Salama Uncle,
Niliona hii documentary ya huyu dada wakati fulani, ila sikumbuki kama ulishaiweka kwenye globu ya jamii.
Huyu dada ni shujaa sana, na nafikiri ukimuweka kwenya globu ya jamii anaweza kufaidika kwa aina moja ama nyingine...you neva no, hata baba yake mzazi anaweza kujisikia vibaya na kujitokeza.
Eneway, naomba uweke hii linki ili watu wajionee wenyewe.
Ahsante sana
Mdau Uwanja wa Fisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. This is the BEST Documentary ever.......Pole sana Eliza, Keep it up, Mungu yupo.

    ReplyDelete
  2. Dah inasikitisha kuona matransit kids wanatendewa haya.Dogo katolewa kwao(iringa) akaletwa mjini akatendewa ufirauni.

    ReplyDelete
  3. recommend to everyone,

    Hi Michuzi How can we contribute! I mean Financially seriously, I would love to be part of It

    ReplyDelete
  4. Michuzi, ukiweza tutafutie contact the huyu dada ili tumsaidie, anaonekana kama vile very smart, do something, sisi watu wa ughaibuni tunaweza kumsaidia kiaina

    ReplyDelete
  5. Michu, sina kawaida ya kutoa maoni zaidi ya kusoma ya watu tu, ila hii clip imenigusa kweli, I wish ningeweza kumsaidia Eliza. Ee Mungu liponye taifa letu

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli I was very touched by Eliza's story. With a spirit like that I think she will have a very long and successful life. It could be another "Magic Johson" in the making! Kuwa 'muathirika' does not mean a death sentence given the right healthcare, environment and resources. I would really like to know the contacts of Eliza so I can help her in some way. I went to http://www.kiwohede.org/ and I saw their contact information but it seems like the site has not been updated since 2007! Hopefully those are the right contacts! But if anyone knows how to reach this girl please let us know.

    ReplyDelete
  7. I was very moved by her maturity and natural intelligence. She gave me the impression that all she needed was a little help from a Samaritan and someone pointing her towards the right direction. I hate telling you what to do but why dont you ua bwana mdogo Ahmad trace her and interview her to give us a follow up. I have this inner feeling that I should somehow help her
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  8. jamani hiyo imenifanya nitokwe na machozi,kwa kweli eliza ni dada shujaa.shida zimemfanya azidi kuwa strong girl.

    ReplyDelete
  9. Inasikitisha sana hii habari, inabidi sisi kama watanzania tusaidiane kuelimisha wananchi kuhusu vitendo vya umalaya na gonjwa la ukimwi.Vile vile serikali itusaidie kukomesha/kuondoa seheme kama hizi wa Uwanja wa fisi

    Sikupenda walivyo-potray "Uwanja wa fisi"..na kuitwa "Hyene Square", sio lazima kila kitu kiwe na tafsiri kwa kiingereza

    ReplyDelete
  10. wote bni anonymous tu mtaweza kumsaidia vipi. Naona watu wa ughaibuni waanzishe Mfuko wa Uwanja wa fisi kusafisha mabaya ya sehemu hiyo. Hii inaonyesha kwa undani namna gani mlala hoi alivyo na taabu.Serikali imechangia kwa namna nyingine kutilia umuhimu wa shule. Elimu iwekwe kama sheria siyo kushauri wazazi wapeleke watoto wao shule!!! It is real sad after you have watched this documentary.

    "School is a drill for the battle of life. If you fail in the drill you will fail in the battle".
    –Karl G. Maeser

    ReplyDelete
  11. Uncle Michu we need a follow-up on this documentary,..
    Kuna anayejua huyu msichana yuko wapi?

    ReplyDelete
  12. Kaka Michu inaliza hii, inatesa akili..Wapi tunaweza kuwapata hawo KIWOHEDE?Weka namba zao za simu...system bado inawasimanga watoto na wenye maisha haya mabaya!Miziki iliyowekwa kama background haipendezi tunawanyanyapaa waathirika..cha msingi tunaomba contact za KIWOHEDE(Hususan watu wa Kontena)...Pia tafsisi naona imegomba..ningeshauri majina yakae vilevile kama Uwanja wa Fisi...Mtaa wa makuma ubaki vilevile na sio kama walivyotafsiri!
    MUHIMU Contacts...Nimeishi mitaa hiyo ya uswahili pia

    ReplyDelete
  13. THIS VIDEO IS TOO OLD, OVER YEARS, SO AGED, I SAW IT IN YEAR 2007, IT WAS A RESEARCH DONE BY ONE OF AN INTERNATIONAL BODY LONG TIME AGO SO I DON'T KNOW THE STATUS OF THIS DADA NOW, I WONDER IF SHE IS OKAY OR NOT NOW IN TERMS OF HEALTH IF REALLY SHE HAD THE PANDEMIC. BUT THE CONTACT IS KIWOHEDE IN DAR YOU CAN GET HER VERY QUICKLY

    ReplyDelete
  14. Mdau wa oct 29 12:25:00 umeniacha hoi kuhusu kubadili majina ya mitaa naunga mkono it got to remain the same tusije kuwa kina kanumba unasema my ex girlfriend was nice sepetu

    ReplyDelete
  15. Unwanja wa fisi in english is uwanja wa fisi ni kama ule mtaa kule kinshasa ya kabila pumbu street no translation period.

    ReplyDelete
  16. MICHUZI NAOMBA UITILIE UZITO ZAIDI HII CLIP, NAONA WATU WENGI HAWAJAIFUATILIA KAMA AMBAVYO INGETAKIWA. IKIBIDI IWEKE KWA MAANDISHI MAKUBWA YA RANGI TOFAUTI KUONYESHA MSISITIZO, PIA FORWARD KWA WANABLOG WENGINE, NADHANI WATANZANIA TUNAHITAJI HII ILI TUJIELIMISHE ZAIDI.

    ReplyDelete
  17. ...at first I said I was not going to watch the video, then I tried it and stopped after a minute or so. On a third visit today, I somehow ran it for a minute, then two, then five and finally all of it. What a masterpiece - it struck me in many ways. One, it is sad to realise that Elisa's fate is commonplace. It reminds me of the CDs I used to see in Dar's red light districts and tells me that they deserved sympathy, empathy and not abhorrence. Is it based on a true story, it appears it is and what is most striking, is Elisa's coherence - as an unfortunate human - epitomised in her great intellect and articulation despite having no much education. He final words of tackling the problem by closing down the Hyena Square is an implicit call for poverty reduction. It is a wake up call to the authorities to fight social vices by tackling the environment and circumstances that mostly trigger them. What a genius this little girl is and one wonders how many such talents roam the streets at night and how many more Elisa are in the making. Only if she had the power...and the power she has in the message she has passed on through this documentary. Passing on the message is one, implementing the call is another - but as we get to this point, Elisa has played her part...

    ReplyDelete
  18. nimeguswa sana na hii kweli nimelia. Eliza kama utaisoma hii blog ninakuhitaji nitakutumia dola 100 kwa sasa kuliko sadaka ninayotoa kanisani huku marekani kila mara wewe itakusogeza nami nitajisikia vizuri kwani nitakua nimetimiza andiko linlosema nilipokuwa na njaa hukunilisha,etc. wasiliana nami kwa email ya grasuj@gmail.com
    Mungu akupe nguvu zaidi kama ulivosema wewe utasavaiv! no doubt, kuwa makini tu na afya yako.
    Mdau In USA.

    ReplyDelete
  19. hii ni matokeo ya serikali mbovu isiyojua nini kazi zake ktk jamii kama kuweka shule za maana mikoani na vijijini kwa ujumla,kuwapatia wananchi huduma bora za afya pamoja kufuata utawala wa kisheria.hizo zote ni kazi za serikali na si za watu binafsi,wizara husika imechukua hatua gani?,kazi zao ni kupitisha bajeti ya wizara na kutafuna pesa za wananchi kwa matumizi binafsi na familia zao.hizi zote ni dhambi namungu atawaadhibu woote wanaohusika na kusababisha maisha haya yanayoweza kuzuilika na utawala wa kisheria na serikali yenye kuwajibika kwa wananchi wake.pole da eliza na mungu takulipia.

    ReplyDelete
  20. baada ya kuona comment za huku ndani, naona ni vizuri kwa wabongo tuliopo nje kuwa na Trust ya kusaidi wenzetu nyumbani. Kama hawa wanaumia sana. KWanza hawapati haki.
    Tusilaumu serikali hata siku moja.

    mtoto

    ReplyDelete
  21. michuzi,kwa nini usitusaidie kumtafuta,watu wengi wanapenda kumsaidia,kwa sisi tulioko nje ya nchi iwe rahisi kwa kupitia kwako.

    ReplyDelete
  22. Muddy Nice TzOctober 29, 2009

    HI KAKA MITHUPU,
    DAH HII KITU SI MCHEZO, YAANI INASIKITISHA SANA KUONA DOCUMENTARY HII, SASA SIJUI HII DOCUMENTARY IMEFANYWA NA WATANZANIA WENZETU AU WAGENI?, MANAKE HAYA NI MAMBO YA AIBU SANA, HIVI FIKIRIA HUU UCHAFU UKO HAPAHAPA DAR ES SALAAM TENA PALE MANZESE, YAANI KWA WASIOLIJUA JIJI NI CITY CENTER KABISA, SASA SIJUI UKO MAPORINI PAKOJE KWAKWELI. HII SERIKALI YA TANZANIA IMEOZA KABISA WADAU, YAANI IT IS VERY PAINFUL SOMTEIMES, NDIO MAANA KUNA KIPINDI WATU HUAMUA KUJIFANYIA MAMBO YAO TU NA KUACHANA KABISA NA MAMBO YA MAENDELEO, LEO HII KILA MTU ANAONGELEA SIASA TU KILA MWANASIASA ANAANZASHA GAZETI NA KUANZA KUMKASHIFU MWENZAKE, NA MBAYA ZAIDI IMEFIKIA HATUA WATU WANATETE MAOVU HADHARANI TENE BILA HATA KIFICHO, LAITI KAMA NYERERE ANGEFUFUKA NA KUONA YANAYOTENDEKA NADHANI ANGELIA SANA, YAANI NCHI IMEKUWA KAMA HAINA KIONGOZI, VIONGOZI KAZI YAO KUCHEKA CHEKA TU, WATU WANAFANYA KADRI WAPENDAVYO BILA KUBUGHUDHIWA. MIMI NIMEMPENDA SANA HUYU DADA ELIZA, YAANI IKI NI KICHWA HASA, KAMA KINAPATA MTU WA KUKITUNZA NA KUKIWEKEA MAMBO VYEMA ANAWEZA KUJA KUWA MTU MASHUHURI NA MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA SANA NA WATU WAKAFAIDIKA NAE, NASHAURI KWA WENYE UWEZO NA FIKRA PANA ZAIDI WAJITAHIDI KUMSAIDIA DADA HUYU.
    MWISHO NATOA MFANO MMOJA HAI UNAOFANYA KAZI MPAKA SASA, MIMI NI MPANZI WA NGUMI KIASI FURANI NA NINAIPENDA MNO NCHI YANGU KULIKO CHOCHOTE UNACHOWEZA KUFIKIRIA, KUNA KIJANA MMOJA ANAITWA ROGGERS MTAGWA, ANAISHI UKO USA PHILADELPHIA, HUYU JAMAA NI BONDIA MZURI SANA, LKN UKIMUONA PINDI ANAHOJIWA UTAFIKIRI KAMA HANA AKILI VYEMA AU HAJACHANGAMKA KAMA BINADAMU WA KAWAIDA, NAKWAMBIA HUYU JAMAA ANGEKUWA ANAISHI TANZANIA ANGEKUWA MASIKINI WA KUFA MTU, LKN ANGALIA WAZUNGU WANAVYOWEZA KUMTENGENEZA NA ANAINIZA PESA KAMA HANA AKILI NZURI. SO WAUNGWANA NAWAOMBENI MUMSAIDIE DADA HUYU.

    NI MIMI,
    MUDDY NICE

    ReplyDelete
  23. kuna kitu kimoja ambacho wakina mama wengi wanakisababisha
    wanachukua ma house girl wadogo na kuwatesa mmpaka wanakimbia, ukisikia house girl kakimbia ujue wengine wanakimbilia sehemu kama hizi

    tatizo jingine ni wakina baba ambao wanatelekeza watoto zao, wako wengi tu

    ReplyDelete
  24. Ombi langu ni kwamba, hii documentary iwekwe kwenye vyombo vyote vya habari TZ. Huyu dada na wenziwe walipwe kiasi kikubwa cha pesa sababu it is the best ever. Yule aloitengeneza naye abarikiwe na aongezewe zaidi.

    ReplyDelete
  25. uwanja wa fisi unaitwa hivyo kutokana na sifa yake mbaya, zamani palikuwa hapaitwi uwanja wa fisi
    kwa hiyo kutranslate uwanja wa fisi kwenda hyena square hakujapoteza maana

    ReplyDelete
  26. MISTER MICHUZI, MBONA UNATIA AIBU, ASILIMIA KUBWA YA WATU WA UGHAIBUNI WAMEONYESHA NIA YAO YA KUTAKA KUMSAIDIA ELIZA, LAKINI WEWE UMECHUNA U SIJUI MAANA YAKE NI NINI? AU UNAMUONEA WIVU NINI?...TOA MAELEZO BASI, UTATUSAIDIA KUMPATA ELIZA AU HAUTAKI????....DAMN MAN !

    ReplyDelete
  27. HII INASIKITISHA SANA! KAKA MICHUZI JITAHIDI NENDA HUKO KIWOHEDE UKAMTAFUTE HUYO DADA ILI AKUPATIE NAMBA YAKE YA SIMU YEYE BINAFC ILI TUWEZE KUMTUMIA JAPO DOLA 50,UKISHAIPATA UIWEKEE KICHWA CHA HABARI KIKUBWA ILI WADAU WOTE WENYE KUTAKA KUMCHANGIA CHOCHOTE ELIZA TUIYONE KIRAHIC. MUNGU AKUBARIKI

    ReplyDelete
  28. This is so real.....It is a very touchy story....

    Kumsaidia Elisa ni just a small part of the puzzle ....

    kwanini Govt isifunge hii sehemu...Kweli kama watu wa humo walivyosema wana wanawake kibao na hao wanawake watakua na wanume zao...wakitoka humo ni kuuengeza tu huu ukimwi kwenye society...Solution ya kuponyesha jipu ni kutoa usaa kwa kidonda nadhani wako wengi sana wenye story kama ya Elisa

    Na pia watuwangeatakiwa kuwa vigilant..ukimwona mtu analeta moto kutoka kijijini kufanya kazi za ndani basi wahukumiwe kabisa

    Na wababa wengi na vijana wakitanzania mulern something here watoto wenu sio lazima waishie kwenye ukumbi wa fisi ndio mjue wanateseka...mahali popote duniani ukizaa mtoto wako halafu usijishughulishe katika kumkuza ...huyo mtoto lazima anaathirika kipsykologia big time....

    Baada ya kuona hii documentary....I need to count my blessing and appreciate more the little things in life...machozi yamenitoka nikajiuliza why her...why them .....

    ReplyDelete
  29. Kwa wale ambao hawana Habari Hii...

    UWANJA WA FISI ... Haupo Tena...

    Serikali iliweza kuwaondoa kabisa.

    UWANJA WA FISI SASA NI HISTORIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...