Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO) jijini Dar leo, kuhusu mwenendo wa hali ya kisiasa kuelekea katika uchaguzi Mkuu. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Hamad Tao.

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Taifa (TLP), Mh. Augustino Lyatonga Mrema, amewataka makada wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wanaomsakama Rais Jakaya Kikwete kutofanya hivyo wakiwa katika chama hicho bali kujiengua na kuanzisha chama chao au kuzungumzia hayo katika vikao vya Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Taifa.

Mrema aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) kuhusu kauli zilizozungumzwa na baadhi ya makada wa CCM na viongozi wastaafu wa serikalini wakati wa kongamano lililoandaliwa hivi karibuni na Taasisi ya Mwalimu Nyerere(MNF).

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo ambaye amewahi kushika nyadhifa nyingi serikalini ikiwemo Uofisa Usalama wa Taifa na Unaibu Waziri Mkuu, vitendo vinavyofanywa na viongozi hao vinatishia na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa Taifa.

“Kuongoza nchi si kazi rahisi hivyo ikiwa wanaona sera za kupambana na ufisadi hazitekelezeki wasipinge wakiwa ndani ya CCM basi wao ndio wanaotakiwa wafanye maamuzi magumu, ama kwa kuanzisha chama chao ama wajiunge na vyama vya upinzani kama mimi nilivyofanya lakini kutoa kauli za uchochezi wakati bado ni wanachama wa CCM, wananchi hawatawaelewa.” Alisema Mrema.

Alisema katika kongamano hilo makada hao walisema kuwa rais amezungukwa na kundi la wezi na kama anashindwa kuchukua maamuzi magumu atoswe asigombee tena urais mwakani na ampishe mtu mwingine.
Jambo hilo Mrema alisema ikiwa zitaachwa ziendelee zinaweza kuleta uchochezi ili wananchi waiasi serikali halali iliyo madarakani hivyo kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. mrema amesahau kuwa kina butiku ni uroho wa madaraka unawasumbua,wao walivyokuwa madarakani walifanya maamuzi gani magumu zaidi ya kuiweka nchi katika njaa na ujinga.kwanza wanatakiwa wajiuzulu mara moja kwenye hiyo ngos ya mwalimu maana wameigeuza sehemu za kuumizana wenyewe kwa wenyewe,hivi wanataka rasi ageuke mugambe,kila kitu aamue yeye,sasa majaji na mahakimu watalipwa kufanya nini,mramba,yona na mgonja wako mahakamani,ni kazi ya mahakama kuhukumu sio rais,wengine mafaili yako kwa ddp n a takururu.

    ReplyDelete
  2. Dada yangu wee angalia mapenzi usiangalie Sijui Dini au Mtu kuoa wake wengi kwani hiyo sheria ya kuoa wake wengi ipo kwa Dini ya kiislam lakini siku hizi hata hao wakristo wanaoa zaidi ya mke mmoja.
    Pia katika dini ya kiislam kuna maadili zinazofanya mtu aoe mke wa pili ingawa kwa upungufu wetu wa imani hatuzifuati.
    kama Anonymos alivyosema kuwa ikiwa imekuwa proved kama mke hawezi kushika mimba hivyo wewe na mume inabidi mkae na muamue kutafuta mke mwenza ila na wewe ushirikishwe sio uje ujue kuwa mumeo kaoa nakishatia mimba.

    ReplyDelete
  3. Mrema ameshindwa kuchambua hii mada kwa kina. Nadhani kama alikuwa amechambua hii mada kwa aungalifu asingetoa hoja ya kuwa hawa watu wahame CCM.

    Kwanza inavyoona mimi kuna njia kuu tatu ambazo zinaweza kutumiwa na mtu aliyeona jambo fulani kuwa ni tatizo. Hizi njia ni kukaa kimya, kukimbia tatizo, na kulikabili tatizo. Njia hizi ninaeleka vizuri sana kwa watu wengi hasa kwa wadau wa blog hii, hivyo sina haja ya kufafanua kila moja kuwa ina maana gani. Ila cha muhimu hapa kila moja ina matokeo tofauti katika tatizo.

    Njia za kukaa kimya na kukimbia hizi huwa sio muafaka sana kwani tija yake ni ndogo kwa sababu tatizo litaendelea kuwepo. Hivyo njia ya kukabili tatizo ndio mara nyingi inakuwa na tija zaidi. Hivyo basi hoja ya Mrema kuwa hawa watu watoke CCM ni kulikimbia tatizo, hawa watu wao wameamua kulikabili tatizo ndani ya chama chao, na wanataka wale wenye matatizo ndio watoke kwenye chama waacha chama chao kikiwa safi.

    Mrema yeye aliondoka CCM, je amefanikiwa kufikia malengo yake? Mimi naona hajafanikiwa, kama hajafanikiwa basi ana sababu gani ya msingi kuwaambia wananchi kwamba wale wanapinga uchafu ndani ya CCM watoke ndani ya chama ili wapiganie usafi wa chama wakiwa nje?

    Wenye matitazo ni wachache sana, na wanajulikana hivyo ni vyema kwa hao makada kumwambia rais na mwenyekiti wa chama chao hawashughulikie. Hawa makada kwa kutoa tu hoja zao tayari wamefanya maamuzi magumu ya kisiasa kwani tayari wameshakuwa na madui ndani na nje ya chama hata kufikiwa kuitwa wehu.

    Mimi sio mwanasiasa ila ni mfuatiliaji na mchambuzi wa mambo mbali mbali ya jamii yetu.

    Mdau MG

    ReplyDelete
  4. tatizo letu wabongo ni kutaka kuendesha mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na utawala wa sheria kwa mfumo wa demokrasia ya chama kimoja na udikteta wa chama kimoja. mojawapo ya nguzo kuu za mfumo wa utawala bora tunaoupigia ngonjera (lakini hatutaki kuutekekeza!) ni watu hata ndani ya chama kimoja kuwa na maoni na mitazamo tofauti, na hata kutofautiana na mwenyekiti/rais wao, kuzieleza hizo tofauti/mitazamo yao kwa uwazi na ukweli juu ya suala husika na hatimaye kufikia muafaka. sio lazima wale wasiokubaliana na mwenyekiti au rais wahame ndio waweze kueleza wanayoona hawakubaliani. HUO NI UDIKTETA ndani ya chama. ndio hayo Mhe Mrema anayofikiria (kumbuka ambavyo huwa hapendi kupingwa na mtu ye yote ndani ya TLP) ndio hayo wanaopinga akina Butiku wanayopenda kuona yanatendeka ndani ya CCM. Tunajikanganya na kujikinzani wenyewe. mfano mzuri ni kuhusu muswada wa sheria ya afya nchini marekani (kwa vile tunapenda sana kuiga kutoka marekani) baadhi ya wabunge wa chama tawala wamekataa hadharani kuunga mkono baadhi ya vipengee vilivyopendekezwa na rais obama na hatimaye wameanza kufikia muafaka. kupinga baadhi ya sera za obama haiwalazimishi kuhama chama - HUO NDIO UTAWALA BORA na si huo udikteta mnaotaka kuimarisha wakati huku mkiimba utawala bora. Kwa vile sio malaika, Rais JK na wengine wajao wataendelea kukosolewa na makada wa sasa, wa zamani, wanachama na wasio wanachama wa ccm - ni haki na kaida ya utawala bora. MSITURUDISHE NYUMA.

    ReplyDelete
  5. IT'S RUBBISH!!

    A NON-VISION MAN, TIRED OF HIM.

    WHEN IS HE RETIRING??

    ReplyDelete
  6. nyoka ni nyoka tuu kimemuuma kamua kusema huu ndio uzalendo wa kweli kweli mwalimu nyerere alijenga vijana wake vizuri sio sisi wa leo kidogo kitambulisho duu

    ReplyDelete
  7. hapa umeongea point bw lyatonga, kama wana nia ya dhati wao ndio wafanye maamuzi mazito wajiengue.NO COMMENT

    ReplyDelete
  8. KATIBA NDIO MCHAWI WETU.NA HUYU KATIBA TUSIPOREKEBISHA TUMEKWISHA.KATIBA NZURI WATAOGOPA ,HATA KAMA MTU ANATAKA KUWA KIONGOZI WATAPUNGUA NA OROHO WA MADARAKA UTAPUNGUA.HAPO WATAKAOSTAWI NI WALE TU MUNGU KAWATUMA BASI.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
    MDAU
    WASHINGTON DC

    ReplyDelete
  9. wakina butiuku kinawauma hawana watu wao walobebwa na JK,hamna cha zaidi,wivu tuu.

    ReplyDelete
  10. Achana na chama bwana, chama kimeshika utamu. Mzee wa Kiraracha amepigika sasa hivi anajaribu kujisogeza kwa JK. Bado kidogo anatangaza kurudi CCM na kuomba walau ubunge wa kuteuliwa.

    ReplyDelete
  11. Anon huko juu, siyo DDP ni DPP yaani Director of Public Prosecution, kiswahili chake ni Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali, au kitu kama hicho.

    pia, ni TAKUKURU na si takururu.

    Eish!

    ReplyDelete
  12. Wananchi mpeni nchi hii Mzee wa Kiraracha atainyosha nchii hii si muliona mavituz yake alipokuwa serikali?

    ReplyDelete
  13. Jamani huyu mzee yaani ndio amefulia hivi?? Nomaa, nomaa, noma! Ila anasema ukweli hao makada wanataka umaarufu tu kwanini wasisema hivyo vitu kwenye vikao vya Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Taifa. Huku ni kujiotafutia umaaruf tu kupitia mgongo wa Raisi.

    ReplyDelete
  14. Mrema umeishiwa, wewe mambo ya CCm yanakuhusu nini??? Tuachie wenyewe tunajua jinsi ya ku-solve haya ya kwetu. Au unataka kurudi?? Basi omba tena uanachama, lakini usahau ukubwa... Rais katoa uhuru wa kila mtu kutoa mawazo yake ili wananchi waamue wenyewe, na washaona na kuamua na tushamalizana. Wewe kinachokusumbua ni nini?? Angalia chama chama, hupati huruma ya CCm hata kidogo ulihama mwenyewe.

    ReplyDelete
  15. Mrema pole!!! Tubajua unajipendekeza ili tukuonee huruma tukupe jimbo la Vunjo, janja hiyo kusa jua...nikuulize wewe Mrema na sisi CCM nani anauchungu na rais, hao jamaa wako ndani ya chama chetu tutamalizana nao kimya kimya wewe hayakuhusu hayo...pili huruma ya kupewa Vunjo sahau, tafuta issue nyingine....

    ReplyDelete
  16. mzee wa bunjuDecember 29, 2009

    Mrema yuko right kabisa, waache unafiki watoke kama anaona mambo yanakwenda mrama bac, kwani wao si ndo wazee?? wameshindwa nini kumshauri rais mpaka wakamnange?? kikwete kama binadam anaudhaifu wake lakini ni msikivu saaaana na ikulu ya kikwete ni kama ya mwinyi milango wazi mbona wakienda wana smile tu hawa hawamshauri??? ashauriwe na nani??

    mimi naona anakwenda vizuri ila makundi ndo tatizo, hawa wazee kama wana agenda sirini waiseme

    kikwete tuko na wewe japo mimi sio CCM

    mzee wa bunju

    ReplyDelete
  17. MREMA NI CCM

    ReplyDelete
  18. mrema kachoka mbaya cheki hio sura kwishnehiiiiiiiii kachemka huyo ulimwengu watatu unajifanya mdomo mrefu ona sasa anatapatapa duh ccm nuksi.angetulia tu akajifisadia mipesa yake kaleta kidomodomo haya mzee safarinjema,mdau greece

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...