Barrick Gold Yatoa Msimamo kuhusu Muswada nambari C-
300 na Kueleza Ukweli


Shirika la Dhahabu la Barrick (NYSE:ABX) (TSX:ABX) leo limeelezea msimamo
wake kuhusu muswada wa wanachama binafsi (C-300) ambao kwa sasa uko mbele ya Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nchi za Nje na Maendeleo ya Kimataifa ya Kanada, kwa kusisitiza kwamba, Muswada hauna umuhimu na kwamba huleta athari mbaya kwa biashara za Kanada. Vile vile Barrick imeeleza ukweli kuhusu madai yasiyothibitishwa ambayo yamekuwa yakitolewa na watu kwenye Kamati hiyo.

Katika taarifa yao ya pamoja na Kampuni ya Goldcorp Inc. na Shirika la Kinross Gold, makampuni hayo yamedokeza kwamba Muswada nambari C-300 utaathiri vibaya sana sekta ya uchimbaji madini ya Kanada kwa vipengele vikuu vitano:


1. Kuihatarisha nafasi ya ushindani ya makampuni ya Kikanada;
2. Kusababisha kushuka kwa heshima ya makampuni ya Kikanada;
3. Kudhoofisha ushirikiano na ubia katika Wajibu wa Mashirika kwa Jamii (CSR);
4. Kuchagiza makampuni kuhamia sehemu nyingine; na
5. Kudharau taratibu za sasa za kisheria za Wajibu wa Mashirika kwa Jamii.
(ili kupata nakala ya mawasilisho, tafadhali ingia kwenye tovuti hii:
www.barrick.com


“Leo hii tunawapa wanakamati maelezo ya kina, ukweli na uhakika ili kujibu
shutuma mbalimbali kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sahihi. Masuala ya uchunguzi makini na hata ukosoaji ni sehemu ya ufanyaji biashara, lakini yanapaswa kuwa ya haki na ukweli,” alisema Bwana Vincent Borg, Makamu Mtendaji wa Rais, Mawasiliano Ngazi ya Shirika.


“Kitu kimoja kimeonekana dhahiri wakati vikao vya mashauriano vikiendelea: baadhi ya watu hawakuletwa hata kuthibitisha shutuma zao kali juu ya sekta ya uchimbaji madini ya Kanada pamoja na Barrick Gold - leo hii nyingi kati ya hizo zimebainika bayana kuwa ni za uwongo. Hawakuipatia Kamati hii
taarifa za ukweli na uhakika wala ushahidi kwa ajili ya kusimamia madai yao wakati wakitoa chokochoko za hapa na pale za kupaka matope kampuni.”

“ Vikao vya kusikiliza kesi hiyo vimetoa nafasi kubwa ya kudhihirisha ni
namna gani Muswada nambari C-300 ulivyogeuka kuwa sumaku ya kuvutia madai ya uwongo na yasiyothibitishwa yatokayo kwa watu mbalimbali kutoka sehemu yoyote ile duniani na hakuna kinachofanyika zaidi ya kuiathiri sekta ya uchimbaji madini ya Kanada,” aliongeza Bw. Borg.

Katika kila nchi huru ambamo Barrick huendesha shughuli zake, kuna taasisi
za serikali, mifumo ya sheria, mamlaka zinazohusika na sera, taratibu za kisheria pamoja na mahakama. Barrick inaamini kwamba katika nchi hizi shutuma za namna hiyo hutolewa inavyostahiki zikiambatana na maelezo yote ya ukweli na yanayohusiana na madai hayo na si kamati ya bunge ya Kanada ambayo haikutoa uhakiki wala maelezo. Zaidi ya mataifa hayo huru, makampuni huwa yanawajibika katika ngazi ya kimataifa na kwa kufuata miongozo inayohusu uwajibikaji.


“Chombo husika kwa ajili ya urekebishi na utatuzi ni mahakama au mamlaka
huria zinazohusika ambapo masuala yanaweza kuchunguzwa ipasavyo kwa wakati muafaka - na si majukwaa ya kisiasa,” aliongeza Bw. Borg.
Dhamira ya Shirika la Dhahabu la Barrick ni kuwa kampuni bora zaidi ya
dhahabu ulimwenguni kwa kutafuta, kutwaa, kuendeleza na kuzalisha rizavu zenye kiwango bora kwa usalama, kwa faida na kwa kuwajibika kwa jamii.

MAWASILIANO NA WAWEKEZAJI:
Deni Nicoski
Makamu wa Rais,
Mahusiano na Wawekezaji
Simu: (416) 307-7410
Barua-pepe: dnicoski@barrick.com

MAWASILIANO NA VYOMBO VYA HABARI:
Vincent Borg
Makamu Mtendaji wa Rais,
Mawasiliano Ngazi ya Shirika
Simu: (416) 307-7477
Barua-pepe: vborg@barrick.com



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. hawa barick juzi tu hapa wananchi wa mgodini huko Argentina waligomea uchimbaji wa dhahabu kwa kudai jamaa wanawaua kwa sumu
    na taarifa yenyewe mbona haipo wazi imekaa kimipasho zaidi

    ReplyDelete
  2. SASA ANKO HII YATUHUSU NINI, MBONA MAAZIMIO YANAYOTOLEWA NA WANASIASA PAMOJA NA NGOs ZETU HUWA HAWAZITOLEI UFAFANUZI.

    ReplyDelete
  3. HILI TANGAZO LINAPASWA KUWA INTERNAL MEMO KWA WANABARRICK WALA HALIKUPASWA KUWEKWA HAPA HALINA MAANA KABISA KWA WATANZANIA, IT'S A JUNK!!

    KUNA OUTSTANDING ISSUES NYINGI TU ZINAZOHUSU BARRICK AMBAZO WATANZANIA HAWAJAPATA MAJIBU.

    TUNGEWAONA WA MAANA SANA KAMA ANGALAU WANGETUONYESHA HATUA MBALI MBALI WALIZOCHUKUA KUHAKIKISHA HAWACHAFUA TENA MTO TIGHITE NA MASUALA MENGINE YANAYOHUSU KUHIFADHI MAZINGIRA.

    POLE.

    ReplyDelete
  4. Is Barrick the center of the universe?
    Mwananchi wa kawaida nitajulia wapi C-300? Ina maana ndio maji ya mto Tigithe yamekuwa safi kwa C-300?

    ReplyDelete
  5. Kwa hamu nimekuwa nikisoma kwa haraka pengine nifike mahala ambapo wanatoa pia maelezo na misimamo yao juu ya yale wanayotuhumiwa au kuwajibika kwayo katika jamii ya Watz lakini sikuona chochote.

    NAJUUUUUUTA KUSOMA ARTICLE HII!

    ReplyDelete
  6. sasa hawa waswahili wenzangu watafanyaje zaidi ya kutekeleza amri toka kanada? pole teweli & co, mradi hela zinaingia mifukoni ila mkiulizwa mnafanya nini, hakuna jibu.

    ReplyDelete
  7. MSWADA NAMBA C-300 UASEMA HIVI:

    If passed, Bill C-300 will:

    •put in place human rights, labour, and environmental standards that Canadian extractive companies receiving government support must live up to when they operate in developing countries;
    •create a complaints mechanism that will allow members of affected communities abroad, or Canadians, to file complaints against companies that are not living up to those standards;
    •create a possible sanction for companies that are found to be out of compliance with the standards, in the form of loss of government financial and political support.

    HUU MSWADA WA SHERIA UNAOJADILIWA KANADA KWENYE KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE NA MAENDELEO YA KIMATAIFA NI MUHIMU SANA KWETU NA UNATUHUSU MOJA KWA MOJA. ANONY WA KWANZA NA WENGINE MLIOSEMA HAUTUHUSU MMEKOSEA.

    TAARIFA ZINAZOTOLEWA NA NGO ZETU HAWAZITOLEI UFAFANUZI KWASABABU HAZINA MADHARA KWAO, TUNAPIGA KELELE TUNANYAMAZA, LAKINI MUSWADA HUU WANAUTOLEA MAELEZO KWASABABU WANAUPINGA USIPITISHWE UKAWA SHERIA KANADA, MAANA WANAJUA SHERIA KANADA ZINAFANYA KAZI. MFANO, KAMA MUSWADA HUU UNGEKUWA UMESHAPITISHWA NA KUWA SHERIA, WANANCHI WALIOATHIRIWA KATIKA MTO TIGHITE WANGEWEZA KWENDA MAHAKAMANI KANADA NA WAKISHINDA BARRICK INGELAZIMISHWA NA SERIKALI YA KANADA KULIPA FIDIA.

    ANGALIA HILI, WAKANADA AMBAO HAWAATHIRIWI NA SHUGHULI ZA HAYA MAKAMPUNI YAO YANAPOFANYA KAZI NCHI ZA DUNIA YA TATU WANATUNGA SHERIA KUTUSAIDIA, WATU HUMU WANASEMA HAITUHUSU!!!

    NATABIRI KWAMBA SIKU ZA MBELENI, WATATUNGA SHERIA NYINGINE ZITAKAZOYALAZIMISHA MAKAMPUNI YA MADINI KUTULIPA KODI ZAIDI NA PIA KUGAWANA FAIDA PIA KWA VIWANGO VINAVYOKUBALIKA.

    KWA MFANO, MADINI HAYA YA DHAHABU YANATOKA KWETU YANAUZWA DUNIA NZIMA, HASA NCHI TAJIRI. SHARES ZA KAMPUNI KAMA HII ZINAUZWA KWENYE SOKO LA HISA LA NEW YORK NA TORONTO. KWA HIYO WENYE HISA WENGI(AMBAO WANAGAWANA FAIDA KWA NJIA YA DIVIDENDS) WAKO HUKO ULAYA NA MAREKANI. SISI TUNABAKI NA KODI AMBAYO KWA MIAKA MINGI KWANZA TUNAISAMEHE ALAFU PILI WANATUMIA MBINU ZA ACCOUNTING KUZIPUNGUZA MNO. PIA TUAPATA MRAHABA AMBAO KAMA NI 3% NA UNAMLIPA ALEX STEWART 1.9%, BASI TUNABAKI NA 1.1%. OFCOURSE KAMA TUNAKUBALI UJINGA HUU WAO SI WATAKAA KIMYA TUU?

    KWA HIYO SIKU ZA MBELENI WAKATAPOTUNGA SHERIA YA KUTUSAIDIA(KWASABABU SISI HATUTAKI KUTUNGA), WATASEMA KWANZA HAKUNA MISAMAHA YA KODI.PILI WATASEMA TUPATE SEHEMU YA FAIDA EITHER KWA KUKUBALIANA KIMKATABA AU KWA KUUNGANISHA, TO LINK NA PERFORMANCE YA SHARES KWENYE MASOKO YA HISA HUKO NG'AMBO. NATURALLY, WATATOLEA UFAFANUZI SHERIA YA AINA HIYO WAKIIPINGA KWAMBA WAO WANATOA MTAJI MKUBWA NA SKILLS, KWAMBA HAKUTAKUWA NA FAIDA, NA KWAMBA WAO NI WAWEKEZAJI LAZIMA WAPEWE VIVUTIO. WATASEMA PIA KU LINK FAIDA ZA MASOKO YA HISA NJE NA GAWIO LETU LA FAIDA HAITAWEZEKANA KWASABABU WANAFANYA BIASHARA(MACHIMBO) NCHI NYINGI DUNIANI.

    KIPINDI HICHO TUTAKATAA(AU TUSEME BUNGE LA KANADA NDIO LITAKATAA, SI NDIO LITAKUWA LINATUNGA HIYO SHERIA!). TUTASEMA HABARI YA KUSEMA UNA MTAJI NA SKILLS ILIKUWA NI SABABU YA KARNE YA 20. KARNE YA 21 HATA MADINI YETU AMBAYO HAYAJACHIMBWA NI MTAJI TOSHA NA TUNAWEZA KUYATHAMINISHA. PILI TUTASEMA SKILLS NA TECHNOLOGY ZAMANI ZILITOKA MAGHARIBI PEKE YAKE, LAKINI KARNE YA 21 ZINATOKA KILA KONA YA DUNIA HIVYO SI SABABU. MWISHO TUTAWAAMBIA KWAMBA KULINK SHARE PERFORMANCE NA GAWIO LETU LA FAIDA INAWEZEKANA, NI MAHESABU TU YA KIFEDHA AMBAYO SI MARAHISI LAKINI YANAWEZEKANA.

    HAYA TUTAKUJA KUYAONA NI MUHIMU KWASABABU TUTAONA(AU WAO WATUNGA SHERIA WA KANADA) WATAONA KWAMBA INGAWA SHARE PRICES ZA GOLD ZINAENDELEA KUPANDA KWENYE MASOKO YA HISA, NA INGAWA WENYE HISA HUKO ULAYA NA MAREKANI WANAPATA GAWIO ZURI KILA MWAKA(DIVIDENDS), HUKU KWETU ZINAKOCHIMBWA HAKUNA KINACHOBADILIKA ZAIDI YA MAZINGIRA KUZIDI KUHARIBIKA NA VIJI CSR PROJECTS HAPA NA PALE!


    KWA HIYO HUU MUSWADA NAMBA C-300 WANAUTUNGA KWA AJILI YETU NA UNATUHUSU MOJA KWA MOJA.

    ReplyDelete
  8. asante mdau DMK. Umetufumbua macho wengi. Michuzi ungeiprint tena hili fafanuzi la mdau ili watu wengi wafaidike, Asante sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...