Mlezi wa umoja wa wanafunzi wa marekani
Meja Jenerali mstaafu Benjamin Msuya akiongea
wakati wa hafla ya kukabidhi madawati hayo katika Shule ya Msingi
Mtakuja iliyopo Kata ya Kunduchi katika Manispaa ya Kinondoni.
Mlezi wa umoja wa wanafunzi hao Meja Jenerali mstaafu Benjamin Msuya akimpa ujira fundi seremala aliyetengeneza madawati hayo kwa ajili ya Shule ya Msingi Mtakuja iliyopo Kata ya Kunduchi katika Manispaa ya Kinondoni.
Mlezi wa umoja wa wanafunzi hao Meja Jenerali mstaafu Benjamin Msuya akimkabidhi Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Faustine Kikove moja ya madawati 32 yaliyochangwa na wadau wa marekani
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtakuja iliyopo
Kata ya Kunduchi katika Manispaa ya Kinondoni wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtakuja iliyopo Kata ya Kunduchi katika Manispaa ya Kinondoni.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtakuja wakifurahia zawadi ya madawati toka kwa wanafunzi wanaosoma marekani
WAZAZI nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya elimu ili siku tatizo la ujinga,maradhi na umasikini ambalo ni adui mkubwa wa Taifa liweze kubakia kuwa historia.

Rai hiyo imetolewa jana na Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Faustine Kikove wakati akipokea msaada wa Madawati 32 yenye thamani ya Sh.1,892000,yaliyotolewa na umoja wa wanafunzi wanawake wa Kitanzania wanaosoma Marekani kwa ajili ya Shule ya Msingi Mtakuja iliyopo Kata ya Kunduchi katika Manispaa ya Kinondoni.

Kikove alisema elimu ni nguzo kubwa na msingi wa maisha bora kwa kila mtanzania anayetambua umuhimu wake na kwamba kama kila mzazi atajitolea katika kuchangia ni dhairi kwamba Siku moja Taifa litapiga hatua kubwa katika maendeleo kufuatia umuhimu huo kutambulika.

“Nachosema hapa ni kwamba kila mzazi atambue kuwa jukumu la kumsomesha ni mtoto ni lake na siyo mtu mwingine, kwa maana hiyo hata jukumu la kuchangia maendeleo ya shule pia ni la mzazi,ni vyema kama tutajenga utamaduni huu ili siku moja nasi tuweze kupiga hatua katika maendeleo ya elimu yetu”alisema Kikove

Akikabidhi msaada huo Mlezi wa umoja wa wanafunzi hao Meja Jenerali mstaafu Benjamin Msuya alisema kwa kipindi kirefu wanafunzi hao wamekuwa wakijitolea kuchangia maendeleo ya elimu katika shule mbalimbali hapa nchini ambapo kwa kipindi hiki wameona ni vyema wakaichangia shule hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa upungufu mkubwa wa vifaa mbalimbali yakiwemo madawati.

Alisema hali hiyo ilitokana na mmoja wa wanafunzi hao kutembelea shule hiyo na kujionea tatizo hilo ambapo aliporudi Marekani yeye na wenzake walishauriana na kuona vyema wajichange na kusaidia japo kupunguza tatizo hilo ili wanafunzi hao wa Shule ya Msingi Mtakuja waweze kupata elimu yao kwa ufasaha.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo David Maleko alisema msaada huo utawasaidia katika kupunguza kero ya baadhi ya wanafunzi kukaa chini na kuwataka wazazi na wasamaria wengine wenye mapenzi mema na shule hiyo kuendelea kuisadia shule hiyo kwa kuwa bado inakabiriwa na upungufu wa madawati kwa kiasi kikubwa.

“Tutafurahishwa sana endapo watajitokeza wasamaria wengine na kuiga mfano wa wanafunzi waliotusaidia madawati haya kwa kuwa mpaka sasa tunakabiriwa na upungufu wa madawati 112 kutoka upungufu wa madawati 144 tuliokuwa tukikabiriwa nao” alisema Mwalimu Mkuu huyo Maleko.

Pamoja na uhaba wa madawati Shule hiyo inakabiriwa na upungufu wa viti 53,Meza 23,Makabati 19,Nyumba za walimu 34 pamoja na matundu ya vyoo 38 huku shule hiyo ikiwa na wanafunzi 1345 ambapo kati yao wavulana ni 657 na wasichana 688.
--------------------------------------------
Globu ya Jamii imeguswa sana na kitendo cha wadau hao wa Marekani kwa kukumbuka wenzao wanaosota katika kusaka nondozzzz. Huu ni mfano wa kuigwa na wito unatolewa kuwe na harambee kama hizi mara kwa mara
-Michuzi







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kwa wadau walisoma Oysterbay Primary School miaka ya mwanzoni themanini 80s. Huyu Faustine Kikove sio yule mwalimu wetu maarufu?? Huyo Mwalimu aliweka discpiline hasa katika shule. Mwl Kikove good to see u again.

    ReplyDelete
  2. Namkumbuka Meja Jenerali Benjamin Msuya aliwahi kuwa Kiongozi wa kijeshi wa Uganda kwa masaa kadhaa mara baada ya jeshi la Tanzania kuipindua Serikali ya Idd Amin Dada. Nadhani atakuwa ni kiongozi wa Nchi aliyekaa muda mfupi sana kuliko wote Duniani. Sina hakika kama anaenziwa au tunangoja atakapofariki?

    ReplyDelete
  3. Go Tuwa, Go!

    ReplyDelete
  4. Good job kwa kuisaidia shule hii ambayo kwangu naikumbuka kuisoma katika kitabu cha kiingereza shule za msingi. Main character alikuwa always Neema & Musa and the Baby Baraka & their parents Mr. & Mrs Daudi

    ReplyDelete
  5. Ooh namkumbuka sana Mr. Kikove nimefurahi kukuona, nakumbuka enzi zako ulipokuwa mwalimu wetu mkuu ktk shule hiyo hiyo mtakuja, miaka ya 88 tuliokuwa drs la 7 hapo natumai mnamkubuka. hongera kwa kuwa Kaimu Afisa elimu wa manispaa, big up

    ReplyDelete
  6. mdau wa 3.00pm 0ct 28 umenifurahisha sana. Nilimsikia wakati wa mahojiano na TBC - maadhimisho ya miaka 30 ya vita vya uganda jamaa aliwahi kuwa prezo wa uganda kwa muda aisee ni prezoo huyo mheshimiwa mkuu wa wilya mpe heshima yake... nilipenda sana anavyojieleza mzee unahitajika bado hongora

    ReplyDelete
  7. Nimefurahi kuziona picha hizi!

    Kumwona Benjamin Msuya, kumenikumbusha miaka yetu hapo Tabora School!

    Benjamin Msuya alikuwa ni Monitor wa Bweni la Biscoe (bila kumsahau Clemmens Orawia (sasa DC).

    Augustine Ramadhani na mimi tulikuwa ndio ma-Prefect.

    Born Again Pagan

    ReplyDelete
  8. Major General Ben Msuya aandike historia yake kama alivyofanya Edwin Mtei. wazee hawa wamestaafu huo ndio wakati mzuri kuandika kuhusu maisha na kazi zao.

    ReplyDelete
  9. KAKA MICHUZI HABARI KAZI NA HALI KWA UJUMLA !

    WATU WAMERUKA NA UKUMBUSHO NA KUSAHAU HALI HALISI . HII NI AIBU KWA SERIKALI YETU HADI LEO TOKEA TUPATE UHURU HATA MADAWATI NAYO MSAADA SASA KAMA DAR MAMBO YAPO HIVI KULE VIJIJINI KUTAKUAJE ?

    VIONGOZI ONENI AIBU !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...