Habari za kazi ndugu Michuzi,
Natumai unaendelea vyema kabisa na shughuli za kila siku.Kuna jambo nataka ushirikiano na wasomaji wa blog ya jamii. Mie ni mwanafunzi na nasoma India. kama inavyojulikana India hawaruhusu kubeba boxi ukiwa denti. Hivyo wengi tunategemea pesa za kujikimu kutoka kwa Wazazi/Walezi ama Wafadhili mbalimbali.
Kuna njia nyingi za kutumiwa pesa lakini wengi tuliona ni muhimu kuwa na account ya Tanzanite(CRDB),mwanzoni nilikuwa nasikia watu wengi wakilalamika kwamba account hii inasumbua, haswa linapokuja swala moja kwamba mtu anaambiwa ame overdraw hivyo account yake ina deni.

Kuna watu wameacha kutumia baada ya kuambiwa wana madeni makubwa wanadaiwa. Je, naomba kuuliza kwenye account kukiwa na millioni 1 bank inaweza kukupa millioni 2? haswa ukifikiria huduma yenyewe tunatumia ni ya Tembocard?

Kwa kawaida viwango vya makato baada ya Transaction huwa vinajulikana lakini kwa bank hii ya CRDB mwisho wa siku mtu unaona maluweluwe na kweli nami wameniambia wananidai hivyo wamekata pesa zote ambazo nilipaswa kupata na bado wanasema nadaiwa 27,000 ya Kitanzania!

Swali muhimu ni hivi Tanzanite account inatakiwa iwe na 5000 rupees ama 100usd na si chini ya hapo?? Je, inakuwaje mtu ana draw pamoja na hizo 5000rupees na zaidi? tuseme machine zina matatizo ama mfumo mzima una matatizo ama wafanyakazi wa CRDB bank wana mbinu zao?

Maana kama mchezo ni huu watakuwa wanatumaliza sie vijana tunaotoka familia za chini. Je wadau tuendelee na Huduma hii ama turejee kwenye West union,money gram ama bank zingine za kimataifa kukwepa hatari hizi?
Mdau aliyelizwa India

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Kimei wafafanulie vijana.

    ReplyDelete
  2. KIUHALISI NCHI MASIKINI NA NCHI TAJIRI HUDUMA YA JAMII NI TOFAUTI. MFANO TANZANIA UKIENDA KUPATA HUDUMA OFISI YA SERIKALI AU SHIRIKA LA UMA MUHUDUMU ATAPENDA AKUONGEZEE VIKWAZO ILI UONE UGUMU WA KUPATA HIYO HUDUMA NA INAFIKIA KWAMBA MWANYA WA RUSHWA UNAPATIKANA.NCHI ZILIZO ENDELEA MFANYA KAZI ANAHAKIKISHA ANAMUHUDUMIA MTEJA KWA HAKI NA KWA URAHISI WA HALI YA JUU . AKIKOSEA KIDOGO ANA HAKI YA KUFUKUZWA KAZI. KWAHIYO MPAKA SASA TAZANIA KWA UFANISI WA WAFANYA KAZI IKO NYUMA KIASI KIKUBWA AJABU. KUNA WATANZANIA WANAPESA ZA HAKI WALIO NJE YA NCHI LAKINI HAWARUHUSIWI KUFUNGUA ACCOUNT WAKIWA NJE PESA ZINAPOTEA HIVIHIVI. ZAMBI YETU YA ASILI NIKUONA WATU HAWAFANIKIWI. NAKARIBIA KUNYOOSHA MIKONO TZ4CHANGE INAKUWA NGUMU SANA

    ReplyDelete
  3. CRDB hawaruhusu overdraft ila kwa huduma ya visa huwa unaweza ukadraw ukalipwa na visa hlf wenyewe wakati wa settlement usiku akawalipa visa so visa huwa na ile initial balalnce ,sasa kama unaweza kuwatyme unaweza ukadraw benki mbili tofauti at the same tym ukia nje kwa hiyo unapata over drat ila ukija baadae kuweka hela wanakata.Mimi nimesha tumia sana hizo na shukuru siku ya mwisho nataka niwapige overgraft ya paundi 200 system ikagoma ikabidi nibaki kuwa mteja wao hivi hivi ningelamba hiyo ningeingia mitini.siunaju a wabongo kulipa deni ukimkopesha tu anainngia mitini kwa mbongo over draft haifai iwe ulaya au bongo wabongo WEZIby nature

    ReplyDelete
  4. nakushukuru sana mdau wa india maana nilikuwa mbioni kumuuliza mzee wa libeneke aende kwa wataalamu wa CRDB aniulizie kama nikichukua pesa kupitia saving account kwa VISA electronic huku india nitakatwa kiasi gani kwa kila nitakapo toa pesa hapa india kwenye benk km icici,citi bank,na benk zingine
    pia nilitaka kujua ni ammount gani wanatumia nikitoa pesa yaani kutoka kwenye madafu kuja kwenye rupees wanatumia kiwango gani? maana pesa huwa inabadilika mara 1rps =27tshs kwahiyo nilitaka kujua hilo kwakuwa kuna ndg zangu wanatumiwa pesa kwenye account yangu na tunapata shida hata tukiangalia exchange rate kwenye net nakuomba sana anko michuzi unisaidie kwa hili
    mdau india hyderabad
    nakupa e-mail yangu kwa jibu jjozzee@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. Tanzanite account ni wezi kweli,mie nilifunga account yao baada mwezi tu,walikua wanakata hela bila ya ridhaa yangu,muwe macho sana.

    ReplyDelete
  6. Doh nashukru kwa hizi comment chAche tu zimenipa mwangaza wa kutokufungua hii account. Tanzania ni moja ya nchi nilioamua kukata tamaa nayo. Hakuna haki kwa chochote kile....Kuna mengi ya kuongea ila hapa si uwanja wake. Asante wadau waliotoa mwangaza kiasi.

    ReplyDelete
  7. Michu kwanini usimshute kigogo au mtu wa CRDB ajibu swali hili maana linatusumbua wengi, na mimi niko kwa Obama kila nikicheki balance nakuta imeshuka

    ReplyDelete
  8. CRDB Tanzanite account ni matapeli wala msijihusiche nao, Mtapoteza pesa zenu bure, kama unataka kuwapa pesa zako bure basi fungua account nao.

    ReplyDelete
  9. mchagga halisiSeptember 01, 2009

    ndugu zangu jaribuni kutumia HSBC BANK kutoa hela zenu utakua na uhakika zaidi kama umeliwa au vipi kwa sababu wanaonyesha balance kwa Tshs.so mapema tuu kabla hujatoa utatua iko kiasi gani,pia hawana makato kibao kama bank nyingine.

    ReplyDelete
  10. Malengo ya hii akaunti ni mazuri sana. Tatizo kama ilivyo katika mambo mengi Tanzania, hakuna watekelezaji wenye kujua wanachokifanya.

    Hii huduma ingetusaidia sana sisi tulio nje, tena ingetufanya tupeleke hela zaidi nyumbani kuliko ilivyo sasa.

    CRDB wangekuwa na kipeperushi kidogo, kwenye tovuti yao pembeni ya Application Form kinachoelezea Terms & Conditions zote pamoja na Questions & Answers za maswali yote wanayoulizwa na wateja kila siku kuhusu Tanzanite account haya malalamiko yangepungua kwa 99%.

    Ushauri wa Bure kwa Ms Jenifer Tondi na timu yako hapo CRDB.

    ReplyDelete
  11. Tumia western union, achana na longolongo za wabongo. Pesa yako inakupa tabu kisa nini?

    ReplyDelete
  12. moneygram ndiyo the cheapest way,western union huduma zao ni ghali.

    ReplyDelete
  13. Asante mdau wa India kwa kutufahamisha kuhusu Tanzanite Account. Nilikuwa nafikiria kufungua hiyo Account lakini sasa basi.

    ReplyDelete
  14. MIMI NIKO CANADA NATUMIA WASOMALI KUTUMA PESA BONGO NA KUJA HUKU HUWEZI KUAMINI JAMAA WAKO SAFI SI MCHEZO.ACHANENI NA HIZO BENKI ZA KIBONGO NI LAANA

    ReplyDelete
  15. E bwana mdau wa India ...bora wewe umepata moyo wa kuirusha hii kwa michuzi!

    Kwanza nchi yetu hatubadiliki ..wao CRDB wanafanya jitihada za kutangaza Tanzanite na kula hela za bure kabisa za wenye Hisa kwa kuwatafuta wateja bila kuweka mipango madhubuti ya kuwatunza...

    Mimi nina hiyo account lakini kwa sababu ya mizengwe nimeshidwa kuanza kuitumia kabisa ..nilikuwa na maswali ambayo yangejibiwa then ningeanza kutumia account yangu lakini jitihada zangu zimekuwa hazizai matunda ikiwa ni pamoja na kumuandikia email Jennifer Ntondi!!

    Swala la mawasiliano nyumbani hata kwa watu wenye exposure na shule zao bado ni tatizo ..kazi umepewa ni kwa nini usiifanye?

    Ngoja nimuulize Jennifer kwa sababu ndi ye mwenye dhamani ya Tanzanite ..em niambie churn rate per month ya TANZANITE...naona inazidi hata subscription rate....

    Em tujifunze ..tuwaelemishe wateje vema ..ili waweze kuweka pesa zao nyumbani kwa maendeleo ya nyumbani!!

    Jamaaaaaaaaani Tanzania tubadilike!! nyakati zile za zamani zimepita ....
    CRDB WE NEED CHANGE NOW!

    ReplyDelete
  16. Asante sana mdau kuleta mada hii. Mimi wameniliza euro 1000 hivi hivi hati hawajui zimeenda wapi. sasa sijui kama bank yenyewe ndo wezi au wafanya kazi ndo wezi. sisahau walivyonisumbua nilipokwenda kuchukua pesa pale azikiwe yaani mpaka nimeenda kuongea na manager ndo wakanipa huku euro 1000 zikiyeyuka kisha wamebakiza euro 100 kama balance nami nimewaachia sitoweka pesa kwao tena hawa jamaa.

    ReplyDelete
  17. pole mdau uliyetokwa euro 1000 kumbe ulikuwa hujui. CRDB wezi sana. na wanaoiba ni wafanyakazi wake si benki. wafanyakazi ndo wana tabia ya kuiba toka kwenye account za wateja. tena wanaoweka hela kwenye tanzanite account ndo wanalizwa ile mbaya kwa maana wanafahamika wako nje ya nchi. tatizo la wafanyakazi wa benki kuibia wateja wao limekuwa sugu sasa tanzania, wafanyakazi wa benki wanaiba sana hela za wateja inabidi uwe unaangalia akaunti yako kila siku hasa kama umeqweka CRDB hupo ndo wanakwiba kwelikweli

    ReplyDelete
  18. ooh..my God..!Nilifungua account 2007,lakini niliweka pesa za madafu Tzsh.

    Account ilikuwa nzuri na familia yangu waliitumia vizuri tu.Lakini sija check my account since June 2008.

    Ngoja ni check sasa hivi.Mnatisha

    ReplyDelete
  19. Wadau, mi ninayo hiyo account kwa miaka miwili na sina tatizo wala sijaibiwa. Nina internet banking in both of my accounts USA Dollars and TSHS.Sina malamiko yoyote wenzangu waliyoyatoa. Tatizo nililoliona nilijaribu kuchukua pesa in Visa card ambayo lazima itoke kwa tshs account ni echange rate ilikuwa chini kidogo.

    Madu, Washington, DC

    ReplyDelete
  20. usiumize kichwa chako, wewe funga Account hiyo ya tembo.
    ukihitaji pesa wakutumie kwa njia nyingine kisha weka kwenye bank za huko,utaumiza kichwa kwani CRDB ina makato mengi.
    Mimi mwenye nina kampuni na ninasafiri nje mara kwa mara situmii A/C za CRDB za nje zina makato ya mizengwe(hidden charge). thanks.

    ReplyDelete
  21. Tatizo watanzania hasa waishio nje wana asili ya kulalamika mno na kujisahau asili yao na nchi waliyotoka kuwa bado ni nchi ya ulimwengu wa tatu na haiwezi kufikia nchi mlizopo zenye technolojia ya hali ya juu mno. Ukweli ni kwamba hiyo Bank ya CRDB imejitoa kafara kuanzisha akaunti ya watanzania waishio nje ambayo hamna benk nyingine imedhubutu..labda tujiulize kwanini. Mimi nadhani Bank inania nzuri sana na wateja na watoa huduma wanajitahidi kwa uwezo wao wote kutoa huduma sahihi ila bado kuna madhaifu yanayokwamisha huduma bora na ya haraka na hili hasa linachangiwa na ufinyu wa tekinolojia. mimi naamini timu ya CRDB bado wanaendelea kujifunza na kurekebisha yale madhaifu yanayojitokeza katika bidhaa zao. Mimi ni mteja na ukiangalia faida za bidhaa pengine ni nyingi kuliko madhaifu. Watanzania tujifunze kuthamini vitu vinavyotoka kwa wazalendo wenzetu na si kukumbatia na kuthamini vya wenzetu waliotutangulia.Roma haikujengwa kwa siku moja,tukishirikiana tutafika.BE POSITIVE!!!!

    ReplyDelete
  22. Anonymous 08:31AM stop making excuses for the CRDB! Matatizo si kutojua matumizi ya technolojia bali ni wizi: plain and simple. Na nyie ambao mnatofautisha kati ya wizi wa Benki na wizi wa Wafanyakazi mnafanya makosa. Management ya Benki ndio ya kulaumiwa kwa usimamizi mbovu ambao unatoa mwanya kwa wafanyakazi wao kuweza kuiba bila consequences. Kuna huduma nyingi siku hizi za kutuma pesa. Kama CRDB wamekuibia, achanena na hudumu zao iwe kama fundisho sivyo tutaendelea kulea uzembe na wizi. Hebu fikiria, kama wanaweza kutumia sababu ya kutoelewa teknolojia kuiba pesa za wateja, watakuwa na incentive gani kufanya mabadiliko ya haraka yatakayosimamisha wizi? Lugha wanayoelewa hawa ndugu zetu ni kukuosa wateja wa kuibia. HAMENI IKIBIDI.

    ReplyDelete
  23. minaona niungane na mdau wa texas. labda kijana wa india utueleze unaibiwaje na iweje wewe tu mbona sisi huku bongo tuna account na crdb natunatumia hiyo visa card nahatuoni hatuoni tunaibiwa?
    CRDB Mko juu msikate tamaa nyie songeni mbele kuwa bank namba moja ya kizalendo!

    ReplyDelete
  24. Mungu ibariki CRDB Mungu ibariki Tanzania,mimi mdau wa hiyo Benki nakua nje ya nchi kibiashara hela natoa kwa tembo card na wala sipati tatizo. Kimei na Timu yako tunawapa bigup hao watanzania wahindi wazushi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...