Profesa Benno Ndulu
Nyumba anamoishi Gavana wa Benki Kuu iliyozua zogo juu ya gharama ya matengenezo yake ambayo amesema haikukarabatiwa bali imejengwa upya toka chini hadi juu.
GAVANA wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu amekiri benki hiyo kutumia zaidi ya Sh1 bilioni za walipa kodi kwa ajili ya kutengeneza makazi yake.

Prof Ndulu, ambaye alikuwa akitoa ufafanuzi wa habari iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi kuwa taasisi hiyo kuu ya fedha ilikarabati nyumba hiyo kwa Sh1.4 bilioni, alihusisha taarifa hizo za ubadhirifu huo wa fedha za walipa kodi na mtandao wa wafanyakazi wake ambao alisema una lengo la kumchafua.

Lakini Ndulu alisema pamoja na kutokuwepo na usahihi kwenye taarifa kwamba nyumba anayoishi ilikarabatiwa kwa kiasi hicho cha fedha, makazi anayoishi yalijengwa upya baada ya nyumba zilizokuwepo awali kubomolewa na akadokeza kuwa gharama zinaweza kuwa kubwa zaidi.
Nyumba haijakarabatiwa, imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya huu ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema, alilalamika gavana huyo.

"Napenda taarifa sahihi ambazo hazipotoshi ukweli, kwa maana taarifa kama hizo zinaharibu kila kitu kizuri na kujengwa taswira mbaya kwa wananchi, kitu ambacho si sahihi.

"Pia si kweli kuhusu hizo gharama kwani hakuna tathmini kamili ambayo imekamilika hadi sasa," alisema.

Gazeti la Mwananchi liliripoti kuwa nyumba anayoishi sasa gavana huyo ilikarabatiwa kwa takriban Sh1.4 bilioni na kwamba zote zilikuwa kwenye mradi wa kukarabati nyumba za vigogo wanne wa BoT - yaani ya Prof. Ndulu na za manaibu wake watatu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nyumba nyingine ni pamoja na aliyokuwa akiishi gavana wa zamani, marehemu Daudi Balali ambayo Prof Ndulu alidaiwa kuikataa kwa kuwa haina bwawa la kuogelea.

"Nashangaa kuambiwa nimekataa kuhamia kwenye nyumba; kisa haina bwawa la kuogelea, huu ni upotoshaji. Kama ni kuogelea, mimi niliogelea hadi kwenye mito, sasa sijui hili linatoka wapi, alihoji Profesa Ndulu.

"Kwanza hiyo nyumba wanayosema ilikuwa kwa ajili ya kuishi mimi nikaikataa kwa sababu haina bwawa la kuogelea, ni uongo kwani ile alikuwa akiishi marehemu Ballali na ilikarabatiwa kwa ajili ya Naibu Gavana Juma Reli... sasa sijui mimi nimeingiaje, alihoji.

Akitoa ufafanuzi wa maeneo halisi ya nyumba hizo, Profesa Ndulu alisema makazi yake hayako karibu na katibu mkuu mstaafu wa CCM na kwamba anayeishi huko ni Naibu Gavana (Taasisi za Fedha na Mabenki) Rila Mkila.

Alisema Naibu Gavana (Uchumi), Dk Enok Bukuku hajahamia kwenye nyumba yoyote ya BoT na kwamba anaishi kwake hadi sasa.

Prof Ndulu, ambaye taasisi yake imelalamikiwa kwa kujiidhinishia mamilioni ya fedha za mikopo yenye tofauti kubwa ya viwango baina ya wafanyakazi wa chini na vigogo, alilalamika kuwa taarifa za ufujaji wa fedha katika ukarabati wa nyumba hizo zinamuweka katika kundi la mafisadi na kwamba ni mkakati wa mtandao huo alioutuhumu kuwa unaundwa na watumishi wa BoT na baadhi ya watu walio nje.

Alidai kuwa miongoni mwa watu walio nje ambao wanaeneza sifa mbaya dhidi yake ni mwanasheria maarufu ambaye anadaiwa kutangaza vita naye baada ya kuzuia mianya ya ufisadi.

Gavana Ndulu, ambaye aliteuliwa baada ya Balali kuachishwa kazi, alisema kamwe hatasita kutekeleza majukumu yake kwa ajili ya kufurahisha au kuhofu watu wenye dhamira ovu.

â€Å“Najua, kuna watu wanafikiri watanitisha au kunikatisha tamaa. Nasema nitaendelea kushikilia uzi ule ule kusimamia sheria na taratibu katika kuongoza benki na si vinginevyo, alisema.

Alilalamika kuwa kuna watu wanataka kuzorotesha juhudi za kujengea nidhamu ndani ya taasisi hiyo na kwamba kwa dhamira zao wanaweza kukaa na kupotosha mambo kwa makusudi.

Kuhusu tuhuma nyingine kwamba, viwanja hivyo vilinunuliwa, Ndulu alisema vyote vimekuwa mali ya BoT kwa muda mrefu na hakuna hata kimoja kilichonunuliwa karibuni.

BoT imekuwa ikiangaliwa kwa karibu tangu kuibuka kwa kashfa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), kashfa ambayo ilihusisha wizi wa zaidi ya Sh133 bilioni.

Taasisi hiyo pia imekumbwa na kashfa nyingine kama za bima ya maghorofa yaliyo jijini Dar es salaam na Zanzibar, kuongeza gharama katika uchapishaji wa noti na matumizi mabaya ya madaraka katika ujenzi wa maghorofa pacha.

Wafanyakazi wa benki hiyo wamejikuta kwenye kashfa za kufanikisha njama za wizi, kuajiriwa kwa kutumia vyeti vya kughushi na tuhuma za watoto wa vigogo kupewa ajira za upendeleo.

Chanzo cha Habari hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. malipo dunianiDecember 25, 2009

    mheshimiwa kwa hiyo anajitetea kwamba imejengwa frm scratch na imegarimu 1.4bn or more, hivo ni sawa! ! ! !
    in this third word country, as poor as we r, evday begging for some money frm rich countries, mr Governor is implying that the amount is fair ? ? ! !
    one world from me, UNBELIAVABLE ! only in TZ could something this outrageous happen. Merry xmas Gov in a 1.4 billion shillings house !

    ReplyDelete
  2. Give Me A Break Please..!!yani professor huyo mbona tanzania kazi ipo?!!!me sioni tofauti ya ulichokanusha zaidi umezidi kunikera.I wish ningekuona live ukiwa unatoa huo ufafanuzi me nauta utumbo.Hivi ni lini tanzania tutapiga hatua?!badala ya kupiga hatua moja mbele sisi tunarudi hatua mia nyuma.Mwananyamala,Muhimbili,Ilala na Temeke hospitali zote hizi huwezi amini amini watu walivyojazana kwenye vitanda wengine wanalala wawili kwenye kitanda kimoja,madawa hakuna,wanafunzi hawana vyooo,wanakaa chini,shida haziishi tanzania kila siku ni afadhali ya jana eti leo mnaenda kutumia zaidi ya bilioni 1.4 tena za walipa kodi yani wale ambao wanatoa jasho kuzitafuta sio nyie kutwa kwenye mashangingi yenu .....hivi ni lini tutafika huku tunakohitajika kufika?!kwani huyo gavana hakuwa na nyumba?!punguzeni gharama zisizo za msingi jamaaaa yani me hata sielewi najiskia kutapika tu.Tazama ramani utaona nchi nzuri yenye visa na uozo mwingi mpaka sasa...nasema kwa kinywa halafu na kufikiri...nchi hiyo mashuhuri kwa nuozo ni tanzania....sina chuki na mtu ila viongozi waliopewa dhamani wanakera jama.Bora Me nibakie huku nilipo nilee wazeee na kubeba mabox ili niendelee kuwafaidisha wamarekani ila sina hofu sababu kodi yangu naiona inafanya kazi so sitalalamika.Niiteni mimi sio mzalendo sawa ila ukweli tanzania kufika huko kunakotakiwa ni mpaka baada ya century 5 ambapo wenzetu watakuwa wanaenda kuishi kwenye sayari nyingine sisi ndio tutakuwa kwenye transition ya kwenda capitalism.Ipo siku Watanzania wataamka ndipo hapo mtakapolijua jiji siombei ila ndiko tunakoelekea.Viongozi hakuna mnayofanya...nchi inazidi kuoza siku hadi siku.Siwapendi kama taka inayotoka mwilini.

    ReplyDelete
  3. Anapochaguliwa rais mpya Tanzania lazima aje DC kujitambulisha.Lengo ni kuwa watoa misaada waweze kumtambua ili waweze kusaidia shughuli za kila siku za serikali yetu masikini.Tutawapa picha gani wafadhili wetu wakisikia kodi za raia wao zinatumika katika huo ukarabati/ujenzi/from scratch/from groung up = $ million moja?Nafikiri tumesikia serikali ya Obama imekatisha msaada sehemu fulani ya Afrika,tukae mkao wa kula.

    ReplyDelete
  4. da hii serikali sio masikini but tanzanian ndio masikini unajenga nyumba kwa gharama hiyo wakati kuna tanzaniani hawajui watakula nini na hata njumba za kuishi hawana wanataka waishi kama wako peponi na sio gavana tu ninaaminimkuna viongozi wa serikali nao wanaishi kwenye mahekalu hivyo. kodi ya mvuja jasho wa kitanzania inatumiwa kiulaini sababu viongozi hawana uchungu nazo inasikitisha sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  5. "..makazi anayoishi yalijengwa upya baada ya nyumba zilizokuwepo awali kubomolewa na akadokeza kuwa gharama zinaweza kuwa kubwa zaidi"

    bajeti ya 2009/2010 imeongezeka kama caution money ilikukabiliana na economy crisis,halafu bado unachoma 1.4bl kwa nyumba moja na hizo zingine za wasaidizi si ni itafika 5bl/=?

    halafu mweshimiwa naona naye ni kama wa mipasho flani hivi, majungu na siasa chafu..nchi imekosa muelekeo na maadili ya viongozi kweli yameporomoka

    ReplyDelete
  6. nahisi watanzania wengi hawajamuelewa beno ndulu ndio maana wamepaniki.hicho ni kiasi kidogo sana kwa ujenzi/ukarabati wa rocker ya taifa. mimi nimemuelewa vizuri saaana... ukweli ni kwamba baada ya yeye binafsi na mawazoyake binafsi amegundua safer ya benk kuu haina security ya kutosha hivyo ameamua fedha pamoja na hazina yote ya tanzania ihamishiwe nyumbani kwake kwa usalama zaidi na kupunguza mikono ya watu wengi kuwa na access ya hazina ya taifa... tumpe nafasi labda ni mbinu nzuri itapunguza ufisadi benk kuu... sasa sijui nae magufuli akiikarabati nyumba yake na kuhamishia wale samaki kwake ili kila anaegaiwa akachukulie nyumbani kwa magufuli ili kupunguza ujanja wa wakubwa kujigawia samaki itakuwaje?

    NONDO

    ReplyDelete
  7. Ndugu wananchi, hii ni kero kubwa sana kwa wananchi ukizingatia serikali yetu na tabia yake ya matumizi mabaya sana ya fedha. Lakini pia tukumbuke kwamba, hii serikali siyo serikali ya kijeshi iliyotwaa madaraka kwa nguvu, bali imechaguliwa na wananchi kwa misingi ya demokrasia. Hivyo basi, wananchi wanastahili wanachokipata. Kama viongozi hawa wanafanya upumbavu huu kwa miongo na miongo na bado wanaendelea kuchaguliwa kuongoza nchi, basi wananchi nao wanastahili kuishi hayo maisha mabovu wanayoyachagua.

    ReplyDelete
  8. Jamani! Bilioni 1.4 kujenga nyumba ya mtumishi wa serikali Tanzania???! Mbona ipo kazi! Nadhani nchi imefikia mahali ambapo wenyewe walishahama siku Mwl Nyerere alipokufa.
    Bila hata soni Profesa mzima anazungumzia sh. 1.4 bilioni kama vile si pesa kitu!!! Mungu, ulije juu, kwa nini hutuui watanzania wooote, na ukaleta uzao mwingine wenye huruma na nchi hii??!!

    ReplyDelete
  9. JAMANI MBONA NIKIINGALIA HIYO NYUMBA KWA NJE HIYO PESA SIIONI. NA KAMA IPO NDANI NI KWENYE VITU GANI?

    KWA MTINDO HUU MIMI NAONA YULE BWANA WANAYEMBANA KUHUSU GHARAMA ZA MAJENGO PACHA WAMUACHIE TU, KWA KWELI.

    ReplyDelete
  10. Ndugu Gavana alichotakiwa kujibu hoja kitaalamu siyo majibu kama yanayolewa na simba na yanga kila wakifungwa wanamsingizia kocha au refa. Yeye anapinga thamani ya nyumba iliyotajwa lakini anashindwa ni kiasi gani cha fedha kilichoidhinishwa kujengwa kwa nyumba hiyo.Anazungumzia kuongelea mtoni hiyo inahusu nini hayo ni ya kale na jibu la kijinga kabisa. Elezea sababu ya wewe kuona una haki ya kujengewa nyumba ya thamani hiyo katika huu wakati ambao hata nchi tajiri kama America, Uingereza nk zinajaribu kubana matumizi ya nchi zao. Tatizo ambalo serikali imefanya ni kumpandisha cheo kuwa gavana wakati ilipaswa serikali itangaze nafasi ya gavana ambae angechukua nafasi hiyo ambae hakuhusiana kabisa na shughuli za benki kuu hapo awali.Kutokana na kwamba alikuwepo wakati wa ufisadi nae ataendelea nao kutokana hiyo ndiyo sera ya benki kuu.

    ReplyDelete
  11. kuna watu walikuwa wanasema watu wa ulaya hamjui mfuko wa cement bei gani??mara mlitaka gavana akae manzese..na utumbo mwingi tu...sasa mmeona gavana mwenyewe anasema kutumia tshs1.4 kwa ukarabati ni kufuru??imejengwa from scratch for that money,still ni nyingi...wengi tunajua unaweza kujenga nyumba hata kwa tshs trillion,ni juu yako kama utaweka gold plated tap,door handles,diamond encrusted floors its up tp you,but when it comes to TAX PAYERS MONEY,lazima tuseme,lazima uwe makini na hela za wavuja jasho,tumia reasonable amount inayoendana na pato la taifa letu,MERRY XMASS WADAU WOTE

    ReplyDelete
  12. Swali kubwa ambalo bado najiuliza ni kwanini serikali bado inaendelea na mchezo mchafu kuwa ku provide nyumba kwa watumishi wake. I hope JK atafuta hii sheria maana ndio inaleta mushkeli hapa. Walipe mishahara mizuri na mambo ya nyumba watajijua wenyewe.

    Prof Ndulu amenisikitisha sana kwenye hili. Hana tofauti na mafisadi wengine.

    Kabaila

    ReplyDelete
  13. watu wenyewe hao mnao wapa nyumba ukifanya utafiti wana nyumba zao binafsi zaidi ya moja. kwa nini wasitumie nyumba zao na kupoteza gharama kutoka serikalini

    ReplyDelete
  14. Kuna msemo wakati wa Morinho anagombana na Wenger. Baada ya mvutano mrefu Mr WENGER akawaambai waandishi wa habari kama ifuatavyo:
    DONT GIVE SUCCESS TO A STUPID MAN, YOU WILL NEVER MAKE HIM CLEAVER BUT HE WILL BECOME MORE STUPID!!

    Jamani tuufuatilie msemo huu tangia wakati wa mkoloni, serikali ya mwanzo,ya pili, mpaka hii tuliokuanayo sasa ivi mtanielewa maana nikifafanua kaka Michuzi hato i post hii msg yangu kama alivyofanya huko nyuma. Si mlalamikii ila namuelewa kua na yeye analinda kazi yake fanisi maana mdomo wa papa ni mpana mno huko baharini.
    Kisiju

    ReplyDelete
  15. Hayatena, hata baba zetu waliokuwa mawaziri wakati wa nyerere na hata nyerere mwenyewe hakukaa kwenye nymba kama hii. Tulikaa kwenye zile nyumba za serikali za enzi zileee.

    ReplyDelete
  16. Prof. Ndulu amefanya kazi nzuri sana. Asianze kuwasikiza wale ambao hata ufanyeje hawana zuri kwa mwingine. Prof. keep doing what you do best: sherparding our economy. Watakupiga madongo tu kama wanavyompiga Rais Kikwete!

    ReplyDelete
  17. Hapo pia kuna jazba na umasikini wetu unachangia sana.Watu wanalala sana bongo.Sio creative, vijiwe vingi na majungu zaidi.Tuamke na tufanye kazi.Serikali haiwezi kuja kukusaidia ulipo, jisaidie! hayo ndio maisha na tutaendelea! Tukiwa kila siku kulalamika tu badala ya kufanya juhudi kujinasua, umaskini hakika hautaondoka kati yetu.
    Kuhusu nyumba, Huyo Prof (GVN amesema namnukuu "Pia si kweli kuhusu hizo gharama kwani hakuna tathmini kamili ambayo imekamilika hadi sasa" kwa hiyo nyumba yake(ya Governor) na zingine gharama bado hazijajulikana.Pia napenda kuchangine kuhusu gharama, watu wengi tu bongo wanajenga nyumba kwa gharama kubwa sana.Na hatujui pia hizo za viongozi wengine wa serikali huwa zinagharimu kiasi gani. Sasa ni wakati wa BOT...kashfa zilizopita zinebebeshwa na wapya...kama Jk na zile zilizopita!

    ReplyDelete
  18. POINTI INAKUJA ZAMANI NYUMBA ZA SERIKALI NYINGI ZILIKUWA SI JUU YA VYUMBA VITATU ZILIKUWA NDOGO TU NA WANARIZIKA WABUNGE, SABABU HAWAKUTANA WANANCHI WAWAONE WANAKULA PESA NI MFANO. TANZANIA LEO SERIKALI UNAONA JUMBAK UBWA ETI KAGARIMU BILLIONI HAPO ZENGINE KANGATA KAWEKA KWAKE. MUWAJENGEE NA WALE MBAGALA WALIOBOMOKEWA NA MABOMU JAMANI NA MA HOSPITALI SHULE NA USAFIRI ANGALAU MA BUS KWA WATOTO WA SHULE TU ZA SERIKALI? ZIPO WAPIIIIIIIIII?. KUHUSU ULIOGOLEA MTONI SAWA NA KUSEMA ULIKAA NYUMBA YA NYASI BASI KAA NYUMBA YA NYASI. "MANGARA"

    ReplyDelete
  19. Mdau, East AsiaDecember 25, 2009

    Huyo jamaa hapo juu anatukumbusha tu wajibu wetu kuondokana na umasikini.Lakini pia kuna hili la kupigana vita kwa viongozi ama kwa makundi au kushindwa ku_fisadi. Kama unakumbuka uchaguzi unakaribia na watu wanatafuta pesa za kifisadi ili wafanikishe malengo yao. Governor huyu ni mchapa kazi na anajua nini kazi yake, hayumbishwi.sasa imekuwa taabu moja kwa moja.
    Keep it Up men...tunataka uimara wa uchumi wetu!

    ReplyDelete
  20. HAHAHAHAAH sasa watu wake wa karibu wameamuwa kuja kutetea humu sasa naona BW MICHUZI utakosa mualiko kwa GAVANA ILA MIE SIONI HIYO NYUMBA KUWA BILLIONI PESA HIZO SIUMEJENGA FLAT NYINGI TU AU VIWANDA MIKOANI AU KISIWANI WATU WAKAANZA KAZI WATOLEO VIJIWENI? OMBAOMBA VILEMA JAMANI MUWARUDISHIE VIBAJAJI VYAOOOOOOO WAANZE KUFANYIA KAZI ILI UOMBAJI BARABARANI UPUNGUE. MWAIPOPO.

    ReplyDelete
  21. Huyu jamaa (Prof ndulu) ni international figure,wachache ndio wanamjua lakini international organisations ndizo zinamjua vizuri.Mwacheni afanye kazi ya ku_stabilize our economy.Pesa za mtelemko pale haziwezi kupatikana, huyo mchumi halisi.

    ReplyDelete
  22. MDAU ANON DEC 25, 02:16 AMELETA POINT YA MAANA SANA.

    SERIKALI IBADILISHE UTARATIBU WA KUWAPA NYUMBA WATUMISHI WAKE NA BADALA YAKE GHARAMA YA NYUMBA IWE SEHEMU YA MSHAHARA. MSHAHARA UNAWEZA KUONEKANA MKUBWA LAKINI PIA SAVING NI KUBWA ZAIDI.

    MBALI NA MSHAHARA ASSUME JAMAA ANAPEWA $3000 KILA MWEZI KWA AJILI YA NYUMBA, KWA MWAKA NI $36000. SHILINGI BILIONI 1.4 ZINATOSHA KULIPIA PANGO KWA MIAKA 30.

    MBALI NA GHARAMA ZA UJENZI KUNA GHARAMA ZA MAJI, UMEME NA UKARABATI (ASSUME) KILA BAADA YA MIAKA 5. KWA MIAKA 30 VYOTE HIVYO KWA PAMOJA GHARAMA YAKE ITAKUWA KUBWA ZAIDI YA MARA MBILI YA GHARAMA ZA UJENZI.

    MIMI NAONA SERIKALI ITAOKOA PESA NYINGI SANA KAMA GHARAMA YA NYUMBA ITAJUMLISHWA KWENYE MSHAHARA.

    ReplyDelete
  23. we anonymous Fri. Dec 25, 07:19
    acha kutukana watanzania wezanko kabla ujabwatuka fikiria vizuri sasa ulitaka wananchi maskini walete umeme, maji wajenge hospitali na serikali inafanya nini si tunalipa kodi pia usitukane watanzania kwa kuwaita wavivu wewe unafikiri kazi zipo zakutosha hata wakienda kulima zana zipo? au mikopo serikali inatoa? inatoa tu kwa mafisadi kijana angalia sana kabla hujabwatuka ungeongea mbele yangu hivyo ungestahili viboko unatetea tu ujinga watanzania mkikaa sana majuu sometimes mnakuwa wajinga unafikiri kuna mtanzania hapendi kufanya kazi kama atapewa nafasi serikali imetusahau hasa vijijini vijana hawana future tatizo lenu mkiwa DAR MNASAHAU KWAMBA PANDE ZINGINE ZA TANZANIA umaskini umekithiri dont be selfish and stupid be reasonable pum&?%$&§%$

    ReplyDelete
  24. kama nyumba IMEJENGWA upya hilo linaeleweka na gharama hiyo bado ni ndogo.
    Lakini tusijetukasikia anapostaafu ANAUZIWA kwa shilingi milioni 60!
    Ako kamchezo ndiko kanatumiwa katika aina mpya ya ufisadi!! ccm ikitoka madarakani TUTAREJESHA MALI YA WANANCHI KWA WANANCHI!!!
    Mungu ibariki bongoland na merry xmas

    ReplyDelete
  25. Naona kuna watu wanachanganya mambo kidogo, nyumba ya kiongozi wa taasisi katika nchi masikini kama yetu kugharimu bilioni 1 kwa pesa za walipa kodi, jamani inasikitisha na inachekesha haswa ukizingatia kipindi hiki.....kwa kweli this system needs overhaul na siyo marekebisho ambayo naona tunapiga marktime sasa

    ReplyDelete
  26. With all due respect, I hate to disagree with honorable Governor’s assertion. Mr Ndulu should understand that when it comes to BOT's issues the bucks stop with him.

    If he really wants the public to continue trust him then he must be forthcoming with Wananchi and explain in detail why BOT, under his watch, has decided to embark in reckless spending spree.

    ReplyDelete
  27. NGOJA WENGINE NAO WATENGENEZE NYUMBA ZAO1
    PATAMU HAPO

    ReplyDelete
  28. TANZANIA TATIZO NI KWAMBA KABLA HUJACHAGULIWA KUSHIKA WAZIFA WOWOTE WATU WENGI HUWA KIFEDHA HALI ZAO SI NZURI SANA. KWA HIVYO WAKIPATA CHEO LAZIMA WAJISAFISHE MAANA KUJINUNULIA VITU WASIVYONANYO KWA KIFUPI KUJIWEKA VIZURI KIMAISHA KILA WASICHOWEZA ZAMANI KUKINUNUA. TUKITAKA KUMALIZA TATIZO KAMA HILI LAZIMA TUACHE MCHEZO WA VIONGOZI WA TANZANIA KUWA KABLA YA UCHAGUZI KUJISIFIA MIMI NA NYUMBA MOJA GARI MOJA. BORA VIONGOZI WALE WENYE UTAJIRI KULIKO HAWA. KWANI KAMA WANA NYUMBA MOJA,GARI MOJA UKWELI WATAKUWA WANATAKA NYUMBA NA GARI NYINGINE UPGRADE. KAMA UNAENDESHA TOYOTA UTAKUWA UNATAKA KUWA NA VOGUE.

    ReplyDelete
  29. labda kiswahili hapa kimenipita lakini mheshimiwa anposema "Pia si kweli kuhusu hizo gharama kwani hakuna tathmini kamili ambayo imekamilika hadi sasa," anamaanisha nyumba inajengwa/imejengwa bila ya kuwa na bajeti? du ingelikuwa ni nyumba ya mtu tu ningelifahamu lakini pesa za wananchi unajenga nyumba na hujui ni kiasi gani itagharimu halafu wewe eti ndio mshika mfuko wa fedha zetu. WATANZANIA TWAENDA WAPI JAMANI?

    ReplyDelete
  30. watanzania tunaendelea kuibiwa mchana kuchwa. Nyumba za serikali nyingi zimeuzwa kwa bei ya vitumbua na zinajengwa nyingine kwa kagharama ya uswazi.tumieni hizo pesa kuendeleza miundo mbinu za kisasa.

    ReplyDelete
  31. Tanzania hata Wauguzi Wasaidizi [Nursing Assistant Aide] na Wafangiaji wa hospitaliwanapewa nyumba na serikali!!!!!Sembuse Muuguzi Mkuu wa Wadi y Watoto!!!!!!! Wacha tuendelee kukaa huku majuaa tukajibebee maboxi. Hatuhitaji kuja huko kuwadhurumu na kitu kidogo wanachochangi wananchi. Kikwete kazi yake ni kuja Ikulu kila siku kuomba omba ya wa Marekani wanayokatwa Taxi kila pay check. Akitaka kuongea na wananchi ni kwa njaia ya redio. Marekani na nchi nyingine inabidi zikatish kutoa msaada Tanzania. Hela ya wanayopewa kwa ajili ya msaada ndo ile inakatwa kutoka kwenye Pay Check yako kwa ajili ya Tax. Na huko Marekani kama hulipi Tax huwezi kufanya kitu, make TAX ni FIRST na HIGHEST PRIORITY. Na Tax ya Marekani inafanya kila kitu katika maisha ya mwanadamu aliyeko ndani na nje ya nchi. Ndo maana hata Kikwete katika hotuba yake huku Marekani alisema kaeni huku mkabebe maboxi akijua kuwa anapata faida kutokana n misaada anayokuja kuomba huku. Tunabeba maboxi, tunakatwa Tax kwa ajili ya kutoa misaada kwa mafisadi. Tanzania Kodi za wtu zinaisha kwenye mikono ya wachache. Wanyone wanaambulia "Ndugu wananchi naombeni kura zenu, Mimi nitakuwa kiongozi mzuri nitahakikisha kila Mtanzania ana chakula, maji safi, elimu bora, kazi, na kuwajengea barabara]. Anamaliza CCM ya mafisadi Juu zaidiiiiiiiii. Marekani hakuna kiongozi anakaa kwenye nyumba ya serikali. Africa ni wizi mtupu.

    Mdau Ohio.

    ReplyDelete
  32. Yeye ni gavana wa benki kuu mlitaka nyumba yake iweje? Maji hufuata mkondo hata mpige kelele hizo pesa hamtapewa.

    ReplyDelete
  33. It's only poor who suffer.

    ReplyDelete
  34. hii picha ya nyumba na hiyo amaount nime ituma kwa senator cornyn,obama white house, rush lumbaugh aAND bill orelly enough is enough .hawa makatibu tawala na wa wizara na gavornor wannaumiza sana

    ReplyDelete
  35. uingereza ni nchi tajiri sana lakini haiwajengei nyumba watumishi wake,haiwakopeshi magari wala haiwasamee kodi..lakini tanzania nchi masikini ila inamwaga mabilioni kwa watumishi wake wa ngazi za juu serikalini..tanzania pula malaka!

    ReplyDelete
  36. Tafadhali governer acha kuchafua roho za watu!!!Hivi mtu wawezaje ukakosa hisia kiasi hiki??Uishi kwenye ufahari kama Mfalme wa Brunei na huku umezungukwa na asilimia 99 ya walala hoi nchini mwao!Hii inaleta kichefuchefu!!

    ReplyDelete
  37. Mimi nina swali, bwana governor alipokuwa anafanyakazi world bank je alipewa nyumba??? na kama akimaalipewa ilikuwa worth how much???... nakumbuka hiyo ni in the USA where the world bank gives mikopo kwa nchi masikini kama zetu je hii ni halali kutufanyia watz je hii nihaki bwana gavana inahusu?? We want an answer!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...