ni kicheko wakati ACP Abdallah Zombe na wenzie wakiwa wamezungukwa na makachero na wanahabari wanaondoka mahakama kuu kupitia mlango wa nyuma mara baada ya mahakama kuwaona hawana hatia kwa mashitaka ya mauaji ya wafanyabiashara wa mahenge baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo
umati mkuwa wa wadau ulijaa hadi nje ya jengo la mahakama kuu
wakili machachari aliyemtetea zombe Mh. Jerome Msemwa, akipewa hongera wakati yeye na timu yake wakiondoka mahakama kuu baada ya kuigalagaza timu ya upande wa mashitaka
washtakiwa wakiwahi kudandia farasi mweupe baada ya kuchoropoka
wahi wahi afande..... zombe akidandia vitara iliyokuja kumchukua
wadau wakiwa wameachiwa vumbi na vitara aliyopanda zombe
mahakama kuu palikuwa hapatoshi
zombe huyoooo anakitoa huku mashabiki
wake wakiimba zombe! zombe! zombe!!










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 93 mpaka sasa

  1. Usenge mtupu

    ReplyDelete
  2. hiyo mbona ilikuwa wazi toka kitambo kuwa jamaa ataachiwa huru!!!
    hii ndo bongo bwana. tambarare!!! nyumaaa geuka kwakwa!! kuliaaaa geuka kwakwa!!, mguuu pande! kwa!! mbeleeee tembea, shotkulia-shotkulia-shotkulia-shotkulia teh teh teh boooongo bwana. bado liyumba naye mtaambiwa hakuhusika katika kuiba mabilioni ya twin towers!! jeetu patel naye mtaambiwa si fisadi!!! sasa wewe mwanawane nenda KAIBE ka-KUKU ka jirani yako uone Libeneke la virungu vya polisi lilivyo!!!, then kesi itasomwa baada siku moja tu, hukumu-tupilia lupango huyo shwain pambafu anareta biashara ya kuyaiba makuku wakati wenzake wanaiba ma-EPA!!! afande Arufonsi hebu riwahishe hiro rijamaa katika rijela ra segerea haraka.
    Pole Babu seya ndo dunia hiyo!!

    ReplyDelete
  3. Majambazi ndio wanashangilia zombe zombe wapate ajira ya wizi. Ipo siku tu.

    ReplyDelete
  4. Hakuna Marefu yasiyo na ncha..

    Haya yote yatakwisha kwa "siku moja tu" na Wanyonge nao watapata nafasi ya "kucheka"

    Shame on you Zombe's..

    ReplyDelete
  5. Kweli Tanzania hatuatafika namna hii,na watu wanfurahia kweli ushindi wa Zombe kuwa ni wa haki,I real feel so sorry for our country,Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  6. Huyu Baba akiwa Mkuu wa Upelelezi Dar "alishafunika" kesi kibao za waheshimiwa na Ndugu zao.

    Sasa leo yamemfika yeye ni nini unategema kwenye hukumu yake?????

    Safari bado ni ndefu sana Tanzania.

    ReplyDelete
  7. Mtajiju ndo hivyo wametoka na mtachonga saaaana, wewe unayelazimisha sheria imepindishwa ulikuwepo wakati mauaji yanatokea?? mbona hukwenda kutoa ushahidi? they are innocent muwaache na maneno maneno yenu kila kitu kibaya kwenu lipi zuri??

    ReplyDelete
  8. hakuna wanyonge Tanzania ni kitendo cha kujua unafanya nini tu basi, kwani akifungwa au akiachiwa anatusaidia nini jamani, mimi naona mwenye ujuzi wa kutengeneza mitambo ya umeme anifundishe niwasambazie watanzania wa vijijini umeme wa bei nafuu

    ReplyDelete
  9. Yaani askari hawapendwi kweli, hata kama mahakama imethibitisha kashinda kesi watu hawataki.

    Mlitaka anyongwe bila kosa? si ndo ungekuwa ufisadi nyangumi? Hivi hiyo haki mnayoililia itatoka wapi kama kila mtuhumiwa ataadhibiwa?

    Msiwe hasi hivyo ndugu zangu.

    Leo kwake kesho kwako.

    ReplyDelete
  10. lazima watu wafurahi maana serikali ya mafisadi imeshindwa kufanya ufisadi.

    ReplyDelete
  11. Tuone atarudi kazini au ndo kafukuzwa?

    ReplyDelete
  12. Umeme ukikatika wanashangilia,..umeme ukirudi wanashangilia..HIYO NDO AKILI YA WATANZANIA...Si unaona wanavyoshangilia!! Kiufupi hawajielewi , wapo wapo tu!!!Atakayekasirika akasirike ila huo ndo ukweli

    ReplyDelete
  13. SASA NAJUA KWANINI WAISLAMU WANATAKA MAHAKAMA YAO.

    ReplyDelete
  14. Mh mi ningependa tu kusema kuwa Mume wa huyo askari wa kike aliyeachiwa huru afande Jeni au mwanaume yeyote atakayebahatika kuwa wa kwanza kupata mchezo hapo, kazi anayo, manake mwana mama huyo kai-miss koni kwa muda mrefu, akiifumania leo hiyo koni mpaka itabadilika rangi na kuwa nyekunduuuu, na usipokuwa makini utanyweshwa hata viagra ili koni isilale usiku kucha ili mradi tu ule upwiro uliodevelopu kule Lupango uishe!!!
    kwa upande wa hiyo mijidume yenyewe haina upwiro sana manake libeneke la nyetozzz kule lilichukua nafasi yake kwa kasi, usikute leo ikawa athumani kapiga moja kachoka anaomba substitution ifanyike haraka!!!

    ReplyDelete
  15. MAAMUZI YA BARAZA LA WAZEE YAMEZINGATIWA NA KUHESHIMIWA..

    sasa hivi ni kumaliza kesi kifamilia tu maana mahakamani ukimpeleka mkubwa wewe mshitaki ndo utaonekana na hatia.

    ReplyDelete
  16. Mr kikwete what are you doing at the moment.jamaaa majambazi unawaachia free. daaa Tanzania huyu zombe alikuwa wakupiga risasi na timu yake. ila ipo siku hata mwaka hautofika.wait n see.

    ReplyDelete
  17. Kwa mimi ambaye nina historia ya muda mrefu na nchi yangu nzuri yenye amani tele, wala sioni cha ajabu. Hivi ni vitu vya kawaida sana na wala hii si mara ya kwanza kwa utumbo kama huu kutokea. Hapa tusubiri huruma ya Mungu tu kuibadilisha nchi yetu kwa kuwa tumejaliwa uoga sana.
    Asante, Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  18. jamani sheria ndio imefuata mkondo msilalamike ndio maana kila mtu anapewa haki ya kujieleza na kujitetea.Washtaki wameshindwa kuthibitisha tendo lilofanyika.Habari za magazeti na vijiweni ni tofauti na mahakama

    ReplyDelete
  19. HIVI KAMA UNAWEZA KUUA UKACHIWA HURU NINI MAANA YA SHERIA BASI HAMNA AJA YA KUWA NA MAHAKAMA HAO WAFANYABIASHA WAMEULIWA NA NANI?TUNAPOELEKEA HATUJUI.EPA HAKUNA USHAHIDI WA KUTOSHA HII PIA HAKUNA USHAIDI WA KUTOSHA DAMU YA MTUU IMEMWAGIKA WATU WAMEKUFA HIVI ZILE FAMILIA ZILIZPOTEZA WAPENDWA WAO LEO WANASEMAJE KUNA HAKI.WENGINE WALIKUWA NA FAMILIA WATOTO WAMEWACHA WADOGO WAKIMULIZA MAMA BABA ANARUDI LINI MAMA ANALIA ANASEMA KUWA BABA ATARUDI KASAFIRI UCHUNGU ANALIAA KILA SIKU AKIOMBA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE ILI WATOTO WAKIWA WAKUBWA AWEZE KUWAMBIA BABA ALIKWENDA KUTAFUTA MAISHA LAKINI ALIULIWA NA WALIOMUUA WAMEKUMIWA LAKINI SASA HIVI HANA CHOCHOTE CHA KUWAMBIA WEWE JAJI ULIOTOA HUKU HII LEO CHUKULIA KUWA HAYA YOTE YAMEKUPATA WEWE UNGEFANYA NIINI FUTURE ZA WATU WATOTO WA FAMILIA YA WAFANYIABISHA WALIOPOTEZA MAISHA MIAKA MITATU ILIYOPITA JE WEWE MWANANCHI MWENZANGU MWENYE UCHUNGU NA NCHI NA SHERIA ZAKE AMBAZO HAZIELEWEKI UNAONAJE SERIKALI INAMUHELEKEO MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA HAKI ITATENDEKA SIO LEO WALA KESHO ILA ITAKUJA

    ReplyDelete
  20. Ni kweli ameachiwa na sheria lakini jamii itaendelea kuwahukumu na dhamira zao hazitakuwa salama maishani mwao.
    Walikamata watu wakiwa hai ilikuwaje wakafa?..anyway mahakama ndo mwamuzi

    ReplyDelete
  21. Ndio maana mimi naamini tatizo letu sio viongozi, ni sisi wenyewe kushindwa kuchagua viongozi.

    Jambazi hili eti linashangiliwa kushinda kesi.!!

    Wizi na ujambazi unaonekana ni ujanja kwenye jamii yetu.

    ReplyDelete
  22. Kamanda! Ninachojua damu ya mtu inasema. Mahakama imafanya zamu yake sasa tumpe Mungu nafasi yake.

    ReplyDelete
  23. Mahakama si uwanja wa siasa. Namfahamu vizuri sana Jaji Massati tangu Morogoro ni mtu wa haki bin haki. Hakuna ushahidi wa kuwaingiza hatiani washitakiwa;Je mlitaka awahukumu kwa kusikiliza umbeya wa mitaani? vitabu vinafanya kazi. Hongera jaji Massati kwa kutoyumbishwa na wanasiasa, hii kesi toka mwanzo ilikuwa ya kisiasa sana.

    ReplyDelete
  24. SIO SIRI BONGO INANUKA DHULUMA SOMETIME NAHISI AIBU KUSEMA NATOKA BONGO.NCHI CHAFU SANA SITAMANI HATA KURUDI ILA WAGIRIKI WANASEMA TINAKANU ntafanyaje kuna wazazi,marehebu ditopile aliua kwa risasi baada yamuda kidogo aliua bila ya kukusudi hivi kweli kamanda wajeshi anatoa bastola yake,anai unlock anashoot mara2?jamanii haya nahili jijamaa nalo lenyesura mbaya kamaaa limeua na wauwaji wenzie huyo nae katemwa tena wote hadharani.kama si wanawake na watoto na wachamungu wallah ningeomba bongo iangamizwe nchi haina haki ni yanini?mdau greece

    ReplyDelete
  25. MTOENI BABU SEYA NA WANAE JAMANI IKIWA HAWA WAMEUA HADHARANI NA MMEWAACHIA KINACHOFANYA MUMSWEKE NDANI NGUZA NA WATOTO WAKE NI NINI NA KAMA KUNAJISI WATOTO WALIFANYIA CHUMBANI HAKUNA MTU HATA MMOJA ALIEWAONA?LAKINI MAREHEM DITOPILE NA HILI SURAMBAYA ZOMBE WAMEUA HADARANI JAMANI.NI UCHUNGU ULIOJE UNAFUNGWA MAISHA NA WATOTO WAKO KWA KESI YA KUBAMBIKIWA.NINAVYOMJUA PAPII KOCHA JINS ALIVYO HANDSOME BOY NA STAR KUNA MABINTI KIBAO WANAMPENDA NA WANAMTAKA HATA BURE AKABAKE VITOTO JAMANI HII SIO HAKI WATOENI INAUMA KILA MZAZI ANAPENDA KUONA WANAE KTK HALI NZURI SI KUA NAO JELA .MANIKIZZ,GREECE

    ReplyDelete
  26. wanyime elimu wape na njaa utawatawala mpaka yesu atakapo rudi.ione mitanzania inashangilia majambazi kurudi mjini ili iwanyonge vizuri hahahaha nacheka kama mazuri.poleni wafiwa ndio bongo hio,kudadadeki kama noma na iwe noma tu jipangeni anaenda kwa waganga haya,albadiri haya,mapanga haya ilimradi na nyinyi mumnyonge zombe coz kama kufa nyinyi mashahidi kifo mnacho tu lazma atawarudia huyo muwahini fasta,manikizz,greece

    ReplyDelete
  27. Nawapa Pole Mnaolalamika Hapa Ila Mkumbuke Yanaishia Hapa hapa Kwa Michuzi Hakuna Kibopa Au Kiongozi Anaesoma Humu Na Michuzi Hana Uwezo Wa Kuyapeleka Huko..Sasa Mnaonaje Michuzi Tukimpa Uwaziri Flani Baadala Ya Ukuu Wa Wilaya Ya Nanii??? Ili Afikishe Haya Maujumbe??Poleni WATANZANIA Wenye Uchungu Na Nchi Yenu Huku Hamna Uwezo Wowote.Asante Mungu Kwa Kunikimbiza Bongo..LIDUMU BOX

    ReplyDelete
  28. Dude limeachiwa huru, kuna usalama kwa ndugu na mashahidi wa upande wa mashtaka kweli? Haya Mitanzania, furahini lakini hii miuaji ndo imeingia mtaani hivyo!

    ReplyDelete
  29. detopile naye aliuwa tena live, but nilishangaa sana kusikia alifariki akiwa nyumbani uraiani, mimi nilidhani alifia jela. any way hata zombe na yeye hana mwisho mrefu, kwani yeye hana mkataba na Mungu, kwani detopile aliua, na yeye yuko wapi sasa hivi??? jamani msicheze na Mungu kwani Mungu hahongwi bwana. Uonevu tu umejaa Tanzania ila ipo siku Mungu atawaona.

    ReplyDelete
  30. Hakika habari hii imetushangaza wengi... Nimejisikia mnyonge na sina raha kama vile ninahusika mojakwamoja.... sijui wenye ndugu zao marehemu wanahali gani... poleni tulioguswa na mkasa huu na hususan hukumu ya leo!!
    Nina bakiu wetu kwa mashauri ya kimahakama?? Nimebakia najiuliza yafuatayo.... 1. hivi ni kwakuwa hatujui sheria na taratibu za uendeshaji wa mashauri mahakamani ama ni vipi tunajisikia wanyonge kwa hukumu hii?? 2. tumlaumu nani kati ya mahakama, vyombo vya habari na wanasheria wetu tanzania kwa umbumbumbu wetu kwa taratibu za kimahakama? 3. ni nanini hakufanya zamu yake kwa usahihi.... polisi mwendesha mashtaka!! mashahidi!! karani mpanga tarehe za kesi11 SHAHIDI ALIYEFARIKI - ALIUGUA, HAKUHOJIWA MPAKA MAUTI IKAMKUTA!! HAPA PAKOJE?? 4 NI NANI AMEWAUWA NDUGU ZETU WA MAHENGE?? Hongera br Zombe.je wajisikiaje? pole sana. Basi.... tusaidie walao kwa hili lamwisho!!

    ReplyDelete
  31. bora tubaki huku huku tubebe mabox na kuchambisha wazeee.TANZANIA is the FUKKING COUNTRY I HAVE NVR SEEN IT IN MA LIFE,Wengine wanatahabika na wengina wanakula bata kwa saana.
    maji shida,umeme shida hadi karne hii kuna mgao.AIRPORT WIZI MTUPU,BANDARINI NAKO WIZI,POSTA NAKO WIZI,UJAMBAZI,UFISADII.
    BABA WA TAIFA SI TULIKUWA BADO KUPATA UHURU,ULIWAHI SANAA KUDAI UHURU WETU.

    ReplyDelete
  32. Laiti wadanganyika wangepata uelewa japo kidogo tu juu ya nchi hii inavyoongozwa, Sidhani kama leo hii watu wangediriki kutoa japo kidogo kati ya maumivu makubwa yaliyojificha ndani ya mioyo yao! Nilipopiga kura ya uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza nilikuwa sijui nini maana ya kumchagua kiongozi bora, Ila kadiri siku zinavyokwenda napata mwanga juu ya mengi niliyokuwa najiuliza! Kumbe kiongozi bora ni huyu asiyejali wananchi wake? Kumbe ndio huyu anayelinda wachache na kunyamazia vilio vya walio wengi? Kumbe ndio huyuhuyu?!?

    Hili mbona ni jambo dogo sana kati mliyowahi kuyasikia juu ya nchi hii?! Msihuzunike sana, Mnatakiwa kushukuru kwa kila litokealo kwani ndio roho, mapenzi na majaliwa ya nafsi zao.

    Hivi ni nani kati yenu anaweza kumuonea huruma kiumbe asiyemuumba? Hawa ni binadamu kama ninyi, jamani ni wakati wao na hata kabla wapo waliokuwa kama ama zaidi ya wao, Cha kushukuru ni kwamba sasa hivi tumefikia katua ya kutambua mambo! Naomba muamini iko siku MUNGU atatusikia na maumivu yetu yatatulia japo sio leo ila palipo na nia hapakosi njia!
    MUNGU TUBARIKI, WABARIKI NA WAO(wanaojiona ndio wanzania peke yao)
    PAMOJA TUTAFIKA

    ReplyDelete
  33. Yaa namuunga mkno aliyesema tatizo ni sisi wenyewe kwa kushindwa kuchagua uongozi wenye kutumia justice. Hakuna hata fisadi mmoja atakayetiwa hatiani kesi zao ni utani tu kwa umma wa watanzania.
    Cha kusikitisha hapa ni kwa familia za wafanya biashara waliouawa ambapo haki haikutendwa. Ndio hivyo serekali yetu kama kawaida yake imetuangusha, mnyonge hana haki. Nawafariji kwamba tusikate tamaa, labda iko siku haki itatendeka, Mungu ni mwenye uwezo mkubwa.

    ReplyDelete
  34. zombe zombe zombe zombe damu ya wafanyabiashara wa mahenge na dereva wa taxi inakulilia mikononi mwako

    ReplyDelete
  35. Duh... yaelekea pana shida mahali... ila kama ni mahakama au vyombo vya habari!! inawezekanaje jamii kubwa hivyo ya watz iwe na mshtuko kwa br zombe kuachiliwa huru?? vymbo vya habari mlitudanganya sana mkiandika habari za kishabiki bila kuujua ukweli wala sheria na shughuli za kimahakama zinaendeshwa kwa kuzingatia mambo gani muhimu... Hii ni aibu yenu milele... kuweni na utaalam wa masuala kwa sekta ili mtuelimishe ama mtupashe mambo kwa usahihi na uhalisia wake...inawezekanaje mjitie utaalam wa kila jambo?? ushabiki unaleta fitina na chuki zisizo na mpango!! ona sasa tutaichukia mahaka yetu... tutamchukia br zombe... yawezekana ni kweli hana/ama ana hatia!! mmeniudhi sana waandishi wa habari bongo!!

    ReplyDelete
  36. tafazali wataalam wa sheria jitokezeni mtuambie la kufanya ama mtuelimishe imikuwaje? mi naona mazganyanza! hata sielewi nimshangilie ama nimzomee nani?? I feel like crying loudly!! plz help.

    ReplyDelete
  37. Jambazi uliua nae?? yanini kumhukumu mwenzio kama jambazi wakati huna uhakika?? wewe kama ulishuhudia jitokeze kama unasoma vyombo vya habari kama sie basi amini sheria imefata mkondo wake.

    ReplyDelete
  38. Ndugu zanguni hapa ndipo unapokuja ukweli wa mambo kwamba sheria zipo kwa ajiri ya kutetea na kuwalinda watawala na siyo kutetea wanyonge kama inavyonadiwa. Kiukweli hili ni suala la kisheria zaidi, according to the letter of the law watuhumiwa hawana hatia na jamhuri imeshindwa kuprove hilo over the court. But kihualisia watuhumiwa wanayakujibu, hata kama wameshindwa kujibu mbele ya mahakama, watajibu mbele ya mwenyezi mungu. Na hii inaonyesha jinsi gani serikali isiyokuwa makini, wanakurupuka kila kukicha imetumia gharama nyingi kwenye tume ya jaji Kipenka na kutoa report kwamba Zombe na wenzake wanachakujibu mbele ya mahakama. Lakini leo hii, serikali hiyohiyo kupitia mahakama inakwambia hawana hatia. It reach a point tunajiuliza umakini wa serikali yetu hatupati majibu!! Kumbe hata marehemu DITO asingejifia naye yangekua hayahaya!!Sasa umefika wakati ndugu zetu tujaribu njia nyingine ya msingi na sio serikali hii ya chi chi M. Siyo wakati sasa wa kulaumu kilichofanywa na mahakama tuanze na stratergies zingine kabisa kuhakikisha tunafunua mfuno mzima uliojawa na kirusi ya rushwa na ufisadi.
    Mdau Mlimani

    ReplyDelete
  39. Muhimu ni kuleta mapinduzi ya haki katika nchi.

    Haki ya kweli ikiwepo, watu wataamini kuwa Zombe hakuuwa ndo maana kaachiwa huru. Ila kama watu wanajuwa haki haipo, vipi waamini mtuhumiwa kaonewa au katenda?

    ReplyDelete
  40. Aliyeua alishatoroshwa, itakuwa ni kurudia kosa kuwahukumu kifo watu ambao hawakuua

    ReplyDelete
  41. kuachiwa huru kwao hakumaanishi kuwa hawakuua, wameshinda kesi kiufundi (technicality). ukweli unabaki pale pale kuna watu wameuawa na hawa ndio sababu ya kufa. kilichoshindikana kwa upande wa mashitaka ni kufikisha ushahidi mzito dhidi yao, lakini they have got blood in their hands hata kama mahakama imewaachia huru.

    ReplyDelete
  42. Typical tanzania and her policies! mnataka kutwambia kuwa hawa jamaa walikufa kiwenyewe wenyewe tu? hapakupita mkono wa mtu? zombe na wenzake hawakuwepo yalipotokea mauaji haya?

    kama msemo wa wataalamu unavyosema kuwa wameachiwa kwa kuwa wameshinda ki-ufundi, watetezi wao walikuwa wazuri kushinda wa upande wa mashitaka, lakini haimaanishi kamwe kuwa hawakuhusika kwa njia moja au nyengine na mauaji haya.

    ReplyDelete
  43. The Law has prevailed over emotions.

    Asanteni sana mahakama kwa kuzingatia ushahidi badala ya hisia.

    Good job mahakama.

    Zombe, sasa utubie.Ukweli unaujua wewe na Mungu wako.

    ReplyDelete
  44. Hii inaonyesha jinsi Mahakama zetu zinavyoendeshwa kwa kufuata upatikanaji wa ''hatia bila ya kuwa na shaka yoyote'' ndiyo msingi wa utoaji hukumu.

    Hivyo vyombo kama ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu DPP pamoja na Jeshi la Polisi wamepewa changamoto kubwa.

    Changamoto hii ni kwa DPP na Polisi kufanya kazi zao kitaalamu na kwa mwendo wa kisasa, kutunza vidhibiti kisasa, kufuatilia nyendo za askari kisasa ktk kufuatilia tuhuma za uhalifu n.k

    Hivyo waliopoteza ndugu ktk sakata hili tupo pamoja ktk wakati huu mgumu wa Polisi na DPP kushindwa kufanya kazi kwa 'sayansi na tehnolojia e.g DNA, utunzaji wa silaha armoury, kufika eneo la tukio mapema na kulikinga lisipoteze ushahidi n.k

    Kwa kweli Haki bila sayansi na technolojia, mawakili waliobobea na idara za serikali(DPP&POLISI& TAKUKURU) ambazo zinafanya kazi zake 'ki-kale', itakuwa vigumu kupatikana.

    Mwananchi Aliyeguswa
    Kivukoni
    Dar-es-Salaam

    ReplyDelete
  45. Walipopigania UHURU (wao))binafsi) lengo lao lilikuwa ni juu yao, familia na wapendwa wao! Sisi mamburukenge (tusio na haki ya kuwa huru wala kuishi) ndio misukule na sadaka zao, 'INAUMA MNAJUA' Kuna mtoto U18 amefungwa miaka mi3 kwa kulisha mifugo ktk eneo la akiba(Nafikiri kwa akiba yao pia) hebu chambua hapo mdanganyika mwenzangu!! Sio dhambi chambua kisha tuambizane.. Nakumbuka sana sinema ya 'ROOTS' ndio haya jamani! Ndio haya haya tufanyiwayo na binadamu wenzetu, viongozi wetu, Inaniuna zaidi kuona WEUSI wenzetu wakitufanyia hivi ikiwa huko nyuma tulikata haya kwa minajili ya kuwa sawa na usawa kwa kila m1 wetu..

    Hii ndio Tanzania kisiwa cha UONEVU na DHIKI mpaka KUFA

    @#%$&#@$%

    ReplyDelete
  46. Michuzi huyo anon wa kwanza siametukana?? au siku hizi unaruhusu watu kutukana?? kama umeruhusu naomba uniambie tu maana nataka kutoa duku duku langu kuhusu hii kesi kwa kuitukana mahakamaaaaaaaaaaaaaaa maana nashindwa kuelewa zile roho zilizotoka ni nani aliyezitoa???????????? ah asee hii nchi inapopelekwa sasa hivi ile tume iliyoundwa na raisi mmeigeuza kuwa haina akili?? na maamuzi ya raisi hayana aklili?? Basi mheshimiwa raisi simama utueleze kama yale mameno uliyoyatoa kuwa waliofanya mauaji ni lazima wafungwe yalikuwa ni kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa tu out of that hatuwaelewi kwa kweli laa sivyo muwaachie wafungwa wote wenye kesi za mauaji,,, mnaboa sana kwa kweli yaani kazi yenu ni kulindana tu wanyonge tunataabika tunashindw akusomesha watoto shule while watoto wenu wanasoma kwenye mashule ya maana na wengine mnawapeleka ulaya hamshibi hayo matumbo yenu mnatunyonya nguvu zetu ah kweli nasikia kulia naandika hapa huku nimejawa na uchungu moyoni.

    EE MUNGU UWAREHEMU MAREHEMU WOTE WALIOKATISHWA UHAI WAO NA AKINA ZOMBE NA WENZAKE NA USHULE MVUA YA LAAANA KWA WOTE WALIOONA KUWA ZOMBE NA WENZAKE HAWANA HATIA
    AMEN

    ReplyDelete
  47. Sasa nani aliwaua wafanyabiashara hao? Je kesi imefungwa au upande wa mashitaka unaweza kupata ushahidi mwingine. Kama hawa jamaa wameshinda kesi basi ni makosa ya upande wa mashitaka.
    Ngojeni sasa mafisadi wote hawana hatia wataachiwa vilevile.
    Tumeridhishwa wameenda mahakamani

    ReplyDelete
  48. mimi nawashauri wabeba mabox mbaki huko huko kama mkipata mchongo maana ukija tanzania unaweza kufa kwa Heart attack kwa jinsi nchi inavyoendeshwa! yaani nchi inanuka ufisadi wa kutisha

    ReplyDelete
  49. MSEMWA KESHO KWA MOLA KUNA MOTO NNAAMINI HIVYO.MOYONI MWAKO UNATAMBUA NINI UNAFANYA .SIKU ZOTE KUMTETEA MKOSA NI RAHISI KWAKUWA UNATUNGA LAKINI MWENYE HAKI HUWA ANASEMA UKWELI ULIVYOKUWA HUWA NI NGUMU KUAMINIKA, MSIJALI WATANZANIA WENZANGU MAHAKAMA KUU IPO KESHO KWA MOLA KUTAKUWA HAKUNA WAKILI ATAKUWEPO HAKIMU MMOJA TU.MSEMWA KIFO DUNIA MAPITO,UWAKILI DHAMANA,DHULUMA DHAMBI,MACHOZI YA MTU MACHUNGU.

    ReplyDelete
  50. nji hii kweli nuksi,mimi naona kesi za mafisadi zote zifutwe kuliko kutumia pesa za wanyonge kutengeneza maigizo ambayo adui anashinda halafu stering anakufa

    ReplyDelete
  51. HII NDO BONGO NCHI ILIYOLANIWA SUBIRI HUKUMU KAMA YA SODOMA NA GOMORO IWAJIE.ILI ARDHI ISAFIRI NDO WAZEE TULUDI

    ReplyDelete
  52. baada uhuru nyerere na nkurumah walijadili namna ya kuziendeleza nchi zao.mawazo ya kwame ni yalikuwa kutoa elimu hili vijana wake waweze kujitambua na kujiendesha. nyerere alisema hapana watu wakisoma watajitambua na watakupindua.sasa leo imeziilika fikra za mwalimu miaka zaidi ya 40 iliyopita

    ReplyDelete
  53. Wala msishangae kwani kama Rais anasamehe mafisadi(EPA) nini cha ajabu kwa Zombe kushinda Kesi.Ufisadi upo Top Down na hivyo hivyo Mapolisi na wakuu wote.Kwani kama ushaidi wa kutosha haukupelekwa kwa sababu ya kumsaidia mwenzao unategemea kesi atashindwaje.Viongozi Wa Tanzania na Sheria zetu za kipuuzi,Wezi wa kweli wapo mitaaani na innocent citizens wapo jela,hiyo ndio Tanzania.

    Mjusi

    ReplyDelete
  54. Heshima yako Mkubwa,
    Mi kusema ule ukweli hapa sina comment, ila naomba niwataadhalishe tu wabongo wenzangu tuwe makini sana na MAJAJI WANAPENDA SANA KUANDIKA HISTORIA. HIVI HATA KAMA SISI WA TANZANIA HATUJUI KUSOMA, BASI HATA PICHA PIA HATUONI? HIYO NI VITARA AU RAV 4 MJOMBA?

    ReplyDelete
  55. HII MWACHIENI MUNGU TU! HII NCHI TUMESHAIZOEA.

    KWANI DITOPILE SI ALIPEWA UHURU WA BENDERA...ALIISHIA WAPI!

    KAMA HAKI INGEKUWA INATENDEKA, BASI HUKUMU YA MUNGU ISINGEKUWA NA MAANA.

    ILA NCHI HII INABIDI IKUMBUKE WANYONGE, LASIVYO NILAANA TUPU.

    ReplyDelete
  56. This is how Tanzania is perceived outside...
    http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/africa/8206056.stm

    ReplyDelete
  57. Zombe hakutendewa haki wakati kesi yake inaendelea. Nje ya mahakama yalijengwa mazingira ya kuonekana ni mkosefu na anastahili kuadhibiwa. Vyombo vya habari viliigeuza kesi ile ni ya Zombe kana kwamba hakuna washtakiwa wengine na wakaendelea kufanya hivyo kuweka picha ya kuwa Zombe tayari ameshapatikana na kosa.

    Makosa kama haya yanaendelea kufanyika katika kesi za EPA, Liyumba na za Mawaziri na Ofisa Mwandamizi wa zamani wa serikali. Hali hii inawaletea usumbufu washtakiwa na hata kupeleka ujumbe usio sahihi kwa wananchi.
    Hebu angalia sasa Zombe na wenzake wameshinda kesi, baadhi ya wanannchi wandhani kuwa siyo sahihi, walitaka Zombe na wenzie waadhibiwe, kwa kosa gani? au kwa habari za magazeti na TV?
    Ninashauri wandishi wawe waangalifu katika kuripoti mienendo ya kesi na kuacha ushabiki usiokuwa na maana.

    ReplyDelete
  58. BONGO! TUTABAKI NA KOMBOLELA YETU.

    ReplyDelete
  59. YEYOTE MWENYE UWEZO WA KUTOA RUSHWA TZ YUKO JUU YA SHERIA.NAICHUKIA NCHI YANGU NA KAMWE SITARUDI KUISHI HUKO MAVUMBINI.
    HATE THIS COUNTRY

    ReplyDelete
  60. Kweli nimeamini Tanzania ina wenyewe, make ni juzi juzi tu dereva wa basi la Mohamed Trans kanyeshewa mvua wa miaka 30, sasa huyu jamaa leo hii yuko huru, ni wapi tunaelekea Watanzania ipo siku itakuwa Kosovo,,,poa tu

    Mdau,,, Malaysia

    ReplyDelete
  61. yaleyale ya ditopile huchezi mbali mungu atakuonyesha muuaji wahed!!

    ReplyDelete
  62. Ipo siku tu! Mpaka wananchi wachukue sheria mikononi mwao ndipo serikali itakapoamka!!

    ReplyDelete
  63. wote tumeongea lakini mi siku zote ua naona hakuna umuhimu wa sheria mtu anapomchukua wakili na kwenda kupanga jinsi ya kupindisa kesi je hii ni sheria. sheria ni haki lakini umu duniani sheria si haki.mawakili ua wanini?hata waislamu wakiwa na mahakama yao atakaekufa ni mwanamke,lini tumesikia mwanaume wa kiislamu ameukumiwa kunyongwa kwasababu amezini? wanaozini ni kina mama. hapa tunatakiwa tutambue kwanza sheria hakuna duniani, haipo watu wengi wako jela eti wanasubiri sheria ichukue mkondo wake,hii sheria ua imekua imesafiri hadi irudi ndo mtu ahukumiwe.imagine mtu anakaa jela anasubiri sheria wakati hana kosa,je hii ni halali. tusilalamike kuhusu sijui tanzania sijui wapi,kwanza tutambue sheria ni nini? hata yesu alikufa kwasababu sheria ilipindishwa hata kama ilikua ni mapenzi ya mungu,hakuna kitu hapa.natamani tungeishi kama wanyama, sheria kwao wanaitambua na hawana mahakama, na maisha yanaenda vizuri.sisi tuna mahakama kila kona lakini maisha mabaya.jamani wanasheria mnafundishwa nini darasani kutetea mtu hata kama amekosa jamani.yani mtu kaiba lakini mnafundishwa jinsi ya kubadilisha mambo hadi mnasema hajaiba. uyu dereva akiua watu tairi limepasuka basi yeye kaua kumbe ajali.jamani tuanze kudefine kwanza sheria ni nini, ni kweli ni haki au ni neno tu kufurahisha wenye nach na kuwaudhi wassionacho. muimbaji aaliuliza kwanini jela maskini ni wengi? jibu tutlipata la maana ya sheria.machozi yananitoka maana bado hatujui sheria ni nini wakati wanaochukua degree ya sheria ni wale wenye Div 1 tupi. jamani sheria ni nini.tujiulize tukipata jibu basi siku moja jela zitafunga wenye makosa.

    ReplyDelete
  64. Jamani, hawa wote walihusika ila tu mahakama imewaachia kwasababu aliyefyatua risasi hajakamatwa. Mimi binafsi nasikitika sana lakini haya mambo yana mwisho. Kwa wale wanaofahamu sheria vizuri naomba utueleze wadau je, hawa watu watarudiswa kazini au kulipwa fidia yeyote? Je familia za marehemu nazo zitalipwa fidia na serikali kwasababu askari walihusika ilivyo thibitishwa na mahakama? Kwa kifupi HAKI ZA MAREHEMU ZIKO WAPI?

    ReplyDelete
  65. acheni kelele wabongo haya mambo yapo dunia nzima sio tanzania peke yake siku hizi kushinda kesi ni kuwa na mwanasheria mzuri na pesa hata kama umefanya kosa, nasema tena hili ni tatizo la dunia nzima sio bongo peke yake angalieni kesi na marekani za ma super stars sina haja ya kuwataja kama ni mtu wa habari basi unazijua oj simpson aliua dunia nzima inajua sio zombe tanzania tu lakini alishinda kesi michael jackson kafanya makosa kibao lakini alishinda kesi zote sasa msikurupuke nakuanza kuipaka bongo swala la kutambua siku hizi ni kama umefanya kosa tafuta mwanasheria wa maana kwa maana nyingine hii fani ya sheria ndio inamatatizo wajanja wameigeuza kuwa tofauti kabisa na kinachokusudiwa na hii yote ni tamaa ya binadamu kwenye kutafuta pesa ukienda kwa mwanasheria swali la kwanza analokuuliza je umeua kweli ili tujue jinsi ya kukutetea namalizia kwa kusema serikali bongo haihusiki kama wengi mnavyolalamika hapa

    mdau wa ukweli UK

    ReplyDelete
  66. Why not, if NOT?

    ReplyDelete
  67. Nakerwa sana na watu wanaotoa maoni eti kuwa kesi hii ilikuwa ni ya kisiasa ni ujinga mtupu!! nafikili wanaosema hivi awakwenda shule!! uwezi kuita kesi hii kuwa ya kisiasa wakati kuna ukweli kabisa kuwa watu waliuawa sasa siasa inatoka wapi? nyinyi mnaoshangilia ushindi wa zombe mnaelewa mnachokifanya? mnajua damu ile iliyomwagika inavyosambaa?
    kwa wale msiojua kilichotokea ni tafsri ya kisheria. lazima mtu asibitishwe kuwa ameua ndipo anaweza kuukumiwa. zombe hakuua moja kwa moja hivyo sheria inamuona hana hatia. sheria itamuona ana hatia yule aliyeshika silaha na kuua, huyo ndiye mwenye kosa kisheria.
    Sina uhakika kama walicheza ama vipi, lakini yule aliyewapiga risasi marehemu alitoroka wakati uleule kabla ya kukamatwa, huyu kama angekuwepo mahakamani ndiye angehukumiwa kwa kuwa aliua kwa mkono wake.
    Serikali kama walikuwa wanataka zombe afungwe, basi angeshitakiwa kwa kusababisha mauaji na sio kuua, hapo ndipo kosa lilipofanyika na wana sheria wakatumia mwanya huo kumtetea na kushinda.
    Ni kweli jaji hana makosa kahukumu kwa kufuata mwelekeo wa shitaka lililopo mbele yake ambalo ni kuua.
    Nawashauri ndugu kukata rufaa ama kukfungulia zombe mashitaka mapya ya kusababisha mauaji ya ndugu zao na wala si kuua.
    Vinginevyo tumuachie mungu, yeye ndiye anajua na siku zote damu ya mtu aipotei bure.

    ReplyDelete
  68. Zombe kaachiwa huru na wenzake wote. Sasa naiomba serikali ya CCM ikishirikia na polisi watutafutie muuaji au wauaji wa hao wafanyabiashara. Naamini kabisa Polisi inajua wazi kabisa nani aliwauwa, kwa hilo nchi hii kwa sasa haitakuwa salama

    ReplyDelete
  69. WANASEMA HAWAKUUWA, SERIKALI ITUAMBIE SASA NANI ALIWAUWA HAWO WAFANYABIASHARA??????????????????? AU WALIJIUA WENYEWE TUJUE. HAKI LAZIMA ITENDEKE NA WAUWAJI WAJULIKANE. POLISI IANZE UCHUNGUZI UPYA. HATUKUBALI KABISA!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  70. zipo sokoni kaka

    ReplyDelete
  71. Natamani yule aliyefyatua risasi zilizowaua kina Chigumbi angejisalimisha na kutoa ushahidi wake sijui kama Zombe angekuwa huru leo.Kweli nimeamini sheria duniani haki mbinguni. Damu za marehemu zitawaandama daima. WaTz hakuna cha kushangilia hapo zaidi ya kuona ukweli unajulikana na wahusika wanawajibishwa. Mungu ibariki Tanzania na walaani MAFISADI na wale wote wanaowanyanyasa raia kwa sababu ya vyeo au pesa zao.

    ReplyDelete
  72. Wadau Msihofu OJ simposon aliua afu akasave jela, mungu kamlipa kwa kuiba cheni na sasa anaozea jela, Ipo siku zombe atarejea huko

    ReplyDelete
  73. KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA KAHARISHA! MUNGU YUPO NA ATAJIDHIHIRISHA MUDA SI MREFU KWA KUFANYA KITU KWA HAO WALIOACHIWA HURU AMBACHO HAKUNA MTANZANIA YEYOTE ATAKAYEKANA KUWA SI KAZI YA MUNGU. HAYA NI MAPITO TU ILA SOON AND VERY SOON HAKI ITATENDEKA TU, JUST WAIT AND SEE!

    ReplyDelete
  74. Namshauri rais JK amteue Mhs ZOMbe kuwa IGP kwani kazi yake ni nzuri ya kula na majambazi na kuuwa watu wasiokua na hatia pamoja na bingwa wa kupeleka migao kwa wakubwa.

    Hurray for ZOMBE THE Zombi...............

    ReplyDelete
  75. HAKI YA MUNGU 2010 CCM SIWAPI KURA YANGU MUNGUUUUUUU NAAPA.

    ReplyDelete
  76. i am deeply disheartened by the judicial system in tanzania. this shows how rich people can survive any danger in the community even if they are guilty, killers, robbers or gluttons. I didn't wonder when I heard about this unbelievable outcome. Lakini ajue kwamba ya yaliomkuta Ditopile yanaweza kumkuta pia huyo Zombe...Ni maoni yangu tu
    mupozile@yahoo.com

    ReplyDelete
  77. Naungana na wale woote waliopata uchgu na huzuni kubwa dhidi ya maamuzi hayo, ingawa ni ya kisheria zaidi. Ni wengi walioshtushwa kuona sheria ikipindishwa huku ikiruhusu wenye mabavu wachache kuendelea kumwaga damu ya wanyonge walio wengi.

    Naheshimu uamuzi wa hakimu huyo kwa kupitia mahakama. Kikubwa ni kwamba, bado nafasi ya Mungu ipo na siku zote ni afadhali kuadhibiwa na binadamu/sheria zilizopo kuliko kuadhibiwa na Mungu. Wanaofurahia jambo hili waendelee kufurahi, na hakika furaha yao ina mwisho, na wanaolia kwa sababu ya jambo hili na wendelee kulia maana machozi yao hayatamwagika bure!

    ReplyDelete
  78. Damu ya mtu haikimbiwi hata siku moja;ulishaona wapi mtu alie ua au kutoa roho ya mtu duniani akaishia mwisho mwema! Ndugu zangu tumwachie Mwenyezi Mungu haitakuwa muda mrefu kila kitu kitajidhihirisha hapa hapa, sheria ya dunia imefanya kazi yake sasa tusubiri ya Mungu. Wale wanzetu walio kuwa wanashangilia je wamesahau kuwa kuna roho za wenzetu waliouawa kutokana na ushiriki wa watu hawa!Hata kama Zombe alikuwa ni ndugu yako lakini ulipaswa kufikiria na familia ya wale waliopoteza wapendwa wao pia shangilia kimya kimya rohoni au nyumbani kwako lakini sio hadharani mana bado kuna msiba mzito. Sio muda mrefu, kila mkono ulioshiriki kwenye vifo vya watu hawa na haki kupindishwa watapata majibu yao toka kwa Mungu.

    ReplyDelete
  79. Wadau woote mnasema msiyojua,,pale bongo kuna jaji gani ambaye atawekewa milioni 50 mpaka 100,akazitema???Hata nyinyi wadau mniambie ukweli mkiwa majaji?make hela ndo inayoongoza dunia nzima bwana,,Zombe nande zako umeshinda.Hela imetumika karibia milioni 100 ndani ya hii kesi nanyinyi hapa mnalopoka tuu.Lakini mi nadhani kwenye utawala wa mwalimu hapakuwa na ufisadi kama wa sasa??eehh!!

    ReplyDelete
  80. HAKUNA MWENYE UHAKIKA THABITI WA NANI ALIWAUA WALE WATU KWANI MIMI NA WEWE HATUKUWAPO PALE TUKIONI-TUSIMHUKUMU MTU KWA KUTUMIA MAGAZETI.....ZOMBE NA WENZAKE WANAWEZA WAKAWA INNOCENT PEOPLE....ILA MUNGU YUPO......

    ReplyDelete
  81. MICHUZI I HAVE NOTICE YOU ARE TAKING SIDES.

    IF YOU ARE RUNNING THE BLOG YOU HAVE TO ACCEPT DIFFERENT VIEWS IN YOUR BLOG.

    SOME OF OUR COMMENTS ARE NOT DISCLOSED IN YOUR BLOG.

    IF YOU ONLY NEED CERTAIN TYPE OF COMMENTS IT IS USELESS FOR THE BLOGING.

    ReplyDelete
  82. Weye unaeyesema 2010 huwapi kura chi chi M huna habari kwamba hiyo 2010 kuna vyandarua vya bure? ohooo utakosa we sema tu hupigi kura uliwe a moskito!

    ReplyDelete
  83. haki husimama siku zote

    Jehovah bdie mtetezi anaeishi milele...

    amen

    ReplyDelete
  84. Nyie wote mnaosema kwamba zombe na wenzie wanahusika na mauaji yale mlitakiwa mkaisaidie serikali yenu ku-prove beyond reasonale doubt. sasa hapa mi cjawaelewa mnailaumu serikali kwa kushindwa ku-prove beyond reasonable doubt???au mnailaumu mahakama kwa kutoa maamuzi kisheri kwa kuona kwamba ushahidi haujitoshelezi??

    kimsingi serikali ndio ya kulaumiwa maana imewashtaki hao zombe na wenzie matokeo yake wameshindwa kutoa ushahidi usioleta shaka.
    na hii ndio itakavyokuwa ktk kesi za epa msipokuwa na ushahidi wa kutosha mchezo utakuwa ni huu huu full stop. ni serikali yenu yatakiwa kujipanga na sio mahakama.

    ReplyDelete
  85. Hivi nyie mmesahau kuwa Zombe alikuwa ni KIGOGO? Mnaumiza vichwa bure. Na kumbuka hakuna kiongozi wa aina yoyote anaingia humu blog kusoma haya tunayoyaandika. Na sisi wenyewe sidhani kama tunasoma maoni ya kila mtu anayeandika, kama kuna watu wanasoma ni wachache sana. Hivi nyie mlikuwa mnafikiria kuwa angefungwa ama kunyongwa? Hizi zilikuwa ni ndoto zenu. Viongozi wa Tanzania huwa hawafanywi kitu chochote. Angelikuwa wewe kamchape usingeachiwa. Na ungeisha hukumiwa siku nyingi sana. Wangapi mmeona wanaachiwa huru? Hii ndo Tanzania yetu na sheria bubu.

    ReplyDelete
  86. ukweli ni kwamba wenyewe wanajua wanalichokifanya wao ni polisi huwezi kuniambia polisi anapodhamiria kuua ataua kama wewe mtu wa kawaida ili hali anajua upelelezi unavyofanyika na yeye laikuwa na mpelelezi kama sikosei sasa mlitegemea waache alama zao za vidole ua vitu vyovyote kuonyesha kwamba wameua? cha msingi hapo mwendesha mashtaka wa serikali alitakiwa awe makini, akijua kwamba hao wenyewe ni wapelelezi hivyo upelelezi wao ungekuwa mgumu iyo kesi ingekuwa nyanya sana na wote wangekuwa hatiani mahakama haina makosa hata kidogo.

    ni mimi mwanasheria mtarajiwa.

    ReplyDelete
  87. samahani wana blog, kuna bwege kutoka uk kanikela sana na comment yake, eti anadai Wabongo achenikelele yaliyotokea kwa Zombe yanatokea dunia nzima, Hivi huyu pimbi yupo Uk ipi? ajiulize T.I mwana hiphop yupo jela, DMX yupo jela na niwengi tu masuperstar kwa upande wa US, kwa Japan yupo Live door kijana mdongo ila anapesa chafu na nimaarufu mara 1000 ya Zombe lakini sheria imefuata mkondo anatumikia jela, bila kusahau bilionea la kirassia nae, mifano ipo mingi kwawale tu wenye upeo. kwahiyo wewe mtu mwenye mawazo yako yaki bwege kutoka uk ambae ulitoa 08:48:00 kama hujui chakusema sivibaya ukawa msikilizaji tu kuliko kutoa bpoint ambazo unajua zinachefua watu.

    ReplyDelete
  88. Hizi ndo nchi zetu za kiafrika..kuendelea kwetu labda tsunami litokee tufe watakaobakia wanaweza kuanzisha nchi mpya...lol Anyway serikari zetu ZIMEOZA!!!! viongozi wetu ni kama wawakilishi wa nchi za kigeni, hawajari chochote ..ni uzuni unapoona viongozi wetu wana kila kitu maisha mazuri na HAWAJARI lakini kinachotokea nini?????... bado tunawapa kula zetu tunawashangilia kwenye mikutano toka asubuhi mpaka jioni huku matumbo yetu yakiwa meupe au na pande mbili za mihogo...Ni wakati wa wananchi KUHAMKA..HAMKENI MMEKUWA MAMBUMBU KWA MUDA MREFU FUNGUENI MACHO MUONE MNAVYODANGANYWA NA VIONGOZI WETU AMBAO WANAWAUZENI BILA YA KUJALI..mabadiliko yatakuja hata kama ni miaka 1000 fundisheni watoto zenu waelewe haki zao labda hiko siku tutaona mabadiliko.

    ReplyDelete
  89. These are the consequences of living in a country with the highest level of uneducated citizens. we will continue see people like Zombe getting away with murder until the people of this country stop thinking what to feed their stomach tomorrow and start asking tough questions about their right!
    You damn sure know that, the easest way to rule people is terrorize their way of thinking, let them think of food the rest is history.Changes in Tanzania will only start from the bottom up and not otherwise, but since the bottom is still very poor, it will take the grace of God to save Tanzanians.

    ReplyDelete
  90. 'Jamani kama mnakumbuka siku ya tukio lile la mauaji ya hao marehemu ni Zombe huyuhuyu akiwa kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Dar es salaam (mzee Tiba hakuwepo) aliutangazia uma kwa njia ya televisheni kuwa majambazi wameuwawa wakitaka kupora duka la Bidco na pesa zilizoporwa akazionyesha juu ya meza,ni zombe huyuhuyu baada ya tukio lile aliteuliwa kuwa kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa na mpaka anashitakiwa alikuwa kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa na ni Zombe huyuhuyu alinukuliwa wakati wa kesi ikiendelea akiwa amepanda basi la mahabusu akitamka kwamba yeye hana kesi na atatoka tu' - SASA NI KAZI YA WATAALAMU WA SHERIA KUPITIA KUMBUKUMBU ZOTE ZA TUKIO HILI i.e TV,Radio ,Magazeti ili kujua mwenendo mzima ulivyokuwa baada ya tukio hilo NINA IMANI BADO KESI YA KUJIBU IPO KWANI ILIDHIHIRIKA MAPEMAAAAA WALE NDUGU ZETU WA MAHENGE PAMOJA NA DEREVA TAX HAWAKUWA MAJAMBAZI!

    ReplyDelete
  91. Haya sasa tusubirie na Chenge naye kushinda case yake. Mie sirudi Tanzania ng'ooo hata kwa rungu.

    ReplyDelete
  92. NDUGU WATANZANIA WENZANGU; THE ONLY THING I CAN SAY NI KWAMBA "ENOUGH IS ENOUGH". NAONA SASA TUMEFIKIA SEHEMU AMBAYO MAMBO MENGINE HAYAVUMILIKI KABISA. NA TUELEWE KWAMBA JESHI LA POLISI HALILINDI SHERIA BADALA YAKE LINA LESENI YA KUUA.
    1) TUKUMBUKE MAUAJI YA MAHABUSU WA ARUSHA MIAKA YA NYUMA. HAWA WALIUAWA NDANI YA KITUO CHA POLISI
    2) HILI LA KINA ZOMBE UNAKAMATA MTU PELEKA PORINI UNACHINJA. SHAHIDI WA KUTHIBITISHA HAYO KOPLO LEMA MAREHEMU, NA WENGINE WATATU AMBAO WALIKUWA NA FUNUNU NA KESI HIYO NAO VILEVILE MAREHEMU.

    SASA NDUGU ZANGU TUSUBIRI NINI TENA. INABIDI KUANZA KUTETEA HAKI ZETU WENYEWE KWA NGUVU KWANI VYOMBO HUSIKA HAVINA MAANA. MUNGU ATASAIDIA VERY SOON HAYO YOTE YATATENDEKA NA OLE WENU MANAOJIITA WAKUBWA TUTAONA MWISHO WENU.

    ReplyDelete
  93. Anonymous was Tarehe Wed Aug 19, 06:02:00 PM utapigana mwenyewe sisi tutaendelea na box huku huku huko kwenye vita hatuji ng'o

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...