WADAU WATUKUFU, HERI YA SIKU YA MABOXI (samahani kiinglishi mie iz noti richebo hivyo kama nimechemsha kutafsiri 'boxing day' naomba radhi na kama itawezekana mdau mwenye kujua tafsiri hiyo msaada tutani).
KAMA AMBAVYO MTAKUWA MMEONA HIVI KARIBUNI KUMEKUWA NA VIDEO KIBAO ZA YOUTUBE KWENYE GLOBU YA JAMII ZENYE MATUKIO MBALIMBALI. KWA TAARIFA NI KWAMBA HII NI KATIKA KUJIANDAA NA MAMBO MAPYA INSHALLAH TUTAPOINGIA MWAKA MPYA KWANI BAADA YA VIFAA KUKAMILIKA LIBENEKE LITAJIKITA PIA KATIKA HABARI KWA VIDEO.
KUTAKUWA NA INTAVYUU NA WADAU MBALIMBALI NA PIA KUONESHA NA KUSIKILIZISHA TASWIRA NA SAUTI KAMA ILIVYO KWA TASWIRA ZA MNATO, HII IKIWA NI KATIKA KUHAKIKISHA MDAU UNAONA NA KUSIKIA KINACHOJIRI.
GLOBU YA JAMII INAOMBA USHAURI,
MAONI NA PIA UKOSOAJI ENDELEVU ILI LIBENEKE LINOGE.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. kwa hapo tu blogu ya jamii itakuwa juu kama cnn

    ReplyDelete
  2. yaani kwanza kaka michuzi nakupa hongera sana kwa kutupa habari hasahasa sisi tunaokaa ughaibuni tunafarijika sana mimi nakuunga mkono kwa hilo itakuwa bomba sana.tutakuwa tunapata vitu live.

    ReplyDelete
  3. Aloo Michuzi,

    Acha utani wakati wa kazi.

    Ati English is not Reachable! Wee hujui unagusa hisia za watu kiukweli ukweli?

    ReplyDelete
  4. Michuzi,

    Nimekuwa offended na hiyo statement ya sikukuu ya maboksi , haya ni matusi kwetu sisi wabeba maboksi ughaibuni.

    ReplyDelete
  5. ALHAJ ABUBAKARYDecember 26, 2009

    MICHUZI NAONA NA WEWE UNANZA KUWAKASHIFU WABEBA BOX WA MAJUU KIMAFUMBO WEKA WAZI BWANA

    ReplyDelete
  6. kaka kiswahili chako kigumu hizi ngeli (taswira) mi selewi.Kwe you tu sendi baba,kumraji me chelewi kabchaaaa

    ReplyDelete
  7. BOXING DAY SIO SIKU YA "MABOX" KAKA, WACHA KUIFANYA FALA.
    NI SIKU YA KUFUNGUA ZAWADI ZA KRISMAS NA HII NI KWA SABABU NYINGI ZINAKUA ZIMEFUNGWA KTK BOXES THATS WHY IMEITWA HIVO....

    ReplyDelete
  8. Udumu kwa kuendeleza libeneke. Shida ya kuweka video kwenye globu inatuzuia kuibia kampuni zetu muda kuchungulia habari. Security software zinatupiga ribiti.

    ReplyDelete
  9. MTU AMBAYE HAJUI KIINGELEZA NI JOHNI MASHAKA. yeye ndiye kiingereza not richebo kwake

    ReplyDelete
  10. kaka hiyo imetulia sana. iko bomba go on man.
    Ni mimi mdau unayenibaniaga comments zangu.

    ReplyDelete
  11. boxing day ni siku ya kufunguwa zawadi kwa vile huku ughaibuni wana utamaduni wa kupeana zawadi wakati wa xmas huwa hawafunguwi zawadi hadi siku ya 26/12/---- na zawadi hizi hufungwa ndani ya mabox wanachofanya ni kwamba familia ikapata zawadi toka nje ya familia upokea na kuzibwaga kwenye mti wa mki-xmas au hata baba akiwapa watoto zawadi nao hubwaga kwenye mki-xmas, wanasherekea xmas kwanza then siku ya pili ambayo ni mapumziko wanakaa pamoja na kila mmoja huchukuwa zawadi alizopata na kuanza kufungua na huwa ndani ya mabox ndo maana wakaita boxing day

    ReplyDelete
  12. Mmnm, Mi siamini!

    Boxing Day siyo siku ya Kupigana kweli?

    ReplyDelete
  13. Boxing Day= Siku ya ndondi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...