mpiga picha akifotoa sehemu ulipotokoea mlipuko wa bomu na kuua watoto wawili nan kujeruhi wengine watatu leo mbagala kizuiani jijini Dar.
mpiga picha selemani mpichi wa guardian akifotoa watoto wawili walionusurika na mlipuko wakiwa na mama wa jirani kwani mama yao ameenda hospitali kumhudumia majeruhi
majirani wakiwa wamemzunguka mama jirani na watoto waliojeruhiwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh. William Lukuvi na kamanda wa Polisi wa Mkoa maalumu wa kipolisi afande Selemani Kova wakipata maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya Mh. Rugimbana mara baada ya kuwasili hospitali ya Temeke leo.

Habari za uhakika zilizoifikia Glob ya Jamii hivi punde zinaeleza kuwa Watoto wawili wamekufa kwa bomu huko Mbagala Kizuiani karibu na kambi ya Jeshi, wilaya ya Temeke, jijini Dar.
watoto waliofariki ni Regina Chawala (6) na Rajab Said (6) ambapo katika mlipuko huo pia kulikukuwepo na majeruhi watatu ambao ni mtoto Sada Seleman (2)Asha Seleman (5) pamoja na Stella Christian Chawala ambaye amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali ya Muhimbili kitengo cha wagonjwa mahututi.

Chanzo cha Mlipuko huo kimetajwa kuwa ni mabaki ya mabomu kufuatia mlipuko katika kambi ya Jeshi hivi karibuni. Jirani na eneo la tukio palikuwa na taka ambazo zinachomwa moto chini ya migomba, ndipo mlipuko ukasikika na watoto watano wote wakatupwa huku na kule, ambapo mmoja alifia hapo hapo na mwingine alipoteza uhai akiewahishwa hospitali ya Temeke.


Mkuu wa mkoa wa Dar Mh. William Lukuvi pamoja na kamanda Selemani Kova ambao walifika hospitali ya Temeke, wamesema kuwa ni kweli tukio hilo limetokea na ni bahati mbaya kwa kilichotokea na kwamba taratibu mbalimbali zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na mazishi na kuwatibu wajeruhia. Mh. Lukuvi amesema serikali iragharamia kila kitu.




















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. Michuzi!
    Great Job Man you are doing! Thanks for keep on updating us from time to time.
    Mungu abariki kazi ya mikono yako.

    ReplyDelete
  2. kaka pamoja na wafiwa wote nawapa pole sana Mungu atulinde na majanga kama haya sasa cjui serikali yetu itasemaje kuhusu hili make hawa ni watoto wdogo jamani kuwazuia ianakuwa ngumu na hawajui lolote ee mungu tusaidie

    ReplyDelete
  3. HAYA HUKU KWETU WANASEMA BAGATI MBAYA KWA WENZETU HIYO ITAKUA NI LAWAMA ZA SERIKALI NA SERIKALI INGETAKIWA KUWALIPA HIZO FAMILIA ZA HAO WATOTO MAMILLIONI YA PESA LAKINI KWETU TANZANIA WATU HAWAJUI HAKI ZAO, NA HATA KAMA WANAJUA WENYE DHIKI HAWAPEWI HAKI ZAO. GOD HELP US ALL AND THIS COUNTRY. INAUTHI!!

    ReplyDelete
  4. serikali ya tanzania, isiyojali wananchi wake, mtu kufa ni jambo la kawaida na wanasema bahati mbaya, serikali inayofurahia kutafunwa kwa kodi na kufanya huduma za jamii kudorora....

    Hivi kweli Mkuu wa mkoa haoni aibu kusema ni bahati mbaya familia kupoteza watoto kwa uzembe wa serikali hiyo hiyo!! walikuwa wapi kuweka quarantine katika maeneo yaliyoathirika na kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mabaki ya mabomu??

    Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, waziri wa ulinzi, waziri mwenye dhamana ya raia ..ni wajibu wao kujiuzulu!!

    Mhh tanzania yetu ...mhhh ama kweli !

    ReplyDelete
  5. Kwa nini lakini serikali inakuwa nzembe namna hii? ina maana hayo mabaki bado yako katika mazingira ya watu? kwa nini jeshi halikusafisha baada ya tukio? Jamani sisi ni wazembe haijawahi kutokea.

    ReplyDelete
  6. JESHI LINALOWEZA KUNUNUA NDEGE NI KWELI LINASHINDWA KUNUNUA METAL DETECTORS ZINAZOWEZA KUTUMIWA KUTAFUTA MABOMU YALIYOJICHIMBIA CHINI? HAIWEZEKANI.

    ReplyDelete
  7. HAYA MABOMU NADHANI BADO YAKO MENGI ARIDHINI HIVYO KWA MAONI YANGU SERIKALI KUPITIA WIZARA YA ULINZI KUFANYA "REKI" ENEO LOTE LA JIRANI NA KAMBI ILU KUTAFUTA MABOMU AMBAYO HAYAJARIPUKA. ENEO LA KAMBI TAYARI ILA BADO MAENEO YA WATU KWANI YATATOKEA KILA SIKU NA KULETA MAAFA UPYA. BOMU HALILIPUKI MPAKA LIKANYAGWE HIYO VYEMA YAKATAFUTWA KABRA.
    Mwanajamii CM

    ReplyDelete
  8. Jamani bahati mbaya wakati yanauwa watu?? Tuwe serious sometym sio kila kitu siasa tu. Walitakiwa wafanye survey kila nyumba iliyoathirika vilivyo na sio kupita juu juu. Tushachoka kusikia vifo vya ndugu zetu kila siku halafu mnasema bahati mbaya. Be serious kny kazi na sio bla blaa nyingi.

    ReplyDelete
  9. DAMU, LAANA NA MACHOZI YA WATOTO HAO WASIO NA HATIA VITAWAANDAMA WALIOZEMBEA KWA HILI HADI MWISHO WA MAISHA YA HAO VIGOGO? HIVI KWANINI JESHI HALIKUSAFISHA MAENEO HAYO KABLA YA KUWARUHUSU WANANCHI KUREJEA TENA KWENYE MAKAZI? VIGOGO WOTE WAKO BUSY KUSIMAMIA MALIPO YA FIDIA FINYU WANAZOPEWA WANANCHI WAMESAHAU KABISA KUCHUNGUZA USALAMA KWANZA! KUNANI? HIVI SERIKALI HII IKOJE? KWANINI HAITHAMINI MAISHA YA WANANCHI WAKE KWANZA? SASA NDIO UTAWAONA WANAJITOKEZA NA UNAFIKI WAO WA KISIASA ATI KWENDA KUWAPA POLE WAFIWA! NINGEKUWA MIMI NINGEWATIMULIA MBALI! MSIKUBALI KUDANGANYIKA WATIMUENI WAKIJA HUKO MBAGALA KUZIKA HAO MALAIKA WA MUNGU! HAYO MAENEO YATANGAZWE KUWA NI HATARI NA YASAFISHWE NA DITECTORS FASTA!!

    ReplyDelete
  10. huu ni uzembe wa serikali iliyojaa wanajeshi wazembe na waliokimbilia jeshini baada ya kukosa kazi au kwa sababu kuna mjomba au baba mdogo jeshini lakini hawa hata ujuzi wowote sasa serikali inatakiwa kuwalipa hao wazazi wa watoto pessa nyingi hata million 100 mpaka 200 kwani wamezoea kuua watu na kuwalipa elfu kumi

    ReplyDelete
  11. Tujaribu kutafuta hasa source ya haya mabomu na tuyaondoe ili yasije kuleta madhala zaidi kwa watu

    ReplyDelete
  12. NDUGU ZANGU WOTE MMEONYESHA HUZUNI NA JINSI GANI SERIKALI HAIJALI TENA WANANCHI.TUME ILIUNDWA YA KITU GANI?PESA ZILITAFUNWA TU NA WACHACHE NINI HASA KIMEFANYIKA BAADA....!
    SIO SIRI RAISI KIKWETE NA WENZAKE KATIKA SERIKALI WAMESHINDWA KAZI.
    KIKWETE KAZI KUSEMA TUNAHITAJI WAFATHILI WAKAT MIJIPESA YNALIWA NA MARAFIKI ZAKE NA MASWAHIBA WAKE.
    HII NCHI INAENDA KUBAYA,NACHOWEZA KUOMBA MUNGU TU,ATUSAIDE.
    WANANCHI HAWAJALIWI HATA KIDOGO,YANI INAUDHI SANA.KAMATI ILIIKUWA YA KITU GANI NA NI KIPI SOLUTION BAADA YA HAPO.
    NACHO SHAURI NI KWAMBA WANASHERIA WAWASAIDIE HAO WATU KUSUEE SERIKALI NA FIDIA ZILIPWE.HII NCHI UTAFIKIRI NI YA WACHACHE TU.
    WALLAH TUMECHOKA,KAMA LIWELIWE TU.

    ReplyDelete
  13. Jamani ehh !! mimi nina hasira tena hasira nishkeni ...

    kuna jipya lingine mmelisikia !kuna shule moja hapo mikocheni ina ugonjwa wa swine fluu na bado wazazi hawajaambiwa confirmed kuna mtoto amelazwa hapo muhimbili na anaumwa uwiiiiiiii serikali kimyaaa hawajachukua hatua yoyote inatisha jamani .michuzi tusaidie

    tanzania tutafika ?

    ReplyDelete
  14. Inasikitisha kuona serikali isiyokuwa na uwajibikaji pindi tatizo linapotokea hapa kwa wenzetu walioendelea wangejiengua madarakani kwa maslahi ya umma yani resignation for public interest lakini huku kwetu wapi ndo kwanza watu wanajali maslahi yao na familia zao na kila statement wanazo sema ni za uongo na siasa za kuwapumbaza watu kifikra kwamba bahati mbaya hakuna bahati mbaya kwa yale majanga yenye kuweza kuepukika kama haya ya mabomu ingekuwa ni ile milipuko ya matetemeko ya ardhi, mafuriko nk tungesema ni mipango ya mungu ila huu ni uzembe wa viongozi wabovu na mjue wazi mtajibu kwa mwenyezi mungu uongozi ni dhima c kama ninyi mnaeingia madarakani kutaka kujinufaisha na kuwasahau wapiga kura wenu mnao wapatia takrima ya pilau nyakati za kampeni, umefika wakati wa kuwajibishwa hawa viongozi wa kiimla, jamani jamani Tanzania tuamke tufanye mabadiliko ya kweli c huu utawali ambao unaonekana una mahusiano na ule wa Monarc Form Of Government, Baba kwenda kwa mtoto kisha mjukuu pia kurithi utawala ni hayo tu mimi mzalendo mwenye uchungu na Tanzania yangu

    ReplyDelete
  15. Nafikiri kuna haja ya Serikali kuanzisha operesheni maalumu ya kuhakikisha kuwa hakuna masalia.
    Lakufanya ni kuwahamisha wananchi wa eneo husika kwa muda mpaka operesheni nzima iishe,ikiisha ndipo wananchi warudi majumbani kwao.
    Poleni sana wafiwa na poleni nyote mliojeruhiwa.

    ReplyDelete
  16. Wananchi wasio na hatia wataendelea kuuwawa na haya mabomu mpaka lini??? Serikali na jeshi mko wapi?? Au kwa kuwa nyie mnaishi Mikocheni, Masaki, Oysterbay. Tuwaelewe vipi? Hivi nilivyokuwa na hasira muda huu.........

    ReplyDelete
  17. Huyo rais wenu na mawaziri wake inatakiwa wajiuzuru mara moja, huu ni uzembe usiofaa kusamehewa na ile timu iliyoshughulikia mabomu yote haya ifikishwe mahakamani, upumbavu kabisa huu.

    ReplyDelete
  18. Nimetokwa na machozi kwa kuona kuwa Serikali yetu haidhamini kabisa uhai wa wanamchi wake. Nini hii kitu ya kusema "SERIKALI ITAGHARAMIA GHARAMA ZA MAZISHI NA MATIBABU" hii ni dharau kwa wananchi. kwani siku zote tukifiwa ni Serikali inayogharamia. Si tunamaliza misiba wenyewe. Ni uchungu sana labda kwa kuwa wao hawaishi maeneo hayo.kama wana hela za kila siku kutoa kwenye misiba wazitumie kuwalipa wataalamu na vifaa vya kutafuta hayo mabomu. Ni uchungu gani wazazi wanaoupata kwa kula siku kuongokewa na watoto. Siyo rahisi kukubali tu eti Serikali itagharamia. They should stop that sentence it is making us more mad please. Wanajeshi hawaendi vitani kwa nini wasiangalie uhai na usalama wa raia.TANZANIA NCHI YANGU HAUNITHAMINI

    ReplyDelete
  19. NAKUMBUKA MKUBWA MMOJA WA JESHI ALISHASHAURI KUWA WATU WAHAME ENEO HILO KWA KUWA KUNA MABAKI YA MABOMU NA JESHI HALIWEZI KUHAKIKISHIA WANAOISHI HAPO USALAMA WAO. ONYO HILI LILIPOKELEWA KIMZAHA NA KEJELI. INASIKITISHA KUWA MZAHA NA KEJELI HIZO ZIMESABABISHA KUPOTEZA WATOTO HAWA. BASI NA TUJIFUNZE KUTOKANA NA MKASA HUU NA KUTAFUTA MAKAZI MBADALA YALIYO SALAMA. TUSISHINDANE NA JESHI MANAKE WAO WAMESHASEMA ENEO HILO NI HATARI KWA RAIA KUISHI NA HAWANA MPANGO WA KUHAMA.

    Poleni Wafiwa.

    ReplyDelete
  20. Poleni wafiwa, ninasikitika kuwa serikali haiweki mbele usalama wa raia, bali wa viongozi. Kwa nini haya yasingewalipukia wao wakati ule walipotembelea kufanya ukaguzi?, walisafishiwa njia, hivyo hivyo ingetakiwa kufanyika kwenye makazi ya watu.

    Haya yote ni matokeo ya watendaji wa serikali walio corrupt. Kuanzia juu mpaka chini tumejaa ubinafsi sana Bongo. Hivi serikali ilishindwa kuwataka askari wa JWTZ, ambao ni wengi sana na sasa hivi hatuna vita, kutumia utaalamu wao hasa kitengo cha kutegua mabomu, kufanya coding ya eneo lote hilo kulikagua kwa metal detector na kabla ya kuruhusu wananchi kurudi?. Huu ni uvivu wa kufikiri na kiutendaji.

    Ingekuwa kwa wenzetu wanaojali maisha ya wapiga kura wao hilo eneo lingewekwa under quaranteen, au hata watu kuhamishwa kabisa kwa kuhofia usalama wao. Sisi tumebakia kutoana macho kwenye nani apate fidia nani asipate huku wakiwaza na mimi ntafaidikaje kwenye zoezi hili. Shame on you authorities, hakuna bahati mbaya bali ni uzembe.

    Bahati ni lugha ya mtu aliyeshindwa kuwajibika huku anajua wazi kuwa amekosea na hastahili huruma.

    ReplyDelete
  21. Serikali iwaweke watanzania sawa kuhusu haya mabomu, kwani kunani jamani? Wasitufanye tufikirie ndio wanatoa sadaka zao za uchaguzi 2010! Waziri wa ulinzi aliahidi kujiuzulu kama mabomu ya awali yalilipuka kwa uzembe! Sasa anasemaje, huu je sio uzembe wa kutupa,kutojali maisha ya watu waliowaweka madarakani! kweli hii serikali inatupeleka pabaya!!!!!!!

    ReplyDelete
  22. DR HUSEIN MWINYI FUTA NYAYO ZA BABA JIUZULU HAIMAANISHI HAUTATOKA TENA.INAKUONGEZEA HESHIMA YA UWAJIBIKAJI

    ReplyDelete
  23. uzembe, uzembe, uzembe... i can't believe this ..' serikali itagharamia kila kitu' awww how sweeet serikali .. arghhh!!!! nahasira saa hizi anyways ngoja niweke maji mdomoni.. nahasira sana. Thank you kikwete na wenzako!

    ReplyDelete
  24. Poleni wote waliodhurika na janga hilo...ila serikali inaboa inaposema itagharamia matibabu na mazishi kama huo ndio msaada mkubwa badala ya kuyatafuta yaliyobaki na wananchi wakae salama??? hawana machozi hawa??

    ReplyDelete
  25. jamani nikisoma habari za nyumbani huwa napata kasira kweli, huyu mpuuuzi anyesema ni bahati mbaya kwa sababu sio mtoto wake aliyefariki ndio maana, vingozi wetu ni wanyanyasaji sana jamani uchaguzi unaokuja watz tunatakiwa kuwa makini sana this IS tooo much, heee uzembe mijiTU kazi ufisadi tu wanyonge wanazidi kuumia, ila iko siku na nyie Yatawafika nyie subirini tu. nina hasira kweli hapa nilipo upuuzi mtuPU, bahati mbaya excuse me, give me a break.

    ReplyDelete
  26. Jamani nyie watendaji wakuu wa nchi hii hivi kazi yenu ni nini haswa?? Kuuza rasilimali za tanzania au kuwaangalia na kuwatumikia wananchi wa Tanzania?? we fep-up kwa kweli we need to see some one is staped down hatuwezi kukaa kimya tena mwanzo mmeua watu kibao now tena jamani jamani ah

    ReplyDelete
  27. "Mh. Lukuvi amesema serikali itagharamia kila kitu"..basi hapo wamemaliiiza, wenyewe - pilau la sadaka!..kufa ni ahadi; kufa kizembe, haikubaliki!..labda vifo vya mwanzo vilikuwa bahati mbaya..hivi sasa ni vya uzembe..alosema 'atajiuzulu' sijui bado yuko 'serious'?..

    ReplyDelete
  28. Mkuu mmoja wa Jeshi Nakumbuka anaitwa Shimbo alitangaza kuwa Mbagala sio salama kuishi .na baadhi ya watawala wakamjibu kuwa ni salama.
    Inauma sanaaa, inasikitisha .hali hii kupoteza mpendwa wako , sijui tufanyeje maana najua mbagala ni sie wanyonge!
    Mungu alaze roho za marehemu salama .
    Amin

    ReplyDelete
  29. Mungu Awalaze mahali pema peponi Marehemu!Na poleni wajeruhiwa na Wafiwa!:-(

    Lakini kweli muda wote huu tokea mabomu yalipuke mara ya kwanza safari ile haikujulikana kuna mabomu ambayo hayakulipuka na yayaonekani?

    Au ndio tuseme jeshi letu halijui hata lina idadi gani ya mabomu?:-(

    ReplyDelete
  30. Halafu eti tunasema I LOVE TANZANIA eti I LOVE AFRICA . mimi sipendi kua mwafrica na sipendi kabisa kjivunia uafrica, Uafrica ni roho mbaya , uchoyo , ubinafsi na kutopenda kujali usalama wa wengine .
    Imagine ingekua ni USA or Nchi za magharibi kitu kama hicho kimetokea ingekuaje? wange watendea haki raia kiasigani, je wange hufu uslama wa raia wao kwa kiasi gani ? je wangeajibishwa wazembe kwa kiasi gani? jibu unalo uliye kaa nje ya TZ.
    tusisingizie bajet wala hali ya uchumi ni roho mbaya tuu , ndio maan hatubarikiwi siku zote sisi wafrica kwani hatupendi majirani zetu kama tunavyo jipenda sisi .

    ReplyDelete
  31. Poleni wafiwa wote, Mungu awapumzishe pema ndugu zetu waliopoteza maisha, Amina.

    Turudi kwenye upande wa pili. Hebu tuache ujinga. Kwa nini serikali haionyeshi kuwajali wananchi wake? Shida ya wananchi wake sio kugharimiwa gharama za mazishi. Wananchi wanataka kuhakikishiwa haki yao ya kikatiba ya kuishi na kufurahia maisha. Kifungu cha 14 cha katiba kinatuhakikishia haki hiyo. Mabomu ya serikali yanapoua raia wasio na hatia ina maana serikali haijatimiza wajibu wake kwa wananchi wa kuilinda haki yao ya kuishi.
    Kwa nini mpaka leo wataalamu wa mabomu (wa ndani ikibidi watafutwe hata nje kama hawatoshi) hawajafanya msako wa nyumba hadi nyumba, mtaa hadi mtaa, kusafisha mabomu yote kwenye maeneo jirani? Kwa nini haijatolewa elimu ya kuwezesha wananchi kutoa taarifa sehemu wanapoona vitu vinavyotia mashaka? Ingekuwa mabomu yamelipukia wawekezaji mpaka leo kungekuwa hakujafanyika kitu???? Kwa nini? Why? Ni roho za wananchi walipa kodi hizi.
    Kunradhi wadau lakini hili tukio limenighadhabisha.

    ReplyDelete
  32. YEH RIGHT! SERIKALI ITAGHARAMIKIA KILA KITU...WHAT ABOUT THE WASTED LIVES? HOW CAN THE FAMILIES RECOVER THEIR LOVED ONES?

    ReplyDelete
  33. Jamani kweli serikali yetu yafanya nini kuhusu hili?kwanini wasihamishe kituo cha mabomu nje ya mji?kweli hii ni haki kuweka silaha hatari kwa makazi ya wananchi na kusababisha maafa si mara moja bali zaidi ya tatu?Huyu Kikwete lazima afanye ufumbuzi haraka lasivyo serikali yake inatuvunja matumaini watu.Michu najua uko karibu na president twaomba ufikishe hili kwa muheshimiwa.shukrani

    ReplyDelete
  34. kaka michu,

    habari za masiku telekuna mdau mmoja amegusia habari ya shule yenye ugonjwa wa swine flu hapo mikocheni.. mimi nimeiskia pia shule hiyo iko hapo kwa mzee wetu mwinyi opposite inaitwa DIS habari yao ni nzito kidogo

    kuna watoto wameumwa hapa na bado wazazi hakuambiwa kama kuna watot wa darasa la nne wanaumwa huo si uuaji?

    nakuomba ufuatilie kwa ukaribu ili swala utupe maelezo ndugu yetu sisi tulio mbali tuna watoto wanasoma hapo

    nenda muhimbili kaongee na wazazi inatia uchunguuuuuu

    hao ni watoto hao !!!!worse enough shule hiyo imechanganywa kwenye compaund moja watoto wa nursery,primary na secondary upo hapo !!!!!

    wapi waziri wa elimu ?haki za watoto wapi ? wazazi nao wapi hal,ashauri husika wapi mi nalia tu


    Tanzania zaidi uijuavyo.....

    Nawakilisha

    ReplyDelete
  35. Naomba mawaziri na wabunge wawaambie viongozi wanaohusika WAJIUZURU.

    ReplyDelete
  36. Shule gani mikocheni? kama jina linaweza kutolewa. Ingependeza jina la shule husika likatajwa, la sivyo kukaa kimya hakuna tofauti na matokea yaliyowakuta watoto wetu wa mbagala.

    ReplyDelete
  37. 1 thing, Waziri wa ulinzi, waziri wa mambo ya ndani, wakuu wa jeshi na vitengo vyao wote wawajibishwe kwa uzembe wa kushindwa kulinda raia na mali zao.

    Uzembe wa kwanza ulifanyika na watu kibao walikufa na wengine wakapoteza makazi yao! Kipi mliwapatia? Pesa za kununua maji! Swali, unaweza kununua uhai wa binadamu kwa pesa? Hatutaki pesa itumike kama kuwafumba macho hawa raia wasio jua haki zao bali tunataka hao wazembe wahusika wafanye kazi ipasavyo ya kuweza kulinda raia na mali zao, kama wakishindwa kufanya kazi wote wakae chonjo.

    Tusichezee maisha ya binadamu wenzetu kwa vitu ambavyo vinaweza kuzuilika kabisa, Serikali inabidi ipeleke haraka sana team ya wataalam wa mabomu na kuweza kuyatafuta na kuyaondoa ktk maeneo yote husika. Ni aibu kwa Taifa hili, kila kitu kinachofanyika ndani ya nchi hii ni ujinga ujinga tu!!!! Hakuna Viongozi wenye kujishughulisha, cha maana wao wanawaza ni jinsi gani ya kuweza kuliibia Taifa na raia zake badala ya kuwalinda na kuwatafutia maisha na mazingira mazuri.

    Pia tunataka tamko la Serikali ikielezea ni kitu gani kimefanyika tokea mlipuko wa kwanza, juhudu gani zimechukuliwa kuzia matukio haya, Ni wakina nani waliwajibishwa?, Je hamkuweza kufikilia after effects za tukio la kwanza????????????????

    Inatia huzuni, Hasira kusikia mpaka leo watu wanapoteza maisha yao kwa kitu kilichotokea mwanzo, Tutajifunza lini? Kama mwanzo mliira bahati mbaya, Hivi sasa nini?

    Kikwete please do something NOW Uozo umezidi.

    ReplyDelete
  38. SASA KAMA NI HIVYO PESA WATAPATA WAPI WAKATI TRA, KUNA MAFISADI WANATEGESHEA WATU WAKILETA VITU WAWALIPISHE KODI 120% BADALA YA 18% KISHA WANAJIKATIA CHA JUU, KWA MTAJI HUO WENGI WAKIMBILIA KUTELEMSHA MIZIGO MOMBASA NA SERIKALI INAKOSA KODI NA VILE VILE BADO HAFINYI HARAKA KUWAKAMATA MAPEMA KAMA AKINA LYUMBA WA BOT.
    FANYENI HIMA ILI NA SISI TUANZE KUPITISHA VITU TENA BANDARI YA BONGO ILI MMPATE PESA YA ZIADA KWA KODI YA 18% ILI MAPATO YENU YAONGOZEKE.

    ReplyDelete
  39. Hayo mabomu naamini bado yako mengi na usishangae miaka kumia kuanzia sasa yakaua tena, serikali ianze shughuli ya kuyategua hayo mabomu kwa kutumia bomb sniffing dogs ambao natumaini wanao hawo mbwa,ama sivyo utaalama wowote utumike kulinda uslama wa raia,hilo jeshi lipo tu limekaa vita vyenyewe hakuna,vitambi tu,
    mdau songea

    ReplyDelete
  40. TANGAZO:
    Ninauza nyumba Mbagala karibu na jeshi ina three bedrooms , car park ,hot water supply, garden ya nguvu na sebule kubwa ya kutosha.
    BEI maelewano ila naanza na SHS 120,000.00 na inaweza shuka maelezo zaidi tuwasiliane.

    ReplyDelete
  41. MASHAKA TAFADHALI SANA TUNAOMBA NA WEWE UCHANGIE HOJA KAMA WADAU TUNAVYOTOAGA MAONI KWENYE MADA ZAKO NDEEEFU MBONA WEWE ZA WENZAKO UNACHUNAGA ?? USIPOCHANGIA NA WEWE USILLETE HOJA HUMU NDANI FULLSTOP!!! sasa wee ni mwanajamii gani ?? toa maoni bwana alah!!

    ReplyDelete
  42. ndiyo maana mimi nina sema bila Mashaka kuwa Rais na Michuzi kuwa waziri wa habari nchi haita enda vizuri watu wengi wamekwisha kuwa corrupt. hafazali michuzi amekaa sana nje na mashaka kwanza kazaliwa over seas Kenya. haya matatizo yanatokana na ulimbukeni wa viongozi wetu hawajasoma na wengine hata ndani ya KLM hawajaonja kama kina Michuzi na Mashaka...Mungu wasaidie wapite wapate madaraka matamu

    ReplyDelete
  43. ikifikia apa ndipo ninatamani ningezaliwa sijui wapi..kuliko ku-keep with these stupid pple na uzembe

    eti bahati mbaya sijui uchizi

    ReplyDelete
  44. MASHAKA YUKO MAWINDONI ,WEMA WAKE WOTE ANASUBIRI MALIPO. INABIDI TUMPIGE SHULE TUMFUNDISHE HESABU APUNGUZE MANENO MEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEENGI. ILI TUWEZE KUMSOMA KWA MUDA MFUPI. ONA KAMA HOTOBA YA JLIAS KAISARI ( WE WENT WE FOUGHT WE WON)JEMEDARI WA JESHI LA KIRUMI.

    ReplyDelete
  45. Naomba watanzania wenzangu tuache kutumia neno BAHATI MBAYA...there is no such excuse ktk dunia ya sasa... Maisha ya mtu hata ukigharmia vipi huwezi kuyalipaaaa...

    Mungu ailaze roho za marehemu mahali pema peponi...
    Ni si bahati mbaya but ni uzembe wa haina flan...ni bora kuomba msamaha na kukili kutorudia tena than using bAHATI MBAYA say...

    ReplyDelete
  46. NI UZEMBE WA SERIKALI KUTO SAFISHA VIZURI BAADA YA TUKIO LA MABOMU LILILOPITA HAO WATU WAPASWA KULIPWA FIDIA, WAIBURUZE SERIKALI MAHAKAMANI, WANASHERIA WA HAKI ZA BINADAMU SAIDIENI HAO MASIKINI YA MUNGU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...