Wikiendi hii kipindi moto cha Mitikisiko ya Pwani cha Times FM kimetimiza miaka 5 tangu kilipoanzishwa kipindi hicho ambacho hurushwa hewani kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 6 mchana hadi 9 Alasiri na mtangazaji wake mahiri Dida.
Kilele cha sherehe za kipindi hicho zitakuwa na Tamasha kubwa la muziki wa taarab tamasha hilo litafanyika katika ukumbi wa PTA HALL viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa ambapo jumla ya vikundi 9 maarufu vya taarab vitashiriki vikundi hivyo ni pamoja na Jahazi, East Africa Melody, Coast Modern Taarab,New Zanzibar Star, Five Star, Tandale Modern Taarab, Super shine na Tanzania One Theatre. Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Kazi Ajira na Vijana Mh Juma Kapuya.

Mbali na burudani hiyo pia kutafanyika mashindano ya kusaka vipaji vya waimbaji wa taarab na washindi 7 watapatiwa mikataba maalum ya kazi katika vikundi watakavyoimbia siku hiyo ya mashindano wadhamini wakiwa ni Zain T Ltd na TBL na kiingilio itakuwa shilingi 5000 na 10.000 viti maalum tamasha litaanza saa 2 usiku
Mtangazaji moto wa mitikisiko ya pwani ya times fm, Dida, akikata keki studio
Dida akilisha keki mmoja wa wasanii wa taarabu
waimbaji wa taarab toka Melody, Five Star na Tandale wakiwa na mtangazji wa kipindi hicho Dida na Meneja wa Promotions wa Radio Times fm Amani Missanah (mwenye fulanazzz ya blue) wakiwa studio za Times fm kuadhimisha kutimiza miaka 5

Hongera Mitikisiko ya Pwani na watangazaji wake bila kuwasahau mashabiki wake!!! Kidumu kipindiiii,kidumuuuuu!!! Amani Missanah mzee wa Pilot talk!!
ReplyDelete5 year's si mchezo
ReplyDelete*sigh*
ReplyDeleteYEARS not YEAR'S
ooh kumbe uyu ndo Dida???
ReplyDeleteooo ok