twanga wakipepeta uwanja wao wa nyumbani, mango garden, kinondoni jijini dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hiyo kinyonga ndo kali zaidi ya maelezo,idumu twanga......

    ReplyDelete
  2. Twanga ugaibuniOctober 19, 2009

    yeah! wapi Bokilo? Rudi nyumbani uchangamshe aquadi!
    Mabinti mnaweza kazi lakini punguzeni intake ya carbohydrates!

    ReplyDelete
  3. Ralph NahatoOctober 19, 2009

    Jesus Christ!

    ReplyDelete
  4. nakushukuru sana ndugu yangu michuzi kwa kutuwekea haya mambo adimu. twanga kwa kweli hivi sasa wako juu sana. unaambiwa huhitaji kuwa mpishi ndio ujue chakula kipi kizuri. hii rap ya kinyonga ni kali. nawafagilia sana ferguson, kalala junior, dogo rama na halidi chokoraa, wanazidi kumpa jeuri asha baraka. GOOD JOB TWANGA, KEEP IT UP. anko nanihii tunaomba uendelee kutuletea mambo haya, na sisi tuendelee kujisikia kama tuko mango uwanja wa nyumbani.

    ReplyDelete
  5. Wakata nyonga wakiongozwa na Aisha Madinda bado mnaweza, ila punguzeni HAMIROJO.

    ReplyDelete
  6. michuzi hujaskia msiba wa charles massanja?

    ReplyDelete
  7. Kwani vi-portable hamna huko mliko? Wengine tunapendelea mashape, ma-curves kama hayo bw. Loh! Msichanganye na minyama ya uvivu, si manaona wenyewe, kazi yao wala haihitaji Gym!!

    ReplyDelete
  8. HII! MKUU MICHUZI! SHUKURANI NYINGI SANA,kwa uazalendo wa kutuwekea mambo makubwa ya TWANGA PEPETA! Baabu kubwa,hivi ndio vitu vya wazawa!!!! Twanga oyeeeeee!!!!!!

    ReplyDelete
  9. MDAU KINONDONIOctober 21, 2009

    SISI WAKAZI WA KINONDONI JIRANI NA HII CLUB YA MANGO GARDEN, YAANI USINGIZI KWETU NI KITU ADIMU. YAANI KWA MIAKA KADHAA SASA TUMEKUWA TUKISUMBULIWA NA HIZI KELELE ZA MUZIKI KUANZIA JNNE USIKU MPAKA JPILI. SIKU PEKEE NI JTATU TU, NDIPO HATUSIKII KELELE HIZI. TUMESHAPELEKA MALALAMIKO YETU SEHEMU ZOTE KUANZIA SERIKALI ZA MITAA MPAKA HUKO JUU LAKINI WAPI.HATUKATAZI KUPIGA MUZIKI ILA WAJENGE KAMA BILICANAS WAJIFUNGIE NDANI HUMO WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO NA SISI TUWEZE KUPUMZIKA KUTOKANA NA UCHOVU WA KAZI KUTWA NZIMA.NAWASILISHA.

    ReplyDelete
  10. lol
    Michuzi mambo ndiyo haya
    unatusuuza roho zetu, sisi tulio mbali.
    Asante sana kaka

    Mdau
    Canada

    ReplyDelete
  11. huyu mdau wa herufi kubwa hapo juu naona anataka kutuharibia mandhari zetu za kibongo. hizo kelele kama zinakukera hama. uzuri wa nyumbani kwetu ni kufurahia muziki chini ya miti na kumbi zetu za wazi. yeye anataka ijengwe bilcanas kinondoni, wangapi wataweza kwenda? mango garden ni uwanja wa walalahoi. jamani huku ulaya tukae kwenye kumbi za kujifungia na woga wa kupigia kelele majirani, na nyumbani nako mseme hayohayo. kwa miaka mingi watu walikuwa wakistarehe kumbi kama ddc magomeni na kata 14 temeke, watu tulikuwa tunasikilizia nje tukipunga hewa wakati huo tukiwa bado wadogo. leo ndugu yangu anasema anapigiwa kelele! twanga endeleeni kuwapepeta, wakileta kelele wakumbuke jinsi mlivyorudi leaders club!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...