Mtangazaji mongwe wa Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Radio Ujerumani, Bi. Oumulkher akimharakisha mkongwe mwenzie kwenye fani Mzee Radhamani Ali afanye haraka ati wawahi mnuso wa Xmas huko jijini Bonn
Toka shoto ni watangazaji mahiri wa DW Ramadhani Ali, Aboubakary Liongo,Abdul Mtullya,Sekione Kitojo na Mohamed Abdul-Rahman ambaye ndiye bosi msaidizi wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio Sauti ya Ujerumani. Hapa ni katika mnuso wa DW wa Xmas.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kumbe Xmas za Germany ni tarehe 2 February!!!!?
    Walaay, nitakuja huko February 2010 tushereheke tena pamoja.

    ReplyDelete
  2. great to see you guys, lakini fix hiyo datestamp, otherwise waosha vinywa watachonga.

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  4. Naona kamera yake date system imekwama haifanyi kazi

    ReplyDelete
  5. Kaka Abou,kweli maisha ya Ujerumani yamekupendezwa sana.Heri huko maana huku mauzauza matupu.
    Wasalimie mkeo na watoto wako 2. namkumbuka moja makanacy yuko huko au yupo bongo tambarare?
    mdau, Kyela

    ReplyDelete
  6. Mkuu Michuzi kwanza asante sana kwa kutuletea habari mbali mbali kwenye blog yako,hasa kwa sisi tuliopo Ughaibuni. tukirejea kwenye maada nilikuwa nakuomba ndugu yangu kuwa kabla kuweka comments za wadau wanaoandika kwa lugha za kigeni, ungetafsiri kabla ya kuiweka(wengine wanaweza kutumia lugha chafu).kwani blog yako yako ni moja ya blog mwanana iliyokuwa kioo kwa jamii. so dont let watu wachache waigeuze blog hii kuwa kama Ze Utamu (Yenye kuwa na matusi na majungu). mfano anon wa 27th 03:04 am aliyeandika kwa kijerumani. kwanza ameandika kwa kijerumani kibovu, 2 moja kwa moja inaonyesha ana chuki binafsi na huyo ndugu Mohamed (bosi msaidizi wa redio D/welle) na kutopenda maendeleo yake. 3 anaonyesha ni mtu mchonganishi mwenye roho ya kwanini na mwenye wivu wa maendeleo ya mtu. ombi langu kwako ndugu yangu usiruhu watu wachache kama hao wakuharibie blog yako na kuifanya kama ZE UTAMU, ambapo wengine kama sisi blog yako ni kama kiburudisho chetu cha kila siku. wakitaka majungu waambie kuwa hapo si mahala pake.
    mdau R.Rutashobya
    Hamburg - Germany.

    ReplyDelete
  7. Iwe au isiwe na date stamp hainuhusu - lakni nimefurahi kuona picha ya Ramadhani Ali (RA) amabye namkuymbuka nilipokuwa mtoto tukisikiliza kipindi cha michezo cha Sauti ya Ujerumani kujua kama Mtanzania mwenzetu Philbert Bayi alikuwa kashinda tena au la. Siku hizo hapakuwa na TV Tanganyika na ni kipindi ambacho kama sasa tulikuwa na uzalendo na mapenzi ya nchi yetu "kwa moyo wote". Tulisubiri kwa hamu - nafikiri ilikuwa ni kawaida saa nane mchana na RA alipotuvunja moyo kwa kichwa cha habari kilichokuwa na maneno "...Sebastian Coe ampita kama vile kasimama." Kila nikimuona Sebastian Coe (bosi wa kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Uingereza) huyakumbuka maneno yale lakini zaidi hujiuliza kama watu bado tuna mapenzi kwa wanariadha wetu, timu zetu na wawakilishi wetu kama tulivyokuwa utotoni. Siku ile kila mmoja wetu mtaani alikosa raha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...