CRDB mmesitisha huduma za Tanzanite Account huku UK kwa sababu ambazo sisi hatuzijui kabisa. Tukiwauliza mawakala wa hapa UK wanadai wao siyo tena. Tukienda ubalozini napo ni taabu. Kwa kweli Mh. Kimei unapoanzisha kitu jaribuni kutazama mbele ili mfahamu matatizo na faida.
Afisa wa Tanzanite Account Jenifer amekuja hapa UK zaidi ya mara nne lakini cha ajabu nothing was done regarding Tanzanite. Alichukua maoni ya clients wote kwamba atakwenda kuyashughulikia lakini hakuna kitu kilichofanyika zaidi ya kusitisha huduma ya Tanzanite kupitia mawakala wake wote hapa UK.
Mlikuwa na mawakala wazuri sana, hasa yule kijana wa Reading ambaye alifanya Tanzanite ikarudi tena kwenye chati kuliko wakati Jennifer ulipokuja hapa UK 2001 ukachukua form bila kuleta majibu.
Huyu bwana alirudisha hadhi ya Tanzanite japokuwa ghafla tukasikia amefukuzwa. Kijana kama huyu alitakiwa kuwa trained ili hata akirudi basi awafanyie kazi. Jenifer na wenzake waulizwe walifanya nini cha maana?Japokuwa wanadai tumeshindwa ku deposit pesa.
Mh. Kimei badilika ili uwafanyie watanzania kazi siyo sie tukufanyie kazi. Majibu tunayopewa na wafanyakazi wako siyo mazuri. Yaani kama ungekuwa na facility ya ku-record msg ungesikitika sana na majibu ya wafanyakazi wako.
We need changes to CRDB bank and to all Tanzania. Tunakuomba utujibu maswali haya kupitia kwenye hii Blog ya Jamii.
Pia new website ya crdbbank ni nzuri but inahitaji iwe user friendly kwa wale wasijua copmputer na pia nilipokuwa naipitia nimeona kuna tatizo kwenye option ya Rates ,when you click nothing happened.
Asante
Mdau Achora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. CRDB matatizo yapo ila sina uhakika na matatizo ya... CRDB matatizo yapo ila sina uhakika na matatizo ya wizi, sidhani kama mfanyakazi anaweza kutoa pesa bila documentation yoyote kwa hivo maneno ya kwamba wafanyakazi wanaiba, nafikiri yanahitaji uthibitisho, tusiseme tu kwa sababu ya hasira. Mambo ninayoyaona ya msingi ni haya.
    1. Benki ina charges zake kwa wateja wenye akaunti za Tanzanite, wakati mwingine hizo charges haziwi wazi kiasi kwamba wateja wanapokatwa wanahisi kwamba wameibiwa. Benki wajitahidi kuwa wawazi kuhusu gharama za namna hiyo.

    2. Mawasiliano ni mabovu kidogo, wateja wengi wanahitaji kupata majibu ya maswali au malalamiko yao, lakini CRDB makao makuu imeweka mtu mmoja tu kuhudumia Tanzanite account, kama hiyo account ni ya wateja wote walioko nje ya Tanzania, maana yake ni kwamba huyo mtu anahudumia dunia nzima, atawezaje kuwa na ufanisi katika mawasiliano wakati anapokea email na simu zisizopungua mia moja kwa siku? Poor planning on the management side!

    3. Siasa katika biashara. CRDB na mzee wao Kimei wamefunikwa sana na siasa kuliko biashara. Mzee Kimei hata apewe maoni gani ya maendeleo, kama hayamfanyi awe maarufu kisiasa, au kama hayampi sifa ambayo wakubwa zake wataiona, au hilo jambo halimnufaishi binafsi, mara nyingi huwa anayafunika. Kimei hukubali kufanya mambo ambayo public itayaona wazi, kwa mfano kutoa dollar 100, 000 za kufadhili mkutano wa Sullivan na kuhakikisha umetangazwa kwenye tv, huo ndo mfano wa mambo anayoytaka, lakini si kuboresha Tanzanite ambayo itawasaidia watu kama mimi na wewe.

    Kwa hivo kwa mtazamo wangu nafikiri tusilaumu wafanyakazi tu, bali uongozi mzima wa CRDB. Kuna ma Director wenye moyo wa kazi, na wanapokea ushauri vizuri kabisa toka chini, lakini wakienda kwa Kimei, hawasikilizwi, labda wapitie kwa watu "muhimu' na nasema "muhimu" kwa Kimei ambao anawasikiliza zaidi, watu aliowashiba. Najua watu watafikiri huu ni uzushi, lakini Mzee Kimei aache kufanya kazi kwa kuwa influenced na siasa, na afanye kazi kama Dr. mwenye profession yake nzuri tu.

    Executive Director huwezi anzisha kitu halafu kikaendelea kulega lega na usiwe concerned, it bothers me kwamba watanzania wenye elimu ya kutosha wanashindwa kuendesha biashara na kumanage vizuri, badala yake wanagubikwa na mapenzi na siasa.
    Ukiangalia uongozi wa Kimei CRDB, kukiwa na jambo atasikiliza wadada fulani tu au amri toka kwa waziri au Raisi. Well stand up for yourself dude, na ufanye kazi. Si kwamba successful managers hawana wasichana, but they differentiate kazi na mapenzi.
    Kwa hiyo ndugu zangu jambo la Tanzanite ni kubwa kuliko hivo tunavyofikiria kuwa ni uwizi wa wafanyakazi. Kimei ameweka mdada kwenye Tanzanite account, na huyo mdada anaripoti kwa mdada mwingine ambaye ndiye anamshauri Kimei. na hawaivi kwa sababu wanajuana. Unafikiri kuna swala la Tanzanite litafanyiwa kazi hapo.
    HEBU KIMEI JISAFISHE UFANYE KAZI YA WATANZANIA, HIVI VILIO VYA WATU MSIVIKALIE KIMYA KAMA VILE NYIE NI MALAIKA. HUWA VILIO KAMA HIVI HAVIENDI BURE.

    Nawasilisha, na nimawazo na maoni yangu binafsi.

    Mdau wa kweli

    ReplyDelete
  2. NAOMBA NA MIE NIONGEZEE KILIO CHANGU, NI MWAKA WA PILI SASA TANGU NIMEFUNGUA HIYO ACCT NA NILICHOPATA NI TEMBOCARD TU, PIN NAMBA NIMEFUATILIA MPAKA NIMECHOKA NA HIVI NASUBIRI NIENDE BONGO NIKAWATUSI KIDOGO THEN NIWATUPIE KADI YAO.
    NI WEZI MAANA WAMECHUKUA PESA ZETU ZA ADMIN HALAFU HUDUMA ZENYEWE BOGUS, MIE USHAURI WANGU JAMANI TAFUTENI NJIA NYINGINE ZA KUHIFADHI PESA ZENU KWANI KAMA TU SASA HIVI MAMBO NDIYO HIVI VP JE KUKITOKEA PESA ZIMEPOTEA KUTOKA KWENYE ACCT YAKO UNAFIKIRI KUNA MJINGA YOYOTE PALE CRDB ATAKUELEWA.
    NIMALIZIE MASIKITIKO YANGU KWA KUSEMA TANZANIA SCORE IS ZERO WHEN IT COMES TO CUSTOMER SERVICES AND HOSPITALITY.
    MDAU.

    ReplyDelete
  3. Maswali, Majibu na maelezo vyote unavyo mwenyewe:

    "Alichukua maoni ya clients wote kwamba atakwenda kuyashughulikia" ...."

    Bila shaka baada ya kuyafanyia kazi maoni yenu

    "kilichofanyika" ni "kusitisha huduma ya Tanzanite kupitia mawakala wake wote hapa UK"

    ReplyDelete
  4. I love the way people do business in Bongo!!! Tehe tehe tehe!!!
    Mimi sidhani kwa nini msumbuke wakati western union ipo. Labda mna hitaji tu kuumiza vichwa vyenu. Iweje umpe business mtu ambaye hakuthamini wewe kama mteja?

    Kwa wale walio Bongo na hawana choice, watumie tu huduma za hawa mataahira. ila kwa wale mliopo nje ya Bongo, tabu zenu mnazitafuta wenyewe, western union wapo na wengine pia, kisa hasa cha kutumia CRDB ni nini? Mimi nadhani ninyi ndo wenye matatizo ya ubongo, mnapaswa kutibiwa.

    ReplyDelete
  5. Wadau mimi pia na account yangu pale CRDB, unajua mwanzo ukifungua akaunti nao hakuna charges zozote, ila nilipokuja kusoma maelezo nikaona kuna monthly charges yule dada Jenipher Tondi alipokuja hapa UK nikamuuliza ni kiasi gani mnacharge kwenye hii akaunti kwa mwezi ni flat rate au kwa percentage akanijibu kwa sasa hatujajua ni kiasi gani tuwacharge ndiyo maana hakuna hata mteja mmoja aliyeanza kuchajiwa ila tukiwa tayari tutawataarifu.
    BASI MIMI NIKAWA NAJUA MKWANJA UPO TU KWENYE AKAUNTI NA NILIKUWA NIKITOKA KUPIGA BOX CHOCHOTE NACHOPATA NATUMBUKIZA MPAKA KAKITABU WALINITUMIA CHA KEWEKEA MKWANJA Lloyd TBS.
    CHA AJABU NILIPOKWENDA BONGO MAHESABU YAKAWA HAYAWIANI NA MIMI NINAVYOJUA KIASI GANI KIPO KAPUNI MWAO. SASA HAPO NDIYO NIKAAMBIWA KUNA CHARGES ZA KILA MWEZI,NIKAULIZA BILA TAARIFA MAALUM KWELI?
    NIKAWATOLEA UVIVU KIDOGO NIKAWAELEZA HUKO TULIPO MNAZANI HAKUNA SERVINGS ACCOUNT AU HATUNA BANK ZINAZOTOA HIZI HUDUMA? KWANZA DUNIA HII UMEONA WAPI SERVINGS ACCOUNT INACHAJIWA RIBA BADALA YA NYIE MNIWEKEE RIBA SABABU NAWEKEZA KWENU SIYO CURRENT ACCOUNT HII NAFAIDIKA KWA CHOCHOTE. KWA MANTIKI HIYO HAWA JAMAA NI WEZI KUTUIBIA VIJISENTI VYETU VYA MABOX FULL STOP.OGOPA CRDB CURRENT ACCOUNT KAMA UKOMA WATAWAMALIZA WANASEMA WANATUSAIDIA MSAADA WAO UKO WAPI WEZI WAKUBWA NYIE.

    ReplyDelete
  6. Kwa ujumla CRDB wana urasimu sana kwa huduma nyingine zaidi ya ku-deposit hela,siku moja niliomba wanitengenezee demand draft ilichukua siku 4. wakati bank nyingine wanatoa ndani ya nusu saa.
    Kwakweli CRDB wanatakiwa wabadilike kuendana na wakati.matangazo kibao kwenye mabako lakini huduma za hovyo kabisa.

    ReplyDelete
  7. Nimekumbuka uzoefu nilioupata nilipojaribu kwenda kujaribu kufungua Tanzanite account. Kama kawaida ya wabeba boksi nilikuwa nimepiga mavazi yangu simpo na casual. Nikaanza kumuuliza mhusika maswali ili niweze kufanya maamuzi. Mhusika alirudiarudia mara kadhaa kwamba hii ni akaunti maalumu kwa Watanzania wanaoishi ughaibuni. Baada ya kuona amekwama hapo ikabidi nimwambie napiga boksi. Nikapewa maelezo lakini nikaona wanatoza pesa nyingi sana, ukizingatia ni akaunti ya akiba na malengo yangu hayakuwa kuchomoa hela mle mara kwa mara. Kwangu uamuzi bora ulikuwa kurudi ughaibuni na kufungua akaunti kwenye benki tofauti na niliyokuwa natumia kwa ajili ya akiba. Sitozwi hata thumuni kwa akaunti hiyo. Nikiamua kutinga bongo nabeba uchache wangu natambaa nao.
    Poleni mliokutwa na ya kuwakuta.
    CRDB hii akaunti ingewasaidia sana kuwa na dola na yuro kama mngepunguza utozaji wa fees. Transfer fees, monthly charges etc zina deter watu wasifungue matokeo yake hamzishikilii hizi pesa. Rekebisheni hiki kitu la sivyo NMB inaweza kuwapiga bao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...