAMISHANA WA TRA NAKUTUMIA SALAMU.....

    ReplyDelete
  20. Mzee utalia sana lakini wa kukusikiliza hakuna.najua inakuuma sana tatizo ndugu yangu hakuna wa kukusikiliza au kukusaidia.Kama serikali yenyewe imeshindwa kudhibiti mafisadi je unafikiria watakuwa na muda kufuatilia mambo kama hayo?inauma sana mtu unajifunga mkanda kutafuta maisha lakini watu wengine wanataka kufaidika kupitia migongo ya wengine.Huu ulimbukeni wa kutafuta utajiri wa haraka ambao haufai hata kidogo.pole ndugu hicho ni kilio cha samaki.Posta nao wamekuwa waizi wakubwa,uwanja ndege tena vitu vinapotea,TRA unadaiwa mlungula mkubwa kuliko thamani ya mizigo yenyewe na serekali wanaliona hili lakini wanalifumbia macho.unakumbuka ile ishu ya mtoto wa jk?mabegi yalipotea kiaina lakini yakapatikana baadaye.wapiga boksi wasio kuwa na wazazi wenye influence kwenye system wamekuwa ni victims wa hii situation.Basi ndugu fight for your right,it might very be challenging experience ,incovinient,and time consuming process but remember this..."justice will alway prevails in this broken system"

    ReplyDelete
  21. JK ALITEMBELEA BANDARI NA KAWASIFU KWAMBA ANAJUA WANACHOKIFANYA,NA KAWAHACHA KIMYA.

    ReplyDelete
  22. Watanzania wengi tunapenda kulalamika sana jamani, yani hakuna hata mtoa maoni mmoja ambae ameweza kuja na mtazamo tofauti! Nakubali kwamba serikali na mamlaka zake zinamapungufu ya wazi wazi na ufisadi umeshamiri, ila na sisi tumezidi tena kushabikia haya malalamiko, kitu kidogo tunatupa lawama tu. Wengi wametoa haya maoni hawajawahi hata kuingiza gari hapo bandarini wakaona viwango vinakuwaje, lakini na wao wamo tu watoe dukuduku lao. Mwaka jana nilienda dubai kununua gari ndogo model 1998, nilipata kwa dola 1,850 na nililipia ushuru wa milioni mbili kule zanzibar, hivo naamini hicho kiwango alitakiwa huyo selu kulipa kina karibiana sana na hicho nilipa mimi ukilinganisha na thamani ya gari yangu.

    Tatizo hapa imekuwa kila jambo tunatafuta mchawi na serikali ndio tunaitupiya kila lawama. ndugu yangu sijui umenunua gari aina gani, ila gari ndogo kama corolla models ya 1996 hizo zinazotumika kama taxi huko nyumbani, dubai zinauzwa dola 1500, na unasafirisha kwa 1400, ushuru karibu milioni mbili, hadi ikifika kutembea barabarani inakuwa imekugharimu karibia milioni 6 baada ya kujumlisha hizo. Uliza mtu yeyote anaemiliki gari aina hiyo. Sasa wewe ndugu yangu na gari la dola 4000 unataka ulipie milioni mbili kweli kutakuwa na haki hapo? Hiyo milioni 5 inawezekana umebambikiziwa ila pia inawezekana kabisa kiwango halali unapaswa kulipa kina karibia hiyo amount. Siku zote ukitaka jambo la gharama lazima ugharamike.

    Kweli, viwango ya ushuru vipo juu sana, ila hebu tutafakari ndugu zangu, licha ya kuwa juu kiasi hicho bado kila kukicha kuna ingizwa magari wakati barabara zenyewe vimeo tu matokeo yake foleni za kufa mtu, hebu niambie ingekuwa ushuru ni milioni mmoja hayo magari tungeyaendeshea wapi? siingekuwa vurugu tu mjini? Mimi kwa mtazamo wangu tupunguzeni hizi lawama na tujikite kwenye uzalishaji, badala ya kuingiza haya magari ya kutembelea na kuendea viwanja, tuwe tunaleta vimashine vidogo vidogo hasa zile ambazo wamewaive ushuru ili tuzalishe bidhaa ndogo ndogo, tusikazane kulaumu tu serikali wakati wengi wetu tumo katika ufisadi huo huo, hao mafisadi wa airport ni miongoni mwetu, kadhalika huko bandari na kwengineko. Hapa tunalalamika kwa vile tumefanyiwa sisi ila tukiwa kwenye idara zetu nasisi tunafisidi bila huruma yeyote. Sina udugu na kiongozi wala mfanyakazi yeyote serikali na wala sitetei serikali kutokana na madhambi yake ila na sisi pia tuna lawama hivo tusitupie kila kitu serikali, yani unataka ufike kwa Kikwete na lawama za gari lilokwama bandarini, jamani kweli yeye ndie mkuu wa nchi na serikali ila lazima tuelewe ana majukumu makubwa, wangapi kati yetu tunashindwa hata kuweka nidhamu kwenye familia zetu zenye mke na watoto watatu kweli umtegemee mtu mmoja aweze kutatua migogoro yote ya kijamii? Si uende agalau kwa mkurugenzi wa TRA ila rais, au kwa vile ulimpa kura yako?

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  23. Hakuna jipya, ni yaleyale.

    TRA can screw anybody as they wish.

    Hakuna sheria, hakuna kufuata documents wala nini, yaani ni umafia tu.

    ReplyDelete
  24. Tatizo la kunyanyasana kati ya Watanzania ni just one side of the coin! Pia tunahitaji ku-invest in modern tools to do the work efficiently!!!! See, with the right tools and technologies, TRA could easily contact Japanese company to confirm, but you can't depend on writing letters to Japan on such issues, lol! It will be ridiculously crazy!!

    Eg:- Email would have worked fine there!!

    Mdau!

    ReplyDelete
  25. Wewe uliyekuja na hii mada unastahili yaliyokukuta ! Tulikushauri upitishe Gari Mombasa ukusikia. Hakuna mtanzania mwenye akili timamu anayetumia bandari ya Dar ..

    ReplyDelete
  26. wewe Ahmed wakati mwingine jaribu kufikiria kabla ya kutoa maoni yako, sio km wewe umedhulumiwa basi na wengine wothe wadhulumiwe, hata siku moja kodi haiwezi zidi kiwango halisi cha fedha inatatwa kwa asilimia, maana ingekuwa hivyo wafanykazi wa serikali wanaokatwa kodi wangekuwa hawapati kitu mwisho wa mwezi.
    Hapo tatizo lipo inabidi liangaliwe..., mimi mwenyewe niliagiza monitors za PC ingawa vifaa vya computer wamesema ni bure walinitoza kodi kisa eti kuna watu wanaagiza TV wakidai ni monitor hivyo kwa sababu nimeleta monitors peke yake bila PC block inabidi nilipie ushuru tena kwa bei ya TV. niliwaruhusu hadi wazifungue wakague ilishindikana ikabidi tu kulip ushuru ina maana hapo TRA wanashindwa kutofautisha PC monitor na TV ? ila niliona bora nilipe huo ushuru kuliko kuwapa hongo wazipitishe bure,.

    ReplyDelete
  27. Bongo yetu. Kwa vile vitu vyao ni overpriced for nothing ndio maana hawaamini gari nzuri iweje uzwa dola 4000 tu.

    Ndio maana mabanda ya kuku yanauzwa million mia 750 na hamna mbongo aliye nyumbani anashangaaa hiyo price. Ati watu husema ndio bei zetu hizi nyie mmelost tu mkija nyumbani mtashangaa...bei zenu gani hizo kufisadiwa tu....Mchuma bomba kwa $2500 unaupata kiulaini tu...

    ReplyDelete
  28. Hii ndio Bongo!! wengine wanadhani wanaijua kumbe hamna kitu, kwa vile we ulipitia Zenji unadhani ndio bara?? jaribu uone cha moto, malalamiko ya mdau ni sahihi kabisa na wachangiaji wengi wamesema ukweli TRA ni tatizo kama ilivyo ktk ofisi za ardhi, hospitali za Serikali, Polisi, Mahakama. n.k

    Mi nimeshaagiza magari kama mara mbili hivi toka Japan na wale jamaa wanatoa invoice halali siyo kama hizo za DUBAI, Moja ya 1995 - cc 8200 na nyingine ya 1997 - cc 1890 ajabu ni kwamba ushuru ulikuwa zaidi ya millioni nne kwa kila gari - yaani tofauti ya ushuru kwa hizo gari ni kama around laki moja hivi za ki TZ. Hiyo gari ndogo ya cc 1890 nilinunua pamoja na usafiri yaani CIF us$ 2700 hadi Mombasa.
    Mombasa tulitumia chini ya wiki kutoa gari bandarini ila cha moto tukakikuta mpaka wa horohoro.

    Suala la JK kusema anajua yanayotokea TRA haisaidii kitu kama hatayashughulikia ipasavyo ni muhimu aonyeshe tofauti kwa sababu uwezo anao, nia anayo na sababu anazo ila vitendo bado hatujaviona.

    ReplyDelete
  29. Pole tusikae kimya, tupambane kuikomboa nchi hii:

    Kaka selu nimepeleka Kilio chako kwa hawa"Corruption Tracker System (CTS)"
    Naomba sisi tulionje tusubscribe na hawa jamaa . Tujaribuni kujikomboa.

    http://www.corruptiontracker.or.tz/index.php?option=com_letterman&task=view&Itemid=38&id=3

    Nimwwaimelia messege yako na kuweka maelezo . Tuone labda watatusaidia.

    MICHANO YENU WAZEE TUANZIE WAPI JAMANI.

    Pia nimekopy hii kutoka kwenye website ya Tanzania coruption Tracker.

    Dear Readers,

    Welcome to the first issue of our Corruption tracker system bulletin.
    This tracker system represents a new era in the effort to combat corruption in Tanzania. Never before has a system of this kind been established in Tanzania. This tracker further represents a new Civil Society Organisation (CSO) and Citizens determination to tackle corruption in Tanzania

    Our aim is to broaden the public debate on corruption in Tanzania and to encourage citizens and law enforcement agencies to take up the fight against this vice. In our editions all cases of corruption will be documented and aired to public for critical debate.

    In this maiden issue, we carry articles on the background to the Corruption Tracker System (CTS), the History of corruption in Tanzania and a case statistics from the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) indicating how far we have gone. You will further find an example of how Corruption has bled the Tanesco to debt. We also include some findings from the Citizens Corruption index published by Research on Poverty Alleviation (REPOA) and insightful articles about Corruption in Tanzania and how it impacts on lives of ordinary citizens

    In the forthcoming issues, we will try to conduct interviews with stakeholders in the fight against corruption and where possible interviews with actual victims of the vice and those accused of corruption.

    We encourage our readers to send us comments and suggestions via our email link info@corruptiontracker.or.tz. Please subscribe to this free bi electronic bulletin via our link www.corruptiontracker.or.tz Look out for more on Corruption in the forthcoming editions-Keep reading!

    Moses Kulaba

    Executive Secretary



    XXXX
    Wenu
    Mzee wa Ununio

    ReplyDelete
  30. YOUR SO LUCKY,
    MUZUNGU WAS ASKED TO PAY $38000.00 FOR HIS USED VEHICLE WORTHY ONLY $16000.00.HURRY UP GO AND PAY THEM BEFORE THE PRICE GOES UP,BRO..
    THX

    ReplyDelete
  31. Ndg yangu tunakoenda ni pagumu zaidi. Hebu fikiria tu huko Dodoma NEC na CC ya CCM imebariki ufisadi unategemea nini? Tumekwisha.

    ReplyDelete
  32. Since they(T.R.A.) ain't faithful, they assume everybody else ain't. Forgetting that there are some people who are faithful to their jobs, who know what a customer service is and respect human rights.

    ReplyDelete
  33. Mimi najua solution..
    Kwa sisi tulio ughaibuni,solution ni kutorudi bongo.Bora kufa huku huku.

    Ilikuwa turudi kusaidia hali...mbina wanaorudi hawasaidii lolote?

    Nchi zingine,km Japan,watu waliosafiri sana wanaheshimiwa kwa uzoefu wao mbali mbali..Bongo ukitoka ughaibuni,ukijaribu ku-share na wabongo mambo uliyoyaona au kufanya wanasema unajidai/unajiona..KWani ulaya ndo nini!

    Ebwana ee!WaBongo hovyo kabisa.

    ReplyDelete
  34. hiyo ndio bongo tambarareee,.

    mwenye nacho anaongezewa na asiye nacho ananyang'anywa kile alichonacho.

    habari ndio hiyo

    ReplyDelete
  35. But nani anaewaweka hao madarakani? (sisi wenyewe) I wont ever again sumbuka kwenda kupiga kura kwa WATAWALA ambao hawasikilizi malalamiko ya watu ambayo ni common miaka yoote!!!
    Halafu unaambia kupiga kura ni haki Yako!!! For the hell what!!!

    ReplyDelete
  36. wee Ahmed hapo juu wacha zako, jamaa kanunua gari kwa dola 4000USD piga mara 1350 za tanzania ni 5400000, anaambiwa ushuru alipe 5000000, insuarance bado hapo, acha haingii akilini kabisa, mie kwa utaalamu wangu wa magari, magari yanayotoka dubai ama uk kuna huwezekano wa kufake invoice, lakini ya japan no way hakuna kabisa, mie yalinikuta nilinunua gari CIF mpaka dar ilikuwa 3800usd na bahati nzuri iliandikwa mpaka kwenye inspection certificate, jamaa walilitia thamani wanayotaka wao ya dollar 5000, niliwamalia kisawa yani mpaka na macopy ya bank kwamba nililipa pesa hiyo.maagent nao wakati mwingine huwa wansema hivyo kisha wanakwambia uwape pesa waonge upate punguzo, kumbe wanatia mifukoni mwao, ni vizuri kula nao sahani moja

    ReplyDelete
  37. Kaka Michuzi upo? What is next? Utatufikishia malalamiko yetu, au ndio tuzidi kushauriana kutumia port zingine kama vile Mombasa??? Ahsante.

    ReplyDelete
  38. USHAURI WANGU KWENU NDUGU ZANGU KWAKUA MNAIJUA JINSI NCHI YETU ILIVYO NA URASIMU WA KUUMIZA,SOLUTION NI KUKWEPA KUUMIZWA KWA KUTUMIA MIANYA ILIYOPO MFANO BADALA YA KUAGIZA GARI TOKA NJE NA MWISHO KULIMBIKIZIWA MAUSHURU ,SOLUTION NI KUNUNUA MAGARI YALIYOINGIZWA NCHINI AMBAYO YANAUZWA.KAMA WEWE NI MFANYABIASHARA KUWA MJANJA KWA KUINGIZA BIDHAA ZISIZOLIPISHWA USHURU.NAMNA HII HUTAUMIZWA .

    ASANTENI.

    ReplyDelete
  39. DAWA YA HAO WOTE NI NI KUWEKA SERIKALI MPYA TOFAUTI NA CCM MADARAKANI LABDA WATAREKEBISHA MAMBO.

    ReplyDelete
  40. NDUGU ZANGU EMBU TUIKIMBIE HII BANDARI YA MAFISADI ,BANDARI YA MOMBASA HAWANA MAMBO YA KIJINGA HIVI WAKO POA SAMA NA HAWANA UBABAISHAJI WA KIJINGA NA RUSHWA SIZIZO NA MAANA KARIBUNI SNA BANDARI YA MOMBASA.....WAKITAKA BASI WATUFWATE HUKO ILA BANDARI YA DAR......MH!

    ReplyDelete
  41. Wadau pamoja na kuhudhunika na mdau selu, mimi naomba msaada tutani. Naona wadau wengi wanashauri kutumia bandari ya Mombasa kupitisha mzigo. Sasa mimi naomba kufahamishwa je wenzetu mombasa rate zao zikoje? je nao wanatoza kodi ya ziada kwa magari ya zamani (zaidi ya miaka 10)?. Na je nitakapoingia na huo mziko pale mpakani kuingia Tanzania hakuna longolongo nyingine? Poleni wadau wote kwa mateso mliopata katika nchi yenu wenyewe

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  42. Kama serikali inaheshimu haki za wananchi na inataka wananchi walipe ushuru wa haki na kupunguza rushwa, basi ingetakiwa itoze ushuru kama asilimia 10-20 ya thamani ya gari kama wanavyofanya nchi nyingi tu duniani. Itapunguza rushwa, italeta biashara zaidi badala ya kukimbilia Mombasa na itaendeleza maendeleo ya nchi. Lakini kwa bahati mbaya, hatuna viongozi Tanzania, napata hasira sana ninapoona wadau hapa wanawafagilia viongozi na kufungua matawi ya CCM nje, lakini magari yao yanaoza bandarini. Inatufunja moyo sana sisi tulioko nje.

    ReplyDelete
  43. Ndio maana tunaogopa hata kurudi nyumbani maana urasimu umezidi kila kona kuanzia bandarini hadi hospitals.
    Mie nitafia huku huku na wajukuu zangu.

    ReplyDelete
  44. OMG, nimechokoza nyuki! Nadhani nimeeleweka vibaya jamani hapa mi simtetezi wa TRA kwanza kule kwetu zanzibar hatuitaki kabisa hiyo mamlaka ila hiyo ni mada nyengine, nachokusudia kusema hapa tusikurupuke tu na lawama nyingi bila kuelewa utaratibu wenyewe ulivo, hayo magari kunautaratibu wa kutiwa thamani sio limekugharimu dola 4000 tu, hapo awali nimeeleza hata kama ulipewa bure huko japan au ulaya basi lazima liwekewe value likifika nyumbani na kwa kutumia hiyo thamani ndio wanacalculate hiyo duty unatakiwa kulipia.

    Pili, Wengi mmekubali huu mchezo wa kughushi hizo invoices upo, japo sina hakika na huko japan kwa vile sina uzoefu nako. Sasa, hebu niambieni hawa wahusika wa TRA watakuwa na uwezo wa kufuatilia invoices ngapi kutambua uhalali wake? Hali kadhalika huyo mdau wa monitor za computer anathibitisha ni jinsi gani tumekuwa crooks, yani kila kukicha watu tunavumbua njia mpya za kukwepa kodi na kufanya ufisadi matokeo yake sasa, hata wale wasafi kama huyo bwana wanapata matatizo. Tubadilikeni kama jamii sio serikali tu.

    Hivi hawa ndugu wanaosisitiza watu watumie port ya mombasa wapo serious kweli? na wao wanajiita wazalendo na wanauchungu na nchi? Huyo aliesema usumbufu wa zanzibar haulingani na wa hapo dar, nakubaliana nae ila ikumbukwe TRA ni hiyo hiyo moja. Kwa kumalizia nampongeza mdau duu kwa ushauri wake hapo juu kuhusu bidhaa waived kama nilivosema kabla. Hata hivo ushauri wa kununua gari linalotembea barabarani napingana nao kwa vile litakuwa ghali zaidi, wengi wanatambua hilo hadi huyo mdau selu ndio maana akaamua kuingiza la kwake.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  45. Pole sana mdau. Huo ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa TRA. Wanapanga bei kutokana na information wanazozipata kwenye internent. wanachangalia ni kwamba gari ya mwaka fulani inapatikana kwa bei fulani bila kujali watu wengine tunanunua kwa bargaining price. Lililokubwa kwao ni kuvuka Malengo ya ukusanjanyi wa kodi na ndio maana hata mameneja wao wako kimya hawasemi kitu. wanajua kabisa kwamba watu wanaonewa na kunyanyasika lakini hakuna anayesema neno. Watanzania tuna silka ya upole na hatuna mtetezi mahali popote, ukishaupliftiwa hiyo invioce wanakwambia usipotoa gari utachanjiwa storage! ndio maana wengi sana wanaamua kutoa rushwa na wasioweza kutoa rushw wanalipia magari kwa bei ambayo ni zaidi ya manunuzi.
    Wizi wizi wizi wizi mtupu!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  46. duh nimelowa jasho apa

    ata me nimeagiza gari naomba Mungu tu yan ntakufa na mtu

    niko radhi nichukue likizo ya mwaka bila malipo

    pole mdau,tafuta "mpiga debe" unaemfahamu api bandari au TRA for teh time being

    asante

    ReplyDelete
  47. Kwanza Ahmed ahsante kwa kujibu, make hata mimi nilikuwa nikurukie kwa lawama.
    Ni kweli tunalalamika, ila swali ni kwanini tunalalamika? Ukweli ni kwamba most of the basic services that we take for granted in the west are not available in our damned country. Hata uhaminifu, just kumwani mtanzania aliye nyuma ya meza anakusaidia hakupo. Why? Because the whole system is rotten.
    We niambie umenunua gari $1850, unalipa kodi $2000, really.....
    Kwa wale tuliosoma uchumi, ukishakuwa na rates kama hizo unachotafuta sio mapato makubwa bali kuepuka mapato...When the country is too corrupt like ours. Having a higher tax rate is another way way to fuel more corruption.
    Ukweli ni kwamba we need a very serious, deep and well thought transformation. From mind, leaders, tax structure and the like.....

    Mdau pole...nikieleza kilichotekea kila mtu atazidi kuchanganyikiwa.

    my two cents

    ReplyDelete
  48. PETER NALITOLELAAugust 19, 2009

    MIMI NINAKUBALIANA KABISA NA TRA HIYO DOCUMENT ITAKUWA NI FEKI KWANZA WATANZANIA TUNA TABIA YA KUBADIRI VITU ILI TUKWEPE USHURU.WANABADILI SPEED METER ILI GARI IONEKANE MPYA SANA SASA UNAFIKIRI MJAPAN KAMA UMEMPA MSHIKO WAKE ATAKATAA KUANDIKA BEI NDOGO KWENYE INVOICE? WEWE LIPA HIYO ULIYOAMBIWA NA TRA USITUBUGHUZI HUMU NDANI. KAMA ULIKUWA HUTAKI USUMBUFU UNGENUNUA GARI HAPO HAPO DAR KUNA MAGARI MENGI TU YA MILLION NNE KILICHOKUTUMA KUDANDIA NDEGE KWENDA HUKO JAPAN KUBADILI BEI YA HILO GARI NI NINI? NEKSTI TIME UTULIZANE HAPO HAPO DAR TAFUTA GARI TENA UNGELIPATA KWA MILLION TATU KWA WACHAGA/WAHINDI. HAKUNA WA KUKUSAIDIA HUMU LABDA MWULIZE MICHUZI ANAUZA KIASI GANI ILE LOVE 4 YAKE YA KIJANI AMA KAMKOPE HASHEEM THABEET AKUPE KIASI KILICHO BAKI KABLA HAJAENDA KUCHEZA MIPIRA HUKO MAREKANI

    ReplyDelete
  49. Hivi hawa Mabosi wa TRA hawasomi habari hizi?Mbona wamekaa kimya? Kwanini hawatuelezi jinsi system zao zinavyofanya kazi? Kwanini wanadharau malalamiko yetu?
    Michuzi naomba uwapelekee hii ishu wakuambie tatizo liko wapi,
    Hii haitokuwa globu ya jamii kama wahusika wakubwa hawaisomi, na kwanini heading umeweka 'yaleyale'?
    MUNGU IFIKISHE GLOBU YA JAMII KWA MAFISADI.
    MUNGU MPE UWEZO WA KUWAHOJI MAFISADI MDAU WETU NAMBA MOJA
    AMEIN.

    ReplyDelete
  50. Anonymous wa Wed Aug 19, 05:56:00 PM asante pia kwa kupitia jibu langu, hata hivo nimeshindwa kujua awali ulicomment vipi juu ya nilichoandika kwa vile kuna anonymous wengi hapa, ingekuwa vizuri tungekuwa tunatumia majina inakuwa rahisi kutofautisha, hata mimi ahmed sio jina langu halisi ila nalitumia kwa utambulisho hapa.

    Sijakataa kwamba matatizo haya yanayolalamikiwa hayapo, na pia nakubaliana na wewe juu ya hiyo point kwamba viwango vikubwa vya kodi vinapelekea watu kukwepa, hata katika posti yangu ya mwanzo kabisa hapo juu nilisema hivo, mimi sina utaalamu wa uchumi ila naelewa basic principles nimefanya 4 classes za economics nilichukua kama electives katika degree yangu.

    Ssasa, hebu tujadilini ni vipi tuta achieve hizo transformations ulizoziita well thoughts, kwa mfano mdau imu, hapo juu yeye kaandika hatopiga kura tena kuchagua viongozi, binafsi nina miaka 27 sijawahi kuvote licha kuwepo siasa kali kule kwetu zanzibar, sasa tusipo vote nani atatuchagulia viongozi? Kwa mtanzamo wangu ni kwamba Tanzania kuna siasa ya vyama zaidi, yani wananchi wamekuwa wakipiga kura kuchagua viongozi kulingana na itikadi zao za kichama. Yani kama wewe ni CCM basi unampigia mgombea yeyote CCM watamsimamisha hali kadhalika na wanachama wa Chadema na vyama vingine mchezo ni huo huo. Naamini hilo ndio tatizo sugu, hatuchagui viongozi kulingana na records zao za utendaji na uwajibikaji ndio maana mafisadi hao hao kila awamu unakuta wamo kwenye serikali.

    Mdau, Peter Nalitolea hapo juu naona anamtaka selu ubaya! ila anachokiongelea kina ukweli tumezidi kuwa waongo sasa ndio tunaishia kuwaponza wenzetu wasio na hatia, tujengene jamii yenye uaminifu bila hivo maendeleo yatasuasua sana.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  51. It is these kinds of injustices that made me to be both ashamed and mad at my country. Watu wamechoka jamani rushwa kila sehemu, Wananchi are being treated like second class citizen! Tanzanians in Diaspora are working their tail off to invest back home, but they end up being disappointed by few corrupt officials.



    Many people don't prefer to use the port of Mombasa but the bureaucrats in Dar es Salaam force them to do so. Where are our leaders? The president visited the port a month ago and nothing has changed! It seems like it was another photo opp for Mr. President. Trust me on this, if this culture of corruption will not be eliminated completely, in our country,then development will continue to be an alien.

    ReplyDelete
  52. kwa kweli kak kero hiyo sio yako peke yako hata mimi na familia yangu ilitukuta gari lilikuwa la dola 2900 lakini TRA walipandish ana kudai kuwa wanataka tulipe kodi dola 7000 kweli njia za panya hazitaendelea kwa njia hiyo tubadilike jamani maendeleo yapo mikononi mwetu lakini ubinafsi wa rushwa umekuwa mwingi hatutakaa kuendelea ng'oo

    ReplyDelete
  53. MICHUZI UKIBANA HII COMMENT POA TU LEO LAZIMA NISEME KWANI NIMECHOKA!!

    WACHA HAO WENYEPESA ZA KULETA MAGARI WAKOMESHWE HUKO BANDARINI MAANA HUKU KWENYE SEKTA MUHIMU NA SISI TUNAKOMA.

    MFANO: (UTANISAMEHE LAZIMA LEO NI SEME NMEKEREKA SANA)
    HAO WATU WENYE ASILI YA UARABUNI WAKIJA HUKU KCMC KWA AJILI YA VIPESA VYAO HIVYO WANAVYOINGIZIA MAGARI WANATUNYANYASA KWA KUWAWEKA SAWA WAHUSIKA UNAKAA KWENYE FOLENI WAO WAKIJA UTADHANI KUNA SPECIAL HUDUMA KWA WATU WA RANGI HIYO.

    MIMI NASEMA TRA KULA HONGO TU WAMEZIDI KULA KULA KWA MIKONO NA MIGUUU

    ReplyDelete
  54. Zile bia tunazo wanunulia mkatusifia mnafikiri pesa tunatoa wapi? Sote twafaudu la sivyo msingekua mnatupapatikia mtaani!

    ReplyDelete
  55. Ahmed, napenda unavyojibu!!!
    Ahsante.

    Mdau Mpya

    ReplyDelete
  56. Inasikitisha sana kuona Tanzania ambaye ni mwanachama wa Shirika la Biashara Duniani inashindwa kutekeleza sheria ambayo imetia saini yenyewe. Ndugu wadau wa blog ya jamii,suala la kutathmini thamani ya kitu siyo la hiari kama maofisa wa forodha wanavyofanya. Thamani ya kitu chochote kilichoingizwa kutoka nje inapatika kwa kanuni kubwa 6 ambazo zimewekwa bayana na WTO. kwa ufahamu zaidi bofya hapa: http://www.wto.org/english/tratop_E/cusval_e/cusval_info_e.htm, na hizi kanuni zipo katika sheria za forodha za Afrika Mashariki.

    ReplyDelete
  57. Mdau usipoteze muda, kopa pesa ukatoe gari yako. Last week nimeingiza gari kwa thamani kama yako $ 4000, CIF,nimepigwa million 6.5 tsh. mbona hapo wamekupendelea? They are a group of robbers, pure and simple

    ReplyDelete
  58. Hakuna sababu ya kuwa mzalendo wakati unakabwa kuuawa na nchi hiyo hiyo. Uzalendo unanisaidia nini? Wenzetu wanajivunia uzalendo kwa kuwa nchi na hasa viongozi wao wanawathamini. Hivi chukulia wale mabinti wamarekani tena wenye asili ya asia waliokamatwa kule Korea Kaskazini, hivi unadhani ingelikuwa ni watanzania wenye asili ya kiasia wametiwa mbaroni nani angepoteza nguvu zake kuwakomboa?

    Nawachukia wabongo kwa unafiki na kukomeshana wenyewe kwa wenyewe. Ningelikuwa ndo wale wenye bahati waliopo ng'ambo wala nisingeli rudi bongo kamwe. Ni ushenzi mtupu kulana wenyewe kwa wenyewe bila kujali.

    ReplyDelete
  59. Eti tunaona sifa kuwa watanzania, mbwa siye!!!!

    ReplyDelete
  60. Hao mafisadi na CCM yao watashinda tu chaguzi zote tena kihalali bila kuiba kura kwa kuwa wanaowachagua ni wale ambao hata pesa ya chumvi ya kuungia mboga hawana, hawana kazi, makazi wala chakula.

    Wasomi wote, wenye akili wote, mliopo na mlowahi kwenda nje wote na wote wenye uwezo au mlowahi kuagiza bidhaa nje au mlio na mpango wa kufanya hivyo, hata muungane, tena wote kwa moyo mmoja muipinge CCM, hamshindi hata siku moja. Kwa kuwa wenye CCM, hata hawajui kesho wataamkia wapi na ndo hao wanaipenda usisikie, lakini ndo wanao nyanyaswa usisikie. Si afadhali hata wewe unauwezo hadi wa kununua jini likufilisi kwa bei ya mafuta bongo, wenzako hata kandambili miguuni hawana lakini ndo CCM kufa mtu.

    Ujanja si kusoma Bongo, ujanja ni kuwafanya watu wawe mbumbumbu na masikini kupindukia kiasi hawawezi kaa wakafikiri wala kusikiliza sera za chama kingine cha siasa wala mawazo ya kuweka serikali mpya.

    Ushauri wangu, wale watakaweza au kupata bahati kuondoka bongo kaeni huko huko (Raisi mwenyewe alishasema wakati wa kujadili suala la duo citizenship kuwa mnataka kula huku na huku na yeye suala hilo haafiki kwa nini mfaidi?), sisi wengine tuvumilie tu kuungua na jua. Unajua, watatunyonya mpaka damu itatuishia, hawatakuwa na pa kunyonya tena, na wao watakufa tu. Ubaya ni kuwa sisi ndo tutaanza, lakini wakisha tumaliza watakula nini? Itabid na wao wafe njaa tu.

    ReplyDelete
  61. Ushauri wangu kwa mdau, waachie hilo gari, save hiyo milioni tano ambayo unataka kuitumia kama ushuru, utakuwa umesave charge za bandarini (maan huo ni ushuru tu, bandari hujawalipa), uta save pesa ya kusajili, then utaave pesa ya bima, plus fikiria ni kiasi gani cha mafuta utalipa kwa mwaka kulitembeza hilo gari kwenye mafoleni ya dar, bado vibaka hawaja kuchomolea vitu vidogo vidogo, bado mafundi hawaja kubadilishia vipuri, ukienda nalo sinza ndo wasiwasi mtupu wa kuporwa, yaani ni msururu mkubwa wa matatizo yatakayo kujia kwa kulichukua hilo gari bandarini na yote yana kosti zake in terms of money. Lipige tu chini wachie.

    Hiyo pesa ulanayo itafutie kazi ya kufanyia itakayo kulipa na amabyo italeta mzunguko wa hela nyumbani wajitegemee. Kwa sasa waache wapande daladala.

    Ila kama suala ni kuwa lazima nawe uwe na gari, haya walipe hao jamaa hiyo pesa haraka, chukua gari bandarini kabla storage charges hazijaanza kupandana maana mimba yake si mchezo inatesa mno (ushajua ni kiasi gani kwa siku?)

    ReplyDelete
  62. Jamani, kabala ya kuagiza hayo magari yenu ni afadhali mkakaa chini kupiga hesabu ya gharama mnazojitafutia kwa kuleta magari hapa bongo, sisi wengine tunapanda tu daladala, si kwamba hatuna uwezo wa kuagiza hayo magari, bali kujiumiza vichwa hatutaki, si lazima kila mtu aendeshe bongo

    ReplyDelete
  63. Nimekuwa nikiendelea kufuatilia maoni, nawapongeza watoa maoni, mdau anonymous wa Thu Aug 20, 06:00:00 PM asante kwa kutuwekea hiyo link ya customs valuation, hata hivo binafsi nimeshindwa kuelewa ulichoandika, hapo una kusudia kumlaumu nani hasa? serikali kwa kuridhia mkataba na kushindwa kuutekeleza kivipi? ulikusudia nini ulipoandika suala la kutathmini thamani ya kitu sio la hiari kama wanavyofanya maofisa wa forodha? sisemi kama umekosea, sijaelewa tu kama utakuwa na muda naomba utufafanulie ulichokusudia tufaidike.

    Kwa mtazamo wangu, hizo kanuni ukizisoma zinaashiria kabisa utaratibu wa kupata thamani halisi ya bidhaa ni mgumu na ndio maana kuna kuwa na dissatisfactions hasa kwa upande wa alieingiza bidhaa husika. Ili kuepusha matatizo kama haya, mdau katoa ushauri hapo juu wa kutafuta hesabu ya gharama za kuingiza bidhaa kabla kununua. Binafsi nikienda kununua gari au bidhaa nyengine sio tu naangalia bei ya kununulia bali nazingatia hadi ukubwa wa gari kwa vile freight inategemeana na cbm, hali kadhalika swala la ushuru, mwaka jana nilipoenda dubai kununua gari, nilisisitizwa na kaka yangu nisinunue chini ya mwaka 2001 kwa vile wanatoza ushuru chakavu kama nyongeza 5%. Hata hivo kutokana na bei za 2001 kuwa juu sana nilishindwa nikachukua la 1998. Hivo nashauri na wengine wazingatie hayo. Au ndio tutafute third party asie na urafiki na serikali awe anahusika na kututilia thamani bidhaa zetu?

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  64. jamani tz kunatia hasira,sijui ata mtu ufanyeje?nyumba unauziwa milioni 700 gari kutoa noma yaani iyo nchi sometimes mi naona bora kubakia huku huku nilipo kupunguza ugonjwa wa moyo,unaweza kuua mtu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...